Mgogoro wa viti maalum CHADEMA: Mbowe ana mkakati gani wa kuvunja kambi ya Askofu Bagonza, kambi ya Askofu Mwamakula, na kambi ya kina Mdee?

Jamani serikali yetu inamambo mengi mazuri inayoshunghulika nayo tena yenye faida kubwa kwa taiga letu, lakini cha ajabu haya mazuri yote huyaoni hata ukatuletea huku mtandaoni, yaani wewe kazi yako nikutuletea umbea wa chadematu! Inatosha sasa chdm waachie wenye kawaambie waliokutuma cove 19 hawaitajiki tena hata huku kwetu hatuwataki
Kwa hiyo wewe unaunga mkono yupi:

covid19?

coovid19+?

au CCM na serikali yake?

Sijakuelewa ujue....
 
Kilichofanyika sasa ni completely different, hoja yako ingekuwa na mashiko kama hilo pia wangeliapply kwenye uchaguzi wa SM. Mbona kwenye uchaguzi ule walisusia wote, ama huu kwakuwa kina Mdee wana maslahi yao binafsi ndio wanaleta utetezi wa kitapeli?
Ninachoongelea mie ni PRINCIPLED ARGMENT.
Tunasusa kwa sababu ya ground zipi?
Hoja lazima ijengwe.
Siasa za nchi hazipaswi kufanyika kwa njia ya hisia, na mihemuko.
Needed: A PRINCIPLED ARGUMENT.
 
Ni mkubwa aisee.
Usipozibwa ni kaburi la chadema
Kwa vile umekamia kutengeneza "neno" kwenye kadhia hii ya Halima Mdee & co. nakuongezea hekima moja muhimu ambayo ni budi usiiweke kando. Uizingatie daima. Nayo ni: CHADEMA si chama cha kawaida cha siasa cha upinzani. (Not your conventional opposition party). Bali kimefikia hatua ya kuwa OPPOSITION MOVEMENT ya taifa. CHADEMA inategemewa na Watanzania toka nyanja zote za taifa hili. Hata makada wa chama tawala (CCM) kibao na viongozi kadhaa serikalini wanaitumainia CHADEMA kama kisemeo pekee credible cha DISSENT nchini. Wakizidiwa, huwa wanaitumia. How? Bila shaka unajua vizuri sana.

Hivyo, leo hii, hata Mbowe akihamia CCM kuunga mkono juhudi, CHADEMA itaendelea kuwepo. Kitu pekee kinachoweza kuua PRESENCE ya CHADEMA nchini ni amri ya kuifuta na nguvu za dola kutumika kufagilia mbali alama zake zote nchini. Hapo ni roho yake pekee ndiyo itabakia ndani ya watu.

Kinachowaharibia sana akina Halima na wenzake ni ile VERY OVERT SUPPORT wanayopewa na nguzo za utawala huu: Spika, Katibu Mkuu wa CCM, Msemaji wa CCM, makada wa CCM, DPP, n.k. Halafu wanaonyeshwa (portrayed) kwamba wako kwenye mapambano dhidi ya "udikteta" wa Mbowe ndani ya CHADEMA. That's preposterous! Hasa ukizingatia hali ya kisiasa inayoendelea na yaliyotokea kwenye uchaguzi mkuu ambayo Halima ni shahidi mkubwa.

CCM pia si chama tawala cha siasa cha kawaida. Ni chama dola (State Party). Hakihitaji mchakato wowote wa kidemokrasia kufanikisha malengo yake. Kinaweza hata kuwaweka Bungeni akina Halima kama wabunge wa viti maalum wa CHADEMA bila ya kubugudhiwa na yeyote.

Nakutakia kila la heri katika mradi huu wa kutengeneza "neno" kwa ajili ya kina Halima. It's intellectually tantalising. Ikishindikana, achaneni na any pretence na tumieni gia ya State Party moja kwa moja. Hiyo haina kushindwa. All the best.
 
Ninachoongelea mie ni PRINCIPLED ARGMENT.
Tunasusa kwa sababu ya ground zipi?
Hoja lazima ijengwe.
Siasa za nchi hazipaswi kufanyika kwa njia ya hisia, na mihemuko.
Needed: A PRINCIPLED ARGUMENT.

Hayo maneno ya principle sijui grounds unayatumia ili kutaka kuonyesha unachambua kisomi. Huyo Mdee kapiga picha kibao yuko na kura za kwenye mabeg, sasa hapo unataka grounds gani? Hivi ww mama Amon unaona unajadili na watoto wadogo? Kabla ya uchaguzi tuliona hujuma za wazi bin dhahiri dhidi ya wagombea wa upinzani, na wakatolewa kwa mizengwe, na waliofanikiwa kupita kilichofanyika vituoni pia tumeona. Kwakuwa sasa hivi mnataka kuwa wabunge kwa kuogopa ugumu wa maisha, mnaleta vijimaneno vya kiingereza sijui principle, grounds nk. Nendeni mkajiajiri acheni kutaka urahisi wa maisha kwa lugha za kitapeli.
 
Huu ni umbea kabisa! Kufikiria kuwa Bagonza anamsupport zaidi mawazo ya Mbowe na siyo mawazo ya Lissu ni ujinga wa hali ya juu! Soma alama za nyakati! Uchochezi wako hauna tija!
 
Hayo maneno ya principle sijui grounds unayatumia ili kutaka kuonyesha unachambua kisomi. Huyo Mdee kapiga picha kibao yuko na kura za kwenye mabeg, sasa hapo unataka grounds gani? Hivi ww mama Amon unaona unajadili na watoto wadogo? Kabla ya uchaguzi tuliona hujuma za wazi bin dhahiri dhidi ya wagombea wa upinzani, na wakatolewa kwa mizengwe, na waliofanikiwa kupita kilichofanyika vituoni pia tumeona. Kwakuwa sasa hivi mnataka kuwa wabunge kwa kuogopa ugumu wa maisha, mnaleta vijimaneno vya kiingereza sijui principle, grounds nk. Nendeni mkajiajiri acheni kutaka urahisi wa maisha kwa lugha za kitapeli.
'Ukitaka kuwa masikini nchi hii, danganywa kwenda kulima. Utalima kwa gharama zako lakini wakati wa kuuza utapangiwa bei na anayeishi mjini"
 
Huu ni umbea kabisa! Kufikiria kuwa Bagonza anamsupport zaidi mawazo ya Mbowe na siyo mawazo ya Lissu ni ujinga wa hali ya juu! Soma alama za nyakati! Uchochezi wako hauna tija!
Hapana. Ni ukweli, ukweli wote na ukweli pekee.
 
Ndio ameshafukuzwa uanachama, hata Membe alikuwa na tambo zaidi ya Haluma Mdee lakini amefukuzwa ccm na si mwanachama wa ccm mpaka dakika hii sawa na hao Covid 19 si wanachama wa Chadema mpaka dakika hii.

Chadema alishindwa Zitto ndio sembuse hawa?
Kwani umiliki wa Chadema unafanana na wa CCM?

Huyo Zitto aliletwa Chadema na Freeman Mbowe lakini Halima James Mdee yuko chadema kulinda hisa " zao"
 
View attachment 1667156
Askofu Bagonza

Jana mchana, mtandao wa Jamiiforums ulitutaarifu kuwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ataongea na umma wa Watanzania. Mpaka sasa hajasikika. Wakati tunasubiri hotuba yake, napenda kumkumbusha kuja na jawabu kwa swali lifuatalo: Mbowe anao mkakati gani wa kuvunja kambi ya Askofu Bagonza, kambi ya Askofu Mwamakula, na kambi ya kina Mdee? Kusudi aweze kuelewa kwa nini nimeuliza swali hili, namwalika kusoma kwa umakini hoja ifuatayo:

Ndani ya Kamati Kuu ya Chadema kuna kambi kuu tatu. Kambi ya kwanza inaongozwa na Mshauri wa Kiroho wa Mbowe, Dr. Benson Bagonza, anayepinga hoja inayotaka Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni. Kambi ya pili inaongozwa na Mshauri wa Kiroho wa Lissu, Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula, anayekubali hoja inayotaka Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni. Na Kambi ya tatu inaongozwa na Halima Mdee, anayekubali hoja inayotaka Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni.

Kwa upande mmoja, mpasuko huu unatokana na ukweli kwamba Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ameshindwa kutofautisha kati yamamlaka ya kuamua (deliberative power) yaliyo mikononi mwa watu ambao ni wajumbe halali wa vikao halali na mamlaka na ya kushauri (consultative power) yaliyo mikononi mwa watu ambao sio wajumbe wa vikao halali.

Na kwa upande mwingine, mpasuko huu unatokana na ukweli kwamba Mbowe ameshindwa kutofautisha kati ya vikao rasmi kikatiba (formal meetings) na vikao visivyo rasmi kikatiba (informal meetings).

Kwa mujibu wa aina za viongozi wa chama zilizotajwa katika ibara ya 6.2.3 ya Katiba na idadi yake iliyotajwa kwa kila kikao katika kila ngazi, washauri wa kiroho wa viongozi sio sehemu ya viongozi wa chama.

Aidha, kwa mujibu wa aina za vikao zilizotajwa katika ibara ya 6.2.1 ya Katiba na idadi yake iliyotajwa kwa kila ngazi, washauri wa kiroho wa viongozi sio wajumbe wa kikao chochote halali katika Chadema. Hata hivyo, mawazo yao yanayumbisha vikao rasmi vya chama mpaka kuzalisha mipasuko iliyotajwa.

Na kwa kweli, kutoa taarifa za chama kwa washauri wa kiroho ni kuvujisha siri za chama, kinyume cha kanuni ya 3(c)(i) ya Mwongozo wa Kamati za Maadili ya Chama.

Kambi ya kina Mdee wanapinga jambo hili. Kwa mfano, “uteuzi wa awali” wagombea ubunge viti maalum unafanywa na kuratibiwa kwa mujibu wa Mwongozo wa Bawacha (toleo la 2019) ibara za 7.4.4(h), 7.6.3(h), na 7.7.4(h), na hatimaye Kamati Kuu “kuthibitisha” uteuzi huu kupitia kura ya wengi kwa mujibu wa ibara ya 7.7.16(q) ya Katiba (toleo la 2019).

Uthibitisho huo ndio hutafsiriwa kama kibali kwa Katibu Mkuu kuwasilisha majina kwenye Tume. Ndani ya kikao kimoja cha Kamati Kuu kura ya wengi ilipigwa na “kuthibitisha” uteuzi lakini Mwenyekiti akapiga “kura ya veto” wakati kikatiba Mwenyekiti hana mamlaka hayo.

Mbowe anasikiliza zaidi Mshauri wake wa Kiroho kuliko maamuzi ya vikao vya Kamati Kuu. Hasa, huu ndio msingi wa mvutano kati ya kina Mdee, kina Lissu na kina Mbowe. Vikao visivyo rasmi vinafuta vikao rasmi.

View attachment 1667133

Askofu Mwamakula

Kwa ufupi, mazingira ya ugomvi unaoendelea sasa kati ya kambi ya kina Mbowe, kwa upande mmoja, na kambi ya kina Mdee, kwa upande mwingine, yanafanana sana na ugomvi uliotokea kati ya kambi ya kina Nyerere na kambi ya kina Bibi Titi Mohamed mwaka 1964.

Paul Bjerk (2015) amesimulia vizuri ugomvi ulitokea kati ya Nyerere na kina Bibi Titi Mohamed. Simulizi hiyo imo katika kitabu chake kiitwacho, “Ujenzi wa Jamii ya Amani: Julius Nyerere Katika Kusimika Mizizi ya Tanzania kama Taifa linalojitawala kwa mujibu wa Katiba, 1960-1964.”

Kwa Kiingereza kitabu hiki kinaitwa, “Building a Peaceful Nation: Julius Nyerere and the Establishment of Sovereignty in Tanzania, 1960-1964.” Kimechapishwa mwaka 2015 kupitia kampuni ya uchapaji ya “University of Rochester Press” ya huko “New York,” Marekani. Nimeambatanisha nakala tepe hapa chini.

Kwa mujibu wa Paul Bjerk (2015), Nyerere alipata misukosuko mikubwa miwili ndani ya siku saba kati ya tarehe 12 Januari 1964 na 19 Januari 1964.

Wakati
tarehe 12 Januari 1964 kulitokea Mapinduzi huko Zanzibar, tarehe 19 Januari 1964 kulitokea uasi wa jeshi upande wa Tanganyika katika miji mitatu ya Dar es Salaam, Nachingwea na Tabora.

Uasi wa jeshi la Tanganyika ulitokea Nyerere akiwa bado anaweka sawa diplomasia ya kimataifa ili kuwahakikishia Wamarekani kwamba Mapinduzi ya Zanzibar sio Mapinduzi ya Kikomunisti.

Paul Bjerk (2015) anasema kuwa uasi wa jeshi ulikuwa na sababu nyingi, lakini zilizotajwa wazi wazi tangu mwanzo ni “mgogoro kati ya mwajiri na waajiriwa uliowahusisha waajiriwa wenye silaha.”

Nyerere aliumizwa sana na uasi huu kwa sababu, “Tanganyika ilipata uhuru bila kumwaga damu lakini uasi huu umechukua uhai wa dazeni mbili za raia,” alisikika Nyerere akilalamika.

Uchunguzi uliofanywa baadaye kupitia Idara ya Usalama wa Taifa, iliyokuwa inaongozwa na Emil Mzena, ulithibitisha tatizo lilikuwa zaidi ya “mgogoro kati ya mwajiri na waajiriwa,” kwani njama za kuangusha serikali ya Nyerere zilithibitika.

Kwa hiyo, watu kadhaa waliotuhumiwa kuhusika walitiwa nguvuni, kuwekwa kizuizini, kuhojiwa, na baadhi kufungwa. Miongoni mwa watuhumiwa alikuwemo Bibi Titi Mohammed.

Uasi huu ulizimwa kwa msaada wa makomandoo wa jeshi la Uingereza, aliyekuwa mkoloni wetu wa awali. Uamuzi wa serikali ya Nyerere kuomba msaada kutoka UIngereza ulichukuliwa baada ya wiki moja akiwa anajishauri kuhusu njia bora ya kumaliza uasi huu bila kuomba msaada kwa mkoloni wetu wa zamani. Baada ya kupata taarifa kamili za mpango wa mapinduzi, Nyerere aliamua kuomba msaada wa jeshi kutoka Uingereza.

View attachment 1667159

Halima Mdee

Lakini, kabla makomandoo wa Kiingereza hawajaanza kazi yao, Nyrere alitoa mhadhara uliokuwa na kichwa cha maneno “The Courage of Reconciliation and a Lockean theory of sovereignty for Africa: Is it based on contract or class conflict?

Yaani “Ujasiri wa Kufanya Maridhiano Kwa Mujibu wa Dhana ya Kujitawala kwa Kuzingatia Katiba Kama ilivyofundishwa na John Locke: Msingi wake ni mkataba au mapambano ya kitabaka?” (uk. 147)

Katika hotuba hii, Nyerere alitofautisha kati ya ya mamlaka ya kushauri (consultative power) yaliyokuwa mikononi mwa wakoloni wetu wa Zamani kutoka Uingereza na mamlaka ya kuamua (deliberative power) yaliyokuwa mikononi mwa serikali huru ya Tanganyika. Nyerere aliyafananisha “mamlaka ya kushauri” na nguo ya kuazima.

Nyerere anasema kuwa, kama wewe ni mwanamume na umeamua kuazima nguo kutoka kwa mtu, akakuwekea nguo hiyo kwenye begi, lakini baada ya kufika nyumbani wakati unajiandaa kuivaa ukakuta ni hijabu ya mwanamke, unaitupa na kuendelea na safari yako kivyako. (uk.148).

Kwa hiyo, Wajumbe wa Kamati Kuu na Baraza Kuu la Chadema wanapaswa kufahamu kwamba, kuna tofauti kati ya mamlaka ya kushauri (consultative power), kwa upande mmoja, na mamlaka ya kuamua (deliberative power), kwa upande mwingine.

View attachment 1667162
Nyerere, Bibi Titi, Sophia Kawawa na Maria Nyerere

Jaribio lolote la Chadema kuendelea kupuuzia tofauti hii ni sawa na kwenda nje ya katiba ya chama ili kuitafuta haki ya kujitawala na kuiweka mikononi mwa chama cha siasa (political party sovereignty). Kwa kigezo hiki, kambi ya Mbowe na kambi ya Mdee hawatofautiani sana.

Kwa sababu ya Mbowe kushindwa kutofautisha mambo haya mawili, au kwa sababu ameamua kutoyatofautisha, kwa muda sasa amegeuka Mwenyekiti kivuli (ceremonial chairperson), Mwenyekiti halisi akiwa ni “Mshauri wa Mbowe wa Mambo ya Kiroho,” ambaye hatambuliwi na Katiba ya Chadema. Jambo hili lisipokomeshwa litamaanisha kifo cha Chadema.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu, ambaye ni mwanasheria, anaelewa zaidi ninachokisema hapa kuliko bosi wake Freeman Mbowe. Lakini, katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu wa 2020, nilimshangaa kuona kwamba naye ameanza kushindwa kuheshimu tofauti hii.

Niliona tayari kuna “Mshauri wa Kiroho wa Lissu,” akiwa anafanya baadhi ya mambo yanayofanywa na “Mshauri wa Kiroho wa Mbowe.” Tofauti pekee kati ya washauri hawa wawili ni kwamba Mshauri wa Kiroho wa Lissu” anaunga mkono Chadema kupeleka wabunge wa viti maalum bungeni wakati “Mshauri wa Kiroho wa Mbowe” anapinga jambo hilo.

Kazi kubwa ya wajumbe wa Baraza Kuu la Taifa la Chadema ni kumaliza mpasuko huu kati ya kina Mbowe, kina Lissu na kina Mdee, kwa kupiga marufuku washauri wa kiroho kuingilia maamuzi ya chama yanayofanyika kwa mujibu wa vikao rasmi.

Mheshimiwa Mbowe anasemaje kuhusu changamoto hii? Mheshimiwa Mdee anasemaje kuhusu jambo hili? Kaeni pamoja myajenge.
Mama Amon Mumeo hakupakati inavyostahili
 
Hao Covid 19 walishafukuzwa so sielewi kwanini unalazimisha kuwa ni kambi ndani ya CHADEMA!
We mwehu kweli wewe, tangu lini mtu aliyefukuzwa anapewa nafasi ya kukata rufaa kwenye vikao halali vya chama? Vinginevyo basi kikao kilichowafukuza hakikuwa na hayo mamlaka! We unadhani Membe ana kikao chochote cha kukata rufaa? Option pekee aliyonayo ni kuomba msamaha!
 
bashiru alisema anahitaji dakika tano tu kuisambaratisha chadema na act vipande vipande, wameanza kupelekana mahakamani saaahv naona bado hawajamalizana
 
We mwehu kweli wewe, tangu lini mtu aliyefukuzwa anapewa nafasi ya kukata rufaa kwenye vikao halali vya chama? Vinginevyo basi kikao kilichowafukuza hakikuwa na hayo mamlaka! We unadhani Membe ana kikao chochote cha kukata rufaa? Option pekee aliyonayo ni kuomba msamaha!
Mwehu mwenyewe!Hata mahakamani mtu akishahukumiwa,hata akikata rufaa bado hukumu itaendelea kusimama mpaka pale itakapokuwa tofauti!So status ya hao Covid 19 ni kwa sasa ni kuwa sio wanachama,full stop!
Kwa maana hiyo hata vikao vya chama hawashiriki na ofisi za chama hawaingii!Nafasi zao za uongozi chamani walishavuliwa!
 
Back
Top Bottom