Mgogoro wa SHAFIH DAUDA wa clouds fm NA WAZEE WA YANGA

Bajabiri

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
9,730
1,201
Jana nimemsikia mzee akilimali akimshtumu mtangazaj wa Clouds media bwana Shafih Dauda kuwa anafanya mawasiliano na Marcio Maximo ili asije kuifundisha YANGA,nilimsikia yule mzee akisema Shafih anamwambia Maximo asije bongo kwakuwa Yanga ni maskini,tangu jana shafih amekana,ila leo nimemsikia kupitia sports xtra kuwa amempa mzee Akilimali siku 7 amuombe radhi kwa kuitisha press conference kama alivyoitisha jana,pia amesema atampeleka mahakaman,,,,,,,,,
soka la tanzania na maigizo,MI NAULIZA TU HIVI MAXIMO HAJI AU YANGA WANATAFUTA SABABU????
 
Maximo awezi kuja kufundisha walugaluga hao wao ni migogoro na sasa wanaupeleka kwa dauda washindwe walegehe wazee tano hao
 
Maximo awezi kuja kufundisha walugaluga hao wao ni migogoro na sasa wanaupeleka kwa dauda washindwe walegehe wazee tano hao

kuna mwanayanga amesema hivohivo kuwa hawa jamaa wanatafuta justification
 
Yanga na Simba ni full GOGORO, hakuna maendeleo zaidi ya fitna.
 
Huyu Dauda mnafiki na mchakuchaku sana. Nasikia ndiyo yeye aliyesababisha hadi Baloteli anapigwa benchi na Manchini. Baloteli alimaindi kinoma ila akaona aipotezee tu.
sweety r u siriaz????halafu dauda ameielezea isho ya supamario balo t
 
Soka la bongo, nimeamua kuwa mshabiki wa Azam, simba na yanga michosho.
 
Kwa nini mzee Akilimali amtaje Dauda kuna kitu hebu tusubiri tutajua.....ukweli ulipo maana Dauda anaweweseka wakati mwingine kujua kwingi!!na misifa ndani yake!acha tuupe muda tutajua ukweli
 
Soka la bongo limejaa ujinga, ndio maana katika mashindano tunakuwa wasindikizaji kila siku.
 
Huyu Dauda mnafiki na mchakuchaku sana. Nasikia ndiyo yeye aliyesababisha hadi Baloteli anapigwa benchi na Manchini. Baloteli alimaindi kinoma ila akaona aipotezee tu.
hata mimi niliambiwa ndiye aliyesababisha Romario kuchwa timu ya taifa ya brazil kwenye world cup ya Korea na Japan
huyu sio mtu mzuri kabisa
 
Huyu Dauda mnafiki na mchakuchaku sana. Nasikia ndiyo yeye aliyesababisha hadi Baloteli anapigwa benchi na Manchini. Baloteli alimaindi kinoma ila akaona aipotezee tu.

na ndiye aliyesababisha hata holland kutolewa kwenye EURO 2012. Huyu jamaa hatari sana.
 
najiuliza sana huyu Dauda kasomea wapi uandishi wake wa habari...yaani yuzi anazungumza tena kwa kurudia rudia eti mzee akilimali aprint hizo enail adress nilizotuma kwa maximo!! ni email address au email??? hovyo kabisa....kali kuliko zote ni huyo mzeee akilimali anasema zimetume emilii kwa Maximo...hahaaaa
 
Kwa nini mzee Akilimali amtaje Dauda kuna kitu hebu tusubiri tutajua.....ukweli ulipo maana Dauda anaweweseka wakati mwingine kujua kwingi!!na misifa ndani yake!acha tuupe muda tutajua ukweli

Mi nadhani issue ya msingi si Shaffih kumzuia Maximo kuja Yanga, kuna kitu kinaendelea hapa ambacho ni muhimu kukitazama kwa jicho la tatu.
Kwanza mashabiki wengi wa Yanga walichukizwa na namna watangazaji wa clouds fm walivyolibebea bango suala la wachezaji wa Yanga kumpiga muamuzi wa mchezo wao dhidi ya Azam. Walifikia hatua ya kumzuia Alex Luambano wa clouds fm assingie klabuni kwao kwenye press conference huku wengine wakitaka kumdunda, baada ya hapo Alex akaonekana kama kanywea hivi.

Punde si punde ndipo imekuja hii issue ya Maximo. Binafsi sidhani kama Shaffih anaweza kumzuia maximo kuja Yanga isipokuwa anaweza kumpa taarifa mbaya juu ya Yanga ili akate tamaa ya kuja Yanga. Hii inatokana na observation yangu kwa watangazaji wa clouds fm wanapotangaza habari za Yanga, mara nyingi wamekuwa wakitoa maneno ya dharau, na kebehi dhidi ya klabu yanga, wachezaji wa yanga, viongozi wa yanga na wanachama wa yanga.

Kwa mfano shaffih alikuwa akihoji sana kuhusu manji kuchukua fomu kuwania uongozi wa yanga, sasa hapa mtu utajiuliza yeye ni nani na kwa mamlaka gani hadi ahoji uhalali wa manji kuwania uongozi wa yanga wakati katiba inamruhusu akiwa kama mwananchama kama wengine? je shaffih ana agenda gani juu ya yanga? je na yeye anatumika au anatumiwa au anajitumikisha mwenyewe?
Nadhani hawa watangazaji wa clouds lazima wajitazame upya namna wanavyotoa na kutangaza habari zao, kwani inaonekana hata wao wana walakini. Mimi najiuliza tu kwanini mara kwa mara wao tu ndio wanaingia katika malumbano na vilabu? tangu walipofanya biashara ya kusimamia mechi za yanga na simba katika michuano ya kimataifa mwaka huu na baadae kusemekana kulikuwa na ujanja ujanja katika mahesabu ya makusanyo ya fedha za kuuza tiketi, hawa clouds fm wameonekana kuzisema vibaya timu hizi. Sina sababu ya kutoamini kwamba hawa jamaa wana agenda yao nyuma ya pazia dhidi ya timu ya yanga.
 
mfa maji haach kutapatapa, hilo ni kumba bovu. ple sana shafiii endelea kukaz uzi wako ktk anga za michezo, usikate tamaa kaka, kwa hapa tziee baada ya dr. ric wewe unaweza kuwa mkali wa pili kwa info za kisports big up.. let them talk talk
 
Ningekuwa mimi ni Yanga hata kama ni kweli Shafii kafanmya hivyo nisingesema hadharani,maana ni aibu kubwa sana kwa kocha kama Maximo ''kushawishiwa'' na mtu kama Shafii ikizingatiwa Maximo anaijua Bongo na Yanga vizuri sana. Kama kweli tatizo sio Shafii bali Yanga kuchagua kocha '' undema'' anayeweza kushawishiwa na mtu mwenye calibre ya Shafii !!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom