PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,203
- 8,723
Mara nyingine kuna hatari kubwa kwa migogoro inayotokea katika nchi zetu hizi kuvishwa sura zenye malengo binafsi ya watu au kundi la watu hasa malengo ya kisiasa na umaarufu au kufuta kashfa fulani zinazoikabili nchi husika.
Tanzania kwa sasa tuko katika mgogoro wa mpaka na nchi ya Malawi, unaohusisha Ziwa Nyasa. Mgogoro huu ni wa ukweli kabisa na si wa kutungwa maana upo tangu enzi za Mwalimu. Lakini kitu cha kuwa nacho makini ni upande wa maamuzi sahihi juu ya kukabiliana na mgogoro huu mzito ambapo usipokabiliwa kwa umakini, tutashuhudia nchi ikiingia kwenye vita na kumwaga damu za Watanzania, maana vita haina macho!
Hapa jamvini kwa sasa kuna threads ambazo zinasema wazi kuwa majeshi yetu yameshaanza kufanya mobilisation ya kusogea eneo la Kyela. Kuna mdau mmoja jana alisema kuwa mida ya saa 3.30 za usiku amekutana na Army Deployment ya hatari ambapo msafara mzito wa magari ya jeshi yapatayo 200 yakitokea PANDE ZA Arusha na Moshi yanaelekea kusini mwa nchi, ambapo kama ni kweli, basi hali si shwari.
Naomba kutoa tahadhari kwa wanadiplomasia, Wanasiasa na Jeshi kuwa tusipokuwa makini mgogogoro huu unaweza kuwa mtaji na kinga kisiasa(political camouflage) wa baadhi ya manyang'au wa hapa nchini kwetu, ambapo wanaweza kuamua ku'capitalize on it kwa kuiingiza nchi vitani kwa malengo kama:
I. Kuwafool wananchi wajue kuwa serikali yao inawajali sana na kulinda mipaka yake, wakati ambapo ukweli ni kuwa kila kona ya mpaka wa nchi yetu inapitika kirahisi tu na wazamiaji toka nchi za jirani(mifano ipo mingi).
II. Ku-divert attention ya wananchi ambapo sasa wako katika mijadala mizito juu ya hatima ya nchi yao. Kuna masuala mazito ambayo yametokea of recent ambapo mengine yameibuliwa Bungeni, na mengine yakiwa yanahusisha migomo na maslahi wa Tanatanzania kwa ujumla.
III. Kujisafisha na kutengeneza image inayopendeza usoni pa wananchi, ili kujiwekea malengo ya kufikiriwa kwa uongozi huko mbele ya safari.
IV. Kupata sababu ya kutotimiza ahadi nyingi zilizoahidiwa kwa wananchi nyakati za uchaguzi.
Isije kuwa tunalazimisha Punda afe lakini mzigo wa tajiri lazima ufike sokoni.
Nawasilisha.