Mgogoro wa Ziwa Nyasa: Serikali ya Mkapa inabeba lawama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa Ziwa Nyasa: Serikali ya Mkapa inabeba lawama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Aug 5, 2012.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Baada ya kufuatilia historia ya mgogoro huu nimepata wazo kwamba Tanzania ilikua na historia ya kipekee ya kushughulikia tatizo hilo wakati wa serikali ya Bakili Muluzi (94-2004).

  Muluzi alikua ni rais ambaye alikuja kua na uhusiano mzuri sana na Tanzania na uhusiano mzuri wa kikazi na Rais mstaafu Mkapa.

  Mkapa ambaye alikuwa anajua tatizo hili kwa undani kama kiongozi wa muda mrefu wa ngazi za juu, angepaswa kutumia muda huo kuanzisha mazungumzo ya kutatua hili tatizo kwa kuongea na serikali "rafiki" ya Malawi ya wakati huo baada ya kuondolewa kwa Kamuzu Banda (aliyekua mtu mgumu kuongea nae lolote la maana).

  Kama kawaida viongozi wetu wamekua hawana malengo ya muda mrefu yenye manufaa ya taifa wanatumikia miaka 10 yao halafu wanajenga mahekalu ya kustaafu na wananchi mtajijua wenyewe. Sera ya nje ya Tanzania baada ya kumalizika kwa vita ya baridi ya dunia imebaki kua shambolic to say the least. Hatuna dira wala mipango ya kimkakati ya kutumia jiografia (geo politics) kutetea na kujilinda kimaslahi katika eneo hili lenye migogoro isiyoisha.

  Sasa hivi na matatizo ya kiuchumi duniani na siasa za ushindani za Malawi kuna uwezekano wa kuendelea kupata reactionary leaders au populist leaders kama huyu Banda na kale kadirisha kalikokuepo miaka ya 94-2004 kua ndiyo kamefunga kabisa.

  Mungu ibariki Tanganyika yetu,


  Mharakati
   
 2. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Kuanza msingizia aliyeondoka wakati aliyepo pia anapaswa dili nalo ni Ishara kuwa limeshakomaa na kumwogopesha. Kwani kiapo cha kuilinda katiba kinampeleka kulinda mipaka inayosemwa na Katiba yetu bila kusema kuwa kama ilianzishwa na presidaa mwingine basi asihusike.

  Makubaliano yalianza Long time, ila kama kawaida ya mazungumzo ya nchi na Nchi huwa hayaishi utawala mmoja,la utawala fulani unaweza kuwa na advantages zaidi au hata disadvantages zaidi ya mwingine.

  Wamalawi wameanza endeleza upande wao so taratibu wataongeza na kuwapa mikataba mataifa ya nje. Sasa baadaye mazungumzo yanaweza tibuliwa. Tanzania mkija juu mnajikuta mataifa makubwa yakilinda vitega uchumi vyao na hivyo kusaidia maadui zetu. Na tayari zoezi la kudilute watu linaendelea kwa kasi sana. Watu wanaoana na wabongo wasiojua malengo ya wenzao katika mipaka yetu.

  Na hili ni sehemu nyingi za nchi.Sijui kama SERIKALI IMEWAHI FANYA OPINION POLL KUJUA MAKABILA YA MPAKANI KAMA YANAPENDA KUWA UPANDE GANI WA NCHI. sijui kama waliwahi wauliza masai wa bongo, Jaluo au hata warombo kuwa wangependa TZ au Kenya, Waangaza na nchi za Rwanda na burundi, wanyaKyusa, wanyasa, na wengine wanoanzia katika border la DRC, zambia, Malawi, na Mozambique.

  Mbaya zaidi ni kwamba Tanzania haijaendeleza sana mikoa ya pembeni kiasi cha raia wa huko kuona kuwa nchi za Jirani ndio wana maendeleo zaidi. Watu wa mipaka yetu huwa hawajiamini mbele ya wenzao.Utakuta wanahofia vitu kama Kiingereza na majengo na bidhaa za viwanda vya nchi jirani.

  Serikali kama haijui haya ni siku wamalawi wanasema zipigwe hata kuwa za watu serikali legelege inashangaa watu kuikataa Tanzania

  Jamani pro Kikwete tunaomba muanze maisha mapya term ya Kwanza ilishapita sasa mambo ya kila kitu kusingizia Mkapa au hata wasaidizi wake ni udhaif na woga. Plse toeni alternative solutions kam Presidaa ataona anweza zitumia basi kazi ianze.
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Wakati huo na wewe ULIKUWA IKULU? Sababu inaonyesha ya kuwa ULIKUWA UNASIKILIZA MIKUTANO YOTE YA

  MKAPA NA MULUZI na INAONYESHA HAWAKUZUNGUMZIA LAKE NYASA...

  INA ONYESHA HATA wewe haujui DIPLOMASIA, ni kulalama kama kawaida ya Mwananchi wa Tanganyika halafu

  Jasho halikutoki Unajinyamazia... hautaki Matatizo... Unajua Mbunge wako nakula PESA KIUFISADI Utalalamika

  Halafu Utatulia Ukija Uchaguzi Utamchagua huyo huyo...
   
 4. J

  JokaKuu Platinum Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Mharakati, ..this is very interesting lakini umesahau kwamba JK alikuwa waziri wa mambo ya nje for 10 yrs wakati Mkapa akiwa Raisi. ..je, JK alimshauri nini Raisi wake, au alifanya jitihada gani kushughulikia tatizo hilo? mbona hatukumuona JK akijishughulisha kutatua mgogoro huu kama anavyofanya Benard Membe sasa hivi??
   
 5. NusuMutu

  NusuMutu JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 423
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lakin jamani rais si anaapa kuilinda katiba ambayo ina-define nchi na mipaka yake? Akishindwa kuilinda na sehemu ya nchi ikamegwa na 'mama' tumfanyeje?
   
 6. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,896
  Likes Received: 5,356
  Trophy Points: 280
  jk anapenda kurefer vitu alivyofanya na marais waliopita lakini hasemi inflation imevunja rekodi katika awamu yake!na hili anataka kumbwagia mkapa?!
   
 7. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,094
  Likes Received: 1,477
  Trophy Points: 280
  Tanzania tumekuwa wadhaifu juzi nilimsikia mbunge mmoja wa Kagera Ntukamazima anamuulizwa swali waziri wa afrika mashariki kwanini mifugo ya wanyarwanda ikivuka kufata malisho inarudishwa waziri akamjibu ana safari ya huko na atakutana nawiri mwenzake watajadili na yeye anakaribishwa nimeshangaa badala ya kutetea watanzania anatetea wageni ingawa tukiangalia jina lina asili ya huko huko
   
 8. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wa TZ kazi tunaya hu Jk kila kitu kina mshinda angalia wasomali wanavyo pitishwa hapa kama mbuzi , wafugaji toka rwanda wanachungia mifugo yao kwenye mashamba yetu kule kagera .lakini jamaa kanyamaza tu ndio maana hata huyo mama wa malawi anatudharau sasa.
   
 9. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Jina tu linaonyesha ni mzamiaji.
  Ntukasomething
   
 10. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #10
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Tatizo lipo kwa Jk na jeshi lake. Mkapa ameongoza vizuri kamaliza.
   
 11. Bejajunior

  Bejajunior Senior Member

  #11
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Sera ya uhusiano mwema iangaliwe vizuri maana tuendako majirani tunaowalinda watakuja "kutunawisha" ili tule. Kama hatutatoa mawazo stahiki ku-deal na hili swala.
   
 12. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,494
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  Jeshi la cha nazi ni matatizo matupu wamepoteza mwelekeo!
  Sasa angalia u.p.u.m.b.a.v.u huu wa kusingizia waliomtangulia ilhali na yeye alikuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka 10!
   
 13. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Hebu tuangalia, kwanini mgogoro huu unakuja kipindi hiki wakati huu ambapo Bi Kiroboto wa Marekani anatembelea Malawi? Hakuna uhusiano kweli?

  Ushahidi uliyopo na wa uhakika ni kuwa marekani wame eye-mark eneo hilo ka Nyanda za Juu Kusini likiwemo eneo lijulianalo kama Rungwa-Ruaha Landscape ambapo linahusisha mito mikuu ya kusini nyanda za juu, milma yake na hasahasa bonde la ufa na huu ni mpaka Ziwa Nyasa.

  Serikali ya Marekani ndiyo inayofadhili mpango mzima wa hifadhi za wanyama pori za maeneo haya ikiwemo ufadhili wa utafiti na upanuzi wa Ruaha National Park ambapo wazee wetu kule bonde la Ihefu waliondolewa.

  Pia NGOs nyingi za Kimarekani zimejikita maeneo haya ikiwemo NGO ya Jeshi la Serikali ya Marekani ijulikanayo kama Walter Reed. Kwa hali ya uchumi wa Malawi, uchumi ambao imefika mahali hawana motuary na walikosa hata mafuta ya kuendeshea majenereta wakati wa mazishi ya raisi wao.

  Ni nchi ambayo ina hali mbaya kiuchumi kuliko maelezo, lakini watu wake hawasikiki kimataifa (isipokuwa yawezekana tukaanza kusikia ukizingatia Bi Kiroboto kaenda huko na inaonekana serikali ya wababe hawa ikawa na vested interest).

  Hakuna safari ya Bi Kiroboto wao kwenda kwa nchi masikini kama Malawi ambayo hailipi, sina uhakika na upendo wowote wanaotaka kuunyehsa kwa nchi hii kama ilvyo Tanzania kwetu, ambapo mpaka yule gwiji wa migogoro duniani alirudi hata baada ya kustaafu. Kuna siri kubwa bila shaka- What a morden neo-colonialism we are already traped in.
   
 14. m

  mharakati JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Nafikiri Jk kama waziri wa enzi hizo anayeshughulikia sera ya nje na maslahi ya nje ya taifa anahitaji lawama kwa kiasi chake..ila kama serikali nzima, Mkapa atabeba political responsibility kwa sababu hatuna notes za vikao vya vyote vya baraza la mawaziri haswa kwenye mambo ya usalama wa mipaka na sera ya nje kwa hiyo hatuna uhakika kama Jk aliwahi kumshauri boss wake au la?

  Mkapa kama na aliyekua na uhusiano na Muluzi angeanzisha mazungumzo ambayo yangeendelezwa katika ngazi ya mawaziri baada ya mahead of state kuyapa heshima haya mazungumzo.

  Kwa hili Mkapa bado anaonekana kama ana lawama zaidi, Jk angeshauri tu ila marais ndiyo walitakiwa wakutane kwanza na kuset parameters za mazungumzo.
   
 15. m

  mharakati JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Kaka jazba haijengi ila kubomoa, sina minutes za mikutano ya Muluzi na Mkapa, ninachojua ni Mkapa kwa sababu anatoka kusini alijaribu kuanzisha hii habari ya mizigo ya Malawi ipate corridor pale Mtwara kupitia Mbamba bay kitu ambacho labda kama Rais mstaafu Mkapa angepata miaka mingine 10 angefanikisha labda..

  Hata kama aligusia mgogoro haikua priority ya sera ya nje ya Tanzania kwa sababu sisi wafuatitiliaji wa mambo ya kimataifa hatujawahi sikia kitu kama summit au task force ya kufuatilia hii kitu, kama mazungumzo ya siri yalikuaeop hayakupewa kipaumbele chake.
   
 16. m

  manucho JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Wamalawi wapewe ziwa waendelee na shughuli zao wanazozitaka kwa sababu tanzania wakiachiwa hiyo sehemu ya huo mpaka wanaosema umepita katikati mwanchi wa kawaida ambaye ndiyo mtanzania halisi atafaidi nini?

  Kama gesi asilia inatoka hapo Mtwara lkn gharama za umeme na maisha ndiyo zinapanda kila siku na wanaopandisha ni hao wachache kwa maslahi yao, kwahiyo hata hapo malawi wanang'ang'ania kwa maslahi yao hao wachache.

  Halina faida yoyote kwa mtanzania, wamalawi wapewe ziwa lao tu
   
 17. m

  mharakati JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Pro-kikwete, he he ..nway, mi naona kila administration ina unique historical opportunities za kulinda na kujenga taifa kwa faida za vizazi vingi vijavyo. Mkapa alikua nazo, Jk amekua nazo na yeye atakuja kulaumiwa akimaliza muda wake kwa kutokua makini sana na hili au lile.

  Mkapa alikua na nia nzuri tu ya kuwaweka wamalawi karibu na tanzania kiuchumi kwa kufungua miundo mbinu ya kusini kwa ajili ya mizigo na biashara za malawi na hii ingewafanya kufikiria mara mbili mbili kuanzisha mzozo wowote na Tz..

  Hii ninachisema ilikua ni wazo zuri na ingebidi liende sambamba na maongezi ya kisiasa ya kutatua mgogoro kwa spidi nzuri kwa sababu serikali ya wakati ule ya malawi ilikua karibu sana na tz na hapa tungepata favorable conditions.

  wataalamu wanasemaje unaingia kwenye majadiliano ukiwa kwenye nafasi ya kupata zaidi kulingo mwenzako (you go into negotiations in a position of relative strength). Tanzania ya wakati ule ilikua kwenye nafasi kuliko sasa na hatukufanya lolote. Na hapa ndiyo namlaumu BM
   
 18. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Sasa Unaongea vizuri unaweka neno LABDA Kama, LABDA Ange... HIYO ni BORA

  Sina Jazba sikipendi Chama Cha Mafisadi ila Habari uliyotuwekea ni kama vile ulikuwapo hapo wakati hao Marais

  wakijadiliana.... Sasa nimekubali na hiyo LABDA kama, LABDA ange.... HIYO INGEPASWA kuwa kwenye Main Story
   
 19. m

  mharakati JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  usibadilishe theme yangu kaka, nimesema Labda kama angekaa miaka 10 mingine labda angebadilisha, ina maana miaka 10 yake hakufanya wala kuchukulia uzito hili jambo zaidi ya wazo la bandari ya mtwara kupitisha mizigo ya malawi.( kitu ambacho ni kizuri kupunguza uhasama kwa kukuza mahusiano ya kibiashara, lakini ingebidi hili wazo liendane na diplomasia ya kujaribu kutatua tatizo lililokuepo).

  ujue ukitaka kuelewa utaelewa tu, usipotaka hautaelewa kaka, jaribu kuangalia na kuelewa kabla ya critique

  **Angalia gazeti la leo the citizen, mbunge zambi anaongelea haya haya niliyosema**
   
 20. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  Sasa kama malawi wanagombea ziwa mbona hawajiulizi hayo maji yanayojaza ziwa yanatoka wapi na mbona mito mikubwa inayokusanya maji kutoka umbali mrefu iko bongo land, hivi hili bara limekumbwa na nini jamani manake viongozi wake hatujui wanatumia nini kufikiri.

  Huyo waziri wa Malawi anajambisha tu na mziki wetu hawauwezi kabisa kama vipi wakichafue wauone mziki wenyewe na tunaichukua nchi yetu.

  Mie sioni sababau yeyote ya huu mjadala its obvious mno.
   
Loading...