Mgogoro shamba la mwekezaji Moshi watua Mahakamani

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,799
21,395
Mgogoro baina ya mwekezaji katika shamba la Makoa, Elizabeth Stegmaier ambaye ni Raia wa Ujerumani na chama cha ushirika cha Uduru umeingia sura mpya baada ya pande zote mbili za mgogoro huo kukimbilia mahakamani.

=======

Moshi. Mgogoro baina ya mwekezaji katika shamba la Makoa, Elizabeth Stegmaier na chama cha ushirika cha Uduru umeingia sura mpya baada ya pande zote mbili za mgogoro huo kukimbilia mahakamani.

Mgogoro huo ulianza hivi karibuni baada ya wamiliki wa shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 368 chama cha ushirika cha Uduru –Makoa wilayani Hai kufunga malango ya shamba hilo wakimwamuru mwekezaji huyo kuondoka katika shamba hilo kwa madai ya kukiuka Mkataba.

Mwekezaji huyo ambaye ni Raia wa Ujerumani, kupitia wakili wake Henry Masaba alifungua kesi ya madai namba 4 ya mwaka 2022, katika mahakama kuu akipinga kuondolewa kwenye shamba hilo.

Katika madai yake, Stegmaier alidai kuwa chama cha ushirika kilikiuka taratibu za kisheria za kumwondoa shambani hapo Huku akiweka zuio la yeye kuondolewa shambani hapo hadi hapo kesi ya msingi itakaposikilizwa.

Hata hivyo, chama cha ushirika cha Uduru –Makoa kupitia kwa wakili wao, Engelberth Boniphace nacho kilipeleka maombi madogo ya kisheria mahakamani kikiomba mahakama kutoa amri ya kuzuia kufanyika kwa shughuli yoyote katika shamba hilo.

Leo Agosti 9, 2022 mawakili wa pande zote mbili walikutana katika Mahakama Kuu kanda ya Moshi ili kutafuta suluhisho la kisheria juu ya maombi ya pande zote mbili, ambapo Jaji Thadeo Mwenempanzi amepanga kuanza kusikiliza maombi hayo kwa mfululizo kuanzia Agusti 10, 2022.

Akizungumza nje ya mahakama, wakili Henry Masaba, anesema maombi ya amri ya kuzuia pande zote mbili kufanya chochote katika shamba hilo wamepanga yaanze kusikilizwa kesho Agusti 10, ambapo yatasikikizwa kwa mfululizo.

"Tumekuja leo kwa sababu kulikuwa na maombi ya haraka ambapo tumekubaliana yaanze kusikilizwa mfululizo kuanzia kesho, maombi haya ni ya zuio ambayo yameletwa na wenzetu wa uduru Amcos.

"Wenzetu waliomba amri ya mahakama ya kusimamisha chochote kisifanyike kwenye shamba lile na sisi tumeona maombi yale hayako sawa sawa hivyo kuanzia kesho mahakama itakuja kutusikiliza," amesema.

Aidha ameeleza kuwa kabla ya maombi hayo tayari kulikuwa na maombi mengine ambayo yaliletwa na Uduru kuzuia mwekezaji asiondoke pale na chochote ndipo mwekezaji nae akapeleka maombi kuomba asiondolewe mpaka shauri la msingi litakaposikilizwa.

Kwa upande wake wakili wa upande wa chama hicho, Boniphace amesema waliheshimu maombi ya mwekezaji huyo, lakini wakati huo waliona bado kuna vitu vinafanyika hivyo nao wakaomba mahakama kuweka zuio kwa pande zote mbili.
 
Back
Top Bottom