Mgogoro mkubwa wa ardhi kati ya wilaya ya Kibaha na Kisarawe – Vita ya wakulima na wafugaji yafukuta

Mu-Israeli

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
2,454
975
Ni muda mrefu sasa kumekuwa na mgogoro wa mpaka kati ya wilaya hizi mbili za Kibaha na Kisarawe. Mgogoro huu ni wa zamani kidogo tangu mwaka 2006.

Juhudi za kutatua mgogoro huu zilifanyika mwaka 2014, na wataalam kutoka wizara ya ardhi makao makuu Dar es Salaam walienda kusuluhisha mgogoro huu kwa kushirikiana na viongozi wa pande zote mbili za Kibaha na Kisarawe.

Wataalam hao walitakiwa kuchora upya mpaka kati ya wilaya hizo za Kibaha na Kisarawe na kuweka mawe ya mipaka ili kumaliza kabisa mgogoro huo.

Lakini tangu mwaka huo wa 2014 hakuna jitihada zozote zilizofanyika ili kukamilisha utatuzi wa mgogoro huo, hivyo kutoa mwanya kwa watu wachache kuuendeleza mgogoro huo kwa manufaa yao binafsi.

Ni hivi karibuni tu mnamo mwezi wa November 2016 mgogoro huu uliibuka kwa kishindo kikubwa sana pale wafugaji kutoka kijiji cha Mafizi wilaya ya Kisarawe walipojichukulia sheria mikononi mwao na kujipa mamlaka ya kuweka mipaka kati ya wilaya hizo mbili.

Wafugaji hao walijipa mamlaka hiyo na kuamua kupeleka bulldozer ambalo walilitumia kuweka alama za mpaka kati ya wilaya hizo mbili.

Uwekaji huo wa mipaka hii uliofanywa na wafugaji kutoka kijiji cha Mafizi wilaya ya Kisarawe, ulimega eneo kubwa sana la kijiji cha Kitomondo kilicho katika wilaya ya Kibaha na kuliweka upande wa wilaya ya Kisarawe.

Viongozi wa kijiji cha Kitomondo ambacho eneo lake lilimegwa walipohoji uhalali wa zoezi hilo walijibiwa kuwa wafugaji ndio wameweka alama hizo za mipaka, na kuwa huo ndio mpaka rasmi wa wilaya hizo.

Cha kushangaza zaidi ni kuwa uwekaji huo wa mipaka ya wilaya uliofanywa na wafugaji hao ulipata baraka zote za viongozi wa wilaya ya Kisarawe akiwemo mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Happiness William.

Mkuu huyo wa wilaya ya Kisarawe katika kikao chake na viongozi wenzake kilichofanyika tarehe 16th November 2016 katika kijiji cha Mafizi wilaya ya Kisarawe, alitamka kuwa anatambua rasmi mpaka huo kati ya wilaya yake ya Kisarawe na wilaya ya Kibaha, mpaka ambao uliwekwa na wafugaji kutoka wilaya yake ya Kisarawe.

Mkuu huyo wa wilaya ya Kisarawe alisisitiza kuwa kitendo cha wafugaji hao kuweka mpaka huo wa wilaya ni sahihi kabisa, na kwamba wakulima wote walioko kwenye eneo lililoporwa na wafugaji hao wanatakiwa kuondoka kwenye eneo hilo.

Hivyo, mkuu huyo wa wilaya ya Kisarawe Mh. Happiness William akatoa agizo kuwa mpaka huo ndio mpaka rasmi kati ya wilaya yake ya Kisarawe na wilaya ya Kibaha, na kuwaagiza wafugaji hao kuweka uzio kwa kutumia mapipa, nguzo na waya kwenye mpaka huo, ili kuzuia mifugo na watu wasiweze kupita kwenye mpaka huo uliowekwa na wafugaji.

Wafugaji hao sasa wamewazuia kabisa wakulima wa kijiji cha Kitomondo kwenda kwenye mashamba yao ambayo yapo kwenye eneo lililoporwa na wafugaji hao. Wafugaji hao wameweka vijana wao ambao wanalinda mpaka huo ili kuwazuia wakulima kwenda mashambani kwao.

Hali hii imechochea uhasama kati ya wakulima wa kijiji cha Kitomondo kilicho wilaya ya Kibaha dhidi ya wafugaji wa Kisarawe, kwani eneo la wakulima hao limemegwa na wafugaji, na sasa wakulima hao hawana eneo kwa ajili mashamba yao.

Mbaya zaidi, ni kitendo cha mkuu wa wilaya ya Kisarawe Mh. Happiness William kubariki uporaji huo wa ardhi ya wakulima wa kijiji cha Kitomondo wilaya ya Kibaha, na kuamrisha wafugaji waweke uzio ili kuwazuia wakulima wa kijiji cha Kitomondo wasiweze kwenda kwenye maeneo ya mashamba yao.

Maoni yangu:-

· Hali ya watu kuchukua sheria mikononi na kuweka mipaka ya wilaya inaweza kuzusha vita maana kila mtu ataweka mipaka anavyotaka yeye.

· Viongozi wasitumike na upande mmoja kukandamiza upande mwingine wa wananchi. Sisi wote ni watanzania wenye haki sawa.

· Uporaji kama huu wa ardhi ndio chanzo kikubwa sana cha migogoro ya ardhi, na migogoro kama hii inachochewa na viongozi.

Swali:-

Ni nani mwenye mamlaka ya kuweka mipaka ya wilaya? Au kila mtu akiamua anaweza kwenda kuweka mipaka ya wilaya mahali anapotaka yeye?
 
Update ya mgogoro huu..
Kutokana na uzito wa mgogoro huu wa ardhi, uongozi wa kijiji cha Kitomondo uliwasilisha rasmi malalamiko yao kwa mbunge wao tarehe 29th November 2016.
Pia uongozi huo uliwasilisha malalamiko yao kwa mkuu wa mkoa wa Pwani.

Uongozi huo wa kijiji cha Kitomondo unaomba sana viongozi wa mkoa na taifa walishughulikie swala hili kwa uzito wake maana linaweza kuleta madhara yanayoweza kuepukika.
Migogoro hii ya wakulima na wafugaji hapa nchini imeshaleta hasara kubwa sana na hata kusababisha vifo sehemu mbali mbali.
 
image.jpeg

Haya mambo yq migogoro ya ardhi yanachangiwa sana na wanasiasa.Na hasa kuwa na RC au DC ambao sio wakazi wa maeneo husika na hivyo kutokujua kiini na historia ya migogoro hii.

Happy William ni sehemu ya "Wanafamilia" wa Mh.Rais JPM,ni mwanae wa kumkuza,kumlea na kumsomesha.Hapo kwenye picha,DC Happy ni huyo katikati na suti za kijivu siku JPM akitunukiwa PhD yake pale Mlimani.Aliyekaa katikati ya JPM na Mama yake JPM
Kwa hiyo;huenda haya mambo aliamua kwa kum-consult Mzee.
 
Nashangaa, wafugaji wa kizaramo - pwani wanataka kuanza kutifuana miaka hii. Hawa jamaa hawana asili ya kugombea maeneo ya malisho.

Itakuwa ni wale walio haribu maeneo ya malisho sehemu zingine zikawa hazifai si kwa kilimo wala kufugia sasa wanataka kuharibu na mazingira ya kwingineko

Hatuwezi kuwa na nchi ambapo wafugaji wanahamahama kila kukicha. Nchi lote lina geuka sehemu ya kufugia. Ovyo kabisa
 
Hakika.
Hawa wafugaji ni wasukuma waliotoka mkoa wa Shinyanga.
Walihamia mkoa wa Pwani mwaka 2006.
Tangu wahamie huko, ni migogoro isiyoisha ya wakulima na wafugaji.
Mbaya zaidi ni kuwa wafugaji hao wana influence ya pesa, hivyo wakulima ndio wanaonekana kuwa ndio 'wakosaji'.
 
View attachment 443119
Haya mambo yq migogoro ya ardhi yanachangiwa sana na wanasiasa.Na hasa kuwa na RC au DC ambao sio wakazi wa maeneo husika na hivyo kutokujua kiini na historia ya migogoro hii.

Happy William ni sehemu ya "Wanafamilia" wa Mh.Rais JPM,ni mwanae wa kumkuza,kumlea na kumsomesha.Hapo kwenye picha,DC Happy ni huyo katikati na suti za kijivu siku JPM akitunukiwa PhD yake pale Mlimani.Aliyekaa katikati ya JPM na Mama yake JPM
Kwa hiyo;huenda haya mambo aliamua kwa kum-consult Mzee.

Kumbe ndio maama DC huyo ana 'jeuri' ya kutoa matamko kama hayo bila hofu yoyote ile.
 
View attachment 443119
Haya mambo yq migogoro ya ardhi yanachangiwa sana na wanasiasa.Na hasa kuwa na RC au DC ambao sio wakazi wa maeneo husika na hivyo kutokujua kiini na historia ya migogoro hii.

Happy William ni sehemu ya "Wanafamilia" wa Mh.Rais JPM,ni mwanae wa kumkuza,kumlea na kumsomesha.Hapo kwenye picha,DC Happy ni huyo katikati na suti za kijivu siku JPM akitunukiwa PhD yake pale Mlimani.Aliyekaa katikati ya JPM na Mama yake JPM
Kwa hiyo;huenda haya mambo aliamua kwa kum-consult Mzee.

Nimeikumbuka hii thread..

Tetesi: - Mkuu wa Wilaya Mpya wa Kisarawe ni "Mtoto" wa Rais Magufuli
 
Wanao sababisha ni wana siasa.

