Inasikitisha sana tunakoelekea, jana Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea kata ya Loliondo mkoani Arusha na kwenye hoja za msingi alizoongelea tena kwa urefu na kuwapa wakazi wa eneo lile fursa ya kuchangia ni kuhusu pori tengefu la Loliondo.
Tena kama haitoshi alisisitiza kabisa kwamba baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi wa kata ya Loliondo atatenga muda kwenda kata ya Ngorongoro kuzungumza na wananchi kuhusu masuala ya uhifadhi.
Kubwa zaidi hakuna mwananchi hata mmoja kwa waliochangia aliongelea hoja ya ngorongoro, wote waliongelea suala la pori tengefu la loliondo na kutoa ushauri kwa Serikali ikiwemo kukubali hoja ya kusaidia kulinda pori hilo.
Hoja hapa ni hivi, Guardian ni kwamba wana maslahi gani na Ngorongoro? kuna mpango gani wa siri ambao upo nyuma ya chombo hicho cha habari? mwandishi aliyepelekwa huko alienda na story yake kichwani?
Umefika wakati wajitafakari na waone kama wanastahili kuitwa waandishi wa habari.