Mgogoro wa vibanda stand ndogo jiji la Arusha ni kwa maslahi ya kundi lipi?

kunena

JF-Expert Member
Nov 29, 2016
506
717
Mtizamo wangu kama mwananchi wa kawaida juu ya mgogoro wa muda mrefu wa vibanda stand ndogo Arusha. Mgogoro huu ukiutazama katika mtizamo wa kutokua na maslahi yoyote (neutral view) unaweza kuyaona makundi makuu manne yenye maslahi;

Kundi la kwanza: SerikaliSerikali katika Jiji la Arusha imechoshwa mno na mgogoro huu kwani umekua unaigharimu sana halmashauri ya Jiji la Arusha kwa maana ya gharama ya kesi mbalimbali zinazofunguliwa na wadau mbalimbali dhidi yake, vilevile imekua inakosa mapato stahiki kutokana na kuvutana na wapangaji na wawekezaji katika vibanda hivyo. Na lengo kuu la jumla ni katika kutafuta suluhu ya kudumu ya mgogoro huu ambao kwa siku za mbeleni unaweza kuhatarisha usalama jijini hapo na ikizingatiwa kuwa agenda kubwa ya serikali ya wilaya hiyo ni kuitunza Amani iliyoanza kustawi katika jiji hilo la kitalii Tanzania. Hivyo basi maamuzi yoyote, msimamo wowote utakaofanywa na serikali juu ya mgogoro huu utaegemea zaidi katika nia zilizotajwa hapo juu.

Kundi la pili: Madiwani na mbunge, kundi hili limegawanyika sehemu tatu.

Mosi, Madiwani maslahi
Kundi hili limekua likichochea (catalyse) mgogoro huu usiishe kwani limekua lina agenda ya kuutumia mgogoro huu kujipatia fedha toka kwa wapangaji na wawekezaji/wajenzi kwa ahadi za kuwasaidia kuweza kumiliki vibanda hivyo(hili litategemea wamechukua fedha toka kwa nani), na hapo nyuma imewahi kusikika wakipita kwa wafanyabiashara wapangaji na kukusanya fedha kwa kuwaaminisha kuwa watawasaidaia kuinfluence maamuzi ya halmashauri ili wao ndiyo wamiliki vibanda hivyo kwa kuingia mikataba na halmashauri.

Pili, Madiwani wazalendo.
Kundi hili linaundwa na madiwani ambao siku zote agenda zao zimekua zinalenga kuibeba halmashauri kwa ujumla wake na wamekua wakimpa sana support sana Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Athumani Kihamia katika maamuzi mengi na kumpa ushauri wa namna ya kutekeleza majukumu yake kwa maendeleo ya wana Arusha.

Tatu, ni Mbunge wa jimbo la Arusha mjini bila kumuonea Mh Lema mgogoro huu haumpi maslahi yoyote ya kifedha na wala hajonaekana hata kufikiria kunufaika kwa mtindo huo, yeye kama mwanasiasa interest yake kubwa ni siasa. Kwa ufupi mgogoro huu anataka kuutumia kumpa political advantage na kama inavyofahamika mbinu za mbunge Lema kujijenga kisiasa ni kutumia migogoro mbalimbali na kuanzisha harakati ambazo mwishowe huleta machafuko. Toka ametoka mahabusu hakua na agenda yoyote ile ambayo inaweza kumpa kiki kama vijana wa mjini wanavyosema na ameona mgogoro huu ndio fursa pekee inayoweza kumrudisha kwenye ramani ya siasa.

Mahali pekee ambapo madiwani maslahi na mbunge wanaweza kuwa na interest za pamoja ni katika kumharibia mkurugenzi wa jiji la Arusha ambao kwao ni maadui wakubwa kwani toka amekuja wamekua na mivutano mingi binafsi kwani mkurugenzi huyo wanamlaumu sana kwa kuwakatia posho mbalimbali ambazo hapo nyuma walikua wanalipana visivyo halali ikiwa ni pamoja na nauli sh. 80,000 na simu sh. 100,000 kila mwezi achilia mbali posho yao ya udiwani.Na kubwa zaidi ni vita ya jumla ya kuwashambulia wateule wa Rais Dr. John Joseph Pombe Magufuli na kumkatisha tamaa kumfanya aone kuwa alikosea katika kufanya maamuzi.

Kundi la tatu:
Wapangaji wa vibanda husika.
Wengi wa wapangaji hawa waliletwa na wawekezaji/wajenzi kwa makubaliano yao wenyewe. Sasa kinachoonekana katika mgogoro huu ni madiwani maslahi kuamua kutumia wingi wao katika baraza la madiwani na kuinfluence halmashauri kuwapora wajenzi haki yao ya uwekezaji kwa maslahi yao binafsi kwani wameshanufaika sana na fedha wanazovuta kwa wafanyabiashara hao.

Kundi la mwisho ni Wawekezaji (wajenzi wa vibanda hivyo).Hawa ni wazee wa mji wa Arusha ambao waliingia makubaliano na halmshauri ya jiji wajenge vibanda katika maeneo hayo kwani kwa wakati huo halmashauri haikua na nguvu ya kujenga.
Kundi hili kilio chao kikubwa ni nini hatima yao baada ya wao kuporwa haki yao, kwani wengi wa wawekezaji hao ni wazee kwa sasa ambapo walitumia nguvu zao ujanani kujenga vibanda hivyo na leo wanaporwa nguvu zao na kwasasa hawana namna ingine ya kuishi zaidi ya kutegemea vibanda hivyo.

Hitimisho: Mgogoro huu si wa kuutatua kwa mihemko ya kisiasa kwani madhara yake ni makubwa sana, ni muhimu serikali ikiwezekana ngazi ya mkoa kuingilia kati na kuweka busara kwani kundi linaloonekana kukandamizwa ni wawekezaji waliojenga vibanda hivi. Serikali yoyote makini haiwezi kuppuza malalamiko ya msingi ya wananchi wake wanyonge. Vilevile ni muhimu serikali na viongozi wa juu wakajua ni mazingira gani Mkurugenzi wa jiji la Arusha anayapitia kufanya kazi na baraza la wapinzani ambao hukubaliani na mitizamo yao hakika itakua ni vita kuu na fitina ya hali ya juu.

Vile vile nitoe rai kwa baraza la madiwani kuacha kutumia wingi wao kutoa maamuzi ya kukomoa utawala na wateule wa Rais Magufuli ili waonekane hawana misimamo na hawafai, kwani maamuzi mengi wanayoyatoa ni kupingana na maelekezo ya serikali ili kuleta kigugumizi katika utekelezaji wake.

Mwisho; Nitoe tahadhari kwa madiwani maslahi ya kwamba serikali ipo macho na inajua kila kitu wanachokifanya na hata serikali ina masikio katika hayo magroup yao ya whatsapp na kujua mikakati yao. Siasa si kushindana na serikali na kua kinyume nayo kwenye kila kitu, uchaguzi ulikwisha sasa tuchape kazi kutekeleza ahadi zetu.
Pia tunasikia hawa madiwani wenye maslahi wakisema wamewasiliana na katibu mkuu TAMISEMI alete Mkurugenzi wake mmoja Jumanne au Jumatatu kuja kumchunguza Mkurugenzi wa jiji wanatamba mitaani kwa hilo wakisema kuwa TAMISEMI itarejesha vibanda hivyo kwa wapangaji waliotoa rushwa.Wanamtuhumu mkurugenzi huyo anashirikiana na DC na RC.

Mwananchi Mzalendo.
 
Fateni ushauri na maoni ya CAG vunja mikataba na madalali wa maduka fanyeni mikataba mipya na wafanyabiashara wa maduka na sio hao madalali.

Mrisho Gambo acha kupuuza ushauri wa CAG kwa nia ya kujipatia umaarufu wa kisiasa kwa kuwa-favor madalali wanaohodhi maduka ya stand Arusha.

Kwa mujibu wa report ya GAG hao madalali wanapata cha juu kwenye malipo ya mapango hayo pesa ambayo haikatwi kodi na TRA yaani hawana faida yoyote kwa halmashauri zaidi ya kuleta migogoro na wapangaji halali.

Kwa hiyo mleta mada rudi kamwambie Mrisho Mgambo akae pembeni madalali watolewe kwenye vyumba tunahitaji wapangaji halali ambao kodi yao halali itakatwa pia mapato na TRA as per CAG report, asitake kutumia hao madalali kama mtaji wa kisiasa kwa kujitia upofu.
 
Fateni ushauri na maoni ya CAG vunja mikataba na madalali wa maduka fanyeni mikataba mipya na wafanyabiashara wa maduka na sio hao madalali.

Mrisho Gambo acha kupuuza ushauri wa CAG kwa nia ya kujipatia umaarufu wa kisiasa kwa kuwa-favor madalali wanaohodhi maduka ya stand Arusha.

Kwa mujibu wa report ya GAG hao madalali wanapata cha juu kwenye malipo ya mapango hayo pesa ambayo haikatwi kodi na TRA yaani hawana faida yoyote kwa halmashauri zaidi ya kuleta migogoro na wapangaji halali.

Kwa hiyo mleta mada rudi kamwambie Mrisho Mgambo akae pembeni madalali watolewe kwenye vyumba tunahitaji wapangaji halali ambao kodi yao halali itakatwa pia mapato na TRA as per CAG report, asitake kutumia hao madalali kama mtaji wa kisiasa kwa kujitia upofu.

Yani we jamaa una kitu kinaitwa "Mrisho Gambo obsession syndrome" yani huwezi kujenga hoja au kujibu hoja bila kumtaja huyo jamaa.....sasa kwa mfano kwenye hili suala anaingiaje??...hili suala ni la mchakato wa kisheria na yeye hawezi tia pua yake hapo ataishia kua mtizamaji kama akienda mbali sana kushauri.....
 
Back
Top Bottom