MGOGORO WA KIFEDHA 2008: Sababu Zilizopelekea Kuporomoka Kwa Uchumi Duniani.

Financial Analyst

JF-Expert Member
Nov 27, 2017
1,605
2,743
Mgogoro wa kifedha 2008 (mporomoko wa uchumi) ulianzia nchini Marekani then kusambaa kwa mara ya kwanza katika nchi za Ulaya baadae Asia na mwishowe Africa.

Baada ya miaka mingi ya kukuwa na kustawi kwa biashara ya nyumba (Housing Business) nchini Marekani, Mashirika mengi ya kifedha yaliweza kuwekeza katika biashara hii. Kutokana na bei za juu za nyumba, Wamarekani wamekuwa wakipata hizi nyumba kama mkopo na kulipia katika riba maalum na nyakati maalum. (MORTGAGE).

Kupitia katika fursa za ukopeshaji wa nyumba kwa wateja, mashirika mengi yaliweza kuwakopesha wamarekani wengi haikujalisha kama hawakukidhi viwango vyote vya kifedha.Pia waliweza kupunguza riba ya mikopo ya nyumba (mortgage loan interest) so hii ilipelekea uhitaji mkubwa wa nyumba nchini marekani, hii ilipelekea kukuwa kwa maradufu kwa bei za nyumba nchini humo (The higher the demand, the higher the price). Ukuaji wa bei maradufu wa hizi nyumba haukuweza kuwakatisha tamaa wateja, manaake waliweza kuzipata hizi nyumba haikujalisha viwango vyao vya kifedha au nguvu/uwezekano wao wa kulipa riba. Kutokana na kukuwa kwa bei za nyumba na kustawi kwa biashara hii, mashirika mengi duniani yaliwekeza katika biashara hii nchini Marekani.

KILICHOFANYIKA:
Mashirika ya nyumba (Mortgage Lenders) hawakuishia hapo, waliweza kuuza hii mikopo ya nyumba (Mortgage Loans) kwa mashirika mengine kama vile FREDDIE MAC, Freddie Mac waliweza tena kuuza hii Mortgage loan kama dhamana kwa benki za uwekezaji (Investment Bank). Hizi Investment banks nazo ziliweza kukusanya hii mortgage loans (zilizotokana na mikopo ya nyumba) na kuziweka katika mafungu ya maelfu au malaki na kutengeneza dhamana inayoitwa MORTGAGE BACKED SECURITIES (yani dhamana inayofungamaniwa na mikopo ya nyumba). Hizi Mortgage backed securities zilikuwa na nguvu ya kifedha kutokana na malipo ya riba ya mnunuzi wa nyumba kila mwezi. Then hizi Mortgage backed securities ziliwezwa kugawanishwa ndani ya ma1000 na kuuzwa kwa wawekezaji katika masoko ya dhamana.

Makampuni ya Bima (Insurance) nayo yaliingia katika huu mchezo. Haya makampuni yaliweza kuja na product moja inayoitwa CREDIT DEFAULT SWAP, waliuza kwa wawekezaji na mabenki ya uwekezaji. Hii credit default swap inamaanisha kumpa mwekezaji uwezo wa kuswap au kuepuka risk au loss itakayotokea katika dhamana yake au mkopo aliotoa. Kwa mfano, kama mwekezaji anahisi atapata hasara katika mikopo aliyoikopesha au dhamana alizouza then ataweza kununua CREDIT DEFAULT SWAP ili iifunike hiyo risk au hasara atakayopata. So Mashirika mengi yaliyokuwa yamewekeza katika biashara ya nyumba yaliweza kujihusisha na hizi credit default swap (CDO). Mashirika yaliweza kufaidika sana kutokana na kutopokea risk yoyote au hasara yoyote. Hii ilisababisha ongezeko la mzunguko mkubwa wa mikopo na kusababisha gap kubwa kati ya madeni na hali halisi ya kipato (Debt and Income gap). Inamaanisha watu walipokea fedha nyingine za mikopo au dhamana zaidi ya viwango vyao vya mapato na nguvu yao ya kukidhi kuyamaliza madeni yao.

MPOROMOKO:
Credit scores companies na regulation bodies waliweza kuwa wazembe au kufumbia macho uongezekaji wa hizi dhamana na isitoshe waliweza kuzipamba na kuonesha kuwa hazina madhara yoyote.
Kutokana na ukopeshaji mwingi wa nyumba kwa watu ambao hawakuwa na sifa za kukopeshwa na kutokana na system zilizoanzishwa na mashirika ya kifedha kupitia kwa fursa ya Mortgage ... ilipelekea waliomiliki nyumba kwa kukopeshwa kutoweza kulipa mikopo yao. Mashirika ya nyumba yaliweza kupata default (hasara ya mkopo pale unapokosa kulipwa). Hii ikapelekea kuanzia mwaka wa 2006 Bei za nyumba kuzidi kushuka bei na hata kuwa chini ya mkopo wenyewe wa nyumba (mortgage loan). Hii ilipelekea mashirika mengi ya nyumba kufunga biashara zao na kuathiri mashirika ya kifedha, mabenki.( ya marekani na duniani kwa ujumla) yaliyokuwa yamewekeza katika fursa hii.

ATHARI:
Kutokana na mashirika mengi ya kifedha kuathirika na pigo hilo, mashirika haya yalishindwa kutoa mikopo na huduma nyingine za kifedha, hali iliyopelekea ukosenaji wa pesa mitaani. Pia masoko ya hisa na dhamana yaliweza kuyumba. Hii ilipelekea kuporomoka kwa uchumi kwa kasi ya juu sana.

Mashirika makubwa ya kifedha yalianza kufilisika kama vile Lehman Brothers,... Na ilipelekea kulemaa kwa sekta nyingine kubwa nchini marekani mpaka pale serikali ya marekani na benki yake kuu ilipoamua kuzikwamua sector nyingine.

Kulitokea ongezeko la hali ya juu ya upotevu wa ajira, uzwaji wa mali, ukosaji wa nyumba na mahali pa kuishi, upotevu wa nguvu ya manunuzi.

KUATHIRIKA KWA DUNIA NZIMA:
Mashirika na serikali za ulaya kama vile Uingereza , waliathirika kiuchumi kutokana uwekezaji mkubwa uliofanywa katika fursa ile. Nchi kama Japan iliathirika kutokana na matajiri wake wengi kuwa waliwekeza marekani. Ilipotekea kuwa nchi kubwa zimeathirika kiuchumi, ilipelekea chini za Africa zinazotegemea mikopo na misaada kutoka nchi tajiri kuyumba pia. Miradi mingi na kazi za kiuchumu vilisimama su kuyumba kutoka na athari za mgogoro wa kifedha ulioanza nchini Marekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mada nzuri kwa fx traders

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom