Shebbydo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2015
- 1,174
- 1,937
Habari wanabodi,
Ni muda mrefu jambo hili limekuwa likinisumbua akilini, aidha ni mimi ndiye nisiyejua au kuna kufumbiwa macho jambo hili.
Nianze na kukumbushana kidogo mgogoro uliokuwepo kati ya shirika letu la umeme(TANESCO) na kampuni iliyoingia nayo mkataba wa kufua umeme wa megawati 100 ya IPTL wa miaka 20.
Mgogoro huo ulitokana na IPTL kukiuka mkataba ambao uliitaka kampuni hiyo kufunga mitambo 5 @1 megawati 20 za msukumo mdogo(Low speed), wao IPTL walifunga mitambo 10@1 megawati 10 za msukumo wa kati(Medium speed) hivyo kusababisha gharama za uendeshaji kuwa kubwa. Mbali na hivyo IPTL walikuwa wanakokotoa gharama za uwekezaji (Capacity charges) kwa mtaji wa wanahisa (Equity Ownership) wa USD 38.16 mil. waliokuwa wamekopa kutoka kwa Umoja wa mabenki wa Malaysia(Consortium of Malaysian Banks), na kusababisha gharama za uwekezaji kufikia 2.6 mil. USD kwa mwezi badala ya kukokotoa gharama hizo kwa kutumia mtaji uliotambuliwa na na BRELA (Paid up shared capital) wa Tsh.50000/= ambapo gharama za uwekezaji zingekuwa ndogo. Baada ya TANESCO kuushtukia mchezo walishitakiana na mteja wao huyo hata kufikia kutolipana hizo gharama moja kwa moja hadi ikafunguliwa akaunti ya Tegeta Escrow.
Sipo katika kuongelea akaunti hiyo pamoja na mauzauza ya pesa iliyokuwepo kwenye akaunti hiyo, bali kinachonipa maswali kichwani mwangu ni kwamba;
IPTL bado wapo wanafua umeme hapa nchini hadi mkataba wao utakapomalizika 2022, je bado gharama za uwekezaji (Capacity charges) ni zile zile zilizoleta utata hadi kufunguliwa akaunti ya Tegeta Escrow? Na kama ni zile zile je, sasa hivi hiyo pesa inawekwa wapi au TANESCO wamekubali kuzilipa jinsi zilivyo wakakubaliana na ujanja ujanja wa IPTL?
Tafadhalini wachangiaji wenye mitazamo ya kichama hili halipo kichama. Wenye uelewa na jambo hili nisaidieni.