Mgogoro wa Eng. Muhando na mabosi wake: Siri yafichuka, anaeimaliza TANESCO NI JK

Kama JK yuko hivi basi hafai. Ila mambo haya yanahitaji uchunguzi wa kina isijekuwa una mchafua Rais wetu mwema.
 
Kwa wasiomjua Maswi, huyu jamaa ni noma, ni mzalendo na mchapa kazi kinoma yaani.......! Makampuni kibao ya madini yamejaribu kumchongea ili apigwe chini kwakua anayabana sana, lakini JK amemlinda huyu bwana. Maswi akiweza kudumu miaka mingine 3, tanzania itakuwa sehemu nzuri ya kuishi.

Wote wanao mlalamikia Maswi ni kwakua, kupitia Muhando, mboma, wanafaidika na matatizo yanoyoendelea Tanesco. Prof; Muhongo naye ni mpiga kazi, nadhani tuwaache wafanye kazi. Kama sheria imevunjwa kwa maslahi ya umma, basi zivunjwe tu na nyingine nyingi, kuliko kuheshimu sheria ili tukangamizwe.

Kibanga Msese
 
ila nachoshangaa mimi cjui y hawaridhiki na pesa walizochota!hiv hawajui km kuna kufa?jk na wenzako waoneeni huruma watz maskini jamani
 
Siku hizi tunaweza kutunga story tamu! Yaani tunafika mahala tunasema Mhando kaonewa? Kiongozi mwadilifu ya nini uchukue familia yako ifanye biashara na kampuni unayoiongoza. Hata kama alipata tenda kihalali lakini sheria ya manunuzi haitaki hasa kama haku declare conflict of interest. Kuhusu Puma kama zerikali iliweza kuokoa Tshs. 400.00 kwa lita ubaya uko wapi hasa ukizingatia Puma inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na serikali. Pia ikumbukwe kwamba kabla Serikali haijaamua hivyo ilipata ushauri toka Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma.
 
Wana JF,

Taarifa za kiintelijensia toka kwa wanaTISS wachache waliobakia na uzalendo kwa taifa lao zinsema, Rais wetu JK ndiye aliyetega mirija kila kona kuhakikisha anachota kila kinachoingia Tanesco.

IKO HIVI:

Mtakumbuka vizuri kuwa kampuni ya Richmond ilitengenezwa mikononi mwake huku akimtumia Lowassa kufikisha ujumbe Tanesco. Mambo yalipoharibika alimtoa kafara rafiki yake. Japo Lowassa amejigamba mara nyingi kuwa hawakukutana barabarani, ukweli ni kuwa bado hamjui vizuri swahiba wake.
Mgogoro uliopo Tanesco baina ya Muhando na wakuu wake ni wa kutengenezwa ili kuwaokoa katibu mkuu bwana Maswi na waziri wake Prof. Muhongo. Pamoja na kwamba Muhando ametengeneza tenda aliyompa mkewe hiyo si ishu kubwa kwa kuwa vifaa kweli vitakuwa supplied ila deal alilopiga katibu mkuu la kuingia mkataba Puma Company Ltd (zamani BP) ambayo haina sifa na pia kufanya kinyume na sheria za PPRA simply because JK anahisa hukoa ndiko kulikokuza ishu ya mhando ili atolewe kafara uma usiangalie deal hilo lenye thamani ya bilioni 26.
Ukweli ni kwamba wabunge wakiamua kukomaa JK bye bye. Lakini taarifa zinasema JK amemwagiza Pinda kuhakikisha anawaziba midomo wabunge wote wazalendo. Taarifa zinasema Anne Kilango ameingia laini na katika moja ya vikao vyao vilivyoongozwa na Pinda alisimama kidete kutetea kuwa joja hii ikijadiliwa bungeni serikali na chama chao cha CCM vitaanguka!
Aidha taarifa zinazidi kusambaa kuwa JK ametoa maagizo kwa viongozi wa wizara ya nishati na madini tangu wakati wa Ngeleja kuwa hakuna kutumia gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme badala yake majenereta yatumie mafuta mazito ambayo asilimia kubwa yatatoka GAPCO ambako yeye anahisa tangu akiwa waziri.Swali la msingi; Kama gesi imetoka all the way from mtwara to ubungo, mafuta ya nini?
Aidha Tanesco hulazimishwa kutengeneza mgao feki ili bwana mkubwa achote chake. Isitoshe maajabu mengine ni kwamba Tanesco wameingia mkataba na kampuni ya Ridhiwani ya kuleta nguzo za umeme toka Afrika Kusini na si Iringa tena. Yapo mambo mengine mengi tangu Richmond, DOWANS, Symbion na haya ma-IPTL, Agreko n.k ambayo JK anayajua vema lakini ameendelea na roho ngumu ya kuwanyonya watanganyika.

