Mgogoro wa Iran Vs Azerbaijan (Israel) Vs Armenia vita vitalipuka soon

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,819
17,409
Israel ilikua inataka kuishambulia Iran kupitia Azerbaijan ambayo ni nchi jirani ni Iran

Tayari inasekemana ndege za Israel za F-35 zipo ndani ya Azerbaijani tayar kuishambulia Iran

Wakati huo huo Iran imeshaonya kwamba ikiguswa tu basi Kitawaka...Iran ilipeleka boti za kivita 400 mpakani na Azerbaijani na tayari wamerusha ndege za kivita juu na mifumo ya ulinzi na jeshi la iran lipo macho

Huku na huku kumbe Azerbaijani na Iran wana mkataba kwamba ni marufuku adui wa kati ya nchi hizo mbili kutumia anga au ardhi yao kuishambulia nchi hizi

Iran ameapa hatoruhusu israel iweke base karibu yake yaani hapo Azerbaijani na baada ya Azerbaijani kumkaribisha Israel kuna taarifa kwamba Amernia ambaye ni adui wa Azerbaijani ameiruhusu Iran kuweka kituo cha kijeshi nchini mwake kitu ambacho Azerbaijani kitamcost sana...

Israel anataka kuishambulia Iran kupitia Azerbaijani

Azerbaijan na Iran wana mfanano wa kidini wote ni waislam wa Shia Lakini Azerbaijani anaungwa mkono na Uturuki ambaye ni sunni japo waazeri na waturuki wanafanana kitamaduni muonekano hadi Lugha kwa lugha rahisi unaweza sema ni waturuki wale

Azerbaijan wanahofia kwa kua wao ni shia basi nchi yao isije ikawa kama ya kimapinduzi km iran yaan anahofia ushawahi wa Iran nchini mwake usije zalisha jamhuri ya kiislam kwa kua ni Shia

Iran anamuunga mkono Armenia ambaye ni adui wa Azerbaijan Armenia ni nchi ya kiikristo na wale wanafanana na Warusi hadi kiitikadi na ukristo wao ni wa kiothodox ambao ni sawa ni warusi walowengi

Sasa huu mgogoro una sura ya hivi

Iran/Russia/Armenia Vs Azerbaijani/Turkey/Israel

Nitazidi kuwapa updates

Pichani ni Rais wa Azerbaijani cheki walivyofanana na waturuki

FB_IMG_16338714756010191.jpg



Update: Iran imepeleka mfumo wa kujilinda wa makombora karibu na mpaka wake na Azerbaijan

Israel inatarajia kufanya mazoezi makubwa kaskazini mwa Israel
 
Armenians hawafanani kabisa na Warusi they are ethnically different. Armenia ni former soviets ndio and are not ethnically Russian s wako tofauti na Warusi kimuonekano hata na lugha. Nilishaletaga hata thread yao kuwahusu humu.

Armenians wana utofauti sana kiitikadi na majirani zao wa karibu Georgians na Azabaijan/Azeris karne na karne.

Halafu kanisa la Armenia ni Armenia apostolic church tofauti na Russian orthodox.

Kuhusu Azeris ama Azarbajain lugha yao ndio inashabiana na turk kwasababu wametoka same language group TURKIC yani kama bantu na turks lakini siyo ethnics turks.

Hata Persians, (Iranians) Uzbek, kyrgyst, Turkmen, Mongols, khazan na Tajik wote hao lugha zao zinashabiana na TURKIC language but are not ethnic Turkish.

Hadi Uyghurs wa China ambao wachina wanawaonea ni TURKIC language group lakini hawafanani na wa Turks lakini lugha yao inashabianashabi
 
Israel ilikua inataka kuishambulia Iran kupitia Azerbaijan ambayo ni nchi jirani ni Iran

Tayari inasekemana ndege za Israel za F-35 zipo ndani ya Azerbaijani tayar kuishambulia Iran...
Urusi ana mkataba wa Ulinzi na Armenia lakini pia ana mikataba ya kibiashara na Azerbaijan, ndio maana hata vile vita vya majuzi kati ya Armenia na Azerbaijan, mrusi alifanya kazi ya usuluhishi tu.
 
Urusi ana mkataba wa Ulinzi na Armenia lakini pia ana mikataba ya kibiashara na Azerbaijan, ndio maana hata vile vita vya majuzi kati ya Armenia na Azerbaijan, mrusi alifanya kazi ya usuluhishi tu.
Zote hizo Armenia Azerbaijan zilikuwa Soviet ya zamani former Soviet.
 
MIMI NTAKUWA REFA .....

ILA SINA KADI .....

WAKANYAGANE TU ....

nipo nakula ugali kisamvu kwahiyo hayo mambo ya war
 
Israel ilikua inataka kuishambulia Iran kupitia Azerbaijan ambayo ni nchi jirani ni Iran

Tayari inasekemana ndege za Israel za F-35 zipo ndani ya Azerbaijani tayar kuishambulia Iran...
Mashetani ya Iran yalikuacha kwa muda naona yamekurudi kwa nguvu na kukupagaisha hapo morogoro, hamia huko Iran kachukue mabomu ukajilipue Israel ili moyo ukutulie uwahi kuzimu
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom