Mgogoro wa viti maalum CHADEMA: Mbowe ana mkakati gani wa kuvunja kambi ya Askofu Bagonza, kambi ya Askofu Mwamakula, na kambi ya kina Mdee?

Nilianza kusoma bandiko lako baada ya kuona limejaa takataka sijamaliza kusoma huu upupu wako.I

Iko hizi, nyinyi Covid 19 mmefukuzwa uanachama na kamati kuu ya Chadema na siyo Askofu Bagonza.

Hoja za kimalaya malaya usituletee hapa JF kutupotezea muda, wananchi wana hasira na nyinyi mbwa kabisa.
Unasumbuliwa na ugonjwa wa selective amnesia?
Soma hoja yote kabla ya kupayuka.
Hasumbuliwi na ugonjwa wowote,
Mama Amon na Covid 19 Wenzio,naona hamlali usingizi,
Chama kimeshawafukuza na mmebahatika kuwa wabunge wa viti maalumu ambovyo amepewa Ndugai na katiba yao,mbona unawashwa,waache chadema na shida zao,na ninyi nendeni mliko unga juhudi.
 
Labda swali moja la msingi kuhusu kufukuzwa kwa COVID-19, jee ni sababu Chadema haitaki kupeleka wabunge viti maalum bungeni au kujipeleka kwao hakukufuata taratibu za chama kukiambatana na kugushi nyaraka?
Maana nijuavyo Mimi suala la wabunge viti maalum kuingia bungeni lilikuwa bado liko mezani na linajadilika lakini orodha iliyopo kwa Spika ni ya kugushi na haramu
Sema orodha iliyoko NEC.

Ikishafika kwa Spika inakuwa ni halali bwashee!
 
View attachment 1667156
Askofu Bagonza

Jana mchana, mtandao wa Jamiiforums ulitutaarifu kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ataongea na umma wa Watanzania. Mpaka sasa hajasikika. Wakati tunasubiri hotuba yake, napenda kumkumbusha kuja na jawabu kwa swali lifuatalo: Mbowe anao mkakati gani wa kuvunja kambi ya Askofu Bagonza, kambi ya Askofu Mwamakula, na kambi ya kina Mdee? Kusudi aweze kuelewa kwa nini nimeuliza swali hili, namwalika kusoma kwa umakini hoja ifuatayo:

Ndani ya Kamati Kuu ya Chadema kuna kambi kuu tatu. Kambi ya kwanza inaongozwa na Mshauri wa Kiroho wa Mbowe, Dr. Benson Bagonza, anayepinga hoja inayotaka Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni. Kambi ya pili inaongozwa na Mshauri wa Kiroho wa Lissu, Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula, anayekubali hoja inayotaka Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni. Na Kambi ya tatu inaongozwa na Halima Mdee, anayekubali hoja inayotaka Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni.

Kwa upande mmoja, mpasuko huu unatokana na ukweli kwamba Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ameshindwa kutofautisha kati ya mamlaka ya kushauri (consultative power) na mamlaka ya kuamua (deliberative power). Na kwa upande mwingine, mpasuko huu unatokana na ukweli kwamba Mbowe ameshindwa kutofautisha kati ya vikao rasmi (formal meetings) na vikao visivyo rasmi (informal meetings).

Kwa mujibu wa aina za viongozi wa chama zilizotajwa katika ibara ya 6.2.3 ya Katiba na idadi yake iliyotajwa kwa kila kikao katika kila ngazi, washauri wa kiroho wa viongozi sio sehemu ya viongozi wa chama.

Aidha, kwa mujibu wa aina za vikao zilizotajwa katika ibara ya 6.2.1 ya Katiba na idadi yake iliyotajwa kwa kila ngazi, washauri wa kiroho wa viongozi sio wajumbe wa kikao chochote halali katika Chadema. Hata hivyo, mawazo yao yanayumbisha vikao rasmi vya chama mpaka kuzalisha mipasuko iliyotajwa.

Kambi ya kina Mdee wanapinga jambo hili. Kwa mfano, “uteuzi wa awali” wagombea ubunge viti maalum unafanywa na kuratibiwa kwa mujibu wa Mwongozo wa Bawacha ibara za 7.4.4(h), 7.6.3(h), na 7.7.4(h), na hatimaye Kamati Kuu “kuthibitisha” uteuzi huu kupitia kura ya wengi kwa mujibu wa ibara ya 7.7.16(q).

Uthibitisho huo ndio hutafsiriwa kama kibali kwa Katibu Mkuu kuwasilisha majina kwenye Tume. Ndani ya kikao kimoja cha Kamati Kuu kura ya wengi ilipigwa na “kuthibitisha” uteuzi lakini Mwenyekiti akapiga “kura ya veto” wakati kikatiba hana Mwenyekiti mamlaka hayo. Mbowe anasikiliza zaidi Mshauri wake wa Kiroho kuliko maamuzi ya vikao vya Kamati Kuu. Hasa, huu ndio msingi wa mvutano kati ya kina Mdee, kina Lissu na kina Mbowe. Vikao visivyo rasmi vinafuta vikao rasmi.
View attachment 1667133
Askofu Mwamakula

Kwa ufupi, mazingira ya ugomvi unaoendelea sasa kati ya kambi ya kina Mbowe, kwa upande mmoja, na kambi ya kina Mdee, kwa upande mwingine, yanafanana sana na ugomvi uliotokea kati ya kambi ya kina Nyerere na kambi ya kina Bibi Titi Mohamed mwaka 1964.

Paul Bjerk (2015) amesimulia vizuri ugomvi ulitokea kati ya Nyerere na kina Bibi Titi Mohamed. Simulizi hiyo imo katika kitabu chake kiitwacho, “Ujenzi wa Jamii ya Amani: Julius Nyerere Katika Kusimika Mizizi ya Tanzania kama Taifa linalojitawala kwa mujibu wa Katiba, 1960-1964.”

Kwa Kiingereza kitabu hiki kinaitwa, “Building a Peaceful Nation: Julius Nyerere and the Establishment of Sovereignty in Tanzania, 1960-1964.” Kimechapishwa mwaka 2015 kupitia kampuni ya uchapaji ya “University of Rochester Press” ya huko “New York,” Marekani. Nimeambatanisha nakala tepe hapa chini.

Kwa mujibu wa Paul Bjerk (2015), Nyerere alipata misukosuko mikubwa miwili ndani ya siku saba kati ya tarehe 12 Januari 1964 na 19 Januari 1964.

Wakati
tarehe 12 Januari 1964 kulitokea Mapinduzi huko Zanzibar, tarehe 19 Januari 1964 kulitokea uasi wa jeshi upande wa Tanganyika katika miji mitatu ya Dar es Salaam, Nachingwea na Tabora.

Uasi wa jeshi la Tanganyika ulitokea Nyerere akiwa bado anaweka sawa diplomasia ya kimataifa ili kuwahakikishia Wamarekani kwamba Mapinduzi ya Zanzibar sio Mapinduzi ya Kikomunisti.

Paul Bjerk (2015) anasema kuwa uasi wa jeshi ulikuwa na sababu nyingi, lakini zilizotajwa wazi wazi tangu mwanzo ni “mgogoro kati ya mwajiri na waajiriwa uliowahusisha waajiriwa wenye silaha.”

Nyerere aliumizwa sana na uasi huu kwa sababu, “Tanganyika ilipata uhuru bila kumwaga damu lakini uasi huu umechukua uhai wa dazeni mbili za raia,” alisikika Nyerere akilalamika.

Uchunguzi uliofanywa baadaye kupitia Idara ya Usalama wa Taifa, iliyokuwa inaongozwa na Emil Mzena, ulithibitisha tatizo lilikuwa zaidi ya “mgogoro kati ya mwajiri na waajiriwa,” kwani njama za kuangusha serikali ya Nyerere zilithibitika.

Kwa hiyo, watu kadhaa waliotuhumiwa kuhusika walitiwa nguvuni, kuwekwa kizuizini, kuhojiwa, na baadhi kufungwa. Miongoni mwa watuhumiwa alikuwemo Bibi Titi Mohammed.

