Mgogoro Ngorongoro: Gazeti la The Guardian, mmelipwa au ni kujitoa ufahamu?

blix22

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
213
645
Inasikitisha sana tunakoelekea, jana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea kata ya Loliondo mkoani Arusha na kwenye hoja za msingi alizoongelea tena kwa urefu na kuwapa wakazi wa eneo lile fursa ya kuchangia ni kuhusu pori tengefu la Loliondo.

Tena kama haitoshi alisisitiza kabisa kwamba baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi wa kata ya Loliondo atatenga muda kwenda kata ya Ngorongoro kuzungumza na wananchi kuhusu masuala ya uhifadhi.

Kubwa zaidi hakuna mwananchi hata mmoja kwa waliochangia aliongelea hoja ya ngorongoro, wote waliongelea suala la pori tengefu la loliondo na kutoa ushauri kwa Serikali ikiwemo kukubali hoja ya kusaidia kulinda pori hilo.

Hoja hapa ni hivi, Guardian ni kwamba wana maslahi gani na Ngorongoro? kuna mpango gani wa siri ambao upo nyuma ya chombo hicho cha habari? mwandishi aliyepelekwa huko alienda na story yake kichwani?

Umefika wakati wajitafakari na waone kama wanastahili kuitwa waandishi wa habari.
 
Kwanza umeandika kwa jaziba, hujatuwekea alichoandika huyo the guardian, alafu unataka mwandishi aandike ya waziri mkuu ahahahaaa...

HAPANA, kama yupo field basi kafanya utafiti pale alipoona kuna angle ya kutoka na habari kama hiyo ambayo wewe hukuipenda, sijaisoma ila nikiipata na kusoma "naweza" nitampongeza maana angeandika ya PM wengine mngesema amepewa bahasha ya kaki na kubebwa na magari ya serikali.
 
Sidhani kama wameshawahi kuwalisha maneno viongozi.

Alichosema mtoa mada hapo ni kwamba, GUARDIAN wameandika kisichosemwa na Waziri mkuu. Swali je wamelipwa?
Unadhani hii ndiyo post yako ya kwanza niliyoona hapa kuhusu Ngorongoro 🤣🤣🤣
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Na jamvi la habari na Kitenge wapo kwenye payroll ya nani???
Mbona unachanga Madesa Ndugu?

Umeona ulicho ripot leo Jamvi??

Na je kina utofauti na Alicho kisema PM?

Acheni chuki Binafsi. Hoja ya Mtoa uzi imeeleweka tujikite Hapo. PM kaongea vingine wao wamesema kwingine
 
nadhan mtoa uzi ana hoja, nimesoma hiyo habari pia nimefuatilia taarifa za habari nimemsikiliza PM, Guardian wanalo la kujibu, kuna mchangiaji anasema eti mwandishi alikuwa na haki ya kutafuta angle, sawa lakini anatafutaje angle ambayo haikusemwa na source huu ni udhaifu, anam quote nani?
 
Mbona unachanga Madesa Ndugu?
Umeona ulicho ripot leo Jamvi??
Na je kina utofauti na Alicho kisema PM?
Acheni chuki Binafsi. Hoja ya Mtoa uzi imeeleweka tujikite Hapo. PM kaongea vingine wao wamesema kwingine
Mbona Jamhuri wameandika kitu kingine? Yaani waziri mkuu kapeleka nuru kule Ngorongoro, wao wanasema kiza nene.
Jamhuri tunawajua kwa kutumika. Waliwahi pia kutumika kumchafua Kigwangala kuhusu vitalu na promotion za utalii kupitia wasanii.

Liliwahi pia kutaka kuichafua serikali ya JPM kwa kuelezea mikopo kinyume na utaalam wa mikopo.
Hata hivyo wameshaumbuka baada ya kuona hao wanaowatumia ndio wakopaji wa hovyo kuwahi kutokea toka nchi hii ipate uhuru.
 
Hawa waandishi wa siku hizi njaa tupu. Inakuwaje mwandishi aandike story tofauti na asichukuliwe hatua na mabods wake wa gazeti? Unapotoshaje kauli ya mmojawapo wa Viongozi wakuu wa nchi wakae kimya? Guardian mna matatizo.

Labda mwandishi naye anatoka Jamie hiyo hiyo iliyoko hifadhini. Watanzania jitahidini kuwa makini na kauli zenu na ufuatiliaji siyo kutoa story mfukoni. Ndo maana ninataka kukimbia upinzani niache siasa.

Siasa za majitaka za waandishi nazo zinakera. Tujenge hoja za mashiko ndo tufikishe kwa wananchi.
 
Mbona Jamhuri wameandika kitu kingine? Yaani waziri mkuu kapeleka nuru kule Ngorongoro, wao wanasema kiza nene.
Jamhuri tunawajua kwa kutumika. Waliwahi pia kutumika kumchafua Kigwangala kuhusu vitalu na promotion za utalii kupitia wasanii.

Liliwahi pia kutaka kuichafua serikali ya JPM kwa kuelezea mikopo kinyume na utaalam wa mikopo.
Hata hivyo wameshaumbuka baada ya kuona hao wanaowatumia ndio wakopaji wa hovyo kuwahi kutokea toka nchi hii ipate uhuru.

sasa wewe nae utakuwa unatatizo hebu kasome story ya Jamhuri wale wamefanya analysis, tena bila nukuu za kubumba kama walivyofanya guardian, ndugu zako hao wamemnukuu majaliwa kuhusu Ngorongoro wakati wote tumesikia ameongelea mgogoro wa Loliondo. Shame kwa Guardian Big failure.
 
Back
Top Bottom