Ombi langu kwa Mungu, Avuruge nchi hii ili tuanze upya.
Wana bodi mnasemaje?

dah! Hapo mwisho pazito ila pa ukweli
 
Hili hitimisho ulilo bold limenifanya nikuone mwongo, nakubaliana na aliyesema unahitaji maombi.
 
lisemwalo lipo kama halipo basi liko njiani hizi tuhuma ni nzito sana lakini ukweli utabaki kuwa ukweli tusubiri hata kama mhando ametenda kosa basi aadhibiwe kulinga na kosa lake lakini kwa upande wapili tuangalie jk na makapuni yake wanavyotunyonya bila huruma hata kidogo wao wana kombeleza tuweni makini sana nchi hii inapoteza mvuto na heshima kama mwanzo.
 
haya ya Tanesco na wizara ya madini na nishati yameshanikifu ngoja nikaangalie kwenye Atm kama kuna chochote nipate safari mbili tatu liwalo n liwe!!
 
Siku hizi tunaweza kutunga story tamu! Yaani tunafika mahala tunasema Mhando kaonewa? Kiongozi mwadilifu ya nini uchukue familia yako ifanye biashara na kampuni unayoiongoza. Hata kama alipata tenda kihalali lakini sheria ya manunuzi haitaki hasa kama haku declare conflict of interest. Kuhusu Puma kama zerikali iliweza kuokoa Tshs. 400.00 kwa lita ubaya uko wapi hasa ukizingatia Puma inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na serikali. Pia ikumbukwe kwamba kabla Serikali haijaamua hivyo ilipata ushauri toka Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma.
kimbunga na mafisadi patamu hapo!!
 
Sasa naanza kuamini kwamba mhando ni mwizi na kwa maana hiyo naendelea kuprove kuwa nchi hii kila mtu ni fisadi.

Wewe ni fisadi? Ufisadi wako unaufanyia wapi na kwa kutumia mbinu zipi? Kingcobra eleza yote ili kupunguza gharama za upelelezi
 
Last edited by a moderator:
Hivi kwanini kampuni imebadili jina kutoka BP?

walifungiwa kutokana na kuendesha mgomo wa kuuza mafuta! pia wanakwepa kodi!

Mkuu chuwaalbert BP haikubadili jina ila biashara za BP katika maeneo mengi ya Afrika zimenunuliwa na Puma.

Mkuu OSOKONI hawa jamaa wa BP walikuwa na viwango vya mafuta ambavyo ni vya kimataifa wao wakawa wanauza bei ya juu kwa kuwa viwango ni tofauti na vya uchakachuaji. EWURA waliposhusha bei jamaa wakagoma, wakafungiwa kiusaniii lakini wakarudi sokoni baada ya muda lakini wakati huo walikuwa kwenye mchakato wa kujitoa kibiashara katika baadhi ya nchi za kiafrika Tanzania ikiwemo.
 
Last edited by a moderator:
Olewao,
Taarifa unayoileta na unachokitetea ni vitu viwili tofauti. Hivi mkurugenzi kutoa tenda kwa mke wake ni jambo la kawaida tu? Serikali kununua mafuta kwa bei nafuu kuliko iliyopangwa na mafisadi ni kitu kibaya?
Ukweli ni kuwa makampuni mengi yanayopewa tenda ya kusupply mafuta serikalini yanahonga kwa kiasi kikubwa. Kampuni pekeee ambayo ilikuwa haiwezi kuhonga hata senti moja, hata kama ungekuwa bosi na unahamu ya kupata tenda nono ni BP na Shell. Kwa kuwa makampuni makubwa yameondoka kwenye soko na kuachia kampuni ambazo nyingi zinamilikiwa na wezi hasa kutoka barani Asia imekuwa ni mtindo wa kushindana nani anatoa pesa kubwa. JK ana matatizo yake na lazima atakuwa anasababisha maovu Tanesco lakini hamiliki PUMA. Puma wana uwezo mkubwa wa kifedha na wana mafuta mazito ya mitambo (HFO). Haya makampuni mengine yananunua toka PUMA na kusupply serikalini kwa bei kubwa zaidi. Huu ndio mchezo ambao umekimbiza makampuni makubwa na yenye uwezo wa kutoa ajira na huduma zenye tija kama BP, Shell na zingine. Ni kwamba BP kwa kuwa walikuwa hawahongi walikuwa hawapati hizo tenda kubwa kirahisi. Walichokuwa wanafanya makampuni ambazo nyingi zinamilikiwa na wahindi au kuwa na ubia na wahindi ni kuwahonga maafisa wa serikali ili wapate tenda. Wakishapata tenda wanaenda kununua mafuta BP na kuiuzia serikali kwa bei kubwa. BP hata wakienda serikalini kwa bei ndogo waliyonayo hawapewi hizo tenda kwasababu hawatamuhonga mtu. Huu ni mchezo mchafu. Kama Maswi na Prof. Muhongo wamekuwa jasiri na kukataa huu mchezo mchafu wa Tanescco lazima tuwape credit. Naamini Profesa ameona udhaifu na kiini hasa cha tatizo ndio maana tangu ameingia amekuwa akituhakikishia kuwa umeme utakuwepo.
Kitu kingine ambacho mjiandae na mkijue enyi makuwadi wa ufisadi na makampuni uchwara ya mafuta yanayonyonya jasho la watanzania kwa ujira wa kimaskini huku mkituibia fedha tunazolipa kodi kwa jasho hilo la damu, mjue PUMA sio BP wala Shell. Si kubwa kama BP wala Shell lakini wamejiandaa kuingia sehemu zote za dunia kila sehemu kulingana na mazingira yake. Wananunua makampuni kila pembe ya dunia hii. Sijui wanatoa pesa zao wapi lakini wana unafuu kwa huduma na ajira kwa wenyeji kuliko hawa wezi wa kihindi wanaonyonya watanzania wenzetu. Biashara ya mabilioni lakini mshahara shilingi laki tatu. Kwa hiyo mchezo wenu wa kutajirikia kwa mgongo wa serikali kwa kutuibia mbali na kusiginwa na watendaji waadilifu ndani ya serikali unaweza kusiginwa pia na uwepo wa PUMA badala ya BP.
 
siku hizi tunaweza kutunga story tamu! Yaani tunafika mahala tunasema mhando kaonewa? Kiongozi mwadilifu ya nini uchukue familia yako ifanye biashara na kampuni unayoiongoza. Hata kama alipata tenda kihalali lakini sheria ya manunuzi haitaki hasa kama haku declare conflict of interest. Kuhusu puma kama zerikali iliweza kuokoa tshs. 400.00 kwa lita ubaya uko wapi hasa ukizingatia puma inamilikiwa kwa kiasi kikubwa na serikali. Pia ikumbukwe kwamba kabla serikali haijaamua hivyo ilipata ushauri toka mamlaka ya usimamizi wa manunuzi ya umma.
rais mkapa alifanya biashara na mkewe akiwa ikulu na kuiba pesa nyingi mbona hakuna anayelalamika???
 
Nji hii ukiichimba sana utapata kichaa .......mungu atulaani tuokote makopo kwani tayari sisi ni wagonjwa wa akili
 
rais mkapa alifanya biashara na mkewe akiwa ikulu na kuiba pesa nyingi mbona hakuna anayelalamika???

Labda wewe na mafisadi wenzio ndio hamlalamiki. Sisi wazalendo tumechukizwa na tunataka mkapa apelekwe mahakamani.
 
Back
Top Bottom