Uasi huu ulizimwa kwa msaada wa makomandoo wa jeshi la Uingereza, aliyekuwa mkoloni wetu wa awali. Uamuzi wa serikali ya Nyerere kuomba msaada kutoka UIngereza ulichukuliwa baada ya wiki moja akiwa anajishauri kuhusu njia bora ya kumaliza uasi huu bila kuomba msaada kwa mkoloni wetu wa zamani. Baada ya kupata taarifa kamili za mpango wa mapinduzi, Nyerere aliamua kuomba msaada wa jeshi kutoka Uingereza.

View attachment 1667159
Halima Mdee

Lakini, kabla makomandoo wa Kiingereza hawajaanza kazi yao, Nyrere alitoa mhadhara uliokuwa na kichwa cha maneno “The Courage of Reconciliation and a Lockean theory of sovereignty for Africa: Is the basis contract or class conflict?

Yaani “Ujasiri wa Kufanya Maridhiano Kwa Mujibu wa Dhana ya Kujitawala kwa Kuzingatia Katiba Kama ilivyofundishwa na John Locke: Msingi wake ni mkataba au mapambano ya kitabaka?” (uk. 147)

Katika hotuba hii, Nyerere alitofautisha kati ya ya mamlaka ya kushauri (consultative power) yaliyokuwa mikononi mwa wakoloni wetu wa Zamani kutoka Uingereza na mamlaka ya kuamua (deliberative power) yaliyokuwa mikononi mwa serikali huru ya Tanganyika. Nyerere aliyafananisha “mamlaka ya kushauri” na nguo ya kuazima.

Nyerere anasema kuwa, kama wewe ni mwanamume na umeamua kuazima nguo kutoka kwa mtu, akakuwekea nguo hiyo kwenye begi, lakini baada ya kufika nyumbani wakati unajiandaa kuivaa ukakuta ni hijabu ya mwanamke, unaitupa na kuendelea na safari yako kivyako. (uk.148).

Kwa hiyo, Wajumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu la Chadema wanapaswa kufahamu kwamba, kuna tofauti kati ya mamlaka ya kushauri (consultative power), kwa upande mmoja, na mamlaka ya kuamua (deliberative power), kwa upande mwingine.

Nyerere, Bibi Titi, Sophia Kawawa na Maria Nyerere

Jaribio lolote la Chadema kuendelea kupuuzia tofauti hii ni sawa na kuitafuta haki ya kujitawala iliyoko mikononi mwa chama cha siasa (political party sovereignty) kutoka nje ya katiba ya chama.

Kwa sababu ya Mbowe kushindwa kutofautisha mambo haya mawili, au kwa sababu ameamua kutoyatofautisha, kwa muda sasa amegeuka Mwenyekiti kivuli (ceremonial chairperson), Mwenyekiti halisi akiwa ni “Mshauri wa Mbowe wa Mambo ya Kiroho,” ambaye hatambuliwi na Katiba ya Chadema. Jambo hili lisipokomeshwa litamaanisha kifo cha Chadema.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ambaye ni mwanasheria, anaelewa zaidi ninachokisema hapa kuliko bosi wake Freeman Mbowe. Lakini, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2020, nilimshangaa kuona kwamba naye ameanza kushindwa kuheshimu tofauti hii.

Niliona tayari kuna “Mshauri wa Kiroho wa Lissu,” akiwa anafanya baadhi ya mambo yanayofanywa na “Mshauri wa Kiroho wa Mbowe.” Tofauti pekee kati ya washauri hawa wawili ni kwamba Mshauri wa Kiroho wa Lissu” anaunga mkono Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni wakati “Mshauri wa Kiroho wa Mbowe” anapinga jambo hilo.

Kazi kubwa ya wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Chadema ni kumaliza mpasuko huu kati ya kina Mbowe, kina Lissu na kina Mdee, kwa kupiga marufuku washauri wa kiroho kuingilia maamuzi ya chama yanayofanyika kwa mujibu wa vikao rasmi. Mheshimiwa Mbowe anasemaje kuhusu changamoto hii?
Ushauri huu si ungemwandikia Mbowe moja kwa moja? Au ungempigia simu. Hivi kweli unatarajia aje akujibu humu JF?

Inaelekea Mbowe anawanyima sana raha.

Amandla...
 
Style za CCM sio za Chadema. Funga bakuli lako!
Narudia tena, Freeman Mbowe, Halima James Mdee, Lucy Owenya na Grace Kiwelu Ndesamburo hakuna mwenye ubavu wa kuwafukuza hapo Chadema!

Wewe ni wakuja tu hapo Ufipa huelewi chochote!
 
Nilipaona tu mtoa Mada (mwandishi) Sikuoni haja ya kusoma. 🚾
Tafuteni chama.
 
Narudia tena, Freeman Mbowe, Halima James Mdee, Lucy Owenya na Grace Kiwelu Ndesamburo hakuna mwenye ubavu wa kuwafukuza hapo Chadema!

Wewe ni wakuja tu hapo Ufipa huelewi chochote!
Nina kila haki ya kukupuuza maana unanishambulia kama unanijua.
Ila kwa taarifa yako 1996 wakati nachukua kadi ya Chadema (hilo sionei aibu kulisema) sijui ulikuwa wapi kijana.
Na mwaka 1997 wakati Chadema ofisi kuu zipo Kisutu na inafanya mkutano mkuu na kumchagua Marehemu Bob Makani kama Mwenyekiti, na Kabouru kama Katibu mkuu pale Starlight Hotel nilibahatika kuwa mjumbe hivyo sio wakuja ndani ya chama kama unavyofikiri kijana!
Hivyo tujadili kwa kuheshimiana
 
Huu ni upiga ramli tu na kuunga unga maneno, hoja ya kwanza ya msingi ni ile ile ya “Mdee kama kiongozi wa wing mojawapo alipaswa kufanya alichofanya, na je italeta maana wasamehewe na kuendelea na huo “ubunge wa kujipeleka” au wasamehewe na kuvuliwa? Story nyingi na reference za similar case za enzi na enZi wala hazihitajiki!
 
Nina kila haki ya kukupuuza maana unanishambulia kama unanijua.
Ila kwa taarifa yako 1996 wakati nachukua kadi ya Chadema (hilo sionei aibu kulisema) sijui ulikuwa wapi kijana.
Na mwaka 1997 wakati Chadema ofisi kuu zipo Kisutu na inafanya mkutano mkuu na kumchagua Marehemu Bob Makani kama Mwenyekiti, na Kabouru kama Katibu mkuu pale Starlight Hotel nilibahatika kuwa mjumbe hivyo sio wakuja ndani ya chama kama unavyofikiri kijana!
Hivyo tujadili kwa kuheshimiana
Hahahaaaa ......mimi kadi yangu ya Chadema nilichukua mwaka 1993 hapo hapo Kisutu majamatini kwenye ofisi za mzee Ndesamburo na nilikabidhiwa na mzee Shanga rip.

So ninapokuambia hakuna wa kumfukuza Halima hapo Ufipa namaanisha, msione vyaelea vimeundwa!
 
Hoja gani hapo mkuu zaidi ya kuokoteza vijimaneno

Kuna hoja mbili.

Mosi, kumfanya mshauri wa kiroho kuwa kiongozi wa chama kinyume cha katiba.

Pili, kukweza maamuzi ya vikao visivyo rasmi juu ya maamuzi ya vikao rasmi.
 
Mleta hoja ni Kati ya timu covid-19 waliotimuliwa hivyo wanajaribu kutengeneza mpambano kwa kuwapiganisha makundi manne at atime ili kuivuruga cdm!
Mama D, nasikitika kukuambia kuwa hakuna Jambo ulilowahi kulianzisha likawa na matokeo chanya badala Yake huishia kujiaibisha tu! Hili nalo litakumwaga shuzi! Acha kutumika na kina polepole!
 
Back
Top Bottom