Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,189
Nchi nyingi za kiarabu zikiongozwa na Saudi Arabia, zikiwemo Misri, UAE, Bahrain, Yemen, Libya, Maldives na Libya, pamoja na Morocco na Mauritania, zimevunja uhusiano na Nchi ya Qatar tangu tarehe 5.06.2017 kufuatia tuhuma kuwa Qatar imekuwa ikifadhiri vikundi vya kigaidi vikiwemo ISIS na vyenye msimamo mkali vikiwemo Hamas, Muslim Brotherhood na Houth.
Hata hivyo Serikali ya Saudia mnamo tarehe 7.06.2017, imetoa masharti kwa Qatar kubadilisha sera zake zinazounga mkono vikundi vinavyotuhumiwa kwa ugaidi vikiwemo Hamas na Muslim Brotherhood. Hali hiyo imesababisha lawama kuwa kutoka kwa Hamas. Aidha maandamano ya raia wa Mauritania yalifanyika kwenye ubalozi wa Qatar Mjini Nouakchott Mauritania.
Kwa jinsi mchezo huo unavyoenda, utasababisha waislamu kuchukizwa na Nchi hizo ambazo zinaonekana kutumiwa na Marekani kupambana na Nchi za kiislamu hasa Iran.