Mgogoro wa Qatar vs Saudi Arabia

Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,581
1,069
Wanajamvi;

Wiki chache zilizopita za Saudi Arabia, UAE, Bahrain na washirika wengine waliamua kuvunja uhusiano na Qatar wakiinyooshea kidole kwa kuunga mkono makundi ya kigaidi. Hatua zilizochukuliwa ikiwa ni pamoja na kufunga ofisi za ubalozi, kupiga marufuku qatar airways kufanya safari kwenda nchi zao n.k.

Tujadili kidogo chanzo hasa cha mgogoro huu pamoja na athari zake kwani kuna kila dalili kwamba vuguvugu hili halikuanza jana wala juzi isipokuwa ni la miaka mingi.

Qatar's Crisis With Saudi Arabia And Gulf Neighbors Has Decades-Long Roots


Nguruvi3 JokaKuu Mchambuzi Mag3 na wengineo karibuni.
 
Mkuu huu mgogoro una vitu vingi sana ndani yake ambavyo si rahisi kuviona haraka

Historia inaonyesha Saudia Arabia ndio 'sponsor' wa matukio ya kigaidi kupitia raia wake
Tunaposema sponsor hatuna maana kingdom bali mashirika na taasisi zinazotoa pesa

Kwa mgawanyiko wa dini ya kiislam kuna makundi kadhaa mkubwa kama Sunni na Shia
Ndani ya Sunni kuna makundi madogo kama Salafi, na Wahabia

Wahabia msimamo wao ni kutaka Uislam katika zama za awali kama ulivyo,wapo Saudia
Shia ambao wengi wao ni wasomi wazuri wa dini na elimu ya kawaida. Hawa wapo Iran

Tumezungumzia mgawanyiko wa makundi kwa maana moja ili mbele ya safari tuweze kujadili vema na si kuhusisha dini na matukio ya kigaidi. Hili lieleweke mapema na vema

Saudia inaona tishio lililopo mashariki ya kati ni Shia wa Iran.
Kwamba, Iran inaendelea kupata nguvu na kuendelea 'ku dominate' siasa za eneo hilo.

Mzozo wa Yemen una asili ya Sunni na Shia. Kule Iraq kuna mgawanyiko wa Sunni na Shia, Iran ikituhumiwa kuingilia siasa za ndani.

Kama utakumbua baada ya anguko la Saddam aliyekuwa na nguvu kiutawala ni Moktada el Sadra ambaye ni Shia na baada ya kuandamwa alikwenda kuishi Iran

Qatar inajihusisha sana na Iran na hilo tu ni tishio kwa Saudia yenye mipaka na nchi hiyo
Lakini pia Qatar inajihusisha na siasa za middle east kama vile ku sponsor Hamas

''Inasemekana'' hata mzozo wa Somalia Qatar wana mkono kwa namna moja au nyingine

Ziara ya Rais Trump nchini Saudia ilikuwa kuwahakikishia usalama wao ndiyo maana kulikuwa na biashara za silaha kuliko mafuta.

Yaani usalama dhidi ya Iran ambaye kwa namna anaonekana ni super power

Ujumbe uliofikishwa kwa Saudia ni kuacha ku sponsor makundi ya wahalifu.
Kwa kufanya hivyo itapata msaada wa Marekani dhidi ya hasimu wake Iran

Trump aliposema Iran ina sponsor ugaidi haikuwa na usahihi wa moja kwa moja
Hakuna rekodi zinazoonyesha magaidi kutokea eneo hilo.

Rekodi zipo za magaidi ima kupata mafunzo nje ya Saudi wakiungwa mkono

Vikwazo dhidi ya Qatar vina maana kadhaa

Kwanza , Saudia kujiosha na tuhuma za Wahabia wanaoonekana kuwa tatizo zaidi
Pili, kumdhibiti Qatar ambaye ni swahibu na rafiki wa Iran
Tatu, kuna mkono wa Israel kwa kuzingatia uhusiano wa Qatar-Hamas na Iran
Nne, kuna mkono wa Egypt anayedai Brotherhood wanaungwa mkono na Qatar

Kuna mtazamo kuwa Iran inajitanua kupitia nchi kama Qatar

Siasa za eneo hilo ni za kuchanganya (complicated) na zinahitaji darubini kidogo kuliko tunavyoona
 
Asante sana Nguruvi3 kwa mchango wako.

Unafikiri athari za mgogoro huu zitakuwa kubwa kiasi gani kwa pande zote mbili hususan Qatar itaathirika vipi kwa kufungiwa milango na Saudia? Huoni kwamba kwa kuitenga Qatar inaweza kuchochea wao kusogea zaidi upande wa Iran? Juzi tu hapa tumeona Iran ikisafirisha shehena ya misaada kwenda Qatar.

Na hapo tusisahau kwamba Marekani ana kambi kubwa ya kijeshi nchini Qatar. Kwa kitendo cha Marekani kuonekana akiegemea zaidi upande wa Saudia inaweza kuathiri mahusiano yake na Qatar na inaweza kuleta sintofahamu juu ya uwepo wa majeshi yake Qatar.
 
"Mwalimu, post: 21757350, member: 11689"]
Unafikiri athari za mgogoro huu zitakuwa kubwa kiasi gani kwa pande zote mbili hususan Qatar itaathirika vipi kwa kufungiwa milango na Saudia?
Mkuu Mwalimu mgogoro unahusu pande mbili zenye mafuta kwa wingi duniani.

Kwa Saudia kwasababu wana 'black gold'' haitegemewi kuathirika
Qatar itaathirika hasa ikizingatiwa kuwa chakula na huduma nyingine zinatoka Saudia

Kumbuka Saudia ni Taifa kubwa sana ukilinganisha na Qatar

Mgogoro ulianza kwa panic ya watu kukusanya vyakula na huduma zingine ambazo Qatar wanategemea nchi ya Saudia. Ndiyo maana baada tu ya mgogoro, Turkey na Iran zili 'rush' kutoa msaada wa chakula ili isiwe ''bargaining chip'' itakayowalazimisha kukaa mezani

Qatar ina shirika kubwa la ndege ambalo linatumika kama 'Hub' ya kuingilia middle east
Shirika hilo linaendeshwa kisasa na linatoa huduma kwa kiwango cha kimataifa haswa

Kufunga mpaka kutaathiri sana shirika, kwani mahujaji wa Mecca katika Hajj na wale wanaokwenda kuzuru 'umra' itababidi watafute mbadala ambao ni Gulfu air au Emirates

Hilo litatoa mwanya kwa mashirika hayo ya UAE kujitanua na shirika lao kuvia

Tatizo lingine ni Television ya Aljazeera ambayo ni maarufu sana middle east and far
Umaarufu wake ni katika kueleza yale yasiyojulikana katika falme za kiarabu

Kwa mtazamo huo, ima Aljazeera itaathirika kwa kulazimishwa kufungwa kama madai ya kurudisha uhusiano, au Aljazeera itaendelea kuanika habari nyeti za mashariki ya kati

Ni aljazeera pekee ndiyo inaeleza migogoro ya ndani ya Arab World kwa kina na uchunguzi ikigusa falme ya Saudia Arabia na Israel kwa undani wake

Kwa upande wa nje, Qatar italazimika kusitisha misaada kwa maeneo kama Gaza ambako wamejihusisha na ujenzi baada ya kubomolewa na Israel miaka michache iliyopita

Raia wengi wa Qatar wanaishi nchi za Uarabuni kama Saudia watalazimika kuondoka
Mahusiano ya kueloeana na taratibu za uhamiaji zitawaathiri wahamiaji kutoka Qatar

Qatar inataraji ku host FIFA 2022 na hilo litakuwa na athari.
Kuna uwezekano vikwazo vikiendelea FIFA ikafikiri upya kuhusu ushiriki wake

Kwahiyo Qatar inasimama ku lose kuliko washirika wa GCC au Aarab world in general
Swali, je watahimili vikwazo walivyowekewa?
Huoni kwamba kwa kuitenga Qatar inaweza kuchochea wao kusogea zaidi upande wa Iran? Juzi tu hapa tumeona Iran ikisafirisha shehena ya misaada kwenda Qatar.
Yes Qatar ni mshirika wa Iran ambaye ni mshirika wa Russia.

