Mgodi wa Resolute hauna manufaa Nzega - Mbunge Dr. Kigwangala

R

rolemodel

Member
Joined
Feb 11, 2008
Messages
11
Likes
1
Points
5
R

rolemodel

Member
Joined Feb 11, 2008
11 1 5
Dk Kigwangala awakaba Resolute
Mwananchi, Jumatano Desemba 1, 2010

Na Mustapha Kapalata, Nzega

MBUNGE wa Nzega (CCM), Dk Hamis Kigwangala, amesema mkataba wa mgodi wa dhahabu wa Nzega Golden Pride Mine Ltd, hauna manufaa na wananchi wa jimbo hilo.
Kauli ya mbunge huyo imekuja ikiwa ni siku moja baada ya kuanza kutumikia wananchi, akianzia ziara yake kwenye mgodi huo.
Dk Kigwangala alifanya ziara ya kushtukiza mgodini hapo jana na kukutana na Meneja Mwendeshaji, Les Taylor, akimtaka kueleza jinsi wananchi wanavyonufaika na mgodi huo.
Hatua ya Mbunge inatokana na kero kubwa ya maji inayowakumba wananchi wa Nzega. Hivi sasa plastiki la lita 20 za ujazo linanunuliwa kwa sh 1,500.
Mbunge huyo alisema mgodi huo hauna msaada kwa wananchi wa jimbo hilo kwani, uongozi wa mgodi huo hautoi huduma muhimu kama maji kwa wananchi, ilhali wanaendelea kukausha vyanzo vya maji.
Dk Kigwangala alisema uhusiano wa wawekezaji hao na wananchi wanaozunguka eneo hilo, ni sawa na chui na paka, hawaelewani kutokana na utawala wa mgodi huo unaodharau raia kwenye nchi yao.
Alisema mikataba iliyofungwa enzi hizo siyo yakinifu ambayo itanufaisha wananchi wa Nzega na watanzania na kwamba, inalenga kunufaisha watu binafsi.
Kuhusu mrahaba unaolipwa kwa halmashauri wa sh 200 milioni kwa mwaka, Dk Kigwangala alisema kiwango hicho ni kidogo ikilinganishwa na rasilimali wanayovuna.
"Kwa kweli kama mbunge, mikataba hii ni ya kihuni , siridhishwi nayo hata kidogo, kiwango wanachotoa ni bora wangechimba bure. Hawana msaada kwa watu wa taifa hili, wanachokifanya ni kuongeza umaskini, naheshimu sana mikataba lakini huu siridhiki nao," alisema Dk Kigwangala.
Alisema muda wa uchimbaji kwa mgodi huo unakaribia kumalizika na wananchi wataachiwa mashimo, yenye madhara makubwa kwa afya zao, huku akimtaka meneja huyo kurekebisha haraka uhusiano wao na wananchi.
Kwa upande wake, Taylor alimshutumu mbunge huyo kwa kufanya ziara isiyo rasmi na kwamba, alitakiwa kutoa taarifa kama mbunge kuingia mgodini.
Taylor alisema malalamiko ya wananchi kuhusu uhusiano siyo kazi ya mgodi, bali serikali ambayo inatakiwa kutimiza ahadi zake.
Alisema kampuni inatoa msaada pindi inapoguswa na tatizo, siyo lazima na halihusiani na mkataba wao.
Awali, Dk Kigwangala alitembelea vyanzo vya maji na Meneja wa maji wilaya ya Nzega, Samuel Buyigi, akimweleza kutokuwepo kwa uhusiano mzuri na mgodi huo ambao unakausha vyanzo vya maji.
Buyigi alisema mgodi huo unachukua maji kutoka vyanzo vya maji na kwamba, vingine vimeanza kukauka, hali inayosababisha usumbufu kwa wananchi.
 
zomba

zomba

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2007
Messages
17,081
Likes
70
Points
0
zomba

zomba

JF-Expert Member
Joined Nov 27, 2007
17,081 70 0
Well done Kigwangala, what's next after the visit? Hope they do not silence you with some pocket money.
 
N

Njaare

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2010
Messages
1,080
Likes
6
Points
135
N

Njaare

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2010
1,080 6 135
Ngoja aingie kwenye pay roll kama mtakaa mumsikie akiongea neno lolote kuhusu mgodi. Selelii na machachari yake hakuwahi kuugusia huo mgodi na usingeweza kujua kama jimbo lake lina matatizo mengine zaidi ya barabara. Tumpe miezi sita.
 
Anfaal

Anfaal

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Messages
1,157
Likes
7
Points
0
Anfaal

Anfaal

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2010
1,157 7 0
Hivi ukomo wa mbunge unaanzia wapi na kuishia wapi? Ni sahihi kwa Mbunge kuvamia eneo la kazi la watu bila taarifa kwa wahusika. Huyu Kingwangala, yeye anapaswa kuwabana wawekezaji juu ya mikataba au serikali? Hii ya kutafuta cheap popularity imepitwa na wakati! Huu ni muendelezo wa ujinga wa viongozi wetu. Inawezekana tatizo lipo, lakini je amejadiliana na serikali? Na kama wananchi wa Nzega wanamahitaji au wanastahili kusaidiwa na wawekezaji kwa nini asiliseme hilo serikalini malipo yanapopelekwa au awaombe wawekezaji wasaidie? Nani wa kulaumia kama mkataba ni wa kijinga, wawekezaji au serikali?
 
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2006
Messages
11,505
Likes
234
Points
160
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined May 5, 2006
11,505 234 160

Anfaal,
Mbunge ndiye anayepaswa kulalamikia mikataba feki na si serikali. Serikali ndiyo iliyosaini hiyo mikataba kwa hiyo haiwezi kuwabana wale unaowaita wawekezaji ambao kama ukiniuliza mimi nawaita wanyonyaji. Kwa kifupi mbunge anafanya kazi yake, acha kumshupalia.
 
Anfaal

Anfaal

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Messages
1,157
Likes
7
Points
0
Anfaal

Anfaal

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2010
1,157 7 0
Anfaal,
Mbunge ndiye anayepaswa kulalamikia mikataba feki na si serikali. Serikali ndiyo iliyosaini hiyo mikataba kwa hiyo haiwezi kuwabana wale unaowaita wawekezaji ambao kama ukiniuliza mimi nawaita wanyonyaji. Kwa kifupi mbunge anafanya kazi yake, acha kumshupalia.
Huenda hujanielewa. Serikali ilinegotiate contract. Yenyewe ikasign. Sasa Mbunge anadhani huo mkataba unatatizo kwa sababu jimboni kwake hawanufaiki. Sasa kwenda kwa muwekezaji na kulalama mkataba mbovu ni sahihi? Kwanini asilalame kwa serikali? Angalia case yake hapo, kaenda kuvamia mgodi bila taarifa.
 
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2006
Messages
11,505
Likes
234
Points
160
J

Jasusi

JF-Expert Member
Joined May 5, 2006
11,505 234 160
Huenda hujanielewa. Serikali ilinegotiate contract. Yenyewe ikasign. Sasa Mbunge anadhani huo mkataba unatatizo kwa sababu jimboni kwake hawanufaiki. Sasa kwenda kwa muwekezaji na kulalama mkataba mbovu ni sahihi? Kwanini asilalame kwa serikali? Angalia case yake hapo, kaenda kuvamia mgodi bila taarifa.
hapana. Wewe ndiyo hujanielewa. Mbunge alikwenda kwenye mgodi kutafuta data zitakazomwezesha kuikaba serikali bungeni kwa nini ilisaini mkataba wa kihuni namna hiyo. Mbunge anafanya kazi yake jimboni kwake. Muda wake wa kuilalamikia serikali utafika atakapowika bungeni. Hata jela ukiwataarifu kuwa unakwenda kufanya ukaguzi wanasafisha ili ionekane kuwa wafungwa wanaishi maisha yanayokidhi haki za binadamu. Vile vile mbunge angetoa taarifa hao wakuu wa mgodi wangemwonyesha mambo wanayotaka wao tu ayaone. Namshauri aendelee kufanya hayo matembezi ya kuwashtukiza hao exploiters.
 
Nyambala

Nyambala

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2007
Messages
4,470
Likes
30
Points
135
Nyambala

Nyambala

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2007
4,470 30 135
Kazi kweli tunayo na hawa waheshimiwa wetu!
 
M

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Likes
61
Points
145
M

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 61 145
hapana. Wewe ndiyo hujanielewa. Mbunge alikwenda kwenye mgodi kutafuta data zitakazomwezesha kuikaba serikali bungeni kwa nini ilisaini mkataba wa kihuni namna hiyo. Mbunge anafanya kazi yake jimboni kwake. Muda wake wa kuilalamikia serikali utafika atakapowika bungeni. Hata jela ukiwataarifu kuwa unakwenda kufanya ukaguzi wanasafisha ili ionekane kuwa wafungwa wanaishi maisha yanayokidhi haki za binadamu. Vile vile mbunge angetoa taarifa hao wakuu wa mgodi wangemwonyesha mambo wanayotaka wao tu ayaone. Namshauri aendelee kufanya hayo matembezi ya kuwashtukiza hao exploiters.
Jasusi,

Huyo mheshimiwa akipigwa risasi kama Dr. Kleruu huko mgodini tutamlaumu nani?

