Mgogoro Chuo Cha St. Joseph Songea

Magarinza

Senior Member
May 9, 2008
122
13
Kuna habari za kushangaza sana kutoka katika chuo kimoja cha St. Joseph kilichopo hapa Ruhuwiko Songea juu ya madai ya wanafunzi kulazimishwa kulipa kiasi cha shs 20,000 kwa wanafunzi wa shahada na shs 15,000 kwa wanafunzi wa stashahada kwa kila muhula na kisha fedha hizo kupelekwa NACTE kwa shughuri isiyofahamika.

Kama hiyo haitoshi, wanafunzi hawa pia wamelazimishwa kukilipa chuo kiasi cha shs 10,000 kwa kila muhula, eti ni malipo kwa ya gharama za chuo kuwatembelea wanafunzi hawa wanapokuwa wamekwenda kwenye mafunzo ya vitendo (Field).

Na kingine cha ajabu wanachodai wanafunzi hawa ni kitendo cha chuo kugoma kuwarudishia wanafunzi wanaomaliza stashahada mwezi huu July fedha yao waliyolipa kipindi wanajiunga na chuo hicho shs 50,000.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom