Mgogoro Wa Kahawa Mbozi Mbeya na Maslahi Ya Wanasiasa(MhZambi, DC Kimolo, Kumbulu)!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgogoro Wa Kahawa Mbozi Mbeya na Maslahi Ya Wanasiasa(MhZambi, DC Kimolo, Kumbulu)!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KING COBRA, Jun 20, 2012.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mimi nimejaribu kufuatilia mgogoro wa Kahawa Mkoa wa Mbeya hususani Mbozi ambapo , Mh Godfrey Zambi, Aldolf Kumbulu, Dc wa zamani Kimolo , RC Mwakipesole na wenzake wote ni wafanyabiashara wa Kahawa mbichi na wamekopa pesa Benk ya CRDB!!

  Ni Jambo la ajabu Wakulima walime Kahawa halafu Wanasiasa wawape masharti ya Kuuza!!! Hapa najisikia vibaya hasa ninapoana makada wa CCM ambao wameingia madarakani kwa wizi wa kura wananyanyasa Wakulima!!

  Kama wakulima wanataka kuuza si ni matakwa yao??? Kama wanapata hasara inawahusu nini wanasiasa??? Mbona Mafisadi wa CCM wanaiba zaidi za 40bils za kagaoda kodi ya wananchi lakini Zambi hamupigi marufuku Lowassa na Rosrtam ambaye ni rafiki yake??

  Tangu lini CCM ikawa na uchungu na wizi wa mali za Wananchi??? Kumbulu naye ni fisadi ?? Mimi naona wananchi waachwe wauuze kahawa wanavyotaka wenyewe kama tunavyotaka katiba mpya!!!
   
 2. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mbunge Zambi ashitakiwa mahakamani 15th June 2012

  Mbunge wa CCM Jimbo la Mbozi Mashariki, Mheshimiwa Godfrey Weston Zambi Jumatano wiki hii mjini Moshi amefunguliwa kesi ya madai na kampuni ya Lima Limited akidaiwa fidia ya shilingi 2.4 bilioni kwa tuhuma za kutoa matamshi ya kuikashifu kampuni hiyo.

  Katika gazeti la Mwanahalisi la Juni 13-19,2012, Mheshimiwa Zambi anadaiwa kutamka" Lima imekuwa ikiwashawishi wakulima kuuza kahawa mbivu kwa bei ndogo sana".

  Kampuni hiyo inamtuhumu Zambi kuanzisha kampeni mbaya dhidi ya kampuni hiyo ili kuondoa ushindani wa soko ili kuvipa fursa vikundi vya wakulima ambavyo Zambi ana maslahi navyo visipate ushindani wowote katika soko la Kahawa. K

  esi hiyo namba CC 7/2012 imefunguliwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi,Eric Ng'maryo ambaye pia ni Advocate Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa.
   
 3. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #3
  Jun 21, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Suala la mkulima mdogo dogo kuuza kahawa mbichi au ile ambayo kaifanyia processing haliwezi kuamuliwa kwa personalisation. ni busara kufanya uchambuzi ambao utatuonyesha Economic Rationale ya mkulima ambayo kuifikia inabidi kutumia kwa uchache tools kama parametric budgets hususan Break-Even Analysis (bellies vs parched). Na ili uweze ku capture maamuzi rationale ya mkulima inabidi utumie Decision Theory - kwa vile kuna arguement ya kwamba kwa wakulima kuuza kahawa mbichi wanahamisha Market RIsk kwa watu wenye uwezo wa kuhimili Risk (risk averse vs risk takers). Hata hivyo ieleweke:
  Mosi Soko la kahawa haliko wazi kiasi hicho- limeegemea kwa multi nationals pamoja na juhudi za ku electronify mnada wa kahawa pale Moshi.

  pili Tanzania huwa hifikii quota yake ya kahawa katika soko la Dunia kwa vile quality ndo inatudondosha. Ni kinyume na wanaosema soko limejaa. Kuna siku za nyuma Vietnam ilikuwa inauza hata kahawa zilizotoka kwenye swamps.

  Tatu dawa yakumsaidia mkulima mdogo dogo akidhi mahitaji yake mara tu baada ya kahawa kiva sio kuiza kwa anaenunua kahawa mbichi. kwa nini Ware House System isitumike kwa hawa wakulima. Mpango huu uliishia wapi??

  Tatu, sio vikundi vyote vya wakulima vina matatizo - njia pekee ya kumkomboa mkulima mdogo ni yeye kujiunga na vikundi. Hapa nieleweke - sio vikundi vya kumlazimisha mtu kujiunga bali ni wale wanaoiva pamoja kuwa na kikundi chao. Wa Denishi (Dernmark) wamefaulu sana katika ushirika ambao upo kwa zaidi ya miaka 200 kwa vile washirika hawaingiliwi na serikali na wanaungana kufuatana na enterprise interest. Ungeweza kuta kikundi cha wauza kahawa mbichi, wauza ngurwe nk Kuna vikundi Mbeya vijijini viliwahi kuwa hivyo na kuuza kahawa yao kwa bei maradufu kuliko hapo awali. maana yangu sio vizuri ku castigate vikundi na kuviona ni vya kitapeli.
   
 4. m

  matengo Member

  #4
  Jun 21, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inaonekana mchangiaji anaelewa mambo ya kahawa kuliko hata wale waliopewa jukumu la kusimamia biashara hii. Hivi Kumburu hasomi maoni kama haya ili yamsaidie kuondokana na kutetea maslahi binafsi.
   
Loading...