Management ni kazi ngumu sana. Tunachoshuhudia sasa ni ile Maggid aliita Real Madrid. Kuna wachezaji wengi sana tena waliobobea lakini kila mtu anacheza lwake na tusitegemea mafanikio makubwa.

Tumeona kila waziri anaenda wizarani kwake na kufoka huku anategemea hao hao anaowafokea ndio walete mabadiliko kwenye wizara husika. Matokeo yake yanaweza kuwa kinyume kabisa; may be we need both hard power and soft power.

Kuna haja ya kuwasikiliza wahusika na kujenga alliances kabla ya kuwatambua wale wachache ambao wanatakiwa washughulikiwe.
 
Mtanzania,
Kama "mwekezaji" akiamua kumtungua mheshimiwa basi naye yamkute yaliyompata Mwamindi kwa sababu mgodi huo sio "sovereign" yake. Ni kweli kuna haja ya kuwasikiliza wahusika na kujenga alliances lakini hawa wawekezaji kwenye migodi wamepewa free ride wamekuwa kama miungu mtu kwa hiyo nikiona mbunge anajaribu kuangalia kulikoni napiga makofi. Hii ni kwa sababu serikali haitimizi wajibu wake au imeamua kulala kitanda kimoja na mwekezaji.
 
Abdulhalim

Abdulhalim

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2007
Messages
16,513
Likes
204
Points
160
Abdulhalim

Abdulhalim

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2007
16,513 204 160
hot air ili kujikusanyia political score..hakuna la ziada..nchi hii imekabidhiwa misukule, hakutokuwa na mabadiliko yeyote ya maana.
 
Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined
Feb 29, 2008
Messages
5,971
Likes
44
Points
0
Mtazamaji

Mtazamaji

JF-Expert Member
Joined Feb 29, 2008
5,971 44 0
Nice start mbunge.
Halmshauri inapata mrahaba wa milioni 200. Hatuwezi kujuakama ni nyingi au ndogo kiasi gani.

  • Ni kiasi gani cha dhahabu inachimbwa huko?
  • Mill 200 ni % ngapi ya kitu gani?
Naomba kukumbushwa base ya calculation za mrahaba
 
M

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2006
Messages
4,818
Likes
61
Points
145
M

Mtanzania

JF-Expert Member
Joined May 4, 2006
4,818 61 145
Mtanzania,
Kama "mwekezaji" akiamua kumtungua mheshimiwa basi naye yamkute yaliyompata Mwamindi kwa sababu mgodi huo sio "sovereign" yake. Ni kweli kuna haja ya kuwasikiliza wahusika na kujenga alliances lakini hawa wawekezaji kwenye migodi wamepewa free ride wamekuwa kama miungu mtu kwa hiyo nikiona mbunge anajaribu kuangalia kulikoni napiga makofi. Hii ni kwa sababu serikali haitimizi wajibu wake au imeamua kulala kitanda kimoja na mwekezaji.
Mkuu Jasusi,

Makofi kama hayo hayana maana sana maana unashangilia chenga za akina Ronaldo dakikia ya tano huku dakika tisini mnafungwa magoli.

Hao Wawekezaji sio watu wajinga na ukitaka kupambana nao ni muhimu uwajue kwanza wanasimamia nini? Hata Simba hashambulii mnyama mpaka aone kuna nafasi ya mafanikio, vinginevyo ni kupoteza bure energy yake ambayo inatakiwa aitunze mpaka apate mlo mwingine.

Lakini kwa siasa za Tanzania ambazo umaarufu wa magazetini ni muhimu zaidi ya mafanikio ya utendaji, basi huenda ndio maana waheshimiwa wengi wanaona hii ndio njia muafaka. Wananchi watajua mheshimiwa wao anawatetea hata kama mafanikio ni zero.

Usione USA wana negotiate na Iran, sio kwamba wanapenda ila kwasababu options zingine huenda ni mbaya kuliko hiyo ya kuzungumza nao.

Kwenye suala la migodi, mwenye makosa ni serikali kupitia wizara ya madini. Wamesaini mikataba mibovu. Sasa unapoongelea mambo ya mikataba inabidi uwe mwangalifu sana. Hasira hazisaidii na busara na uongozi bora vinawza kusaidia kumtoa nyoka pangoni. Vinginevyo tutaendelea kufungwa magoli kama Tanesco.
 
