kamati ya ufundi
JF-Expert Member
- Sep 30, 2014
- 416
- 439
MGOGORO WA CUF:
LEO BUNGE LINAISHAURI SERIKALI KUINGILIA MWENENDO WA MAHAKAMA?
Nimesoma katika gazeti la mwananchi la leo, kuwa kamati ya Bunge ya sheria na Katiba limeitaka ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kuharakisha kuutatua mgogoro wa kiuongozi wa chama cha wananchi CUF kwa madai kuwa mgogoro huo unaweza kuhatarisha muungano, Sidhani kama kamati ipo sahihi kwenye hili.
Kwa mujibu wa uelewa wangu, kutokana na mapitio mbalimbali ya taarifa za vyombo mbalimbali na kusoma mitandaoni. Mgogoro wa CUF hauwezi kumalizwa na Msajili kwa namna ambavyo kamati hiyo ya Bunge inataka.
Ningeishauri kamati hiyo kwanza ingeipongeza ofisi ya msajili wa vyama kwa hatua ilizochukua kuumaliza mgogoro huo, ambapo sote tuomeona namna pande zote mbili zinazolumbana kuhusu tafsiri ya kikatiba ya chama chao wakikutanishwa na msajili wa vyama na kila upande kupeleka utetezi/maelezo yake kwa msajili na hatimaye msajili kutoa muongozo kulingana na hoja zilizotolewa na pande zote mbili.
MGOGORO WA CUF UPO MAHAKAMANI.
Jambo jema ambalo kamati hiyo ilipaswa kulifahamu kuwa kwa sasa pande mbili hizo zinapambana kupata haki yao kupitia mahakama.
Upande wa maalim Seif Sharrif Hamad umefungua kesi mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Dar es salaam kuwashtaki Msajili wa vyama vya siasa na Lipumba .
Kwa utaratibu wa taifa letu na taifa lolote linalozingatia na kufuata utawala wa sheria, si vyema jambo lililopelekwa katika muhimili wa haki kuamuliwa ama kuingiliwa na muhimili mwingine.
Kwa sasa Jaji Mutungi na Ofisi ya Msajili wanawakilisha muhimili wa Serikali (Executive), Wakati Kamati ya Bunge inawakilisha Muhimili wa Bunge (Parliament) na Mahakama inawakilisha muhimili wa tatu (Judiciary).
Kwa kuwa Mahakama ndio chombo cha mwisho cha utoaji wa haki, na tayari baadhi ya wananchama na viongozi wa CUF wameamua kuifuata haki yao Mahakamani, si busara Bunge kuishauri serikali kuingilia muenendo wa mahakama.
Nasema hivi kutokana na ukweli kwamba, Bunge Kuishauri ofisi ya Msajili wa vyama iharakishe kumaliza mgogoro uliokimbilia Mahakamani ni sawa na Bunge kuiambia serikali iingilie kesi iliyopo mahakamani.
USHAURI
Tafiti ziaonyesha migogoro yote mikubwa Duniani iliisha kwa pande zote zinazolumbana kuamua kuweka chini maslahi yao binafsi na kusimamia maslahi ya pamoja yanayowaunganisha.
Mgogoro wa CUF kadharika, hauwezi kumalizwa na mtu mwengine yeyote wala taasisi yoyote kama wenyewe hawatakaa mezani na kuachana na ung’ang’anizi wa maslahi binafsi na badala yake wasimamie maslahi ya pamoja ya uanzishwaji wa CUF.
Mgogoro ungeweza pia kutatuliwa kwa mashauriano baina ya viongozi wetu wakuu kupitia BARAZA LA VYAMA VYA SIASA. Ambapo chama chetu ni mjumbe wa baraza hilo.
Na ni vyema taasisi muhimun kama Bunge linalolilia na kupigania haki na usawa, kujitahidi kujiepusha kugombanisha ama kugonganisha Mihimili ya Dola.
Saidi Namjata
Mwanachama wa CUF
University of Dodoma.