Mgogoro wa Madiwani wa CHADEMA Arusha: Lema anahusika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro wa Madiwani wa CHADEMA Arusha: Lema anahusika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngongo, Jul 4, 2011.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Katika hali ya kushangaza tume inayochunguza muafaka baina ya madiwani wa CCM na CHADEMA imegundua mbunge wa Arusha mjini Mheshimiwa G Lema alijua na kushiriki katika hatua mbali mbali kabla ya kufikiwa kwa muafaka.

  Madiwani wa CHADEMA wamemshutumu Lema kwa kutoa tamko la kulaani muhafaka huo wakati alikuwa na fursa ya kufanya hivyo ndani ya vikao kwakuwa hata yeye ni diwani kwa wadhifa wake wa ubunge.

  Kabla ya kutiwa saini muafaka mheshimiwa alipigiwa simu na kupewa taarifa na maafikiano ya kikao baina ya madiwani wa pande zote mbili.

  Madiwani wa CHADEMA wamemtaka Lema kuwaomba radhi na kukanusha shutuma zote dhidi yao kinyume chake watamburuza mahakamani.

  Tume imebaini mapungufu makubwa kuanzia ngazi ya wilaya hadi taifa.
   
 2. n

  nzom Senior Member

  #2
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Na nini hatma ya hilo kama alikua na taarifa na ameweza kuktoa tamko hilo je nini mwisho wake
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Huh! Come again!
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,702
  Trophy Points: 280
  Source: Radio UHURU
   
 5. M

  Molemo JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Hiyo habari imeandikwa na gazeti la Habari leo na Uhuru yote ya leo
   
 6. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hatushangai yanayofanywa na huyu Lema - Msanii wa kisiasa.
  Anatakiwa arudi shule. Elimu yake ya Form 2 haitamsaidia katika usanii huu.
  Matokeao yake ndiyo haya.
   
 7. harakat

  harakat JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  kwa maana hiyo mheshimiwa alitaka ouzo unaofanyika uonekane ili kila mtu aone suala hilo linavyofanyiwa kazi
   
 8. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #8
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Ngongo,

  Too early my dear. . . let's just wait till all the reports and results are in.Everything will remain transparent, free and fair

  Na pia,wengine tuwe tu watulivu tuache papara,ushabiki na jazba.Tujiandae kupokea repoti ili tusije tukahukumu watu pre-maturely(i mean kabla ya kusikiliza kesi).
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Unajua hii maneno imetapakaa hapa mujini AR nikashangaa JF haijatinga kweli kupenda upofu.Bahati nzuri nimezungumza na madiwani wawili wa CHADEMA ambao walikuwemo kwenye kikao.Ningeweza kuwataja lakini kwakuwa ripoti yenyewe imepelekwa CDM taifa nitakuwanawaaribia.Subiri Dr Slaa akitoa tamko utaona watavyona aibu.  Mkuu Lema anajua kila kilichokuwa kikiendelea lakini akaamua kuwaruka wenzake matokeo yake madiwani wa CDM wanaonekana wasaliti mbele ya jamii.


  Hupendi kusikia ya upande wa pili !!!!!!!.  Bahati nzuri nina accesss na karibu madiwani wote wa CDM.Source yangu si gazeti la Uhuru sijawahi kulisoma yapata mwaka wa 10.  Mkuu sijasoma Uhuru wala Habari leo.Nimeongea na wahusika wakuu [Madiwani wa CDM]
   
 10. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Ben.

  Mkuu umesahau JF ni yakwanza wengine wanakuja baadae.Mkuu hizi habari zingekuwa zinawahusu chama cha magamba ungetoa nasaha hizi ???????.
   
 11. Kishongo

  Kishongo JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MGOGORO uliofumuka baada ya mwafaka kati ya madiwani wa Chama cha Demokrasia na
  Maendeleo (CHADEMA) na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), umeziweka pande hizo mbili njia ya panda.

  Tume iliyoundwa imegundua kwamba pande zote mbili zinazolumbana katika Chadema zinabeba aina fulani ya lawama katika mchakato wa mwafaka, mwafaka wenyewe na kutangazwa kwake.

  Imebainika kwamba pamoja na kelele za Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, kuhusu mwafaka huo, inadaiwa kwamba yeye (Lema) ameamua kuwaruka tu viongozi wenzake wakati akijua fika juu ya maendeleo ya vikao hivyo na hatimaye kufika mwafaka huo.

  Hivi karibuni, madiwani wa Chadema Arusha waliopinga kumtambua Meya wa Jiji hilo, Gaudence Lyimo kwa madai hakuchaguliwa kihalali, waliamua kuondoa tofauti zao na kumtambua Lyimo na kueleza kuwa muafaka huo ni kwa maslahi ya wananchi wa kata zao.

  Mwafaka huo ulipingwa vikali na Lema na kueleza kuwa ni batili na hauna baraka za viongozi wa juu wa Chadema; hatua iliyopingwa na madiwani hao na kudai kuwa kauli ya mbunge huyo ni batili yenye kulenga kutaka kuwachafua kwa wananchi.