Hakika.
Nimefuatilia kidogo sakata hili la kuporwa ardhi ya wanavijiji maskini wa kule kijiji cha Kitomondo, ukiwaona mpaka unawahurumia jinsi walivyo wanyonge.
Wafugaji wanatamba kabisa kuwa 'awamu' hii ni 'yao'.
Wanafanya wanavyotaka maana mkuu wa wilaya ya Kisarawe ni 'mwenzao'..!!
Hivyo hawana wasi wasi wowote.
 
Tujitahidi kupiga kelele hivihivi mwisho baba mkubwa kilio kitamfikia.
 
Tujitahidi kupiga kelele hivihivi mwisho baba mkubwa kilio kitamfikia.

Kwa kweli, maana inaonekana kama vile hata uongozi wa mkoa nao 'umefumbia macho' dhuluma hii.
Viongozi wa mkoa wa Pwani wanafahamu kabisa kuhusu sataka hili la mkuu wa wilaya ya Kisarawe kuidhinisha uporaji wa ardhi ya kijiji cha Kitomondo na kuwapa wafugaji wa Kisarawe.
Lakini uongozi huo uko kimya kabisa, kama vile hakuna kinachoendelea.
Labda wote hao ndio 'wale wale'.
 
KIBAHA ILIMEGWA KUTOKA KISARAWE,JE BAADA YA KUMEGA KUANZISHWA WILAYA YA KIBAHA MPAKA ULIWEKWA WAPI?LAZIMA WAWE NA RAMANI MBILI HAPO RAMANI KABLA KIBAHA HAIJAANZISHWA NA BAADA YA KIBAHA KUANZISHA THEN KM KUNA AMENDMENT ZILIFANYIKA RAMANI ZAKE NI MUHIMU
 
Ramani iliyochorwa mwaka 2006 ipo, na inaonyesha mipaka ambayo wizara ya ardhi inasema kuwa ni 'conflict boundary'.
Kwa sababu hiyo basi, wizara ya ardhi ilipeleka wataalam wake mwaka 2014 kwenda kuhakiki mipaka hiyo ili kuondoa utata huo wa mipaka.
Walipohakiki mipaka hiyo, walisema kuwa watachora ramani mpya. Mpaka sasa bado hawajachora ramani hiyo.
Hivyo kutoa mwanya kwa wafugaji kupora ardhi ya kijiji cha Kitomondo na kujichukulia mamlaka ya kuchora mipaka wao wenyewe (wafugaji).
 
Update ya mgogoro huu leo..06th December 2016.
Wafugaji wameweka vijana wao wenye silaha za jadi wanalinda 'mipaka' waliyoiweka ili kuwazuia wakulima wa kijiji cha Kitomondo wasiende kwenye mashamba yao yalioko kwenye eneo lililoporwa na wafugaji hao.
 
Ramani iliyochorwa mwaka 2006 ipo, na inaonyesha mipaka ambayo wizara ya ardhi inasema kuwa ni 'conflict boundary'.
Kwa sababu hiyo basi, wizara ya ardhi ilipeleka wataalam wake mwaka 2014 kwenda kuhakiki mipaka hiyo ili kuondoa utata huo wa mipaka.
Walipohakiki mipaka hiyo, walisema kuwa watachora ramani mpya. Mpaka sasa bado hawajachora ramani hiyo.
Hivyo kutoa mwanya kwa wafugaji kupora ardhi ya kijiji cha Kitomondo na kujichukulia mamlaka ya kuchora mipaka wao wenyewe (wafugaji).
je mnajuaje km bado hawajachora ramani eidha kukifuta kijiji au kumpa kisarawe haki(inawezekana pia kumpendelea) baada ya kuona kuwa wameshindwa kugawana au wakaona busara apewe mzazi?inapaswa wakuu wa hizo halmashauri wakutane na watoe ramani yake kila mmoja.matatizo mengi yanasababishwa na wizara ya ardhi kwa kuweka mipaka ya utata.
 
Kama ulikuwepo vile.
Vikao kati ya wilaya hizo mbili vilikaa mara nyingi sana, ikashindikana kabisa kufikia muafaka.
Hivyo swala hilo likapelekwa wizara ya ardhi makao makuu Dar es Salaam mwaka 2014.
Wizara ya ardhi ikapeleka wataalam wa kuhakiki mipaka hiyo mwezi September 2014.
Baada ya hapo wizara haikumalizia zoezi lake la kuchora ramani mpya na kuweka mawe ya mipaka.
Hapo ndipo 'wajanja' (wafugaji) wakatumia mwaya huo kupora ardhi hiyo, na kuchora mipaka yao wenyewe kinyume cha sheria.
Mbaya zaidi ni kuwa wajanja hao (wafugaji) wamepata support ya mkuu wa wilaya ya Kisarawe kwa kila walichokifanya.
Dhuluma kubwa sana wamefanyiwa wakulima maskini wa kijiji cha Kitomondo.
Je? wafugaji wana mamlaka ya kuchora mipaka ya wilaya badala ya wizara ya ardhi.???
Upo hapo...???
 
Back
Top Bottom