Mgogoro wa viti maalum CHADEMA: Mbowe ana mkakati gani wa kuvunja kambi ya Askofu Bagonza, kambi ya Askofu Mwamakula, na kambi ya kina Mdee?

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,019
2,473
1609563275601.png

Askofu Bagonza

Jana mchana, mtandao wa Jamiiforums ulitutaarifu kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ataongea na umma wa Watanzania. Mpaka sasa hajasikika. Wakati tunasubiri hotuba yake, napenda kumkumbusha kuja na jawabu kwa swali lifuatalo: Mbowe anao mkakati gani wa kuvunja kambi ya Askofu Bagonza, kambi ya Askofu Mwamakula, na kambi ya kina Mdee? Kusudi aweze kuelewa kwa nini nimeuliza swali hili, namwalika kusoma kwa umakini hoja ifuatayo:

Ndani ya Kamati Kuu ya Chadema kuna kambi kuu tatu. Kambi ya kwanza inaongozwa na Mshauri wa Kiroho wa Mbowe, Dr. Benson Bagonza, anayepinga hoja inayotaka Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni. Kambi ya pili inaongozwa na Mshauri wa Kiroho wa Lissu, Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula, anayekubali hoja inayotaka Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni. Na Kambi ya tatu inaongozwa na Halima Mdee, anayekubali hoja inayotaka Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni.

Kwa upande mmoja, mpasuko huu unatokana na ukweli kwamba Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ameshindwa kutofautisha kati yamamlaka ya kuamua (deliberative power) yaliyo mikononi mwa watu ambao ni wajumbe halali wa vikao halali na mamlaka na ya kushauri (consultative power) yaliyo mikononi mwa watu ambao sio wajumbe wa vikao halali.

Na kwa upande mwingine, mpasuko huu unatokana na ukweli kwamba Mbowe ameshindwa kutofautisha kati ya vikao rasmi kikatiba (formal meetings) na vikao visivyo rasmi kikatiba (informal meetings).

Kwa mujibu wa aina za viongozi wa chama zilizotajwa katika ibara ya 6.2.3 ya Katiba na idadi yake iliyotajwa kwa kila kikao katika kila ngazi, washauri wa kiroho wa viongozi sio sehemu ya viongozi wa chama.

Aidha, kwa mujibu wa aina za vikao zilizotajwa katika ibara ya 6.2.1 ya Katiba na idadi yake iliyotajwa kwa kila ngazi, washauri wa kiroho wa viongozi sio wajumbe wa kikao chochote halali katika Chadema. Hata hivyo, mawazo yao yanayumbisha vikao rasmi vya chama mpaka kuzalisha mipasuko iliyotajwa.

Na kwa kweli, kutoa taarifa za chama kwa washauri wa kiroho ni kuvujisha siri za chama, kinyume cha kanuni ya 3(c)(i) ya Mwongozo wa Kamati za Maadili ya Chama.

Kambi ya kina Mdee wanapinga jambo hili. Kwa mfano, “uteuzi wa awali” wagombea ubunge viti maalum unafanywa na kuratibiwa kwa mujibu wa Mwongozo wa Bawacha (toleo la 2019) ibara za 7.4.4(h), 7.6.3(h), na 7.7.4(h), na hatimaye Kamati Kuu “kuthibitisha” uteuzi huu kupitia kura ya wengi kwa mujibu wa ibara ya 7.7.16(q) ya Katiba (toleo la 2019).

Uthibitisho huo ndio hutafsiriwa kama kibali kwa Katibu Mkuu kuwasilisha majina kwenye Tume. Ndani ya kikao kimoja cha Kamati Kuu kura ya wengi ilipigwa na “kuthibitisha” uteuzi lakini Mwenyekiti akapiga “kura ya veto” wakati kikatiba Mwenyekiti hana mamlaka hayo.

Mbowe anasikiliza zaidi Mshauri wake wa Kiroho kuliko maamuzi ya vikao vya Kamati Kuu. Hasa, huu ndio msingi wa mvutano kati ya kina Mdee, kina Lissu na kina Mbowe. Vikao visivyo rasmi vinafuta vikao rasmi.

1609562945014.png

Askofu Mwamakula

Kwa ufupi, mazingira ya ugomvi unaoendelea sasa kati ya kambi ya kina Mbowe, kwa upande mmoja, na kambi ya kina Mdee, kwa upande mwingine, yanafanana sana na ugomvi uliotokea kati ya kambi ya kina Nyerere na kambi ya kina Bibi Titi Mohamed mwaka 1964.

Paul Bjerk (2015) amesimulia vizuri ugomvi ulitokea kati ya Nyerere na kina Bibi Titi Mohamed. Simulizi hiyo imo katika kitabu chake kiitwacho, “Ujenzi wa Jamii ya Amani: Julius Nyerere Katika Kusimika Mizizi ya Tanzania kama Taifa linalojitawala kwa mujibu wa Katiba, 1960-1964.”

Kwa Kiingereza kitabu hiki kinaitwa, “Building a Peaceful Nation: Julius Nyerere and the Establishment of Sovereignty in Tanzania, 1960-1964.” Kimechapishwa mwaka 2015 kupitia kampuni ya uchapaji ya “University of Rochester Press” ya huko “New York,” Marekani. Nimeambatanisha nakala tepe hapa chini.

Kwa mujibu wa Paul Bjerk (2015), Nyerere alipata misukosuko mikubwa miwili ndani ya siku saba kati ya tarehe 12 Januari 1964 na 19 Januari 1964.

Wakati
tarehe 12 Januari 1964 kulitokea Mapinduzi huko Zanzibar, tarehe 19 Januari 1964 kulitokea uasi wa jeshi upande wa Tanganyika katika miji mitatu ya Dar es Salaam, Nachingwea na Tabora.

Uasi wa jeshi la Tanganyika ulitokea Nyerere akiwa bado anaweka sawa diplomasia ya kimataifa ili kuwahakikishia Wamarekani kwamba Mapinduzi ya Zanzibar sio Mapinduzi ya Kikomunisti.

Paul Bjerk (2015) anasema kuwa uasi wa jeshi ulikuwa na sababu nyingi, lakini zilizotajwa wazi wazi tangu mwanzo ni “mgogoro kati ya mwajiri na waajiriwa uliowahusisha waajiriwa wenye silaha.”

Nyerere aliumizwa sana na uasi huu kwa sababu, “Tanganyika ilipata uhuru bila kumwaga damu lakini uasi huu umechukua uhai wa dazeni mbili za raia,” alisikika Nyerere akilalamika.

Uchunguzi uliofanywa baadaye kupitia Idara ya Usalama wa Taifa, iliyokuwa inaongozwa na Emil Mzena, ulithibitisha tatizo lilikuwa zaidi ya “mgogoro kati ya mwajiri na waajiriwa,” kwani njama za kuangusha serikali ya Nyerere zilithibitika.

Kwa hiyo, watu kadhaa waliotuhumiwa kuhusika walitiwa nguvuni, kuwekwa kizuizini, kuhojiwa, na baadhi kufungwa. Miongoni mwa watuhumiwa alikuwemo Bibi Titi Mohammed.

Uasi huu ulizimwa kwa msaada wa makomandoo wa jeshi la Uingereza, aliyekuwa mkoloni wetu wa awali. Uamuzi wa serikali ya Nyerere kuomba msaada kutoka UIngereza ulichukuliwa baada ya wiki moja akiwa anajishauri kuhusu njia bora ya kumaliza uasi huu bila kuomba msaada kwa mkoloni wetu wa zamani. Baada ya kupata taarifa kamili za mpango wa mapinduzi, Nyerere aliamua kuomba msaada wa jeshi kutoka Uingereza.

1609563430868.png

Halima Mdee

Lakini, kabla makomandoo wa Kiingereza hawajaanza kazi yao, Nyrere alitoa mhadhara uliokuwa na kichwa cha maneno “The Courage of Reconciliation and a Lockean theory of sovereignty for Africa: Is it based on contract or class conflict?

