Ndugu wana-Mara naomba nasi tuungane kutetea mali zilizopo Mkoani kwetu kufaidisha Wanamara kwanza, hii ni kama Mtwara watakubaliwa ombi lao. Mara imekuwa nyuma kwa siku nyingi na wala huwezi amini kama Baba wa Taifa hili alitokea huku. Mtwara wanataka gesi ila sisi tuombe tu vitu viwili vinufaishe kwanza Mara ambavyo ni;
Naamini yote haya yakifanyika wananchi wa Mara tutapata ajira na umasikini tutautokomeza kabisa, kama wenzetu watakubaliwa nasi serikali sikivu haina budi kutujali kwa haya machache yasema. Kila mtu ale kulingana alipozaliwa ndipo Mungu alipompendelea kuwa. Wana-Mara nawomba nasi tuungane tutetee mali zetu tulizopewa na Mungu kwani siku ya mwisho atakuja tuuliza; Niliwapa taranta hamkuzitua mkawachia wengine. Tuamke sasa tuache kutoana roho kwa imani ya kishirikina tuchukue mali zetu hadi kieleweke.
- Mbuga ya Serengeti - Hii Mbuga imekuwa inawanufaisha sana watu wa Arusha sana bila kujali wananchi wa Mara. Hivyo tunatakiwa tuombe watarii wote wanaoenda kwenye Mbuga ya Serengeti waanzie Mara na wala siyo Arusha kama ilivyo sasa. Nyumba zote za Watalii zijengwe Mara, Usafirishaji wa wanyama poli wenye vibali ufanyikie Mara ikiwa ni pamoja na kujenga uwanja wa Ndege wenye hadhi.
- Migodi ya dhahabu - Kwasasa kuna mgodi mmoja wenyemuwekezaji hivyo ajira zote zitoke Mara, labda wawekwe wasimamizi tu wa vitengo husika kutoka mbali na Mara na wao wapewe masharti ya kuwafundisha wazawa ujuzi, ili kesho kujiendeshe wenyewe.