  Walidai kwamba Mbunge Lema na baadhi ya viongozi wa juu wa chama hicho wana taarifa asmi ya tukio hilo la mwafaka.

  Katika majumuisho ya Tume ya Chadema yenye wajumbe wanne iliyokuwa ikiongozwa na Mwanasheria wa chama hicho, Mabere Marando, imebaini mtafuruku huo na kusikitishwa kukuzwa kwa tatizo hilo na Lema kwa kukimbilia kutangaza kutoutambua mwafaka huo
  wakati akijua wazi kuwa anajua kinachoendelea, hatua ambayo ilieleza kuwa kwa kiongozi kama yeye hakupaswa kufanya hivyo.

  Tume hiyo iliyomaliza kazi yake Julai 2 kwa kuwahoji madiwani wote na baadhi ya viongozi wa Chadema Wilaya na Mkoa, inaelezwa kuwa ilibainika kupitia mahojiano na watendaji
  hao kuwa kila kiongozi alikuwa akijua hilo ikiwemo vikao vya awali kabla ya kufikia mwafaka.

  Aidha, kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, Tume imewalaumu madiwani wa Chadema waliofikia mwafaka huo wakiongozwa na Naibu Meya Estomih Mallah kwa kuwa na haraka ya kuutangaza bila kusubiri kauli ya mwisho ya viongozi wa juu wa Chadema Taifa.

  "Ni kweli Tume tumebaini kila kitu kilikuwa kinajulikana kwa viongozi wa Chadema Wilaya, Mkoa na Taifa na hata Mbunge Lema, lakini mlipaswa kusubiri kauli ya mwisho kabla ya kuutangaza muafaka huo!

  "Hilo hapo ni tatizo lazima mkubali mmekosea lakini tatizo hilo sio kubwa kama lilivyokuzwa," alisema mtoa habari wetu akimkariri Marando wakati wa majumuisho ya
  pamoja.

  Katika kujitetea kwa mara ya mwisho mbele ya Tume hiyo, mmoja wa madiwani (jina tunalo), anakaririwa akisema walishindwa kusubiri kauli ya mwisho ya viongozi wa juu wa Chadema kwa madai ya kuwa wazito katika kutoa kauli ya mambo mengi ya kichama na ndio maana walitoa muda bila majibu na kuamua kuendelea na taratibu za muafaka.

  Diwani huyo alidai hata Lema alipigiwa simu kuelezwa taratibu za mwisho zilipofikia juu ya mwafaka huo, na pia alikaa kimya.

  "Mheshimiwa Mwenyekiti hapa nani wa kulaumiwa, ni sisi ama hao wanaopata taarifa, lakini wanashindwa kuzitolea maamuzi na kuzikalia?

  Jibu, wa kulaumiwa juu ya mwafaka huu ni viongozi wa juu wa Chadema na Mbunge Lema," alikaririwa akidai diwani huyo.

  Taarifa ndani ya kikao hicho zilidai kwamba madiwani walieleza kuwa msimamo wao uko pale pale kwa maslahi ya wakazi wa Arusha na kueleza kuwa madiwani, viongozi wa chama hicho wa ngazi zote kuwa mstari wa mbele kueleza ukweli na sio kutaka kupotosha umma kwa kujitafutia umaarufu kwa njia ya upotoshaji.

  Chanzo chetu cha habari kiliwakariri madiwani hao wakimtaka Marando kumuonya Mbunge Lema kuacha mara moja kutoa kauli za kejeli dhidi yao kuwa wamenunuliwa na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa ili waingie katika kamati mbalimbali za Jiji ili wawapitishie zabuni zao.

  Madiwani hao walieleza kukasirishwa na kauli hiyo na haitavumiliwa na kumtaka mbunge
  huyo akanushe, vinginevyo watapeleka katika vyombo vya sheria.

  Baada kumalizika kwa majumuisho hayo na kila diwani kutoa kauli yake, Marando aliwaambia kuwa wamemaliza kazi na wanapeleka taarifa hiyo kwa viongozi waliowatuma ili waamue nini cha kufanya.

  Julai 3 Marando alipopigiwa simu na gazeti hili kueleza walichokigundua Arusha baada ya kazi hiyo, alisema atafutwe Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Willibrod Slaa kwani ndiye aliyewatuma.

  Source: Habari Leo
   
 12. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Chadema kwa kuchagua magazeti hamjambo!

  Juzi Daily News limeandika habari ya Pinda kumpasha Lowasa kwa ufasaha zaidi kuliko hata magazeti yenu mnayoyapenda.

  Well Lema ana kesi ya kujibu kwenye hili swala, lakini wananchi wameshastuka nest time watakapoitisha maandamanow akina Slaa wajuwe wazi wananchi hawatakurupuka tu kukimbilia.
   
 13. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #13
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Ngongo,

  Heshima ikurudie pia mkuu wangu!

  Nilitoa angalizo tu mkuu,hata kama ingekuwa CHAUSTA. Kuna tabia ya watu kutanguliza ushabiki,na papara tu bila kujali haki na usawa.Hilo lipo kwa vyama vyote vya siasa na wafuasi wa vyama hivyo kwa ujumla.The keyword hapa ni Patience,justice na rationality katika mambo kama haya.Huwa ndiyo maana unaona kwenye posts zangu nyingi nawatetea baadhi ya wana-CCM hasa ninapoona kuna uwezekano wa watu kutolewa kafara.Injustice ni lazima ipingwe hata kama inafanyika against your foe.I wish kama ungechukua muda kunielewa.Otherwise,Thank you Ngongo! ! !

  Na kwa wengine tusipende tu kusikia yale tunayotamani,tuepuke mazingira ya kuishi katika illussion.Hii ndiyo sababu inayofanya taifa letu kuwa gizani hadi leo kwa sababu wanasiasa wanajua kutumia appeasement tone.wanajua wananchi wanataka kusikia mgawo wa umeme mwisho julai,na watasema hivyo hivyo.wanajua huwa tunapenda kusikia uchumi umeimarika na watasema hivyo hivyo.Kwa hiyo ukitaka kuzingatia haki na usawa,uhalisia ni lazima uwe tayari kwa lolote hata kama linakukera.

  Cha msingi baada ya hapo ni kuangalia jinsi ya kutoka katika hiyo "Mess" and move on!
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Nimezungumza na mwandishi wa hii habari muda huu Bwana John Mhala kanihakikishia bila shaka yoyote madiwani wote wa CHADEMA Arusha mjini wamemtaka Lema afute tamko lake la kichochezi dhidi yao ndani ya siku saba ama wamburuze mahakamani.Nimesema na ninarudia tena na tena nimezungumza na madiwani wa CHADEMA kwa nayakati tofauti wote wanazungumza lugha mmoja "Maslahi ya wapiga kura wao"
   
 15. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Whats so hard to comprehend wana Chadema?

  Is it that Chadema as a party is too organized to make such a stupid blunder?

  Get over it!
   
 16. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Arusha inatiwa aibu na chalii...
   
 17. HOMOSAPIEN

  HOMOSAPIEN JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 719
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Madiwani wa CDM Arusha fanyeni kweli basi huyu mtu ni wa migogoro na visasi tu,haelewi kuwa anatakiwa awatumikie wananchi au uchaguzi uliisha mwaka jana bado anadhani kampeni zinaendelea,wananchi wanahitaji maendeleo siyo malumbano alitegemea bajeti ya jiji apitishe nani kama siyo madiwani na ingepitishwaje kama madiwani hawaelewani,huyu anaelewa lakini amejaa sifa mfanyieni kweli apunguze ushamba
   
 18. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Haya unayoyaeleza hayana mtiririko unaofuatana wa kile ambacho kimeshasemwa na viongozi wa juu wa CDM, hasa Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CDM taifa.

  Walisema kwamba, kweli kulikuwa na mazungumzo yanayoendelea kati ya kiongozi wa kambi ya upinzani na waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ninachokumbuka (nipo tayari kwa masahihisho) kuwa CDM ilitoa masharti matatu kwa serikali (kupitia waziri mkuu) kuwa ili wafikie muuafaka kuhusu suala la Arusha:

  1. Serkali ikiri kuwa ilikosea kwamba kweli uchaguzi wa Meya wa Arusha haukuwa halali.
  2. Wafute kesi iliyoko mahakamani ambayo inawahusu viongozi wa CDM na wanachama wao.
  3. Askari waliofanya mauaji pale Arusha wachukuliwe hatua.Hivyo ni wazi kuwa kulikuwa na mazungumzo na Mh. Lema alikuwa anapata habari (endapo itatafisiriwa kama ushiriki) kuhusu kilichokuwa kinaendelea kwa kila hatua.

  Uhitimishaji wa mazungumzo wenye lengo la kugawana madaraka ndiyo unaoleta mashaka hasa ukizingatia kuwa kama viongozi wa juu walikuwa wanashiriki mazungumzo na waziri mkuu, ilikuwaje hatua za umaliziaji haikuwahusisha wao?
   
 19. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #19
  Jul 4, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Wakuu,

  Hivi hatuwezi kujadili mambo yetu bila kuingiza udini na ukabila? Jamani dini hata kama haufuati,tujaribu kuheshimu dini za watu wengine.Hebu tuwe wastaarabu,sidhani kama mwanachadema wa kweli anaweza kuibuka na kuanza kukejeli imani za watu wengine.Huyo atakuwa ni mtu mwenye lengo baya chadema na au si mwanachama mwaminifu kwa kuwa chadema ni ya watanzania wote bara na visiwani,wakristo,waislamu,hindu,wenye dini za asili na wasion na dini.

  Let us not indulge in sectarian discussion! Jamani sisi ni watanzania kwanza.Tusiharibu mijadala hapa na kwingineko.Tushindanishe sera za vyama vyetu na tuzitetee kwa hoja,tusishindanishe imani au Miungu katika muktadha wa kisiasa vile vile tusishindanishe mababu zetu au makabila yetu katika muktadha wa kisiasa.Sio sahihi.
   
 20. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Mkuu hapo kwenye red ndipo penye mzizi wa fitina. Maandamano ususiaji wa kila aina ulisababishwa na Umeya [Cheo]
   
Loading...