CRITICAL MIND
JF-Expert Member
- Sep 1, 2013
- 415
- 386
JK na Nyalandu tumewapa mandate sisi wananchi na kazi yao ni kutuwakilisha kama taifa na maslahi ya taifa. Haimaanishi kuwa JK ni Sultan hivyo asitueleze kinachoendelea au asiwajibike kwa sisi wananchi. JK asipowajibika kwetu inamaana atakuwa anakwenda kinyume na katiba aliyoapa kuitetetea na maslahi ya nchi hii.
Hivyo bas, tunaweza kusema kuwa kinachoendelea na mgogoro na Kenya ni aibu kitaifa na mbaya zaidi kuna issues za NATIONAL INTEREST ambazo ziko at stake na moja wapo ni mapato.
Sasa kwa nini hawa masultani wetu hawataki kutuambia kwa nini waligoma kwenda kwenye mkutano na Kenya kutatua hili tatizo? Kwa nini tunafichwa? hii hiki kimya maana sisi kama wananchi tukitafsiri vipi?
Kwa sababu hawa watawala wetu hawataki kuwa honest na sisi basi wengine hatuna namna bali kuweka wazi tunayojua halafu ikifika AlHamis wiki hii Kurugezi ya mawasiliano ikulu itatoa statement kupinga tunayosema humu JF, Wizara ya Utalii nao watatoa statement kupingana na Ikulu, kule mambo ya nje nako wapambe wa Membe watatulea story kupingana na Ikulu na wizara ya Utalii na mwisho kabisa bodi ya utaliii nao watakuja na yao na bila kusahau MAELEZO watakuja na ngojenra tofauti ambazo zitalenga kuishambulia JF.
In short serikali hii ya BIG RESULTS NOW imekuwa incompetent kuliko club ya wendawazimu.
So far FACTS ni hizi:
1. Serikali ya JK ilijulishwa kuhusu mkutano na Kenya kujadili na kusuluhisha hili jambo zaidi ya miezi 3 iliyopita na walikubali watahudhuria na wenzao kule kenya waliwapa list ya agenda za mkutano
2. Serikali ya JK wakakumbushwa tena na wakasema hamana neno. Lakini out of blue KAMA VINYONGA wakaaanza na mambo ya "SUBRA" na mwishowe wakadai kuwa pamoja na facts zote kuwa on the record na wao kuwa na wasomi walio bobea wakadai waongezewe muda, ili wataalam or who ever those wonks are eti watengeneze comprehensive list ya madai ili kupata mbadala wa mkataba wa 1985 baina ya Kenya na Tanzania juu ya utalii.
3. waziri wa utalii wa Tanzania NDUGU Nyalandu amekuwa kama vile anaongoza team ya wapiga ramli ambayo kila mmoja anasema lake. Inaovyoonekana kuwa kulikuwa hakuna coordination kama kawaida ya hii serikali, Maofisa wake walikuwa wanaendelea na mikakati ya kufanya huo mkutano lakini wakapigwa STOP na mabosi wa Wizara ya Mmabo ya Nje bila kupewa sababu zizote zile. Wakati huo huo Ndugu Nyalandu alikuwa anaendelea kuwaambia waziri mwenzake wa kule Kenya kupitia e-mail yake kuwa : "the meeting will take place without any delays considering it might cost Tanzania greatly if nothing has been agreed"
4. Nyalandu alijua kuwa mkutano uliongezwa tena wiki 2 zingine lakini si yeye wala maofisa wa serikali ya JK walifanya juhudi zozote zile huku wakijua wazi kuwa muda wa huo mkutano usingeongezwa tena na walijua fika the price watu wetu wangelipa kama kusingekuwepo na makubaliano hata ya muda mfupi ili faifa lisipate hasara.
5. Ukweli ni kuwa tatizo ni JK na serikali yake kwa sababu watalii wanashindwa kutua Kilimanjaro kwa sababu hakuna connectivity kubwa na hii inatokana na serikali ya nchi hii kutoona umuhimu wa kuongeza investments kwenye KIA na wanajua kama investments kwenye uwanja wa Kia mapato yangezidi na ndege nyingi zingekuwa zinatua hapo na hii kadhia ya kutua JKIA isingekuwepo.
6. Kma serikali iligoma kwenda kwenye huo mkutano wa tarehe 5 kwa nini hawakuwajulisha TATOA mapema? Hivi serikali ita wa refund haya makampuni au itakuwaje? na kwa nini serkali haitaki kuwa wakweli kwa watanzania? na kwa nini kila kitu chenye maslahi kwa wananchi kinafanywa kisiri siri? na je nani ananufaika na huu mgogoro?
Sasa ngoja nitafute CAG report juu ya hii wizara ya utalii na maliasili nione wana madudu gani.
Last edited by a moderator: