Mgogoro wa matumizi ya maji mto Nile wachukua sura mpya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa matumizi ya maji mto Nile wachukua sura mpya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by M-bongotz, May 17, 2010.

 1. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Lile sakata la muda mrefu juu ya matumizi ya maji ya mto Nile baina ya Misri na Sudan dhidi ya nchi za maziwa makuu limeendelea kuchukua sura mpya baada ya nchi tano za maziwa makuu ikiwemo Tanzania kusaini mkataba mpya wa matumizi ya maji ya mto huo unaolenga pia kuanzisha taasisi moja itakayoratibu matumizi ya maji ya mto Nile na wakati huohuo nchi ya Misri ikitoa msimamo kuwa itatumia nguvu za kijeshi ili kulinda monopoly yake ya matumizi ya maji hayo iliyotokana na mkataba uliosainiwa na kuratibiwa na serikali ya kikoloni tarehe 7 Mei 1929.
  Kinachonishangaza ni kwamba hawa wamisri wana akili timamu kweli kutaka kuhodhi matumizi ya maji ambayo chanzo chake ni katika nchi hizi za maziwa makuu, hata kama wao wana matumizi nayo zaidi hawaoni kuwa maji ni resource muhimu sana kwa uhai wa kila kiumbe, au wao ndio wanajiona viumbe bora zaidi?.,kweli sisi tufe kwa ukame wakati maji yanatiririka kwetu yakielekea Misri na Sudan, si itakuwa ni uzembe wetu wenyewe?.,nionavyo mimi kama ni vitani twende tu maana naamini nchi zote tano zitaungana dhidi ya Misri na Sudan na hapo ndipo watakapojua kuwa pamoja na unyonge wetu, tunaweza kusimama pamoja na kutetea maslahi yetu.
   
 2. jossey1979

  jossey1979 Senior Member

  #2
  May 17, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  I think there is a better way to resolve this rather than going to War. In my Opinion we would rather thirst than going to war. Ni wazo langu tu
   
 3. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Uko sahihi mkuu, Waarabu kwa vita ni hatari sana, sisi watanzani tusijidanganye kuwa tunaweza kupigana vita na Misri, tutapigwa
  hapa mpaka tutajua kama chura kachutama au kachechemea!!!!
   
 4. M

  Mtata Member

  #4
  May 18, 2010
  Joined: Jan 3, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watabiri wanasema vita kuu ya tatu ya Dunia itakuwa ya kugombania maji!
  Sasa kwa nyie ambao mnasema bora tukae bila maji, hamjayakosa! Ukiyakosa hautasema hayo. Maji ni uhai, kuna haja gani ya kufa kwa kiu, bora uyanywe halafu kama ni vita tutajua baadae, vita ni vita mura na haina mwenyewe!
   
 5. Maverick

  Maverick JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2010
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 308
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mie nadhani kuna haja ya kuwa na haki sawa ya kutumia maji haya. Kama kweli wamisri wana shida kubwa sana na maji inabidi wawe wanyenyekevu kwetu.
   
 6. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  .

  Kwa maoni yangu mimi hizo nchi 5 katu hazina ubavu hata zikiungana zidi ya Misri. Me nadhani tutumie lugha nyepesi watatuelewa tu!. Kuna vitu vya kuviangalia unapotaka kupima uwezo wa nchi kijeshi, kwanza angalia uchumi wa nchi hiyo, halafu linganisha na nchi yako. Pili angali nani adui wa nchi hiyo, hakuna ubishi maandalizi ya jeshi la misri ni zidi ya Israil. Inamana nguvu za jeshi la Misri ziko sambamba na Israil, hatuwawezi waarabu katu. Huyo Marekani hawavai waarabu bila kuishikisha dunia.
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  wale waliokuwa wanamsaidia Amini kutoka libya walikuwa ni watu gani?
   
 8. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2010
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  BinMgen umeongea point kubwa sana, ni bora ulivyowajulisha watu hapa jamvini......wengi wanashabikia tu. hawajui HALI HALISI kama ulivyoeleza
   
 9. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Watumie kwanza maji walio nayo ndo waende nile mf Tz mto rufiji upo hapo hakuna lolote una tiririsha maji kwenda baharini bila kutumiwa, kwani nini msianza na hayo ndo muende mto nile?msikute kuna shinikizo hapa kwa maslahi ya watu,tuwe macho jamani
   
 10. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana na wewe, tunaweza kutumia maji ya mto Rufiji na mingineyo kunufaisha watanzania wanaoishi maeneo ya karib na mito hiyo mfano kwa huduma ya maji safi, umwagiliaji n.k lakini hebu fikiria wananchi wa mikoa inayozunguka ziwa Victoria wanawezaje kufaidi maji ya mto Rufiji, Pangani, Wami, Ruvu, Ruaha n.k, tunaweza kuzalisha umeme sawa na ukawafikia, lakini watatumiaje maji hayo kwa umwagiliaji?.,fikiria na gharama ya kuyafikisha maji hayo katika mikoa hiyo?.,sasa kwanini tuache wananchi wetu wafe kwa ukame wakati tuna uwezo wa kutumia maji ya mto Nile ambao moja ya chanzo chake kipo katika ukanda wetu?.,kweli tuzubae tu wamisri na wasudan waneemeke eti kisa sisi tunaogopa kupambana na waarabu?.,wanaweza kutushinda kwa nguvu za kijeshi lakini unadhani ni haki kweli kukumbatia mkataba wa kikoloni unaowamilikisha wao matumizi ya maji ya mto huo, eti yeyote anaetaka kuingilia matumizi ya maji hayo shurti aombe ruhusa ya Misri, huku kama si kuendeleza ukoloni ni nini?..
  Mimi naunga mkono juhudi za serikali za nchi za maziwa makuu katika kutafuta haki yao, napinga vikali sana huo ukoloni wa Misri.,maji haya ni rasilimali tuliyobarikiwa kuwa nayo ambayo ni lazima yanufaishe wote waliobahatika kuwa karibu na mto huo na ningependa jumuia za kimataifa zikaingilia kati mgogoro huu ili haki ya kila mmoja itambuliwe.
  Kumbuka kuwa kufa na kiu baharini ni uzembe wako.....
   
 11. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Siajuona hu mkataba unasemaje? Mwenye copy au pa kuupata tafadhali naomba au kama kuna dondoo za mkataba kipi nchi za maziwa makuu wanatakiwa kunufaika nacho na kipi wanakatazwa na hao Misri na Sudan wananufaika na nini na ni nini limitation yao kwenye matuzmizi ya maji hayo
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  May 18, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Huo mkataba walifanya na Tanganyika. Waende waidai Tanganyika kwani sasa kuna Tanzania.

  Egypt wanapigika kirahisi. Ukitaka uwape ONYO mapema kuwa wasikuvamie basi ni kuzidisha uhusiano wa karibu na Izrael. Wayahudi wakija kwa wingi Tanzania na kuwekeza mali zao na ikibidi ndiyo wawe wasimamizi wa kuchukua maji ya Ziwa Nyanza (Victoria) basi na tuone Egypt ikija kushambulia kama wana ubavu. Pia hiyo inabidi ifanyike Kenya na Uganda.

  Waarabu kwa vita Mayai sana wale. Sema tu wana vifaa vingi kutoka USA. Watakachofanya sanasana ni kuja na ndege kurusha mabomu na kukimbia. Wakisema wavamie basi lazima wafahamu kuwa huku siyo jangwani. Misitu ya Sikonge tunaifahamu sana wenyewe. Wakivamia tutawaruhusu tu waingie na wakishaingia tutawatengenezea vita ya msituni hadi wenyewe wakome. Na kama wanafikiri kuja kupigana Kenya, Tanzania na Uganda ni rahisi basi acha waje. Lazima wafahamu kuna akina Kagame na Museven huku, watawatandika kama watoto wadogo.

  Ila nakubaliana na wote kuwa VITA si kitu kizuri na hakuna vita ya bei RAHISI.
   
 13. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kwa mida kama hii ndo huwa nasapoti vita, kwasababu sipendi kutawaliwa hata siku moja. To tell you, kati ya makosa makubwa kuliko yote ambayo misri watafanya, ni kuanzisha vita dhidi yetu...I tell you, they will regret it...kwasababu sasahivi tunawagwaya kwasababu tunaona wao kama ni rafiki zetu, wakileta za kuleta tukawaona kama maadui zetu hapo ndo tutatumia kabisaa bila hata consultation nao...ethiopia wamesema kuwa wako tayari kwa vita and the egyptians are welcome for that....hivi unafikiri mtu kupigwa vitani ni rahisi? si rahisi hata siku moja...uganda tu hapo wamechemsha kwa LRA tu miaka yote hii, misri hawana uwezo wa kupigana vita na nchi zote hizi, si rahisi kabisa i tell you, we are not that infat you know....waulize marekani kama wanapenda tena kwenda mogadishu...., and somalia doesn't have any airforce...

  Misri haina uwezo mkubwa wa kipesa hata hivyo, the moment wakiingia kwenye vita, uchumi wao utatetereka sana, and remember, wakiingia vitani, basi itabidi miaka yooote mia ijayo wawe wanaweka majeshi yao kulinda vyanzo vya maji kama wanajeshi wa marekani walivyo iraq, afghan etc, hivyo itabidi waje wamonopolise baadhi ya mikoa ndani ya nchi hizi ili waweke majeshi yao ya ulizi maisha yao yote kitu ambacho hawana uwezo huo...

  kwani wakitupiga, wakaondoka, si tutaanza kutumia tena wakiondoka, ndo maana itabidi wakae hapahapa nchini miaka yote. THE ONLY REMEDY MISRI WANAYO, ni kupiga kampeni nchi za kiarabu ili watunyime mafuta kama alivyofanya gadafi, hiyo ndo itatupatapata, ila wakija kwa military operation, watachemsha na ndo tutatumia maji kwa uhuru zaidi...hapo itakuwa ni kupambana ili kuikomboa nchi toka kwenye ukoloni wa wamisri, and we need to do that. wakati mwingine vita ni muhimu/necessary...so let them come and they will regret it. waanzie ethiopia, waje uganda, waende rwanda, waje tz, Burundi and kenya are betrayers, they are coward, hawana lolote, ndo maana hawajasain, na wasubirie tz itakapokataa kushirikiana nao pia kwenye mambo yao binafsi.
   
 14. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  you are out of your mind, misri hawana uwezo wa kujilinganisha na Israel, hata waarabu wooote wajiunge, hawana uwezo wa kujilinganisha na Israel...madrasa imekudanganya. israel walipokuwa wanawapiga wamisri pamoja na uwingi wa jeshi lao, walikuwa hawamalizi hata wiki, wameshawa drive away mbali kabisa...hahaha., uchumi wa misri si mzuri hata kidogo, google sasaivi uone uchumi wao wa kupigana vita miaka mingi kama wanao...pili, si rahisi kuingia kupiga nchi, nchi hizi si vitoto vidogo kiasi hicho, tatizo tunao watu wanaotawaliwa na waarabu kwenye akili zao, wanaowaabudu ndo maana chochote anachosema mwarabu wanaona kikuuubwa....
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mfano mzuri ni vita ya 1979 ambapo waarabu kibao walitekwa nyara na majeshi yetu huko uganda. Lakini la muhimu hapa ni lazima nchi za maziwa makuu ziweke msimamo wa kuwa huru kutumia rasilimali maji ya ziwa victoria bila bugdha ya waarabu hao. Mkataba wa mwaka 1929 na 1959 kati ya waingereza na wamisri haituhusu kabisa kwani Tanzania siyo uingereza...kama wanataka wakadai waingereza.

  Kama mkuu Sikonge ulivyosema kama kweli wanataka kuleta nyodo ni wakati muafaka wa kuwakaribisha waisrael na kuwapa miradi ya mashamba makubwa ya umwagiliaji kule shinyanga na kwingineko na watumie maji kutoka ziwani. Hiyo ni mbinu tosha ya kuwanyamazisha kwani wanamjua muisrael ni nani na tayari waliingia mkataba wa kutopigana vita.

  Kingine ni kwamba kama waking'ang'ana bado tuna uwezo wa kupambana nao bwana!! najua tutaomba misaada ya wanajeshi na vifaa kutoka sehemu mbali mbali lakini kwa vita ya ardhini tunawamudu sana. Tukipata S-300 air defence systems kama 5 tu kwa ajili ya kutungua vindege vyao basi wamekwisha.
   
 16. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  mkataba wenyewe waliuingia na wakoloni, hawakuingia na sisi, ukoloni haujawa justified kuwa kilikuwa ni kitu kizuri, wakoloni walikuwa wezi waliokuja kuiba raslimali zetu na kututawala sisi bila kupenda, we were under duress kutawaliwa, hivyo mkataba wowote walioingia nao ni illegal kwa wale wanaojua law of contract, hivyo waliingia mkataba na waingereza, sio na sisi. we are not bound by that contract.

  ni vigumu sana, na hawana vyombo vizuri vya kuja na ndege kudondosha mabom na kukimbia kwasababu si tutazitungua, hiyo hatuhitaji utaalam sana...pia, wakija kwa vita ya ardhini, ni vigumu sana kupiga kuanzia nchi moja hadi nyingine, uwezo, pesa, silaha, etc hawana...wasitutishe, waje kwa adabu tu wakiomba msaada pengine tutawafikiria, ila wakija kwa kutuamrisha na kututisha kama sisi ni mabwege, kwakweli tunatakiwa kukubali tu vita ije...tutaikomboa nchi yetu kama wakija...na vita si siku zote ni dhambi....
   
 17. M

  Magezi JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mkuu hata wakitunyima mafuta waarabu tutachukua Nigeria, Angola na kwingineko duniani.
   
 18. M

  Magezi JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Edward lowasa aliweza kujenga mradi wa maji wa shinyanga kutoka ziwani chini ya Mkapa sasa sijui mkwere kama ata waogopa waarabu kwa sababu ya dini.
   
 19. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #19
  May 18, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  oh yes, na Uganda wanachimba mafuta, angola pia..na sisi ndo tutapata akili ya kutafuta mafuta na vyanzo vingine vya power sasa. actually, hiyo ndo njia pekee watakayotumia kusolve hii kitu, hawana uwezo kwenda vitani mimi ninavyofikiri, nchi nyingi sana hizi tena zina uchungu na hili jambo so si rahisi kuwapiga, hata wakitunyong'onyeza kabisa, bado tutajitahidi kuamka kupambana tena, itakuwa ni sawan a kipindi cha ukoloni, na kama walivyo sema wengine, watakuwa wamejiweka kuwa maadui zwtu wa milele sasa.
   
 20. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  that is why tunahitaji watu kama lowasa, na si ajabu ndo maana alipigwa mtama kwa mitego ili anase aondolewe kwasababu waarabu walimwambia mkwere amuondoe mtu huyo kwasababu ni mtu hatari kwao...this is obvious.
   
Loading...