Baada ya uhusiano wa Saudia na US kulega lega (Obama) Saudia iliwageukia Russia.
Saudia haiamini Russia kutokana na ukaribu wake na Iran.Russia ni rafiki wa adui

Kwa kuona hilo, Saudia wakaamua kumpa Trump mapokezi makubwa na mbadala wake ukawa kuuziwa silaha kwa mabilioni ya dola, yaani wakiondoka Russia na kurudi US

Hilo limechagiza Iran kuingia kati na kuisadia Qatar kwa chakula ikishirikiana na Turkey
Wakati huo huo Turkey inaona kama haitaingizwa EU basi itageukia Iran.

Kumbuka Turkey ni mwanachama wa NATO na hivyo US inamwangalia kwa jicho la karibu
Uhusiano wa US na Turkey ni muhimu kwa Europe na Israel
Kumsogeza Iran kwa ukaribu na Turkey kunafanya equation kuwa complicated (Complicated)
Na hapo tusisahau kwamba Marekani ana kambi kubwa ya kijeshi nchini Qatar. Kwa kitendo cha Marekani kuonekana akiegemea zaidi upande wa Saudia inaweza kuathiri mahusiano yake na Qatar na inaweza kuleta sintofahamu juu ya uwepo wa majeshi yake Qatar
Ndiyo US wana base Qatar wana air base Kuwait.

Kwa kutambua nature ya mzozo na jinsi unavyoweza kuathiri nchi hiyo, US wamemuomba (nyuma ya pazia) Kuwait awe msuluhishi wa mzozo wa Qatar

Hili litaisumbua sana US kwasababu ni upanga unaokata sehemu mbili (double sword)

Kumwacha Qatar ni kuruhusu influence ya Iran na Russia kusambaa middle east
Kumhodhi Qatar ni kuwakimbiza washirika kama Saudia ambao ni chimbuko la ''magaidi''

Kwa kitendo hicho, US wata play safe, bila kuathiri mahusiano na nchi za Uarabuni dhidi ya Qatar na bila kutoa mwanya kwa Qatar kuangukia Iran-Russia kikamilifu
 
MASHARTI 13 KWA QATAR KUTOKA S.ARABIA,EGYPT, KUWAIT NA UAE

Msuluhishi Kuwait amefikisha masharti 13 kwa Qatar kuhusu vikwazo ilivyowekewa
Hii ni kwa mujibu wa Associate Press

Here’s the demands:

1. Curb diplomatic ties with Iran and close its diplomatic missions there. Expel members of Iran’s Revolutionary Guard from Qatar and cut off any joint military cooperation with Iran. Only trade and commerce with Iran that complies with US and international sanctions will be permitted.
My take
Hapa kuna hoja tulizozungumza kwamba Iran ndio tatizo kwasababu ya uhusiano na Qatar
Saudi Arabia imepata 'maagizo kuhusu Bishara kutoka US ili iwe sehemu ya vikwazo kwa Iran
US inaona Qatar kwa ushirika na Iran vikwazo 'haviumi' kama ilivyotarajiwa
Utaona visingizio ni ugaidi lakini kuna mengine makubwa nyuma yake
2. Sever all ties to terrorist organisations, specifically the Muslim Brotherhood, ISIL, Al Qaeda, and Hizbollah. Formally declare those entities as terrorist groups.
Saudia iliwahi ku declare lini makundi hayo ikiwa 'inahusishwa' na yote kuanzia Sept 11?
Brotherhood wanapata support y nani na akina Al Zawahir walikuwa na itikadi ipi tofauti na itikadi ya Wahabia kutoka Saudia?

Hapa kundi lililolengwa ni Hezbollah kwasababu ya kuwa tishio kwa Israel wakati huo huo likiungwa mkono na Iran. Tunaweza kuona Iran inarudi katika picha tena
3. Shut down Al Jazeera and its affiliate stations.
Hii ni kwasababu station inaanika madudu ya falme hasa kuhusiana na suala la mahusiano ya Kingdom na US na jinsi gani inaathiri nchi za kiislam. Aljazeera ina highligh human right violation kuanzia Saudia Arabia hadi Israel. Kwahiyo Qatar inagusa interest za 'US'
4. Shut down news outlets that Qatar funds, directly and indirectly, including Arabi21, Rassd, Al Araby Al Jadeed and Middle East Eye.
Kwa maneno mengine Qatar isiwe na station zake na itegemee habari za GCC na UAE. Saudia inataka iwe na uwezo wa ku control nchi za kiarabu kama ilivyofanya wakati wa ziara ya Trump kwa kukusanya nchi zote zikaja 'Kingdom' kupokea maagizo

5. Immediately terminate the Turkish military presence currently in Qatar and end any joint military cooperation with Turkey inside Qatar.
Well, nchi hizo hazitaki Turkey iwe na shughuli za kijeshi Qatar. Kwa taarifa Turkey ina jeshi Qatar. US ina base Qatar. Kwanini majeshi ya Turkey tu ndiyo yanayotakiwa kuondoka?Hili nalo linarudi pale pale kwamba kuna ushirika wa Trukey, Iran unaoponza Qatar
Haiwezekani nchi za Kiarabu zikapinga nchi ya Kiislam kuwa na base zikikumbatia US
6. Stop all means of funding for individuals, groups or organisations that have been designated as terrorists by Saudi Arabia, the UAE, Egypt, Bahrain, the US and other countries.
Angalia, nchi za Kiarabu na US na wengine. Kwanini wengine hawatajwi ? Hii inaelekeza kuwa maagizo ni ya wale viongozi wa nchi waliokutana na Trump Saudia Arabia
Katika makundi hayo moja ni Hamas ambalo US wanaliona ni la kigaidi.
Picha inarudi Israel ambako Qatar ina miradi ya ujenzi wa Gaza chini ya Qatar

7. Hand over terrorist figures and wanted individuals from Saudi Arabia, the UAE, Egypt and Bahrain to their countries of origin. Freeze their assets, and provide any desired information about their residency, movements and finances.
Saudia iliwahi ku freeze assets za washiriki wa 9/11? Iliwahi kutaja makundi inayofadhili kule Afganistan na Pakistan? Kwanini Saudia inatuhumiwa kuficha habari za magaidi?
8. End interference in sovereign countries’ internal affairs. Stop granting citizenship to wanted nationals from Saudi Arabia, the UAE, Egypt and Bahrain. Revoke Qatari citizenship for existing nationals where such citizenship violates those countries’ laws.
Wanaposema interference wanamaanisha asiingilie mambo ya 'Gaza'. Qatar kama nchi huru ina uwezo wa kuwa na mahusiano na taifa lolote. Si kazi ya Arab world kuwapangia nani awe rafiki nani awe adui. Kama Qatar inaingilia mambo ya nchi zingine, wanaopaswa kulalamika ni nchi husika si nchi za Kiarabu. Pili pili shambani ....?

9. Stop all contacts with the political opposition in Saudi Arabia, the UAE, Egypt and Bahrain. Hand over all files detailing Qatar’s prior contacts with and support for those opposition groups.
Hapa wanamaanisha Brotherhood, Hamas na moderates wanaotaka Arab spring kama ilivyokuwa Bahrain na kwingineko.
Saudia inaona Arab spring ni tishio isipoziba haraka wanaweza kujikuta mahali pagumu.
Mbona Saudia ipo Yemen na ina influence katika masuala ya middle east?
10. Pay reparations and compensation for loss of life and other, financial losses caused by Qatar’s policies in recent years. The sum will be determined in coordination with Qatar.
Hey! Magaidi wa 9/11 walitokea Saudia. US kuna kundi linadai compensation hadi leo, iweje wao wasilipe kwanza waanze kunyooshea vidole wenzao. Je, Saudia italipa yanayotokea Yemen ambako Raia wasio na hatia wanakufa kwa mabomu?
Saudia wataishauri US ilipe compensation kwa matatizo ya Iraq?
11. Align itself with the other Gulf and Arab countries militarily, politically, socially and economically, as well as on economic matters, in line with an agreement reached with Saudi Arabia in 2014.
OK! kwamba wajiunge na majeshi ya nchi za Kiarabu. Qatar ni sovereign state ina kila haki ya kujiunga au kukataa bila kuingilia au kuingiliwa, kwanini ilazimishwe
Kulazimishwa maana yake ni kutoa mwanya kwa nchi za Kiarabu kushinikiza Turkey iondoe majeshi, Qatar isiwe na uhusiano wa majeshi na Iran of course na Russia
Kwanini nchi chache zinataka kuamua hatma ya nchi nyingine za eneo hilo na haki hiyo Saudia kapewa na nani dhidi ya wenzake.

12. Agree to all the demands within 10 days of it being submitted to Qatar, or the list becomes invalid. The document doesn’t specify what the countries will do if Qatar refuses to comply.
Non sense kwasababu masharti waliyoweka ni kuilamisha Qatar na kuondoa uhuru wake. Ni kutaka Qatar iwe chini ya Falme za Saudia kama zilivyo vinchi vingine visivyojiweza. Kwanini Qatar asipewe nafasi ya kujadiliana bali apewe masharti? ile sovereignty ipo wapi
13. Consent to monthly audits for the first year after agreeing to the demands, then once per quarter during the second year. For the following 10 years, Qatar would be monitored annually for compliance.
C'on! ni nchi gani nyingine inayofanyiwe audit kama Qatar. Haya yote ni kutaka kutoa nafasi kwa US kutimiza azma yake hayana faida kwa nchi za Kiarabu na Saudia inatumika kama mpini.
Kinachoshangaza inatumika kama mpini wa kukata kuni za kukaanga ndugu zao

Hoja tunazojadili hapa ni kwa muktadha wa bandiko la 2 hapo juu
Tulisema kuwa tatizo si Ugaidi kama inavyoaminishwa, kuna mambo mengine zaidi na kwa hoja zilizotolewa picha nzima inaonekana kama tulivyoijadili

Siasa za middale east zina mengi

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3

Masharti haya kwa kifupi hayatekelezeki na sijui Saudia walikuwa wanawaza nini au wanataraji kupata nini kutokana na kutoa masharti haya tena yakitakiwa kutekelezwa kwa muda mfupi.

Hii inamuweka mmarekani njia panda sababu mwisho wa siku asingependa kumpoteza Qatar kama mshirika muhimu.
 
Mkuu Mwalimu

Bandiko lako linarudi kwa kuzingatia hali ya mambo ilivyo katika uhusiano baina ya Saudia na US
Kwa bahati mbaya Saudia wanadhani US ipo kwa masilahi yao

Kurushiana maneno kati yao ni dalili za kuchokana.
Saudia waliwatosa Wapalestina wakisema ni wakati wa kukubaliana na Israel

Saudia walimaanisha Palestina wachukue chochote kitakachowekwa mezani. Jambo hilo lilizidi kuwatia kiburi US ambao wamekata misaada na kufunga ofisi za Wapalestina

Saudia wanashindwa kuelewa US si msuluhishi(honest broker) mzozo wa Israel na Palestina. US ina upande wa Israel na inalinda masilahi ya nchi hiyo kwa gharama zozote

Lengo la US na Israel kuikumbatia Saudia ni kupata mwanya wa kuiumiza Iran
Iran ndio tishio kwa Israel baada ya Saadamu Hussein.
Tofauti na Saudia, Iran imeendelea kiteknolojia na uwezo wa kubuni na kutengeneza vitu vyake

Vikwazo dhidi ya Iran vilivyowekwa na US vinaiumiza na kuidhoofisha Iran.
US na Israel hazioni tena umuhimu wa Saudia na ndicho chanzo cha kauli tata baina yao

Saudia wanajiweka katika mazingira magumu. Kununua silaha kutoka US/Israel ni kujianika

Wanaouza silaha wanajua wanauza nini. Kwa maneno mengine usalama wa Saudia ni kushambulia nchi jirani na mahasimu. US na Israel wanajua uwezo wao kiulinzi

Kuingilia kati kwa Turkey mzozo wa Qatar kumesaidia kupunguza joto kidogo
Turkey inaonekana taifa dhaifu ndani ya bara ulaya, ukweli ni tishio la kiusalama kwa Israel
Hili nalo kinachagiza US kuingilia siasa za ndani za Turkey kwa kisingizio cha haki za binadamu

Siasa za middle east zina mazonge zonge mengi. Ikiwa Saudia ni mshirika wa US/Israel, silaha za mabilioni ni kwa ajili ya nani? Jibu ni rahisi , ni kuwaadhibu ndugu zao waarabu majirani

Ikiwa Saudia ni nchi takatifu inayolindwa kutokana na imani kama kitovu cha Uislam, silaha nyingi ni za kulinda nini? Saudia inaweza kulindwa na Waislam kwa mabilioni, ni vipi basi nchi hiyo takatifu ijilimbikizie misilaha?
 
