Katika moja ya hotuba zake Mwalimu Nyerere anasema, "...... nje ya Muungano hakuna Wazanzibar, bali kuna Waunguja na Wapemba". Hapa alikuwa akimaanisha kuwa Muungano umewafanya Wazanzibar kuwa wamoja kwa maana halisi ya umoja, kuwa hawabaguani na ndiyo moja ya malengo makuu ya wao, Nyerere na Karume kuunganisha Tanganyika na Zanzibar.
Na kama waliamiani hivyo, kwa nini baada ya nusu karne ya Muungano Wazanzibar si wamoja na Muungano unafaida gani kwao kama unaendelea kuwagawa?
Kwa nini Tanganyika kwa kivuli cha Tanzania inaendelea kuwang'ang'aniza Wazanzibar kuendelea na Muungano ambao malengo yake yakuwafanya wazanzibar waishi bila chuki, yameshindwa na badala yake kuonekana kama Tanganyika imeteka Nyara Zanzibar!
Hata kama Nyerere na Karume walikuwa na dhamira safi, kwa nini kuendeleza mawazo yao ambayo yanaleta chuki kwenye jamii ya Wazanzibar.
Mwisho, hivi haya Mapinduzi yanayong'ang'aniwa na wana CCM wa Zanzibar, malengo yake yalikuwa kugawa Wazanzibar ama kuwaunganisha, kwani inaonekana kuwa Mapiduzi hayo ni Mungu wa kuabudiwa, lakini kwa akili ya kawaida tu, ni moja ya mambo yanayowajengea chuki na utengano mkubwa.
Kwa kuwa mgogoro wa Zanzibar ni wa miaka mingi, nadhani watawala wanaolindwa na magobole, wametia pamba masikioni mwao kwa faida ambayo sisi hatuijui.
Tujadili.