Mgogoro wa Israel na Palestina ndio utakaohitimisha dunia

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Feb 26, 2021
933
2,810
MGOGORO WA ISRAEL NA PALESTINA NDIO UTAKAOHITIMISHA DUNIA.

Leo 11:15hrs 22/05/2021

Nianze kwa angalizo,ugomvi wa Palestina na Israel ni wa mapacha wawili toka wakiwa tumboni mwa Mama yao kabla ya kuzaliwa,Mapacha hao ni Esau na Jacob,sababu ya njaa Esau aliuza haki ya mzaliwa wa kwanza kwa Jacob na ilipofika muda wa Baba yao Isaka kumbariki mtoto wa kwanza,ni Jacob(Israel) aliyebarikiwa badala ya Esau ambae baadae aliitwa Edom(Jordan/Palestina),vita ikaendelea duniani baada ya vita ile ya tumboni,Palestina wapo Wakristo,Waislamu na Wayahudi na Israel wapo Wakristo,Waislamu na Wayahudi,awa ni ndugu wa Baba mmoja,Mama mmoja,Mwamuzi wa kweli wa ugomvi wao ni Mungu mwenyewe, Marekani,China watajaribu,wote watashindwa,vivyo hivyo kwa Urusi.

Nini sababu ya ugomvi ? Siyo tatizo la kugombania ardhi wala kugombania mji wa Yerusalem kunakosababisha ugomvi kati ya mataifa haya mawili,ugomvi wa Palestina na Israel ni ugomvi wa ndugu wa damu,ugomvi wao unahusu nani ana haki ya mzaliwa wa kwanza,hivi leo Israel hataki kutambulika kwa Palestina na vivyo hivyo Palestina hataki kutambulika kwa Israel,kwa lugha rahisi Taifa la Israel halilitambui taifa la Palestina na taifa la Palestina halilitambui taifa la Israel,Hii inamaanisha kwamba hata kama taifa la Palestina litahamia katika bara jingine au Israel kuhamia bara jingine bado ugomvi na vita ingeendelea kati ya mataifa haya mawili ,ugomvi kati ya mataifa haya unakwenda mbali zaidi tangu watoto wawili mapacha wakiwa tumboni kabla ya kuzaliwa.

Katika kitabu cha (Mwanzo 25:22) inasomeka;"Bwana akamwambia Rebecca ,Mataifa mawili yamo tumboni mwako ,na kabila mbili za watu watafarakana tangu tumboni mwako,kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili na mkubwa atamtumikia mdogo."Alizaliwa kwanza Esau ambaye baadae aliitwa Edom ambao ukoo wao unapatikana katika nchi ya Jordan na Palestina kisha akafuatia Yakobo ambaye baadae aliitwa Israel ambao ukoo wao upo Israel.Wakati Edom ni taifa la Palestina, Israel ni taifa la Israeli, hakuna ubishi kwamba Israel ni hodari zaidi ya Palestina.Mwaka 1947, Umoja wa Mataifa ulipiga kura kwa Palestina kugawanywa kati ya mataifa ya Wayahudi na Wapalestina huku mji wa Jerusalem ukiwa mji wa kimataifa.

Mpango huo ulikubaliwa na Wayahudi lakini ukakataliwa na Waarabu na haukutekelezwa.Israel inadai kumiliki Jerusalem kama mji mkuu wa Israel huku Palestina ikidai kuwa Jerusalem ya mashariki ndio itakayokuwa mji wake mkuu wa taifa lijalo la Kipalestina.Ni Marekani pekee inayotambua kwamba Jerusalem ni eneo la Israel . katika kipindi cha miaka 50 iliopita , Israel imekuwa ikijenga makaazi katika maeneo hayo ambapo takriban raia 600,000 wa Kiyahudi wanaishi.Palestina inasema kuwa makaazi hayo ni haramu na kinyume na sheria ya kimataifa na kikwazo cha kuleta amani , lakini Israel imekana hilo.

Hali ya wasiwasi ipo juu kati ya raia Israel na Wapalestina wanaoishi mashariki mwa Jerusalem, katika eneo la Gaza na lile la West Bank,Gaza inatawaliwa na kundi la wapiganaji wa Kipalestina kwa jina Hamas, ambalo lilipigana na Israel mara nyingi,Israel na Misri wanadhibiti eneo la mpakani la Gaza ili kuzuia silaha kusafirishwa hadi kwa wapiganaji wa Hamas,raia wa Palestina wanaoishi Gaza pamoja na West Bank wanasema kuwa wanateseka kutokana na vitendo vya Israel na vikwazo,Israel nayo inasema kuwa inatekeleza vitendo hivyo ili kujilinda dhidi ya ghasia za palestina.

Itakumbukwa kwamba, Mwanasayansi mashuhuri aliyejulikana kama Albert Einstein alitoa tafsiri ya neno " Insanity" yaani " kuchanganyikiwa au uwendawazimu " akisema ;"wakati mtu anapojaribu kutumia kanuni ya zamani ambayo ilishindwa kwa wakati na wakati mwingine tena, akiamini kwamba ,kwa vyovyote atapata matokeo tofauti mtu huyo amechanganyikiwa au ana uwendawazimu.Israel, Palestina, Marekani na Umoja wa Mataifa kwa zaidi ya miaka 50 wamekuwa wakijadili uwezekano wa kuleta suluhu kwa kuifanya Palestina kuwa Taifa huru pamoja na Israeli. Hata hivyo ,wapalestina wamekuwa wakijiondoa kwenye suluhisho hilo kwa sababu mpango huo unaifanya Israel iendelee kuwa Taifa huru ,wapalestina wamekuwa wakipinga wazo kwamba Israel ina haki ya kuwepo na kuishi kama Taifa.

Lengo ni kuwafutilia mbali wayahudi wote,jambo ambalo hata Adolf Hitler alikuwa nalo lakini hakuweza ,kwa mujibu wa Mwanasayansi Albert Einstein " suluhisho la mataifa mawili ( two state solution) limeshindwa kufanya kazi na wale wanaoendelea kupendekeza suluhisho hilo, ama wamechanganyikiwa na ni wendawazimu au wanafanya kwa makusudi wakiwa wanafahamu matokeo yake,Raia wa mataifa yote mawili wanamtambua Ibrahimu kama Baba wa Mataifa yao, Ibrahimu aliishi miaka 4000 iliyopita akisafiri Kwenye eneo la Taifa linalojulikana leo kama Iraqi, na akafika Kwenye eneo la taifa linalojulikana leo kama Israeli.

Ibrahimu aliahidiwa na Mungu kwamba atapata mtoto katika uzee wake,akiwa amesubiri utimilifu wa ahadi hii kwa muda mrefu bila kupata mtoto ,alimchukua kijakazi wake na akafanikiwa kuzaa naye mtoto aliyeitwa ishmail. Lakini mungu hakuwa amepanga kumpatia Ibrahim mtoto kwa njia hiyo,bado aliendelea kumhakikishia kwamba atapata mtoto kupitia kwa mkewe,kwa sababu alikuwa na imani ,alifanikiwa kumpata mtoto aliyepewa jina la Isaka,kisha Mungu akamuagiza kwenda kwenye mlima Moria, ili akamtoe kafara mtoto wake Isaka ambaye alikuwa amemsubiri Kwa muda mrefu,huu mlima Moria upo wapi? Ingawa wakati wa siku za Ibrahimu ,miaka 2000KK ,eneo kubwa lilikuwa jangwa ,miaka 1000KK baadae Mfalme Daudi alijenga mji wa Yerusalem katika eneo hilo na mtoto wake aliyejulikana kama Mfalme Sulemani alijenga hekalu la kwanza kwenye eneo hilo la mlima Moria .

Imeandikwa " ndipo Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya bwana huko Yerusalem ,juu ya mlima Moria ..." (2 Nyakati 3:1). Lakini kwa Ibrahimu Mungu anamwambia : " umchukue mwanao ,mwana wako wa pekee, umpendaye ,Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka, ..." ( Mzo. 22:2) Hivyo basi mji wa Yerusalem anajulikana kama nchi ya Moria au mlima wa Moria au mji wa Daudi mahali palepale alipoambiwa nabii Ibrahimu kwenda kutoa kafara ,ndipo hapo hapo Mfalme Sulemani alipojenga hekalu la kumuabudia Mungu na kumtolea kafara za wanyama,lakini zaidi ni katika mji wa Yerusalem ndipo yesu aliposulubiwa msalabani na hapo ndipo lilipo chimbuko la dini ya ukristo iliyoanzishwa kwa ujumla uzao wa Ibrahimu ndio chimbuko la dini kubwa tatu ,yaani uyahudi, uislamu ,na ukristo.

-Kwa nini Jerusalem ni Mji unaogombaniwa na Wayahudi,Waislam na Wakristo?

Baadhi ya maeneo matakatifu ya kidini duniani yapo katika mji wa zamani wa Jerusalem : Dome of the Rock, Msikiti wa Al Aqsa, hekalu la Mlimani na Ukuta wa magharibi wa dini ya wayahudi na kaburi takatifu wa dini ya Wakristo,na pia unatambulika kuwa mji mtakatifu zaidi wa Wayahudi,Wakristo na ni mji mkuu mtakatifu wa Waislamu.Ukijulikana kiHebrew kama Yerushalayim na kiarabu kama Al Quds, ni mmoja wa miji ya zamani zaidi duniani,umetekwa, kuharibiwa na kujengwa kwa mara nyingine na kila safu ya dunia kipande tofauti cha historia yake hubainika.

-Kanisa

Ndani ya Mji huo wa zamani ni kanisa la mtakatifu Sepulcher, mojawapo ya maeneo takatifu ya Wakristo duniani,kanisa la mwanzo lililopata kujengwa na Mfalme Suleiman kwa ajili ya Baba yake Daudi,lipo katika Jerusalem eneo ambalo historia yake inamuhusisha Yesu Krsito,kifo chake,kusulubiwa kwake na kufufuka kwake,kulingana na tamaduni za Wakristo, Yesu alisulubiwa katika eneo la Gogotha,Mlima wa Calvary, na kaburi lake lipo hapo na ndipo eneo alilofufuka,kanisa linasimamiwa na wawakilishi wa makanisa tofauti ya Kikristo,hususan Kanisa la Orthodox la Ugiriki,kanisa la Katholiki la Franciscan Friars na kanisa la Armenia Patriarch,lakini kanisa la Ethiopia la Coptic na kanisa la Syria pia yanahusishwa.

-Msikiti

Msikiti wa Al Aqsa ndio mkubwa kati ya maeneo matakatifu yaliopo katika mji huo katika eneo linalojulikana kama Haram al Sharif,Msikiti huo ndio eneo la tatu takatifu kwa ukubwa na husimamiwa na ufadjhili wa fedha unaojulikana kama Wakfu,Waislamu wanaamini kwamba mtume Muhammad alisafiri kuelekea eneo hilo kutoka Mecca wakati wa safari ya usiku na kuombea roho za mitume yote,hatua chache kidogo, The Dome of The Rock linamiliki jiwe ambalo mtume Muhammad alienda mbinguni.Waislamu hutembelea eneo hilo takatifu kila mwaka , lakini kila Ijumaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramdhan, mamia ya maelfu ya Waislamu huenda katika eneo hilo kufanya ibada,na wakati huo wa mwezi mtukufu ndipo vurugu na vita uwa inatokea.

-Ukuta

Eneo hilo linamiliki Kotel- ama ukuta unaolia, mojawapo ya milima iliosalia ya mlima Moria,Ndani ya hekalu hilo ni eneo takatifu la matakatifu ya Wayahudi,Wayahudi wanaamini kwamba eneo hilo ndio eneo la jiwe la msingi ambapo dunia iliundwa na ni eneo ambalo mtume Abraham alitaka kumchinja mwanawe Isaac,Wayahudi wengi wanaamini kwamba The Dome of The Rock ndio eneo la maeneo yote matakatifu,hii leo ukuta huo unaolia ndio ulio karibu zaidi kwa Wayahudi kufanya ibada,Unaongozwa na Rabbi na mamilioni ya wageni hutembelea eneo hilo kila mwaka.

-Historia ya Msikiti wa Al-Aqsa ambao chini Msikiti na Juu Kanisa.

Msikiti wa Al-Aqsa ndio Qibla ya kwanza ya Waislamu. Kwa miaka kadhaa, Waislamu walisali wakielekea Msikiti wa Al-Aqsa. Katika mwaka wa pili wa Hijria, Mwenyezi Mungu Mtukufu Alitoa amri kwa Mtume wake Mohammed (S.A.W.) na Waislamu kubadilisha Qibla yao kutoka Msikiti wa Al-Aqsa mjini Quds na kuelekea Msikiti wa Al-Haram katika mji wa Makkah. Aya za 142 hadi 150 katika Suratul Baqara zimezungumzia tukio hili. Katika sehemu moja ya aya ya 150 Mwenyezi Mungu Anamwambia Mtume Mohammed (S.A.W.) na Waumini kwa kusema: "Na popote wendako elekeza uso wenu kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo..."

Nabii Adam AS baada ya kujenga Masjidul Haram huko Makka, aliamrishwa na Mwenyezi Mungu kuweka msingi wa Msikiti wa al Aqsa,Mji wa Baitul Muqqadas au Quds. (Kwa kiingereza -Jerusalem.) ni moja kati ya miji muhimu ya kihistoria duniani wenye utambulisho wa kidini. Kwa mujibu wa baadhi ya maandishi ya kihistoria, mji huu uliasisiwa zaidi ya miaka elfu nne iliyopita,Mitume na Manabii wengi wa Mwenyezi Mungu walizaliwa au kuishi katika mji huo mtukufu,Ni kwa sababu hii ndio maana mji huu ukazingatiwa na kuwavutia wafuasi wa dini tatu,yaani Uyahudi,Ukristo na Uislamu,wakati Nabii Ibrahim AS alipohajiri kutoka Misri hadi Palestina, aliishi katika Mji wa Quds. Katika zama hizo Mji wa Quds ulijulikana kwa jina la Yabus na ulikuwa mashuhuri kama mji wa amani na utulivu. Kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Nabii Ibrahim AS aliujenga upya mji huo na kukarabati eneo lake takatifu yaani Msikiti wa al Aqsa ili wafuasi wa Tauhidi waweze kumuabudu Mwenyezi Mungu hapo.

Mji wa Quds pia ni mtakatifu kutokana na kuwa Nabii Mussa AS aliona nuru ya Mwenyezi Mungu na kuzungumza Naye akiwa hapo. Katika zama zake, Nabii Mussa AS aliamua kuihamisha kaumu ya Bani Israel kutoka Misri hadi Palestina kutokana dhulma na ukandamizaji wa Firaun, lakini kwa sababu ya kaumu hii kukataa kutii amri, Mwenyezi Mungu aliwaacha watapetape jangwani kwa muda wa miaka 40 na hakuwaruhusu kuingia Palestina. Hali hii iliendelea hadi mwisho wa umri wa Nabii Mussa AS. Inaaminika kuwa Nabii Mussa AS alizikwa karibu na mji wa Quds. Baadhi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu ambao majina yao yako katika Qurani Tukufu, wamezikwa katika ardhi ya Palestina. Mitume hao ni pamoja na Nabii Ibrahim AS, Nabii Yusuf AS, Nabii Yaaqub AS, Nabii Ishaq AS, Nabii Daud AS, Nabii Sulaiman AS na Nabii Zakaria AS.

