Mgogoro Hifadhi ya Ngorongoro kuna siri nzito. Nani wapo nyuma ya Wamasai?

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,269
5,368
Mgogoro wa Hifadhi ya Ngorongoro kuhusu wakazi wanaoishi ndani ya eneo hilo umekuwepo kwa miaka mingi, kwa muda wote huo hakuna utatuzi rasmi wa nini kinatakiwa kifanyike.

Juzikati baada ya bwana Maulidi Kitenge na wenzake kutembelea hifadhi hiyo, alitoa ushauri wa Serikali kufanya mpango wa kuwahamisha wakazi waliopo ndani ya eneo hilo kwa sababu kadhaa.

Baadhi ya sababu ni kuwa mara kadhaa raia wanashambuliwa na wanyama wakali, hakuna huduma za kijamii na ongezeko la watu ni hatari kwa uhai wa hifadhi hiyo.

Kitenge alishambuliwa kila kona japo wapo ambao walimuunga mkono kuwa alichozungumza ni mtazamo wake kwa kile alichokiona.

Nimeingia chimbo kufuatilia kiundani kuna nini nyuma ya pazia katika sakata hilo, nilichobaini ni kuwa kuna nguvu kubwa sana baina ya pande mbili.

Kwanza ilinishangaza kuona kama kweli wananchi wapo katika mazingira magumu kama alivyosema Kitenge, inakuwaje wao hawataki kuondoka kwa kisingizio kuwa ‘wamezoea’.

Baada ya kuzungumza na vyanzo rasmi kadhaa kutoka kwenye hifadhi hiyo ni kuwa suala hilo la kuwahamisha ni ngumu sana kwa kuwa kuna nguvu kubwa ya ‘WAZITO’ nyuma ya pazia.

Sababu ya KWANZA ni kuwa WAZITO hao wa ndani ya nchi na wengine wa nje ya nchi wanaowasapoti wakazi wanaoishi ndani ya hifadhi (Wamasai) wana maslahi yao binafsi, ambayo yanawapa faida kuwa na ndiyo maana wanafanya juu chini kuwaunga mkono ili kuhakikisha hawaondoki.

Ile hoja kuwa idadi ya watu inavyoongezeka wanahatarisha uhai wa hifadhi hiyo, ikapingwa na wenyeji kuwa wamekuwepo eneo hilo kwa miaka mingi na hakuna kilichoharibika, nimeona siyo hoja ya msingi.

Kwa kawaida kila binadamu ana mahitaji yake, kadiri idadi ya watu inavyoongezeka ni wazi kuna mahitaji nayo yanatakiwa kuongezeka.

Wakati wanaanza kuishi hapo hifadhini miaka ya 1950 inaelezwa kuwa idadi ya wakazi ilikuwa elfu 8 au 9, lakini sasa hivi takwimu zisizo rasmi inadaiwa wapo zaidi ya watu laki mbili.

Tuwe wakweli, hii ni mbaya na wanapoelekea lazima kutakuwa na madhara ndani ya hifadhi.

Jiulize kama mtu ana nia njema ya kuwahamisha sehemu wanapokuwa hatarini kushambuliwa na wanyama, kupewa huduma za kijamii, kuboreshewa mahitaji binafsi, lakini yote bado wanakataa! Kwa nini? Kuna nini?

UPANDE WA PILI ni ule ambao wanaitazama kesho ipoje na maslahi ya taifa. Hao sasa ndiyo wapo upande wa aliozungumza Kitenge, lakini wanashambuliwa kinoma.

Ni kweli haiwezekani taifa liwepo bila wananchi, lakini hao wananchi hawawezi kuwepo bila kuwa na utaratibu maalum wa jinsi ya kuishi na kuendelea, na kama nchi lazima iwe na mfumo na utaratibu wa kufanya mambo kwa maslahi ya watu wake na maslahi ya taifa kwa jumla.
 
Nchi hii ardhi yote ni mali ya umma iko chini ya mamlaka ya Rais wanaojidai kuwaambia wamasai kuwa ngorongoro ni kwao na haiwezekani wao kuondoka wajue wanawadanganya
 
Kitenge ni mtetezi wa wamasai badala ya wazaramo wenzake? aanze na wazaramo wenzake kwanza kuwatetea na umaskini mkubwa walioletewa na CCM, pia tujue elimu yake.
Kwahio hapo kuna ambae sio Mtanzania ? Pia hao Wazaramo wenzake nao wapo kwenye hifadhi ?, Tatu umasikini wa Wazaramo wenzake una impact sawa maisha yako kama vile uharibifu / uhatarishi wa hifadhi ambayo ni mboni ya dunia / taifa?
 
Wakati wanaanza kuishi hapo hifadhini miaka ya 1950
Sasa kama hauna taarifa sahihi inafaa kabisa usiandike kitu. Ngorongoro Conservation Area ndio ilianzishwa miaka hiyo. To be precise ni mwaka 1959.

Lakini Maasai hatujaanza kuishi Ngorongoro miaka hiyo mkuu tumekuwepo since time immemorial.

Sasa mnaotaka tuondoke inabidi na sisi tuhoji kwanini hamuondoki huko mnapoishi.
 
Mkuu watu walihamishwa kwenda kwenye vijiji vya ujamaa sababu ya sera za serikali, itakuwa na utofauti gani masai wakihamishwa kwenye Ngorongoro Crater ambao ni urithi wa dunia kama ilivyo Serengeti au Selous national park

Na pia wamasai wana asili ya kuhama hama ndio maana hadi muda huu wameshaingia msumbiji, sasa kuna siri gani inayofanya kung'ang'ani hilo bonde. Labda unielimishe
 
Sasa ukisema Ngorongoro ni world heritage inamaana na kila kilichopo hapo ikiwemo Wamasai.

Moja ya vitu unique na vinavyoipa hiyo hadhi Ngorongoro ni ule muingiliano kati ya Mmasai na maliasili. Hiyo ni sifa moja wapo. Sasa ukitutoa unakuwa umeharibu.
 
Dawa ya hili swala ni KUWAACHA WAANGAMIZANE. Kama binadamu wataweza basi waue wanyama wote wao ndio watamalaki hifadhi yote. Au wanyama wakiweza basi nao wawaangamize binadamu eneo lote la hifadhi wakae wao wanyama.

Serikali ISIINGILE IWAACHE WAPAMBANE. Kama mbuga itapotezwa basi poa tu.
 
Mgogoro wa Hifadhi ya Ngorongoro kuhusu wakazi wanaoishi ndani ya eneo hilo umekuwepo kwa miaka mingi, kwa muda wote huo hakuna utatuzi rasmi wa nini kinatakiwa kifanyike.
Kitenge ni nani? Kuna watu wenye akili na elimu waliokwisha kuandika mengi kuhusu hili suala na siyo huyo Kitenge kanjanja anayechumia tumbo lake bila haya.
 
Kitenge ni mtetezi wa wamasai badala ya wazaramo wenzake? aanze na wazaramo wenzake kwanza kuwatetea na umaskini mkubwa walioletewa na CCM, pia tujue elimu yake.
Achana na mambo binafsi ya Kitenge.

Ngorongoro ni lazima ilindwe kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo.
 
Sasa kama hauna taarifa sahihi inafaa kabisa usiandike kitu. Ngorongoro Conservation Area ndio ilianzishwa miaka hiyo. To be precise ni mwaka 1959.

Lakini Maasai hatujaanza kuishi Ngorongoro miaka hiyo mkuu tumekuwepo since time immemorial.

Sasa mnaotaka tuondoke inabidi na sisi tuhoji kwanini hamuondoki huko mnapoishi.
Kwani nako kuna Ngorongoro?
 
Sasa ukisema Ngorongoro ni world heritage inamaana na kila kilichopo hapo ikiwemo Wamasai.

Moja ya vitu unique na vinavyoipa hiyo hadhi Ngorongoro ni ule muingiliano kati ya Mmasai na maliasili. Hiyo ni sifa moja wapo. Sasa ukitutoa unakuwa umeharibu.

Kwani wamasai hawaishi kwa muingiliano na wanyama katika mbuga zingine zozote ila Ngorongoro crater hadi iwe unique factor ya watu kwenda kuitembelea ??...

Kwa ukubwa wa Ngorongoro na ikolojia yake unadhani hii haitoshi kuwafanya watu kuitembelea ??..

Leo tukisema tukimege kipande cha ruaha au mikumi ili kitumike kwa shughuli za kibinadamu bado kuna serengeti au selous inayotoa same experience Je, tukiiweka Ngorongoro crater hatarini kuna option gani nyingine tuliyonayo kui_replace
 
Mgogoro wa Hifadhi ya Ngorongoro kuhusu wakazi wanaoishi ndani ya eneo hilo umekuwepo kwa miaka mingi, kwa muda wote huo hakuna utatuzi rasmi wa nini kinatakiwa kifanyike.
Hii mada ya Ngorongoro Conservation Area, inatakiwa izungumzwe bila jazba.
Ni kweli kabisa kuwa hali ya Hifadhi ya Ngorongoro inaendelea kudhoofika na ni lazima maamuzi magumu yafanyike.
Na maamuzi magumu lazima yazingatie matokeo ya Tafiti za Kisayansi, Kiekolojia na Kijamii ambazo zimeisha fanyika katika eneo la Hifadhi hii.

Na zipo nyingi.
Cha kwanza kabisa ni Historia ya Ngorongoro.
Cha pili ni Muingiliano wa Binadamu na Wanyamapori katika eneo hili.
La tatu, ambalo binafsi naliona ni muhimu kuliko yote, tunatakiwa tujiulize kwa nini maeneo ya Wafugaji Wamasai, hapa Nchini kwetu, na Nchi jirani ya Kenya, yameendelea kuwa na Wanyamapori mpaka leo, wakati maeneo yanayokaliwa na Wafugaji Wamang'ati, Wafugaji Wasukuma na jamii nyingine za Wafugaji, (ambazo zote zilikuwa na Wanyamapori), hakuna Wanyamapori siku hizi.
Hapa ninataka kujenga hoja kwamba, tunatakiwa kulijadili hili kwa kuanza kuwapongeza Wafugaji wa Kimasai.
Taratibu zao za maisha zinatakiwa ziheshimiwe.

Wakati sehemu nyingine zenye muingiliano wa Binadamu na Wanyamapori zimeshuhudia kutoweka kwa Wanyamapori, Umasaini Wanyamapori wapo.
Kitu kingine muhimu ni kuangalia idadi ya Hoteli za Kitalii na Kambi za Utalii ambazo zina madhara katika Hifadhi.
Baada ya hapo, tuangalie Tafiti za Kisayansi juu ya Idadi ya Binadamu na Wanyamapori ambao ni 'sutainable' ndani ya Hifadhi.
Haya yote ni muhimu sana kwa Ngorongoro kwa sababu umuhimu wa kipekee wa Hifadhi hii ni maajabu ya Binadamu kuishi na Wanyamapori.

Kitu kipya ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ni Majumba yanayoongeka, hakiongozwa na Mahoteli.
Ikibidi, Hoteli ndani ya Hifadhi zibomolewe, lakini kamwe, Wafugaji wasiondolewe Ngorongoro.
Inawezekana.
 
Kwani wamasai hawaishi kwa muingiliano na wanyama katika mbuga zingine zozote ila Ngorongoro crater hadi iwe unique factor ya watu kwenda kuitembelea ??...

Kwa ukubwa wa Ngorongoro na ikolojia yake unadhani hii haitoshi kuwafanya watu kuitembelea ??..

Leo tukisema tukimege kipande cha ruaha au mikumi ili kitumike kwa shughuli za kibinadamu bado kuna serengeti au selous inayotoa same experience Je, tukiiweka Ngorongoro crater hatarini kuna option gani nyingine tuliyonayo kui_replace
Ili upate jibu, jiulize kwa nini Ngorongoro haipo chini ya TANAPA, lakini Ruaha, Mikumi, Serengeti na nyinginezo zote zipo chini ya TANAPA.
Yes, Ngorongoro is unique.
 
Kwel
Sasa kama hauna taarifa sahihi inafaa kabisa usiandike kitu. Ngorongoro Conservation Area ndio ilianzishwa miaka hiyo. To be precise ni mwaka 1959.

Lakini Maasai hatujaanza kuishi Ngorongoro miaka hiyo mkuu tumekuwepo since time immemorial.

Sasa mnaotaka tuondoke inabidi na sisi tuhoji kwanini hamuondoki huko mnapoishi.
Kweli maasai akisoma ni hatari. Tuhame twende wapi sasa.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom