Mgogoro mkubwa baina ya Serikali na wananchi waishio ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro

Hawana nyumba za kudumu, ni tope tu..walipwe fidia ya nini? Wamasai hawataki kuondoka mle kwasababu mle hawaruhusiwi kulima, hivyo serikali huwa inawapa msaada wa chakula Cha kutosha kila mwaka. Sasa wamezoea vya dezo.. hawataki kuondoka
Wamasai wamekuwa wakiishi hapo kabla ya sisi Wabantu kuhamia Afrika ya Mashariki na wamekuwa wakiishi kwenye vijumba hivyohivyo mbona Serikali ya Kenya huwa inawalipa fidia nono.
 
Wamasai wamekuwa wakiishi hapo kabla ya sisi Wabantu kuhamia Afrika ya Mashariki na wamekuwa wakiishi kwenye vijumba hivyohivyo mbona Serikali ya Kenya huwa inawalipa fidia nono.
Wana jaribu mazingira.. angalia sehemu yoyote masai ameishi nje ya hifadhi ni jangwa
 
Wasalaam kutoka Ngorongoro.

JF na Great thinkers wote wa humu wamekuwa na mchango mkubwa kwa matatizo yanayowakabili wananchi wa Tanzania kutoka maeneo mbalimbali...

Nawandikia hivi ikiwa kuna mgogoro mkubwa ndani ya Ngorongoro ikihusishwa na nia ya Serikali kutaka kuwaondoa wananchi hao wapata takriban 100,000 ili kupisha shughuli ya uhifadhi na utalii

Wananchi hawa wamedai baada ya ahadi ya kuhamishwa kutoka Serengeti kuja Ngorongoro hapakuwa na makubaliano ya kwamba baada ya kipindi fulani wataondolewa tena kutoka Ngorongoro kupelekwa pasipojulikana!!

Wananchi wameendelea kuwa na imani na Rais Samia Suluhu lakini wamekuwa wakilalamika kwamba huenda Rais anadanganywa na wataalam haswa mhifadhi mkuu bwana Manongi pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Angalia malalamiko ya wananchi hapo chini
Kupanga ni kuchagua
. Kama taifa, labda tumeshatosheka kabisa na kuendelea kuwepo kwa hifadhi hii, na tumeruhusu uvamizi wa aina hii uendeleee kwa kisingizi cha wavamizi kuwa na imani na SSH
. Kama ambavyo tumeshidwa kutunza vyanzo vya maji, mpaka jiji kama Dar es Salaam linakosa maji, kisha tunaanza usanii wa kukamata pump za wachina na kesho yake maji kurejea ndivyo hivyo tunavyofanya kwenye maeneno mengi muhimu
. Haiwezekana kwa makusudi tunaharibu eneo ambalo lina UNESCO World Heritage Centre kwa sababu za kijinga kijinga
. Tukishaharibu bioanua / biodiversity ya Ngorongoro - restoration yake itatuchukua miaka mingi na budget kubwa kuirudisha kweli uasili wake
 
Wana jaribu mazingira.. angalia sehemu yoyote masai ameishi nje ya hifadhi ni jangwa
Wamasai hawaharibu mazingira sema kuna haja ya kupunguza Mifugo yao kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Wamasai wamekuwa wakiishi na Wanyamapori kwa maelfu ya miaka bila ya kuwamaliza
 
Wasalaam kutoka Ngorongoro.

JF na Great thinkers wote wa humu wamekuwa na mchango mkubwa kwa matatizo yanayowakabili wananchi wa Tanzania kutoka maeneo mbalimbali...

Nawandikia hivi ikiwa kuna mgogoro mkubwa ndani ya Ngorongoro ikihusishwa na nia ya Serikali kutaka kuwaondoa wananchi hao wapata takriban 100,000 ili kupisha shughuli ya uhifadhi na utalii

Wananchi hawa wamedai baada ya ahadi ya kuhamishwa kutoka Serengeti kuja Ngorongoro hapakuwa na makubaliano ya kwamba baada ya kipindi fulani wataondolewa tena kutoka Ngorongoro kupelekwa pasipojulikana!!

Wananchi wameendelea kuwa na imani na Rais Samia Suluhu lakini wamekuwa wakilalamika kwamba huenda Rais anadanganywa na wataalam haswa mhifadhi mkuu bwana Manongi pamoja na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii.

Angalia malalamiko ya wananchi hapo chini
Mbele kwa mbele ni kuisoma kila Kona....
 
Walipwe fidia.
walipwe fidia ya nini, kwani ardhi walikuwa wanamiliki ile? si mbuga ya wanyama? tangu lini wamemiliki ili walipwe? halafu wanataka kufanay mbuga iwe jangwa halafu wakimaliza kabisa majani waondoke wakatafute maeneo mengine wakati wanyama pori watahama au kufa kwa kukosa majani. wanasababisha jangwa. wamesomesha watoto kadhaa wanasheria kina Ole ngurumo wako kibao kwenye mitandao, ati wanapigania haki ya kubaki pale, ndio nikaamini kumbe kuna watu unaweza kupeleka shule lakini bado uporipori upo kichwani hata ufanyeje. wafumuliwe kwa nguvu wanaharibu mbuga.
 
Wamasai hawaharibu mazingira sema kuna haja ya kupunguza Mifugo yao kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Wamasai wamekuwa wakiishi na Wanyamapori kwa maelfu ya miaka bila ya kuwamaliza
hivi kweli inakuja kichwani mtu anashadadia kuendelea kuishi na wanyamapori ati ni haki yake? hao wanyamapori sio domesticated, wanaondoa hata ladha ya kutalii wanyama wanaoishi kivyao, manake unafika mahala wamechanganya pundamilia na ngómbe sao, si wataambukiza magonjwa kwa wanyamapori, magonjwa toka kwenye hayo mambusi yao.
 
Hao wananchi wasichekewe kabisa....Baada ya muda mchache Ngorongoro itafutika katika uso wadunia..

Waondolewe haraka sanaa
 
hivi kweli inakuja kichwani mtu anashadadia kuendelea kuishi na wanyamapori ati ni haki yake? hao wanyamapori sio domesticated, wanaondoa hata ladha ya kutalii wanyama wanaoishi kivyao, manake unafika mahala wamechanganya pundamilia na ngómbe sao, si wataambukiza magonjwa kwa wanyamapori, magonjwa toka kwenye hayo mambusi yao.
Hebu soma historia ya Wamasai kuishi na Wanyamapori imeanza lini kwanza.
 
Watolewe tu, maana baada ya miaka 50 watakuwa zaidi ya milion5, yani milion tano kwenye hifadhi?????
 
Ngorongoro itakufa kabisa ndani miaka 10 ijayo kama Serekali itashindwa kuhamisha wamaasai ambao wamezidi kuongezaka na mifugo imekuwa mingi.

Tanzania ni kubwa ni vyema Serekali ikaunganisha Ngorongoro na TANAPA na kuondoa upuuzi wa uhifadhi wa wanyamapori na binadamu.
Idadi ya mifugo imekuwa kubwa kuliko hao wanyamapori wenyewe. Ni kweli pale hamna kitu baada ya miaka michache sana. Siasa zimepigwa nyingi mpaka hifadhi siyo hifadhi tena na wasiwasi inaweza hata kuondolewa kwenye World Heritage Site.

Kwa hilo musimbambikie mama Samia hilo la kuhamishwa wananchi limekuwepo kwa miaka mingi sana.
 
Hawana nyumba za kudumu, ni tope tu..walipwe fidia ya nini? Wamasai hawataki kuondoka mle kwasababu mle hawaruhusiwi kulima, hivyo serikali huwa inawapa msaada wa chakula Cha kutosha kila mwaka. Sasa wamezoea vya dezo.. hawataki kuondoka
Sasa wameanza kujenga nyumba za kudumu kabisa mimi nimeziona
 
The bottom line is NgoroNgoro should be protected at all costs.
 
Waondolewe Wamaasai kama Ngorongoro itaendelea kuvutia watalii mnaowataka.
Na maamuzi ya serikali hayafanyiki kwa mihemko ya mtu. Na nusu ya ardhi ya mkoa wa Arusha ni ipo wilaya ya Ngorongoro. Sasa wanaotaka watu waondoke waseme ni eneo kiasi gani limeharibika?
 
Umaarifu wa Hifadhi hiyo ni kwa sababu ya mfumo wa maisha Jumuishi (Wanyamapori na Jamii). Ukiondoa jamii pale, maana yake umeiondolea sifa Hifadhi yake ya multiple Land na umaarufu. Haitakuwa tofauti na Hifadhi ya Manyara na Tarangire. Haitakuwa tena moja ya maajabu ya Dunia.

Niliwahi kuona mkataba wao na serikali ya mkoloni muingereza wakati wanapisha kuanzishwa Hifadhi ya Serengeti, hivyo kisheria ni haki yao kuwepo pale. Babu zao kukubali kuachia Serengeti ni jambo kubwa walilofanya, hii ndiyo Hifadhi Bora Afrika kwa sasa.

Tanzania tunajivunia kuwa na maeneo mengi ya Hifadhi lakini ukijaribu kuangalia yalikuwa maeneo ya wafugaji zaidi wakiwa wamasai, kwa maandiki hiyo wanastahili kuheshimiwa na kudhaminiwa. Nina Imani ingekuwa makabila mengine hakika tusingekuwa na wanyama/hifadhi hao/hizo wengine tunakula mpaka konokono.

Shida nyingine huenda wahifadhi wa mle hawana mipango mizuri ya kuendeleza mfumo ule wa matumizi Jumuishi kama sheria inavyotaka, wakae na jamii wakubaliane watafute majawabu ya changamoto kwa pamoja, lakini pia ushirikishwaji na elimu uimarishwe. Serikali itazame hili huenda na wahifadhi wanashindwa majukumu yao ikiwezekana ibadilishwe mfumo wa usimamizi wa eneo hilo.
 
Hebu soma historia ya Wamasai kuishi na Wanyamapori imeanza lini kwanza.
Hebu tumia akili kidogo basi .. Leo wapo laki Moja na mifugo laki 2, fanya projection ya miaka 20 mbele hali itakuwaje,? Serikali iwaondoe kwa utaratibu mzuri, walipwe fidia na wapewe maeneo wasitolewe kibabe tu. Hiyo hifadhi Mimi na wewe tutaiacha vizazi vijavyo vifaidi pia ..bila kuchukuwa hatua mapema, miaka 30 ijayo hamna mbuga.
 
Back
Top Bottom