Baada ya Nabii Daud AS kupewa Utume na Mwenyezi Mungu, aliamua kuupanua mji wa Quds na kulijenga upya eneo la ibada la mji huo ambalo kwa mujibu wa riwaya za kihistoria lilikuwa limeharibiwa na kukarabatiwa mara kadhaa,kati ya matukio mengine yaliyojiri katika ardhi za Palestina na hivyo kuongeza umuhimu na utukufu wake miongoni mwa wafuasi wa dini ya Tauhidi ni kuzaliwa hapo Nabii Issa AS. Nabii Issa AS alikuwa mbeba bendera ya amani, utakasifu na ucha Mungu. Nabii Issa AS alizaliwa katika kijiji cha Baitul Lahm (Kwa kiingereza -Bethlehem) karibu na mji wa Quds. Nabii Issa AS alianza kuhubiri katika mji wa huo wa Baitul Muqaddas na hapo ndipo alipopaa na kuelekea mbinguni. Na mwisho kabisa Masjidul Aqsa katika mji wa Quds ndiyo sehemu ambayo Mtume wa Mwisho Muhammad al Mustafa SAW alipaa kuelekea katika mbingu katika tukio maarufu la Miiraj,Palestina na Mji wa Baitul Muqaddas ni muhimu kwa Waislamu kutokana na kuwepo maeneo matakatifu hapo. Mwenyezi Mungu SWT katika kitabu Chake cha mwisho yaani Qur'ani, ameutaja mji huo kuwa ardhi yenye Baraka na takatifu.

Masjid Al-Aqsa ni eneo la tatu kwa utukufu katika Waislamu baada ya Masjid Al-Haram huko Makka na Masjidun Nabii huko Madina,Masjidul Aqsa ndicho kibla cha kwanza cha Waislamu. Kwa miaka kadhaa Waislamu walisali kuelekea Masjidul Aqsa. Katika mwaka wa pili wa Hijria, Mwenyezi Mungu alitoa amri kwa Waislamu kubadilisha kibla chao kutoka Masjidul Aqsa mjini Quds na kuelekea Masjidul Haram katika mji wa Makkah. Aya za 142 hadi 150 katika Suratul Baqara zimezungumza kuhusu tukio hili. Katika sehemu moja ya aya ya 150 Mwenyezi Mungu anamkhutubu Mtume SAW na Waumini kwa kusema: "Na popote wendako elekeza uso wako kwenye Msikiti Mtakatifu. Na popote mlipo elekezeni nyuso zenu upande huo..."

-Kufutwa kwa Israel katika ardhi ya Dunia.

Miaka ya 50 iliyopita, yaani mwaka 1967 ,kulitokea vita kati ya Israel na mataifa jirani zake, Vita hii ilipiganwa kwa siku 6 tu(Juni 5---Juni 10,1967) lakini madhara yake yapo mpaka leo ,ilikuwa ni miaka michache kupita baada ya wa--NAZI wa Hitler,kuwaua wayahudi milioni 6 ,ndoto ya kuanzishwa kwa Taifa la Israeli kama ilivyotabiriwa kwenye biblia ilitimia,Mwishoni mwa mwaka 1948 ikiwa ni miaka 3 tangu kumalizika kwa vita kuu ya pili ya dunia ,Mataifa ya kiarabu majirani mwa Israel yaliivamia Israel yakijaribu kuliangamiza Taifa changa ambalo muda mfupi tu lilikuwa limetangazwa na Umoja wa Mataifa kuwa Taifa huru, lakini hayakufanikiwa.

