kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,991
- 17,888
Asallam alyekum/shalom wapendwa
Kwanza nianze kumshukuru mungu kila siku anatubariki njia na mawazo mapya ya maisha na teknolojia mbalimbali.
.
.
Kumekua na mgogoro wa kibiashara kati ya marekani na China muda mrefu..mgogoro huu umestafidi sana toka rais Trump alipoingia madarakani
.
.
Wote ni mashahidi mnakumbuka jinsi marekani wakati wa kampeni alivyoahidi kuibana China endapo angeshinda
.
.
Jee sababu zote hizo ninini?
Sababu kubwa naweza kusema ni chuki,kiburi,na wivu wa marekani dhidi ya kasi ya maendeleo na kukua kwa china...
.
.
Wote tunashuhudia maendeleo makubwa ya kiuchumi,kijamii na kisiasa inayopiga china hatua zinazoifanya Washington ijitafakari sana
.
.
Hofu ya Washington ninini?
Hofu ya marekani ni kuwa wanaiogopa china itawapiku kwa kila kitu hatimaye kuwa super power mpya duniani
.
.
Lakini naweza kukiri kitu kimoja kwamba Beijing imeiacha mbali Washington kwa ushawishi kwa sasa kiuchumi hususan katika nchi za dunia ya tatu mfano Africa na America ya kusini (latini)
.
.
Vita vya kibiashara kati ya marekani na China kampuni kubwa ya Huawei imepata pigo kubwa baada ya marekani kuanza kuishughulikia kampuni hiyo ya kichina kwa tuhuma ambayo ni za kushangaza...wote mnajua kuwa huawei ni kampuni iliyoongoza kwa mauzo ya simu duniani ikizipiku ,apple,lg,google nk
.
.
Ndipo marekani ilipoanza figisu za kutaka kuiangusha kampuni hii huku makampuni ya teknolojia kama google,facebook,instagram wakipiga marufuku huawei kutumia apps na teknolojia yao..Jee huawei itashinda hili jambo?Yetu macho....
.
.
Tuhuma ambazo Washington inaishutumu china ni kuwa anaiba teknolojia.Tuseme ukweli jee ni nchi gani iliyoendelea ambayo haitumii au kucopy au kupambana teknolojia kutoka nchi nyingine?
.
.
Ukifatilia historia ya marekani wakati wa vita vya pili utagundua teknolojia nyingi za kijeshi waliiba,kucopy na kutoa kwa manazi wa ujerumani wakati huo
.
.
Suala la China kucopy teknolojia sio la ajabu wala kushangaza madhali ni jambo zuri la maendeleo basi sioni tatizo...laiti na nchi za africa zingalikua na uwezo hata wa kucopy au kuiba teknolojia kama china basi tungelikua mbali mno
.
.
Kwanini nasimama na China???
Katika hii vita ya biashara kati ya China na marekani nasimama na china dhidi ya marekani kwasababu zifuatazo:--
.
.
1.China ndo ameifanya Africa tuwe walau hapa tulipo leo, mfano bila China sisi africa tusingekua na uwezo wa kumiliki bidhaa nyingi za kiteknolojia ambazo kwa dunia ya magharibi na bei zao ni ghali mno...mfano simu kama sio China tungeweza kumiliki?Tv,redio,magari,s imu,computer,na vinginevyo vingi tusingeweza kuvimudu kama sio china maana china wanajitahidi kuwa na bidhaa na vitu vya bei nafuu...
.
.
2.China amesaidia kuleta ushindani na kuleta ahueni ya bei za bidhaa dunuani:Uwepo wa bidhaa za china unazoshindana na za magharibi umezifanya nchi na makampuni kushusha bei ya bidhaa au bidhaa zao kuwa katika affordable price ambayo inawezesha watu wengi kuwa navyo..
Nawaambia ukweli kama sio China hata hizi simu tunazotumia zingekua zinatoka magharibi tu tungeuziwa bei kubwa na tusingemudu kununua na zingekuja na masharti kibao.
.
.
3.China kama rafiki wa kweli wa wa tanzania:Nikiri kuwa china alikua rafiki wa kweli wa tanzania hususan kipindi cha baba wa taifa reli ya Tazara,kujenga viwanda nchini wakati wa ujamaa,uungaji mkono wa hali na mali katika vita ya kagera...tukumbuke kipindi hicho china alikua rafiki wa dhati kwa wakati ule na pia alikua ni hali duni ya uchumi ya kiuchumi iliyofanana na sisi lakini ajikiongoja hivyo hivyo akatusaidia.Lakini utawala wa ccm ulishindwa kuendeleza viwanda vile au kuvibinafsisha na kuendelea kuvisimamia kwa umakini kwa ubia na private sector leo tungekua mbali.
.
.
4.Mikopo na misaada na ushirika wa kiuchumi toka China:Nikiri tunamuhitaji china sana katika kipindi hichi hususan tukipambana tufikie uchumi wa kati...Tunahitaji support kubwa sana kutoka china..wengi mnajua kidemografia china ni nchi yenye watu zaidi ya milioni 1600...Idadi kubwa ya watu ni fursa kubwa kwetu sisi kuuza bidhaa zetu china na kuleta wawekezaji wa kutosha..
.
.
Kisiasa na kijamii
Kuna maneno mengi yanazungumzwa kuwa China inawalinda madikteta Africa hili ni jambo lina ukweli lakini pia Washington inawalinda madikteta tena nchi zenye rasilimali..au madikteta wa kistatejia wa kulinda maslah yao mfano nchi jirani hapo...na nchi za kidikteta zinazolindwa na marekani ni nyingi mfano Saudi arabia...
.
.
Nikiri jambo moja kuwa tunazihitaji both side west na china....likija suala la democracy na utawala bora tunahitaji sapoti kutoka marekani na nchi za magharibi maana Africa bado tuna safari ndefu sana....
.
.
HITIMISHO LENYE MANENO YA KUTILIA MANANI
-Tunalia mikopo ya China hailipiki jee mikopo ya IMF na WB ndo inalipika??Jibu ni kuwa mikopo yote si mizuri ila wb na imf ni mibaya sana. Halafu pia tunafeli kuifanyia mikopo kinachostahili kwasababu ya watawala wa africa wengi wao hawatumii bongo zao kufikiri wanatumia sifa na ulimbukeni wa kufanya miradi isiyoweza kulipa deni na isiyokua na tija na wengine wanafanya miradi mikubwa tu ili washinde chaguzi
Mfano misaada inayotolewa ingelikua inagusa miradi kwa 100% au kwa wananchi kwa 100% tungekua mbali na sio tegemezi tena..mfano nchi nyingi za Africa pesa ya misaada inaliwa kuanzia kwa mkuu,mawaziri,wabunge,mikoa wilaya mpaka watendaji wa chini mpaka ifike kumgusa mwananchi wa kawaida inabaki 30% huku 70% ya pesa ikiishia kudonolewa huko kote inapita ikidonolewa kidogo kidogo halafu mnataraji misaada au mikopo itatusaidia?
.
.
Tunahitaji pande zote ili kufikia mbali kimaendeleo...suala la kusema tumuache mchina halifai tuende na marekani tu?hapana marekani si yule anayetoa msaada kwa masharti ya ajabu ajabu mfano ushoga na usagaji?...Tukiegemea upande mmoja hatuwezi tukasonga mbele...Tunahitaji yote hayo hususan china kwa sasa ndo maana nasimama na china
Imeandikwa na Ridhiwani Kimaro (kimsboy)