Mgodi wa Tulawaka kufungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgodi wa Tulawaka kufungwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkungo, Jun 23, 2009.

 1. Mkungo

  Mkungo JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Jumatatu, 22 Juni 2009

  Mgodi wa Tulawaka kufungwa


  na Mobini Sarya

  KAMPUNI ya Barrick ambayo inaongoza kwa kumiliki migodi kadhaa ya madini nchini imetangaza kufunga mgodi wa dhahabu wa Tulawaka uliopo Biharamulo, mkoani Kagera, wakati wowote kuanzia sasa baada ya dhahabu kumalizika.

  Mgodi huo utakuwa wa pili kufungwa kwa madai ya kumalizika dhahabu, baada ya mgodi wa dhahabu wa Buhemba ulioko Wilaya ya Musoma Vijijini, mkoani Mara kufungwa kwa madai kama hayo mwaka juzi.

  Mgodi huo ulikuwa ukimilikiwa na Kampuni ya Meremeta.

  Akizungumza katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima, msemaji mkuu wa Kampuni ya Barrick, Teweli Teweli, alisema wameamua kuufunga mgodi huo baada ya kuona kiwango cha madini kimepungua na wameijulisha serikali kuhusu nia yao hiyo.

  Alisema kampuni yake imeanza maandalizi ya kuufunga mgodi huo ambao ulianza rasmi uzalishaji mwaka 2005, ambapo waliwekeza kiasi cha dola za Marekani mil. 85 na kutoa ajira kwa watu 239.

  “Kiwango cha madini kimepungua katika mgodi huo ndiyo maana tumeanza utaratibu wa kuufunga, tumeshawataarifu wananchi wanaozunguka mgodi huo ambao wamekuwa wakiutegemea waanze kujiandaa,” alisema Teweli.

  Aliongeza kuwa moja ya maandalizi waliyoyaanza ni kupanda miti pamoja na kuwaweka wananchi katika hali ya kujitegemea baada ya kuzoea kupata mahitaji yao kutoka kweye mgodi huo.

  Kwa mjibu wa mtaalamu mmoja wa miamba ya madini, amebainisha kuwa sheria ya migodi duniani inatamka kuwa maandalizi ya kufunga mgodi lazima yafanyike katika kipindi kisichopungua miaka miwili.

  “Mgodi kama ule wa Buhemba wahusika walikiuka taratibu za kimataifa zinazohusu mazingira, sheria zinasema kabla hujafunga mgodi anza maadalizi mapema, ikiwamo kupanda miti na kuvunja mabanda pamoja na kuhamisha mitambo,” alisema mtaalamu huyo.

  Mtaalamu huyo aliongeza kuwa kampuni inayoshindwa kufanya hivyo inaweza kushitakiwa au kunyang’anywa vifaa vya uchimbaji madini, kwa kuacha migodi wazi, jambo linaloweza kuleta madhara kwa binadamu na viumbe vingine.

  Mpango huo wa Barrick kufunga mgodi wa Tulawaka inasemekana ni sehemu ya maandalizi ya kufungua mgodi wa Buzwagi uliopo mkoani Shinyanga.

  Inasemekana kampuni hiyo inasubiri kukamilisha utafiti wa madini ya nikel katika mgodi wa Kabanganiko, Ngara ambao umechukua miongo kadhaa.

  Wakati baadhi ya migodi ya madini ikifungwa kwa sababu ya kumalizika madini hayo, takwimu za watu maskini nchini zimezidi kuongezeka kwa kasi.

  Taarifa za kufungwa kwa mgodi huo zimekuja huku serikali ikitangaza nia yake ya kufuta misamaha ya kodi ya mafuta kwa kampuni za madini ili kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato.

  Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuunda kamati iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Mark Bomani, kuchunguza mikataba ya madini na kutoa mapendekezo serikalini kwa ajili ya kuboresha sekta hiyo ambayo kwa muda mrefu inadaiwa kuwanufaisha zaidi wawekezaji.

  Kampuni za madini hapa nchini zimekuwa zikishutumiwa kwa kuvuna rasilimali nyingi kuliko kile wanachotoa serikalini kutokana na mikataba mibovu iliyoingiwa na serikali.
   
 2. JosM

  JosM JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2009
  Joined: Oct 11, 2008
  Messages: 684
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Shamba la Bibi limeisha mazao,wameshachukua walichokitaka watatushia mashimo
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  he! mbona nimeona juzi juzi tu wanatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya mgodi huo huo... isije ikawa mwandishi aliambiwa kuna mpango wa kufunga mgodi dhahabu itakapoisha yeye akaelewa kuwa mgodi unafungwa sasa hivi
   
 4. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,646
  Likes Received: 1,472
  Trophy Points: 280
  Masikini, namkumbuka Mwalimu na wosia wake.....sasa ndo tumefulia...kodi hatujapata ilivostahili, na madini yameisha, sasa tutakuwa wageni wa nani?
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Shame on you Serikali kwa kutupiga changa la macho

  Nashawikika kusema kwamba mmefaidika na mikataba ya wawekezaji kibinafsi na hamkuangaliamaslahi ya nchi

  Laana iwe juu yenu gademit
   
 6. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  du! ewe mungu baba wasamehe hawa.
  jamani tumefulia au wao wamefulia?
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Heri yaishe. Hatimaye Mafisadi watakosa cha kufisadi na akina Barrick wataondoka na hapo tutapata viongozi wa kweli kweli na siyo hawa wanaowekwa na akina RA. Japan haina kitu ila ni tajiri sana. Akili kichwani, kama tutaitumia vizuri, bado UTAJIRI TUNAO kwenye UBONGO. Thank you God, Tanzania yaitwa Bongo land.
   
 8. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  umefulia na nimefulia hivyo kwa ujumlatumefulia

  ila viongozi hawajafulia kwani watatunga sheria za kujilinda ikiwa watastaafu wasishtakiwe kwamakosa ya maksudi waliyoyafanza wakati wanatekeleza shughuli zaokikatiba
  shwain
   
 9. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Basi na wawe wastaarabu kidogo. Kabla ya kuondoka angalau kwanza wafukie hayo makorongo waliotuachia. Wanategemea hata hiyo kazi tufanye sisi?
   
 10. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mungu inusuru rasilimali za Tanzania zisiendelee kuisha kabla ya kusaidia vizazi vijavyo.
   
 11. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  imefikia mahala hata kuandika chochote wengine TUNASHINDWA!hasira zimekuwa nyingi hadi kwenye vidole!tunabaki kuwa wasomaji tu,maanake tunaogopa kesi

  anyways,YANA MWISHO HAYA!
  let's pray for the best
   
 12. F

  FrankGM Member

  #12
  Jun 23, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kufungwa kwa mgodi wa Tulawaka nadhani ni sahihi kulingana na ahadi ya Barrick tokea walipoufungua mgodi huo. Wao walisema kuwa dhahabu katika mgodi huo itakuwa imemalizika kwa kipindi cha miaka mitano.
  Binafsi nimekuwa nikitafakari sana juu ya uvunaji wa madini hapa nchini na faida ambayo taifa na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakinufaika na sekta hii ya madini. Wakati mwingine inaonekana wanaofaidika zaidi ni wale wanaohusika katika kuweka saini kuidhinisha mikataba ya uvunaji madini hapa nchini. Kwasababu wawekezaji wanatoa malipo ya mrahaba ambayo ni asilimia 3 tu ya mapato yao, na katika hizo 1.9% ni malipo kwenda kwa wahakiki wa uvunaji (Assay Stewart Co ya Marekani). Hii ina maana kuwa ni 1.1% tu inayobaki kama pato linalotokana na madini kwa taifa.
  Nadhani utaweza kuona sasa katika hali kama hii ambapo mgodi huu unafungwa, dhahabu yote ikiwa imeshavunwa, tulichopata hapa kulinufaisha taifa ni kidogo sana.
  Serikali imekuwa ikiwabembeleza wawekezaji hawa kwa kuwasamehe kodi nyingi, kama si zote, kwasababu tu wamewekeza kwa wingi. Hili linatuumiza sana.

  Hata hivyo kumekuwa na faida zisizo za moja kwa moja, ingawa nadhani hizo zimetokea tu hazikuwa zimefikiriwa kabla, ambazo tumeweza kuzipata.
  Ni pamoja na teknolojia ya uchimbaji madini, ambapo kwa sasa tayari tumeshatoa wataalamu wengi sana walioko Congo na nchi nyingine za jirani. Hili kwa baadaye litazidi kutunufaisha.
  Pia mashirika ya usafirishaji yamenufaika sana na sekta hii ya madini kuliko sekta nyingine zozote, hii ni pamoja na usafiri wa ndege, mizigo nk.
  Mahoteli makubwa, wateja wao wakubwa ni wafanyakazi katika sekta hii.
  Makampuni mengi ya ujenzi yamenufaika sana na sekta hii kwa kupewa kandarasi kubwa kubwa.
  Wafanyabiashara wengi wamenufaika kwa kupewa tenda mbalimbali katika migodi.
  Watanzania wengi pia wamepata ajira katika shughuli mbalimbali zinazohusiana na sekta hii.
  Nina uhakika miji kama Kahama na Geita hata Mwanza na Shinyanga pia isingekuwa jinsi ilivyo kama si kwa sekta hii ya madini.

  Midhali tumeshayavulia maji nguo sharti tuyaoge. Kilichopo sasa ni serikali pamoja na wadau wote katika sekta ya madini kukaa pamoja na kujadili kuona ni jinsi gani sekta hii itachangia katika pato la taifa moja kwa moja. Hili ni vizuri likafanyika kwakuwa tayari tunao wataalamu sasa ambao wanaweza kutumika kwa kusaidiana na wachache kutoka nje wakashauri jinsi ya kujikwamua katika hili.
   
 13. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Zak Malang, Hawa Jamaa wa PML - Tulawaka hawawezi kufukia hayo mashimo, hawajapanga Budget ya Kufukia. Labda kama kuna mtu mwenye Rehabilitation plan atupatie ili tuone hilo shimo wanataka kuliacha vipi. Kulifukia najua itakuwa kama ndoto.
   
 14. a

  agika JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  mhhh...... mmweee!!!!
   
 15. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,322
  Likes Received: 1,788
  Trophy Points: 280
  Kulikuwa na mpango wa kufanya underground mining baada ya ore iliyokuwepo kwenye open pit kumalizika. Is the plan still there? Maana such a possibility is still there as long as it is commercially viable
   
 16. Van Walter

  Van Walter Senior Member

  #16
  Jun 23, 2009
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 171
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  iishe mara ngapi rasilimali yetu?..ndo twaachiwa mashimo tu
   
 17. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Ndo hivo Agika, wameisha jichotea haooooo wanaondoka zao na kutuacha na mishimo yetu na umasikini hadi funza kwenye vidole! Inauma sana
   
 18. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Mwandishi kapotosha uma kwa kusema kuwa wakati wowote....mpango wa kufunga mgodi upo tena ni migodi yote...mala dhahabu itakapo malizika ardhini which is right...kama hakuna madini wanafanya nini.

  Rehabilitation itafanyika ila sio kwa kiwango cha kufukia kabisa mashimo mpaka yakaisha.Kwani udongo mwingine si ndio umekuwa prossess na kutoa dhahabu...so wanacho fanya kwa maeneo ambayo walisha maliza kuchimba(Open pit)Wanapanda miti na kufukia kwa kiwango wanacho weza na hiyo badget huwa inapangwa kabla hata mgodi kufunguliwa..inakuwa ni katika hizo fedha wanaita za uwekezaji.

  Underground ilisha anza toka mwaka jana.Na dhahabu hapa january ilikuwa ni ngumu kupatikana chini ya ardhi...kulingana na gharama za uchimbaji chini ya ardhi(Underground) ila recently mwezi wa nne matumaini yameanza kuonekana...kwa kupata dhahabu zaidi..hii inapelekea kusema kuwa kuna uwezekano wakawepo mpaka mwaka huu mwishoni au mwakani mwanzoni....kwani underground dhahabu yake ilikuwa ni ya kuchimba miaka miwili.

  Unajua tewele naye ni msemaji lakini si mtaalamu...so anasema kwa ujumla ila tafiti zinaendelea...mnaweza msikia huyo huyo akija sema tunaendela na utafiti ziadi...si hatufungi tena...mgodi.
   
 19. s

  samvande2002 JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2009
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 413
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  wameshamaliza madini yote sasa hivi wanaondoka zao wanatuachia mashimo tu,na serikali inachekelea kuwa wameliingizia taifa mapato,wakati ni upumbavu mtupu..
  hamna lolote linaloendelea,
  serikali nayo haina lolote inalolifanya,mi naona wanatuzingua tu,mhusika mkuu aliyebinafsisha migodi na akasaini mikataba ya kizushi ambayo haitunufaishi sisi si yupo mbona wanamchekelea tu? mbona wenzetu wameanza kudili na bakili muluzi kwa kesi kama hizi?kwani yeye hakuwa rais? sisi hapa serikali imezidi kuwekeana mambo ya ushikaji,inatugharimu sisi walipa kodi...tumeshachoshwa na huu upumbavu unaoendelea katika nchi hii..
   
 20. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni kweli faida hizi zipo, lakini naziona so petty ukilinganisha na rasilimali iliyoondoka
   
Loading...