Jeshi la misri lilipigwa lakini askari waliokuwa kwenye eneo dogo linalojulikana kama Falluja walikataa kusalimu amri ,kundi la askari wa Misri na Israeli walipambana vikali ,Miongoni mwa askari Vijana waliokuwa kwenye kikosi cha jeshi la Israel alikuwa ni Yitzhak Rabin ambaye alikuwa na umri wa miaka 26 wakati huo, Pamoja na Meja Gamal Abdel Nasser wa jeshi la Misri aliyekuwa na miaka 30,Wapalestina wanauita mwaka 1948 kuwa ni "al--Nakba" yaani 'Janga' .Zaidi ya wapalestina 750,000 walifukuzwa kutoka kwenye eneo ambalo sasa linajulikana kama Taifa la Israel na hawakuruhusiwa kurudi tena mahali hapo,Mataifa ya Misri, Jordani, na Syria yaliungana pamoja kuishambulia Israel ambayo hata hivyo ndiyo kwanza ilikuwa imepewa hadhi ya kuwa taifa huru. Lakini kwasababu Mungu alikuwa amesema kwamba "Kabila moja litakuwa hodari kuliko la pili" ni wazi kuwa Israel ,likiwa taifa changa ,bado lilifanikiwa kuwashinda majirani zake tena ndani ya siku 6 tu.

Nimalizie kwa masuala kadhaa ambayo Israel na Palestina hawawezi kukubaliana,Masuala hayo yanashirikisha maswali kama vile ni nini hatma ya wakimbizi wa Palestina,kwa sasa vurugu zinapoendelea kutokea wapalestina wanayakimbia maeneo yao ya West bank na Waisrael wanayachua kwa kupeleka wakandarasi wao na kujenga majengo ya Waisrael,tukifikia hapo sasa tunajiuliza makaazi ya Wayahudi ya West bank yanafaa kuondolewa ama yaachwe , iwapo wawili hao wanafaa kutumia kwa pamoja mji wa Jerusalem na pengine kubwa zaidi ni iwapo taifa la Palestina linafaa kutengenezwa pamoja na lile la Israel,bado Wayahudi wanaishi kwa mtindo wao wa zamani,wanakivamia ukikimbia wanajenga nyumba zao,wanaishi,walifanya hivyo kwa miaka mia nne waliyokuwa njiani kutoka Misri kurudi Israel,

Baraka za Mungu bado zinaishi,Mkono wa Baba Isaka ulipotua kichwani kwa Jacob,baraka zikajaa kwa Jacob na uzao wake,na kaka yake Esau kwa kukosa baraka za Baba yake,basi akageuka mtumwa wa mdogo wake,Nani mtoa baraka!? Ni Mungu,nani wa kumaliza mgogoro wa Esau na Jacob ni Mungu mwenyewe,hii itadhiirishwa kwenye vita kuu (Armageddon)baina ya Esau (Palestina) na Mbarikiwa (Jacob) vita hiyo itasababishwa na Mataifa yatakayokwenda kusaidia Mataifa ya Israel na Palestina,Mji mtakatifu wa Jerusalem utaharibiwa na kitovu cha vita hiyo kitakuwa katika Mji wa Megido lilipo bonde la Armageddon linatenganisha vilima vya Galilaya,hapo ndipo Yesu Kristo atakaposhuka kwa mara ya pili na kuituliza dunia na kuanzisha miaka elfu moja ya Utawala wa amani hapa duniani (Millenium) ambapo Simba atacheza na Swala na Chui atakaa pamoja na mwanakondoo,Ufu 21:1-2 Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya,kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita,wala hapana bahari tena,Nami nikauona mji ule mtakatifu,Yerusalemu mpya,ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu,umewekwa tayari kama Bibi harusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.

-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;-
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Nikisoma habari za Israel na Palestine nikaona tu kipengele zimenukuliwa Aya za dini, basi naishia hapo hapo kusuma. Na namuona mwandishi hajui kuhusu mgogoro huo, bali amejaa 'ukungu' wa dini kichwani. Nikukumbushe tu viongozi wengi mfano wa Israel ni atheist. Mfano hai ni Benjamini Netanyahu.

By the way huu mwisho wa dunia, just like religion is a human made concept. Babu yangu alinisimulia kuwa yeye tangu mtoto anasikia mwisho wa dunia umekaribia, way back hata taifa la Israel halijazaliwa. Its about 100 years na maisha yanazidi kuongezeka. Watu wa Mayan walidai 2012 ndio mwisho wa dunia, leo ni 2021 and we got a female President in here!

Fanyeni kazi mtengeneze maisha bora ya vizazi vyenu. Dunia ipo tu.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom