Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Ikiwa ni miaka 6 ikielekea kutimia miaka 7 tangu kuanza kwa mapigano nchini Syria aidha mpaka sasa takwimu zinaonyesha kuwa watu zaidi ya 465,000 wameuawa katika mapigano, huku zaidi ya milioni 1 wakijeruhiwa na wengine zaidi ya Milioni 12 wameikimbia nchi hiyo.
Hata hivyo mpaka sasa hakuna dalili zakumalizika kwa mgogoro/vita hivi huku makundi kadhaa yakiendelea kushikilia maeneo mbalimbali katika ardhi ya Syria.
Serikali ya nchi hiyo, Kikundi cha Kurdi, Dola ya Kiislamu na Vikundi kadhaa vya waasi kwa pamoja bado wanapambana kuhakikisha wanashikilia maeneo muhimu ya taifa hilo linaloongozwa na Rais Bashal Al Assad.
Vikosi vya Serikali vikiungwa mkono na ndege vita za Urusi vimefanikiwa kushikilia kurudisha maeneo kadhaa waliyokuwa wameyapoteza hapo awali. Ikumbukwe kuwa mwishoni mwa mwaka jana vikosi vya Serikali viliukomboa mji muhimu wa Aleppo ambayo ilikuwa ni Sehemu muhimu katika mapigano.
Hebu kupitia ramani ifuatayo tufahamu ni nani anashikilia eneo lipi katika nchi hiyo;
UFUNGUO;
Damu ya Mzee - Ni eneo linaloshikiliwa na Serikali ya Syria.
Nyeusi - Ni eneo lililochini ya Dola ya Kiislamu.
Njano - Ni eneo linaloshikiliwa na Wakurdi.
Plascon - Ni eneo linaloshikiliwa na Vikundi vya Waasi.
Damu ya Mzee na Nyeusi - Eneo linalopiganiwa kati ya Serikali na Dola ya Kiislamu.
Blu Bahari - Ni eneo linaloshikiliwa na Waasi wanaoungwa mkono na Serikali ya Uturuki.
Blu - Ni eneo linaloshikiliwa na Israel(Vilele vya Golan).
Kwa msaada wa Aljazeera