Yaani “Ujasiri wa Kufanya Maridhiano Kwa Mujibu wa Dhana ya Kujitawala kwa Kuzingatia Katiba Kama ilivyofundishwa na John Locke: Msingi wake ni mkataba au mapambano ya kitabaka?” (uk. 147)

Katika hotuba hii, Nyerere alitofautisha kati ya ya mamlaka ya kushauri (consultative power) yaliyokuwa mikononi mwa wakoloni wetu wa Zamani kutoka Uingereza na mamlaka ya kuamua (deliberative power) yaliyokuwa mikononi mwa serikali huru ya Tanganyika. Nyerere aliyafananisha “mamlaka ya kushauri” na nguo ya kuazima.

Nyerere anasema kuwa, kama wewe ni mwanamume na umeamua kuazima nguo kutoka kwa mtu, akakuwekea nguo hiyo kwenye begi, lakini baada ya kufika nyumbani wakati unajiandaa kuivaa ukakuta ni hijabu ya mwanamke, unaitupa na kuendelea na safari yako kivyako. (uk.148).

Kwa hiyo, Wajumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu la Chadema wanapaswa kufahamu kwamba, kuna tofauti kati ya mamlaka ya kushauri (consultative power), kwa upande mmoja, na mamlaka ya kuamua (deliberative power), kwa upande mwingine.

1609563803719.png

Nyerere, Bibi Titi, Sophia Kawawa na Maria Nyerere

Jaribio lolote la Chadema kuendelea kupuuzia tofauti hii ni sawa na kwenda nje ya katiba ya chama ili kuitafuta haki ya kujitawala na kuiweka mikononi mwa chama cha siasa (political party sovereignty). Kwa kigezo hiki, kambi ya Mbowe na kambi ya Mdee hawatofautiani sana.

Kwa sababu ya Mbowe kushindwa kutofautisha mambo haya mawili, au kwa sababu ameamua kutoyatofautisha, kwa muda sasa amegeuka Mwenyekiti kivuli (ceremonial chairperson), Mwenyekiti halisi akiwa ni “Mshauri wa Mbowe wa Mambo ya Kiroho,” ambaye hatambuliwi na Katiba ya Chadema. Jambo hili lisipokomeshwa litamaanisha kifo cha Chadema.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ambaye ni mwanasheria, anaelewa zaidi ninachokisema hapa kuliko bosi wake Freeman Mbowe. Lakini, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2020, nilimshangaa kuona kwamba naye ameanza kushindwa kuheshimu tofauti hii.

Niliona tayari kuna “Mshauri wa Kiroho wa Lissu,” akiwa anafanya baadhi ya mambo yanayofanywa na “Mshauri wa Kiroho wa Mbowe.” Tofauti pekee kati ya washauri hawa wawili ni kwamba Mshauri wa Kiroho wa Lissu” anaunga mkono Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni wakati “Mshauri wa Kiroho wa Mbowe” anapinga jambo hilo.

Kazi kubwa ya wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Chadema ni kumaliza mpasuko huu kati ya kina Mbowe, kina Lissu na kina Mdee, kwa kupiga marufuku washauri wa kiroho kuingilia maamuzi ya chama yanayofanyika kwa mujibu wa vikao rasmi.

Mheshimiwa Mbowe anasemaje kuhusu changamoto hii? Mheshimiwa Mdee anasemaje kuhusu jambo hili? Kaeni pamoja myajenge.
 

Attachments

  • Building a Peaceful Nation Julius Nyerere and the Establishment of Sovereignty in Tanzania, 19...pdf
    10 MB · Views: 24
Kuna hoja za kujibu usiposijibu uanonesha wewe ni mpuuzi sana
Umeandika upuuzi mwingi,hakuna kambi kama hizo CDM!Hao Covid 19 walishafukuzwa so sielewi kwanini unalazimisha kuwa ni kambi ndani ya CDM!
Uzandiki tu ndio umekujaa!
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom