Mgogoro wa Mtibwa na siasa za zima moto

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Kuna watanzania wengi sana wanaonewa na kunyanyaswa na wawekezaji kutokana na wawekezaji kubebwa na watawala.

Katika hali ya kawaida, siyo kawaida mtu aende nchi ya ugenini halafu akawafanyie dhihaka wenyeji wake pasipo kuwa na sehemu ya kujikinga vinginevyo lazima atafukuzwa ama kufungwa bila kupoteza muda.

Masharti ya kupewa visa katika nchi yeyote ni pamoja na kuheshimu sheria za nchi unayotembelea, na ni nadra kero za mgeni mmoja kusubiri rais wa nchi ndiye azishughulikie, kuna idara ya uhamiaji, kuna idara za kazi na kuna mkuu wa wilaya ama mkoa ambaye anatarajiwa atatue matatizo haya madogo madogo, kama rais ndiye atatemewa kusuruhisha migogoro ya aina hii basi kuna tatizo kubwa sana la kiutendaji na tuna kazi ya kufika tunakokwenda.

Wananchi wa Mtibwa wamenyanyaswa na meneja yule kwa miaka sasa mbele ya watoto, watawala wao na mizimu ya watawala wao bila hata watawala kuonyesha dalili za kuishughulikia kero ile. Kwa sababu watawala sasa wanawahitaji wakulima masikini wale wameondolewa shetani yule ambaye nina imani atarudi (kama siyo yeye basi mdogo au kaka yake) tarehe 1 December 2010 mara baada ya watawala kumaliza shida yao ya sasa na atakaa kwa raha mstarehe akifidishia muda ambao hakuwepo (wakati wa kampeni).

Njia pekee ya kuhakikisha wageni wa namna hii hawarudi kamwe ni kuitoa serikali iliyoko madarakani ili wakae pembeni wajifunze kama ambavyo wenzao wa Kenya, Malawi, Zambia, Japan, n.k walivyofanya na wajipange upya wakiwa kama wapinzani.

Hatutaki watawala wanao sikiliza/tatua kero zetu wakati wa kampeni tu na miaka inayobaki wanatuacha kama watoto yatima huku wakigawana rasimali na uridhi wetu na wageni (wawekezaji) bila hata chembe ya aibu.
 
Mkuu upo sahihi kabisa, hawa watawala wamekuwa ni matapishi kabisa, kwa ujumla wawekezaji ambao tumeambiwa na Mkwere kuwa tusiwasumbue wamekuwa wanyanyasaji wakubwa wa watanzania, ni kama ka ukoloni fulani hivi, wananchi wanafahamu mambo mengi kuhusu uozo huu, lakini ni wapi pa kwenda kulalamika?

Ni sawa na kupeka kesi ya mbuzi kwa fisi. Nilisikia bado kesi ya mkurugenzi moja kaburu wa kampuni moja ya uchimbaji wa tanzanite inazungushwa toka mwanzoni mwa mwaka huu. Inadaiwa alitukana wafanyakazi wake kwenye kikao ikiwa ni pamoja kuwanyanyasa kwa mda mrefu, wafanyakazi ambao kimsingi walimfungulia mashtaka. Tetesi zinasema bado serikali inamkingia kifua. Sijui hawa wananchi wasubiri ujio wa Kikwete kwenye mikutano yake ya kampeni ndipo wamweleze?

TUFANYE MAAMUZI SAHIHI SASA ILI MAMBO YAISHE. MABADILIKO NI SASA AMKENI.
 
Usishangae kusikia Rais amamemfukuza nchini katika ziara zake za kampeni!
 
habari kwa hisani ya mtandao wa wavuti!!

08/09/2010

Serikali imemfukuza kazi aliyekuwa Meneja Mkuu wa kiwanda cha kutengeneza sukari cha Mtibwa kilichopo mkoani Morogoro, kutokana na malalamiko aliyoyapokea kutoka kwa wananchi dhidi ya meneja huyo ya kutumia lugha chafu za matusi na za kudhalilisha wananchi, hasa waajiriwa.

Kufutwa kazi kwa Meneja huyo ambaye ni raia wa Afrika Kusini, kumetokea baada ya Raisi Jakaya Kikwete kufika Turiani, Mtibwa mkoani Morogoro akiwa katika mikutano yake ya kampeni, ambapo alielezwa na Wananchi kero na matatizo yanayowakabili dhidi ya uongozi wa Kiwanda hicho.

Raisi Kikwete amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Fatma Mwasa, kukutana na makundi yanayohusika yakiwemo ya menejimenti na ya wakulima wa miwa.

Source: WAVUTI
 
Back
Top Bottom