Mgogoro wa CUF unavyokoleza kero za Muungano. RITA, Ofisi ya Msajili ijitathmini

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Kwa wazanzibari walio wengi sasa ni wazi kuwa wanaamini kwamba taasisi za muungano zinaendelea kutumika kuhujumu haki za Zanzibar na imefika pahala vyombo hivi vinahusishwa na hujuma za wazi.

Malalamiko dhidi ya TRA, Uajiri kwa vyombo vya muungano, mgao wa misaada kwa Zanzibar na mengineyo yamelalamikiwa kitambo kiasi cha kupelekea kuwa na chombo rasmi cha utatuzi wa kile kinachoitwa Kero za Muungano ambazo haziishi. Vyombo hivi viko chini ya uratibu wa ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais kule Zanzibar na kama sikosei ofisi ya Makamo wa Rais (SMT) kwenye wizara ya Muungano.

Imeelezwa mara kadhaa kuwa kuna kero nyingi hazipatiwi tiba na kila kukicha zinaongezeka.
Taasisi za Muungano zimelalamikiwa kwa njia tofauti ikiwemo kutozingatia usawa wa uwakilishi wa kimuungano kwenye mambo mengi na kufanya maamuzi ambayo kwa namna moja au nyengine yanaathiri Mamlaka za Zanzibar.

Sasa ni zamu ya RITA na Ofisi ya msajili.
Wazanzibari walio wengi wanahusisha mgogoro wa CUF kuwa ni wa kupandikizwa ili kuzima sauti ya wazanzibari ya kuchagua hapo 2015. Kujiingiza kwenye mgogoro huu kwa taasisi za Muungano za RITA na Ofisi ya Msajili kuchagua upande wa Lipumba na kujiegemeza wazi wazi kumeleta hasira nyengine huko Zanzibar kuhusu muungano. Kwa mujibu wa vyanzo vyetu, vinabainisha kuwa kuna joto kali na hisia kali zikihusishwa na hujuma dhidi ya CUF ili kupoteza SAUTI YA ZANZIBAR kwa mambo ya Muungano.

RITA na OFISI YA MSAJILI vinashutumiwa kwa kutaka kufanikisha Mission ya kuimaliza Zanzibar kwa kisingizio cha kesi ya Lipumba na kushutumiwa kuvuruga Maslahi ya mapambambano ya kudai HAKI ZA ZANZIBAR KWA NJIA YA KIDEMOKRASIA Kupitia CUF. CUF imebebeshwa jukumu la kudai Maslahi ya Zanzibar baada ya CCM kushindwa kutokana na mfumo wake.

Wazanzibari wanashutumu kuwa si tu kwamba Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania aliamuru jeshi kuvamia bwawani na kulazimisha mchakato wa kumalizia kutangaza matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar hapo 2015 kufanikiwa na Jeshi la Polisi kumshikilia Makamo Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ZEC kule Madema ili asiendelee kutangaza, Lakini kulipandikizwa Mgogoro wa Lipumba na sasa RITA na Ofisi ya Msajili inataka kukamilisha Mission. Zanzibar kuna fukuto.
Wazanzibari wengi wamelichora Jeshi letu, Polisi, TRA, na sasa RITA na OFISI YA MSAJILI kama kikwazo kwao kuelekea madai ya Haki.

Hali hii inazidisha chuki ya wazi na kuwafanya wazanzibari wajione wanyonge kwa kila hali.

Kupitia JF , tunatimiza wajibu wetu kuwakumbusha watawala na kwa sasa RITA na Ofisi ya msajili na Mahakama kutenda haki na kujitathmni kwa Maslahi yetu wote.

Huko Zanzibar kuna gumzo kutokana na mwenendo wa kesi za CUF na zimechochewa na kauli za Lipumba hapo jana alipohojiwa na DW aliposikika akibainisha kuwa mgogoro wake na Maalim Seif ni kutokana na kuunga mkono Muungano wa mkataba jambo analoona linataka kuvunja muungano. Hapa Lipumba amezidi kutonesha kidonda na kuwazindua wengi.

Jambo hilo limezua hisia kali kwamba kumbe Lipumba anatumika kuviza madai ya usawa wa Muungano kwa Zanzibar na wanahusisha huu mgogoro kuwa umepandikizwa makusudi. RITA na Ofisi ya Msajili zinatajwa kumbeba Lipumba ili kutimiza mpango huo. Hicho ndicho kinachoendelea huko Zanzibar.


Nini kitafuata wakati utasema.


Ni wakati wa RITA na Ofisi ya Msajili kujitathmini



Kishada
 
Back
Top Bottom