Mkuu Mwalimu

Bandiko lako linarudi kwa kuzingatia hali ya mambo ilivyo katika uhusiano baina ya Saudia na US
Kwa bahati mbaya Saudia wanadhani US ipo kwa masilahi yao

Kurushiana maneno kati yao ni dalili za kuchokana.
Saudia waliwatosa Wapalestina wakisema ni wakati wa kukubaliana na Israel

Saudia walimaanisha Palestina wachukue chochote kitakachowekwa mezani. Jambo hilo lilizidi kuwatia kiburi US ambao wamekata misaada na kufunga ofisi za Wapalestina

Saudia wanashindwa kuelewa US si msuluhishi(honest broker) mzozo wa Israel na Palestina. US ina upande wa Israel na inalinda masilahi ya nchi hiyo kwa gharama zozote

Lengo la US na Israel kuikumbatia Saudia ni kupata mwanya wa kuiumiza Iran
Iran ndio tishio kwa Israel baada ya Saadamu Hussein.
Tofauti na Saudia, Iran imeendelea kiteknolojia na uwezo wa kubuni na kutengeneza vitu vyake

Vikwazo dhidi ya Iran vilivyowekwa na US vinaiumiza na kuidhoofisha Iran.
US na Israel hazioni tena umuhimu wa Saudia na ndicho chanzo cha kauli tata baina yao

Saudia wanajiweka katika mazingira magumu. Kununua silaha kutoka US/Israel ni kujianika

Wanaouza silaha wanajua wanauza nini. Kwa maneno mengine usalama wa Saudia ni kushambulia nchi jirani na mahasimu. US na Israel wanajua uwezo wao kiulinzi

Kuingilia kati kwa Turkey mzozo wa Qatar kumesaidia kupunguza joto kidogo
Turkey inaonekana taifa dhaifu ndani ya bara ulaya, ukweli ni tishio la kiusalama kwa Israel
Hili nalo kinachagiza US kuingilia siasa za ndani za Turkey kwa kisingizio cha haki za binadamu

Siasa za middle east zina mazonge zonge mengi. Ikiwa Saudia ni mshirika wa US/Israel, silaha za mabilioni ni kwa ajili ya nani? Jibu ni rahisi , ni kuwaadhibu ndugu zao waarabu majirani

Ikiwa Saudia ni nchi takatifu inayolindwa kutokana na imani kama kitovu cha Uislam, silaha nyingi ni za kulinda nini? Saudia inaweza kulindwa na Waislam kwa mabilioni, ni vipi basi nchi hiyo takatifu ijilimbikizie misilaha?

Baada ya majibizano ya hivi karibuni nafikiri Saudia ndio wataanza kujifunza kwamba marekani especially chini ya utawala huu sio mshirika anayetabirika. Kama utakumbuka Trump ziara yake ya kwanza middle east alienda Saudia na kuwamwagia sifa kedekede pamoja na kuwauzia silaha... sasa anawageuzia maneno na kupiga kijembe kwamba hawawezi kusurvive bila US kitu ambacho ni dharau kwa watawala wa Saudia.

Msingi mkubwa wa yote haya ni kwamba nchi za kiarabu hawana umoja kutokana na uhasama wa kidini kati ya SUNNI na SHIA unaokwenda karne nyingi nyuma. Na uhasama huu ndio umechangia kwa kiasi kikubwa uadui dhidi ya Iran pamoja na vita inayoendelea huko Yemen ambapo Saudia na Iran wanapigana "proxy war". Nafikiri pia uhasama huu ndio unachangia Saudia isiipe kipaombele strugle ya wapalestina wanaoungwa mkono na makundi kama HAMAS & HEZBOLLAH wanaosaidiwa na Iran/Syria.

Uhasama na uadui huu SHIA vs SUNNI ni mkubwa mno na Saudia wako tayari kushirikiana na Israel kuliko kukaa meza moja na mahasimu wao wakubwa IRAN.
 
"Mwalimu, post: 28688609, member: 11689"]Baada ya majibizano ya hivi karibuni nafikiri Saudia ndio wataanza kujifunza kwamba marekani especially chini ya utawala huu sio mshirika anayetabirika. trump ziara ya kwanza middle east, Saudia na kuwamwagia sifa kedekede na silaha... sasa anawapiga kijembe hawawezi kusurvive bila US kitu ambacho ni dharau kwa watawala wa Saudia
Mkuu Saudia si kwamba walimpenda Trump.

Walilazimika kufanya hivyo kutokana na Obama kutofautiana nao hasa katika mambo ya haki za binadamu akina mama na ushoga.Mbadala ni Hillary hivyo walidhani hakuna tofauti.

Katika mizania ya kiusalama, Saudia hawakupenda sera za Obama kuhusu hasimu wao Iran. Walitaka US waishambulie Iran kama alivyotaka Netanyahu

Huo ndio msingi wa Saudia kuwa na ushirika na Israel hata kuwatosa Wapalestina

Kwamba, walikuwa na 'common enemy' Iran na hadi sasa wanaushirika wa kukabiliana naye

Kwanini Trump anawapiga vijembe?
Ni kwasababu amewauzia silaha na zingine kutoka Israel na wanajua uwezo wa silaha hizo. Kwa ufupi wamempa Saudia 'jambia' wanalojua makali na ubutu wake
Msingi mkubwa wa yote haya ni kwamba nchi za kiarabu hawana umoja kutokana na uhasama wa kidini kati ya SUNNI na SHIA unaokwenda karne nyingi nyuma. Na uhasama huu ndio umechangia kwa kiasi kikubwa uadui dhidi ya Iran pamoja na vita inayoendelea huko Yemen ambapo Saudia na Iran wanapigana "proxy war"
Mkuu kwa mtazamo wa Kishia na Kisuni hakuna Uhasama.

Kinachotenga makundi haya ni 'ideology' ambayo ni ndogo sana
Ni mtazamo wa mitume ambao ni ndugu, kila upande ukiwa na mtazamo wake katika Uislam

Uhasama uliopo sasa umekuzwa na siasa za dunia hii.
Kwamba, njia nyepesi ya kuwagawa Waislam ni kutumbukiza siasa za kisasa katika imani

Kingine ni uwezo wa kielimu ambako Shia wana wasomi wazuri kulinganisha na Sunni

Kujitanua kwa Shia ni kutokana na nguvu ya elimu, na kuzuia Suni wanatumia silaha.

Hayo ndiyo unayoyaona kwa Saudia kubomu majirani

Kwanini US na Israel wanamkalia kidete Iran?
Ni kwasababu Iran ina Shia ambao wana influence ya Fikra kuliko silaha.
Uwezo wa Shia unawasumbua Israel kupitia Hamas na Hezbollah

Tathmini ya Vita ya Israel na Hezbollah ya Nasra miaka ilionyesha Israel walishindwa.

Walishindwa kwasababu nguvu walyotumia haikulingana na upinzani walioupata.
Haya wamesema wenyewe Waisrael kupitia kamati waliyounda kutathmini vita
Na hata baada ya hapo Hezbollah bado wapo imara na hilo ni tishio kwa Israel

Influence ya Shia ime base katika elimu ambayo ni silaha kubwa
Nafikiri pia uhasama huu ndio unachangia Saudia isiipe kipaombele strugle ya wapalestina wanaoungwa mkono na makundi kama HAMAS & HEZBOLLAH wanaosaidiwa na Iran/Syria.
Nadhani nilimelichangia hapo juu kwa kina
Uhasama na uadui huu SHIA vs SUNNI ni mkubwa mno na Saudia wako tayari kushirikiana na Israel kuliko kukaa meza moja na mahasimu wao wakubwa IRAN
Kama nilivyoeleza, tatizo siyo Shia na Sunni, ni Shia kutoka Iran na Sunni wa Saudia wakigombea utawala na umiliki wa middle east, siyo dini kama Uislam

Tofauti iliyopo ukiitazama haina mantiki ya kuleta chuki. Kuhasimiana kunaletwa na siasa

Mtume Muhhamad Pubh na Imamu Hussein ni ndugu wa damu katika Uislam mmoja. Kilichofuata ni theory kwamba nani ameusimamisha? (Kama sitakuwa nimekosea)

Kama utanielewa huu si mgogoro wa Uislam au kitu unique, ni mgororo wa kisiasa unaotumika kiislam

Kwa atakayeshindwa kuelewa mantiki nitaububusa busa kwingine (nisahihishwe nikikosea).

Ni mgogoro unaofanana na ule uliozaa Catholic na Protestants
Kilichowagawa si imani ya Ukristo, ni siasa zilizoingia katika imani kwa muktadha wa kutawala

Tusemezane
 
KUTOWEKA KWA KHASHOGGI NA UTATA

SAUDIA WAKANA, TRUMP 'AJIUMA UMA'

Baada ya kauli ya kuilinda Saudia US inajikuta katika mzozo mwingine na MbS Saudia

Mwandishi wa gazeti la WAPO(Washington post) ambaye ni Raia wa Saudia anayeishi uhamishoni ametoweka katika mazingira ya utata ndani ya Ubalozi wa Saudia nchini Turkey

Khashoggi ni mkosoaji mkubwa wa Saudia crown, MbS katika makala zake magazetini.
Ni mkazi wa kudumu wa US. Kilichompeleka ubalozini ni kufuatilia karatasi zinazohusu ndoa

Serikali ya Turkey chini ya Rais Erdogan, imekuwa katika sintofahamu na US kwa muda
Tukio la Khashoggi linaiweka, Saudia, US na Turkey katika mzozo wa kidiplomasia 'diplomatic row'

Awali mitandao ya usafiri ya US ilionyesha safari za watu 15 waliokodi ndege ya Gulstream
iliyofika Instanbul usiku wa saa 9 siku ya Oktoba 2

Walifikia hotel ya Movenpick na nyingine kisha walielekea ubalozi wa Saudia

Katika kujiandikisha hotelini walisema watakaa siku kadhaa nchini Turkey

Saa 7 Khashoggi aliingia katika ubalozi akimwacha mchumba wake nje na simu na kumtaka kutaarifu mamlaka kama hata toka. Hakutoka na mchumba wake alitoa taarifa serikalini

Baada ya habari kutoka ubalozi wa Saudia umekanusha kuhusika.
Camera za ubalozi zikiondolewa. Hakuna habari za mlango aliotokea Khashoggi

Turkey wametoa cctv za majengo ya jirani zikionyesha Khashoggi akiingia ubalozini, maafisa wakitoa mizigo haraka nyuma ya ubalozi katika mifuko katika magari maalum

Ndege ya Gulfstream iliyoleta wale wageni waliofika saa 9 usiku iliondoka nao mara moja

Turkey wanasema Saudia huenda imemua Khashoggi kupitia watu waliofika na Gulfstream
Marekani inajichanganya kwa kusema inafuatilia na kuwa na mawasiliano na Saudia

Turkey ambayo ni mwanachama wa NATO inasisitiza Saudia imefanya mauaji.

Rais Trump anasema kitendo hakikubaliki bila kusema nini kitafuta. Ingekuwa Iran, tungesikia
Trump ni muasisi wa chuki dhidi ya waandishi 'enemy of the people' na huyu ni wa WAPO

Nchi za Ulaya hasa UK wanakumbukumbu ya kutoka wauaji wa Russia
Marekani ina interest kwa Saudia wakishirikiana na Israel dhidi ya Iran

Ukiyaweka yote kwa pamoja, ni wazi kutoweka kwa Khashoggi kunaweza zua jambo

Tusemezane
 
SAKATA LA JAMAL KHASOGGI LAZIDI KUPAMBA MOTO

TURKEY WADAI KUWA NA SAUTI NA PICHA ZA WATESI

Sakata la Msaudia Jamal limechukua sura mpya huku kukiwa na habari za 'kuuawa' ndani ya ubalozi wa Saudia nchini Turkey

Gazeti moja la Turkey limekariri maafisa wa serikali wakisema wanao mkanda wa maneno na picha katika wakati wa mateso na hitimisho la maisha ya Khasoggi ndani ya Ubalozi
Gazeti limedai baada ya mahojiano, mateso na kuuawa, mwili ulikatwa na mashine za mbao

Turkey inasemekana kushea habari hizo na mataifa mengine ambayo yameanza kuchukua hatua
Mataifa kama UK , Ufaransa na mengine tayari yamechukua hatua dhidi ya Saudia

Taifa kiongozi la US linasita sita kutokana na Rais Trump kuwa na msimamo tofauti. Trump anasema kiasi cha biashara ya silaha kutoka Saudia ni kikubwa mno karibia Bilioni 110

Hata hivyo wachunguzi wanasema kiasi hicho ni mauzo tarajiwa ya silaha katika miaka 10 na si kwa mwaka ambao inakadiriwa kuwa Bilioni 14.

Trump anasema kazi inayofanywa na mkwewe Kushner mash. ya kati inaweza kuingia doa ikiwa US itaitolea macho Saudia

Kushner ni msuluhishi wa mzozo wa mashariki ya kati kati ya Israel na Palestina.
Kwa asili Kushner ni Myahudi na Rafiki mkubwa wa MbS, mfalme wa Saudia

Mabunge ya US, Senate na House wajumbe wake bila kujali itikadi wanaungana kulaani kitendo na kudai hatua zichukuliwe ili kusimamia thamani za kimarekani 'values' kuhusu haki za watu

Msimamo wa mabunge na Rais utaleta mzozo kama ule wa Russia ambapo mabunge yaliazimia kwa pamoja kuiadhibu Russia hata kumlazimisha Rais Trump kufanya hivyo kwa shingo upande

Ushahidi wa sauti na picha unazua utata. Inasemekana, Jamal aliacha simu nje kwa mchumba wake na aliingia na saa ya mkononi iliyonukuu mambo yaliyoendelea

Watesi walibaini hilo hata hivyo hawakuweza kufuta data zilizokuwa zimetumwa

Utata ni kuhusu picha kwa kujua haikuwa rahisi saa ya apple kuchukua vivuli vya watesi

Kama si hivyo, picha inazosema Turkey, imezipata kutoka wapi?
Hapa ndipo inapoonekana huenda kulikuwa na Camera zilizowekwa ndani ya ubalozi

Kama ni hivyo, hilo litakuwa kukiuka sheria za kidiplomasia kwani ubalozi ni 'sehemu ya nchi husika' na kwamba kutenda hilo ni kuingilia unyeti wa taifa jingine kinyume na diplomasia

Kutokana na pressure ya mataifa Saudi imetuma ujumbe utakaofanya kazi na Turkey

Kwa hali ilivyo, Saudia ina pressure kali ya mataifa, US kuna mvutano kati ya Rais na Mabunge.

Turkey inamvutano na Saudia ikiwa haielewani vema na Trump.
Mataifa ya Ulaya yanaingalia Saudia kwa jicho pande.

US wanakumbukumbu ya 9/11 ambapo walipuaji walitoka Saudia.
US inaihitaji Saudi ili kukabiliana na Iran. Israel inaihitaji Saudi kama US

Saudia inaitumainia US kiulinzi ili kukabiliana na wimbi la upinzani wa tawala la kifalme linalojitanda, na ili kukabiliana na kushamiri kwa makundi hasimu

Hili la Khashoggi litazua makubwa hasa kidiplomasia

Tusemezane
 
Asante Mkuu kwa kudadavua mambo haya. Mimi mwenyewe nimeshangazwa na tukio hili; ila nadhani tukio hili lina hila ya Marekani(msisitizo ninadhani). Nitaeleza baadaye baada ya kupitia baadhi ya hoja zako na kuongeza kile na mimi ninachokijua kutoka kwenye vyanzo mbali mabali vya habari juu ya sakata hili na mengine.

Awali mitandao ya usafiri ya US ilionyesha safari za watu 15 waliokodi ndege ya Gulstream
iliyofika Instanbul usiku wa saa 9 siku ya Oktoba 2

Walifikia hotel ya Movenpick na nyingine kisha walielekea ubalozi wa Saudia

Katika kujiandikisha hotelini walisema watakaa siku kadhaa nchini Turkey
Kwa taarifa hii inaonekana kuna ufuatiliaji wa tukio hili kama lilikuwa limepangwa na waliolipanga nikama walikuwa wanahakikisha utekelezaji wake.


Nchi za Ulaya hasa UK wanakumbukumbu ya kutoka wauaji wa Russia
Mkuu hapa ungetusaidia ufafanuzi kidogo. Ni mauaji yapi yale mapigano kati ya Russia na UK miaka ya 1600, ama mauaji yapi. Kama unazungumzia matukio ya karibu na Salisbury basi utakuwa utendi haki; nadhani maelezo yake yatahitaji mjadala mwingine. Ngoja tuendelee na hii ya 'Jamal'
Marekani ina interest kwa Saudia wakishirikiana na Israel dhidi ya Iran
Hii ni sahihi kabisa. Na interest zake si kwa manufaa kwa wasaudia wala ufalme wa saidia. Interest zake ni za win(US)-lose(Saudia).
Kuhsner ni msuluhishi wa mzozo wa mashariki ya kati kati ya Israel na Palestina.
Kwa asili Kuhsner ni Myahudi na Rafiki mkubwa wa MbS, mfalme wa Saudia
asante kwa taarifa juu ya asili ya Kuhsner. Ndiyo maana wamarekani walikaa kimya juu kuteuliwa kwake kama mwandani wa WH. Hata hivyo, Phalestine imekataa usuluhishi wa US (Kushner) kati yake na Israel. Kwa hiyo kuendelee kumtambulisha Kuhsner kama msuluhishi nadhani si sahihi
Ushahidi wa sauti na picha unazua utata. Inasemekana, Jamal aliacha sim nje kwa mchumba wake na aliingia na simu ya mkononi iliyonukuu mambo yaliyoendelea
Nadhani utata haupo. Inasemekana 'Jamal' hakuingia na simu bali aliingia na saa. Saa ambayo ilikuwa 'synchronised' na simu aliyokuwa amemuachia 'mchepuko' wake (Maana alikuwa bado hajamuoa huyo Mturuki wala kumtariki mkewe wa huko Saudia). Saa ndiyo iliyonukuu tukio zima. Na inasemekana watesi walipogundua hilo, waliamua kutumia vidole vya 'Jamal' kuifungua hiyo saa na kisha kufuta baadhi ya matukio.
Kama si hivyo, picha inazosema Turke, imezipata kutoka wapi?
Hapa ndipo inapoonekana huenda kulikuwa na Camera zilizowekwa ndani ya ubalozi
Turkey wanasimamia kwenye hizo kamera za majirani na video na sauti zilizotumwa na saa ya 'Jamal' kwa mchepuko wake uliokuwa umemsubiri nje.
Saudia inaitumainia US kiulinzi ili kukabiliana na wimbi la upinzani wa tawala la kifalme linalojitanda, na ili kukabiliana na kushamiri kwa makundi hasimu
Kwa jinsi US ilivyokwisha kuchukua 'coordinates' zote za nchi ya Saudia ni halali kuwa kwa sasa kusema US ndiye mlizi wa ufalme ule wa Saudia.
=====
Kuhusu 'kudhani' US ana hila na tukio hili.

'Jamal' alikuwa mwandishi wa Washington Post, jarida linaloaminika kuwa 'mouth piece' ya chombo muhimu cha ulinzi cha nchi ya Amerika. KWa vyovyote vile 'Jamal' alikuwa 'liquid asset' wa chombo hiki. Inajulikana kwa vyombo vya ulinzi vya nchi hiyo vilivyojidhatiti katika masuala ya 'Blackmailing/Hypocrisy'.

Kulikuwa na fununu Saudia alikuwa anataka kununua silaha kutoka Russia. Na kutokana na sheria yao US ya mambo ya vikwazo, kitendo cha Saudia kufanya hivyo kingeipa wakati mgumu US kuiwekea vikwazo kwani US ana interest nyingi sana hapo Saudia kama ulivyoeleza. Sasa US wameishagundua kuwa huyu kijana aliyekabidhiwa madaraka ya Saudia ni 'volatile' kunauwezekano wamemtengenezea 'mtego' ili kumdhibiti. Maana na yeye(MBS) ameishagundua kuwa US anaihitaji sana Saudia. Na kunauwezekano atakuwa aliwajibu US isivyo, kuwa msinibabaishe naweza kwenda Russia nikapata silaha bora zaidi.

1539450511598.png


Ndiyo maana nasema kunauwezekano huu mtego ni wa chombo cha usalama cha US. Chombo kimeamua ku' liquidate ' asset yake 'Jamal' ili kumdhibiti MBS. Na kwa kweli kwa hili (MBS) atakuwa amedhibitiwa. Hataweza tena kuamua anachotaka. Hawezi tena kujiamulia kwenda na kutafuta marafiki wenginie. US inaijua Saudia ndani nje, ki-ulinzi Saudia wako 'utupu'. Pia ninadhani ile kauli ya Trump kusema ufalme ule unaweza kusimama wenyewe kwa wiki mbili nadhani ililenga 'kuprovocke' ufalme na ilikuwa inatoa 'go ahead' kwa chombo hicho kufanya kilichofanywa. Ile kauli haikuwa ya kawaida. Kuna jambo lilikuwa limepangwa.

Sijaunga vizuri nukta zangu nikipata muda nitaziweka sawa.
Yangu ni hayo.
 
SAKATA LA JAMAL

Bandiko #10 tulieleza kujiuma uma kwa Rais Trump kuhusu sakata la Jamal Khashoggi anayedaiwa kuuawa ndani ya ubalozi mdogo (consulate) wa Saudia mjini Instambul

Jana Rais Trump akiwa WH kwa ushahidi wa kutosha itakuwepo 'adhabu' kwa Saudi Arabia. Hata hivyo aliendelea kusisitiza biashara ya mauzo ya silaha itaendelea

Alipohojiwa ni 'adhabu' gani hakuweza kueleza bali kurusha swali kwa mshauri wa usalama bw. John Bolton ambaye aligusa gusa bila kuwa na jibu kamili

Swali linabaki, congress itakuwa na hatua gani? Je, ikiidhinisha vikwazo vya biashara itakuwaje!

Hoja inayoisumbua Saudi ni kutoa majibu nini hasa kilitokea. Jamal alitokea mlango gani?
Wale watu 15 walifika kwasababu gani, na ikiwa kuna rekodi za kauli za Jamal nini utetezi

US wanatambua Khashoggi kauawa, hata hivyo masilahi yao 'interest' yanakinzana

US inaitaka Saudi Arabia kimkakati hasa wakati huu wa mtafaruku na Iran
Kuiendea kombo Saudia ni kuweka masilahi yake katika wakati mgumu

Katika mipango mikali ya kijasusi (covert operations) kuna mengi ya kuangalia.
Saudia ipo katika 'radar' ya nchi za magharibi. Usafiri Gulfstream ulifuatiliwa kwa ukaribu

Katika zama za teknolojia ufunguo wa mawasiliano upo nchi za Magharibi
Kuna uwezekano mawasiliano yalinaswa kabla kama inavyoripotiwa na baadhi ya vyombo

Kauli zinaweza kutoa mwanga inapofanyika 'covert operation' mahali popote
Ni moja ya vitu vinavyoweza kufungua operation nzima kutoka ''covert kuwa overt''
Wataalamu wa covert operations huzilinda sana ndimi zao wakizutmia kwa umakini na uangalifu

'Balozi' wa Saudia alitoa kauli mapema ya kukanusha tukio akisema Jamal aliondoka ubalozini

Bila kujua kulikuwa na Camera mbele na nyuma ya jengo, kauli yake inampa wakati mgumu
Jamal alitokea wapi na saa ngapi ikiwa Camera za pande zote zinaonyesha ''activities'' ?
 
Gulf sources maintain that "Jamal Khashoggi was never the loudest critic of the House of Saudi he is widely portrayed as being. In some articles in Western publications, he combined mild criticism with occasional praise for the economic and social reforms introduced by the young crown prince. Therefore, the sensational reporting about Saudi intelligence assassins executing Khashoggi on the orders of MbS should be treated with caution, if not a grain of salt." Such reports may in fact precipitate his murder, if he is still alive. He may even have been the victim of a conspiracy by the crown prince’s rivals inside the royal house to show him in a bad light and torpedo his policies.

Turkish President Tayyip Erdogan loathes the Saudi royal family, and the crown prince in particular, and would not be above capitalizing on a putative Saudi operation against Khashoggi for blackening their name. Who knows what bargaining may be afoot – and between whom – before he makes a surprise appearance? It may be too soon therefore to decide whether the missing journalist is alive or dead.

"It is also possible that certain US and Western undercover agencies, dedicated to the downfall of President Donald Trump", jumped on the Turkish bandwagon to undermine the Saudi crown prince and so stigmatize the Trump administration’s alliance with the Saudi royal house – and Jared Kushner’s friendship with MbS in particular.

Khashoggi case: Vile murder, palace intrigue against crown prince or plot to torpedo US-Saudi ties? - DEBKAfile
===
Bado kuna mambo mengi yanayoweza kusababisha kupotea kwa 'Jamal'. Ni vyema kufuatilia kwa makini kila kauli inayotolewa na kuifanyia tathimini. Kulalia upande mmoja wa taarifa katika jambo hili ni kupunguza nguvu ya kuupata ukweli.
 
PRESSURE INAONGEZEKA KWA SAUDI ARABIA

UK, France na Germany zimetoa kauli zikitaka Saudia kueleza nini imetokea kwa Jamal
Kauli inafuatia mashirika na makampuni kujitoa maonyeshe ya SaudiA mwishoni mwa mwezi

Saudia nayo imejibu kwa kauli ya 'jino kwa jino' ikieleza athari za kiuchumi zinazotoweza kutokea

Saudia ni nchi ya 17 katika uchumi wa dunia, hata hivyo mafuta yake yanaguvu sana
Mafuta yameipa kiburi sana kwani athara za soko la mafuta zinategemea sana nchi hiyo

Saudia imejitahidi sana kutengeneza hadithi, ukweli ni kuwa muda na ushahidi si mshiriki wao

Operesheni inaonekana kuwa na baraka za Riadhi ikiwa imefanywa kipuuzi sana
Kwa upande mwingine ujinga huo unakokota watu wengi akiwemo Rais wa US

Kuna taarifa zinazoelezwa bila uthibitisho kuwa Saudia ipo katika hatua za kukiri kuhusu tukio

Ni jana tu Rais Trump kasema mauaji yanaweza kufanywa na yoyote kama roger killers

Taarifa ya Trump ni kinyume na mazoea ambapo US ilikuwa kiongozi wa mtaifa ya magharibi
Nchi za ulaya kuwa na misimamo yake ni kuiacha US pekee inaeleza jambo

Rais Trump ana vyombo kama CIA vinavyoweza kumpa ukweli wote na si kubahatisha nahatisha

Ikitokea Saudia kutoa taarifa rasmi, tukio hilo litakuwa limemdhalilisha Trump na Marekani

Kwa upande mwingine wa shilingi, iwe ameuawa au la halina athari zozote kwa taswira na haiba ya Rais Trump. Ni Rais ambaye Wamerekani wamemkubali ndivyo alivyo
 
''PRESSURE'' IMEZIDI, JAMAL KHASOGGI NI 'MAREHEMU'

Nchi za Ulaya zimeweka pressure kuhusu uchunguzi wa Jamal Khashoggi anayesadikiwa kuuawa katika ubalozi wa Saudi Arabia uliopo Instanbul , Turkey

Ushahidi unatolewa ,Saudi ya MbS wana deal na 'majeraha' na uharibifu wa ''kifo' cha Jamal.

Kuna uhusiano unaosemwa wa makala za Jamal na Qatar na Saudia

Rais Trump peke yake ndiye anayeamini suala hilo linahitaji uchunguzi.
Akihojiwa na AP Trump alisema mtu anabaki kuwa huru hadi atakapotiwa hatiani

Hili ni katika kujinasua na hoja ya vikwazo dhidi ya Saudi ambayo Congress inafikiria

Inaelezwa kuna 'conflict of interest' za masilahi yake binafsi na Saudi Arabia kibiashara

Taarifa zilizopo ni kuwa 'something went terribly wrong' wakati wa mahojiano ndani ya ubalozi

Inaarifiwa Jamal alikuwa apewe dawa ya usingizi ili asafirishwe, akafariki kabla.
Kilichofuata ni kuukata kata mwili wake vipande vipande chini ya usimamizi wa afisa wa MbS

Rais Trump anasema ameongea na MbS aliyemhakikisha uchunguzi unafanywa kuhusu suala
MbS ''anathibitisha'' lilikuwepo tatizo na kwamba Jamal ni marehemu

Miongoni mwa wale watu 15 waliofika na ndege, yupo mshirika wa karibu wa MbS

Kukiwa na pressure kwa Saudi Arabia kuna pressure kwa Rais Trump kuchukua hatua
Republicans ndani ya Congress hawaridhishwi na kauli za Trump za kujiuma uma

Kwa wanaofuatilia siasa za mataifa hii operation imetia doa Saudi Arabia.
Umuhimu wa Saudia si mafuta bali wenyeji na custodian wa holy land.

Tatizo si mtu kuuawa, bali ilifikiaje hadi kuuawa. Kila nchi ina taratibu zake na si jambo geni

Je kulikuwa na due process? ''Morally and ethically'' ni ipi nafasi ya Saudi Arabia?

Kilichotokea ni kama kisa cha Waziri wa Nigeria, Bw Umar Diko miaka ya 80
Tutaeleza
 
KISA CHA UMAR DIKO NA ''UFANANO'' WA JAMAL KHASHOGGI

Mwaka 1984 aliyekuwa waziri wa usafiri wa Nigeria, Umar Dikko alitekwa mjini London
Bw Dikko alikuwa waziri wa serikali ya Alhaji Shehu Shagari aliyepinduliwa mwaka 1983

Dikko alituhumiwa na serikali ya Nigeria kuiba kiasi cha dollar bilioni moja kutoka serikali

Serikali ya Nigeria kwa kushirikiana na Israel yenye Mossad waliandaa mpango wa kumteka
Akiwa anatembea katika mtaa wa Bayswater jijini London, Dikko alitekwa na kuwekwa katika Van

Gari ilibadilishwa njiani eneo la London Zoo kuelekea uwanja wa Stansted nje kidogo ya London

Ndani ya gari kulikuwa na makachero wa Israel na Nigeria akiwemo Dr aliyetoa dawa ya usingizi kuhakikisha Dikko anakuwa hai kwa muda wote wa safari kutoka UK kwenda Nigeria

Katibu wa Dikko aliona tukio la kutekwa na kutaarifu mamlaka zilizobaini upo mpango wa kumteka kwa lengo la kumrudisha Nigeria.

Dikko alikuwa katika ''vikontena'' na Dr tayari kusafirishwa kama mzigo wa kidiplomasia

Ndege ya Nigeria airways 707 ilikuwepo uwanjani jambo lisilo la kawaida tena kuchukua mzigo mdogo uliodaiwa ni nyaraka za kidiplomasia

Watumishi wa uhamiaji walishtuka kuona mzigo hauna alama za kuonyesha ni wa kidiplomasia
Kukawa na wasi wasi juu ya mzigo huo na kuweka ugumu wa kuukagua, ni wa diplomasia

Mfanyakazi mmoja alishtuka kuona kuna watu ndani akapiga simu Polisi ambao walilazimisha kufunguliwa kwa mzigo uliokuwa tayari unaingizwa katika ndege.

Hapo wakamkuta Dikko akiwa na Dr bila fahamu. Wahusika walikamatwa na kufungwa UK

Makosa yalifanyika kidogo na kutibua operation nzima.

Uwepo wa dege la Nigeria 707 halikuwa jambo la kawaida. Dege lilichelewa bila sababu za kueleweka.Mzigo haukuandaliwa kama wa diplomasia na kuzua maswali yaliyotibua mpango

Ukiangalia hayo kwa ufupi sana, ukalinganisha na tukio la Turkey kuna uhusiano fulani
MbS na uhusiano mzuri sana na Israel. Hata kama hawakuhusika pengine walichora ramani

Kama ni kweli Jamal alifariki kutokana na 'makosa' pengine ya afya, pengine alitakiwa kusafirishwa kama Dikko

Tusemezane
 
Kwenye sakata la Khashoggi Saudia wameshikwa pabaya sana.

Mpaka sasa Uturuki wameonyesha ushahidi wa CCTV footage bwana Khashogi akiingia ubalozi wa Saudia siku ya mwisho kwake kuonekana. CCTV za airport zimewanasa raia wa Saudia wanaoshukiwa kuhusika na upoteaji wa Khashoggi wakiingia nchini uturuki. Pia muda mchache kabla ya wachunguzi wa Uturuki kuingia ubalozi wa Saudia camera zimewanasa kampuni ya usafi ikiingia ubalozi humu na inashukiwa walienda kwa kazi ya "kusafisha" ushahidi... Na baada ya kuruhusiwa kuingia ndani ya ubalozi wameripoti kuona baadhi ya vyumba vikiwa vimepakwa rangi upya hivi karibuni huku kukiwa na dalili za kufanyika usafi usio wa kawaida...
 
Mkuu Mwalimu
Hili suala lilikwisha mapema sana. Jamal alipoingia hakutoka na Saudi consulate hawakuwa na maelezo. Hawakujua kuna ushahidi wa kutosha ambao kila uchao unatolewa

Inaripotiwa kuwa Pompeo kamweleza MbS achukue dhamana ya suala zima, ni mbaya

Trump anawahadaa wasiojua au kufuatilia siasa za dunia hii,weledi wanamuona mtupu
conspiracy au theory zote ni ubutu wa weledi wa current affairs, ililikuwa wazi toka siku ya kwanza.

Hata hivyo Trump ni mjanja, ana deal binafsi za biashara na Saudi Arabia
Kinacho mkwaza si ushahidi, ni namna gani atawatosa Saudi bila kuathiri biashara zake binafsi

Congress na Republicans wanamtaka asimamie values za nchi yao na si trade ya silaha
 
Pompeo stressed to Saudi Crown Prince his future as king is at stake, source says
From CNN's Jamie Gangel

627ee08e-9fea-453b-acbf-9b2dd3843353.jpg


A source familiar with the meeting between Secretary of State Mike Pompeo and Crown Prince Mohammed bin Salman on Tuesday tells CNN that the smiling photo-op should not be read as to indicate the meeting was friendly. The source said the smiles ended at the end of the photo op. Pompeo told the crown prince in no uncertain terms that he had to own the situation and that every fact is going to get out and he must own it, the source said.

The source said Pompeo also made it clear to the crown prince that the Saudis had to get their investigation done very quickly. Pompeo stressed that time is short and that the Saudis have to deal with the people involved sharply, the source said. Pompeo went on to tell the crown prince bluntly that if they don't, the US will have to deal with this. Pompeo told the crown prince the US will take action because the world will demand it and that President Trump’s hand will be forced by the global pressure. Pompeo told the crown prince he had to own what happened and that even if the crown prince didn't know about it beforehand, he has to own it. Pompeo stressed to the crown prince that his future as king is at stake.

The source did not describe how the crown prince or the Saudis reacted but said the message had been received.
The source said the proof will be in what action the Saudis take, when asked if Pompeo felt crown prince would do anything.
======
Maelezo ya Pompeo yana vimelea vya 'Blackmailing' nilivyokuwa na vihisi. Pompeo yeye naye ni mmoja wa familia ya Ufalme wa Saudia? Anatoa wapi mamlaka ya kuelezea nani awe ama asiwe mfalme kwenye utawala wa Saudia? Binafsi naona hili haliko sawa na linazidi kuashiria kuwa vimelea vya 'blackmailing' siyo myth bali vyaweza kuwa reality. Mambo yatajulikana tu.
 
Back
Top Bottom