Mgogoro wa muafaka wa umeya arusha, hili ni jaribio kwa chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa muafaka wa umeya arusha, hili ni jaribio kwa chadema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nakei, Jul 8, 2011.

 1. N

  Nakei Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 10, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Inawezekana kabisa kulikuwa na mawasiliano kati ya madiwani wa CHADEMA na uongozi wa juu. Inavyoonekana uongozi wa CHADEMA umeona jinsi hili suala lilivyopokelewa na watu ndio wakaamua kutumia busara jinsi ya kuli solve. Watu wengi wameona sio busara kuwa na muafaka kwa sababu ya damu iliyomwagika lakini pia mitazamo ya watu ni kwamba shida ya CHADEMA ilikuwa ni madaraka ndio maana walipopewa unaibu meya wakaamua kukubali muafaka. Kwa maoni yangu, maamuzi yaliyochukuliwa na madiwani wa CHADEMA yana pande mbili:-

  UPANDE WA KWANZA
  Wanapata pressure kubwa kutoka kwa wananchi kuhusu utekelezaji wa ahadi walizotoa wakati wa kampeni, kwahiyo ili kutekeleza hili inabidi wafanye kazi pamoja kama team(CHADEMA na CCM) ili kutatua matatizo ya wananchi. Kuleta maendeleo kwa wananchi ndio lengo pia la baadhi ya viongozi wa juu wa CHADEMA ndio maana labda wakashiriki kwenye muafaka katika zile hatua za mwanzo, na kwa sababu mapokeo ya muafaka hayakuwa mazuri viongozi wa juu wameamua kutumia busara ili kufanya hali ya hewa iwe shwari. Kuunda tume ya kuchunguza hili suala ni hekima kubwa sana.

  UPANDE WA PILI
  Viongozi wa CHADEMA wameona upepo wa kisiasa sio mzuri kwa kukubali muafaka, kwahiyo walipigwa na butwaa kuona jinsi wananchi walivyopokea hili suala la muafaka. Njia ya kwanza ni uongozi kuchukua maamuzi magumu kwa kukataa kwamba hawajashirikishwa alafu kuunda tume ambayo italeta mapendekezo ili uamuzi uchukuliwe, hapa viongozi wa juu watakuwa wameshatulia na kutoa maamuzi yenye busara.


  MAONI YANGU:
  Huu muafaka ukitekelezwa CHADEMA watajiweka kwenye nafasi nzuri ya kuelekeza mawazo yao katika suala la maendeleo ya mji wa Arusha na kutekeleza ahadi walizotoa katika kampeni. Wakiendelea kupambana kisiasa katika hili suala muda utaenda na watajikuta hawajafanya lolote katika kipindi cha miaka mitano. Agenda kubwa kwa madiwani wa chadema na uongozi wa chadema sio maendeleo bali ni mapambano ya kisiasa ambayo hatimaye wananchi watayachoka(ukisikiliza wimbo mmoja kila siku unauchoka). Sasa CHADEMA mna kila sababu ya kubadili wimbo.
   
 2. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  ndugu mbona maelezo yako yana 'labda labda' nyingi? Yaelekea basi huna uhakika na unachokiandika! Time will tell what happened,let's wait and our eyez will be our witness
   
Loading...