Anfaal

Anfaal

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Messages
1,157
Likes
7
Points
0
Anfaal

Anfaal

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2010
1,157 7 0
hapana. Wewe ndiyo hujanielewa. Mbunge alikwenda kwenye mgodi kutafuta data zitakazomwezesha kuikaba serikali bungeni kwa nini ilisaini mkataba wa kihuni namna hiyo. Mbunge anafanya kazi yake jimboni kwake. Muda wake wa kuilalamikia serikali utafika atakapowika bungeni. Hata jela ukiwataarifu kuwa unakwenda kufanya ukaguzi wanasafisha ili ionekane kuwa wafungwa wanaishi maisha yanayokidhi haki za binadamu. Vile vile mbunge angetoa taarifa hao wakuu wa mgodi wangemwonyesha mambo wanayotaka wao tu ayaone. Namshauri aendelee kufanya hayo matembezi ya kuwashtukiza hao exploiters.
Hivi Data za kuikaba serikali zinapatikana mgodini? Yaani Resolute wampe data zitakazowaletea matatizo wao? Zitakazo waharibia maslahi yao. Kama ndiyo lengo lake basi wapiga kura wake wanahitaji kufikiri upya. Pia Mbunge hana haki ya kuvamia tu eneo la watu la kazi eti yeye ni Mbunge? Hata Polisi wakitaka kwenda sehem kwa suala nyeti linalogusa maslahi ya Taifa lazima wawe na kibali cha kufanya hivyo. Basi itakuwa shida, maana si muda mrefu wabunge wataanza kuchukua hadi wake za watu kwa kuwa ni wabunge.
Njia rahisi ya kuelezea kutokubaliana na maslahi kwa wapiga kura wake ni kukaa na kujadili na uongozi wa Mgodi huo, tena basi huu utakuwa msaada tu kwake. Maendeleo hayawezi kuletwa na pesa nyingi tu kupelekwa Halmashauri, hata wangeongelea vipaumbele vya ajira, maji, elimu nk (benefit in kind) kwa wananchi wa eneo husika, ingekuwa ni vyema.
 
HKigwangalla

HKigwangalla

Verified Member
Joined
Feb 6, 2008
Messages
718
Likes
28
Points
0
HKigwangalla

HKigwangalla

Verified Member
Joined Feb 6, 2008
718 28 0
Pamoja na kuwa na mikataba na serikali lakini kufuatilia mambo huzaa matunda! Tayari nimeshagundua kuwa hawa jamaa hawajalipa corporate tax toka kwa zaidi ya miaka 10...mgodi ulianza mwaka 1998, wamekuja kuanza kulipa kodi hiyo mwaka jana (2009) na walilipa pesa kidogo sana...na pia wamelipa mwaka huu, vile vile pesa kidogo sana pia...wakisingizia kuwa hawatengenezi faida yoyote ile, lakini utashangaa kuona kuwa walikuwa na original mkataba wa miaka 7 mwanzoni, waka-extend miaka miwili, waka-extend tena miaka miwili, je bado tu hawapati faida? na kwa nini wanaextend tu kila siku? kuna maswali mengi watanzania tutatakiwa kujiuliza na pengine kuyafanyia kazi kidogo...leo hii wametangaza kufunga uzalishaji mnamo mwaka 2012 na kuanza kuweka sawa mazingira kwa kipindi cha miaka mitano...usijeshangaa sasa wakaamua ku-extend tena miaka miwili [maana tayari wameshaanza mchakato wa kuwasogeza wananchi pembeni zaidi kwa maana ya kuwa wanataka kuanzisha shimo lingine]! sasa leo hii taarifa nilizonazo si zinaweza kuisaidia serikali kuamka na kusaini mkataba mzuri zaidi endapo watataka ku-extend mkataba na sisi?
 
Mbunge, keep up with them. Tanzania tunaibiwa kwa sababu hakuna mtu yeyote kwenye madaraka mwenye ubavu wa kuwahoji. Mpaka ionekane kuwa jimbo lako linafaidi madini hayo.
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
14,368
Likes
8,746
Points
280
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
14,368 8,746 280
Dr.Kingwangala,

..sasa usiwe peke yako ktk huu ufuatiliaji, unless unataka kununuliwa au upewe chochote.

..hamasisha wabunge wenzako wa Mara ambako pia kuna migodi ya dhahabu, na wale walioko mikoa ya kusini kwenye gesi.

..mkiwa na united front ya kutetea wananchi wafaidike na rasilimali hizi ndiyo mafanikio yatapatikana.

..ukiendelea kivyako-vyako utapewa hongo ambayo hujaiona maishani na uzalendo wote utakuisha.

NB:

..halafu hapa umeshajichomea.

..miaka 2 au 3 watu wanaweza kufukua thread hii kupima kama msimamo wako umebadilika.
 
Hakikwanza

Hakikwanza

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2010
Messages
3,969
Likes
356
Points
180
Hakikwanza

Hakikwanza

JF-Expert Member
Joined Dec 11, 2010
3,969 356 180
Tanzania hatuna mgodi wenye manufaa yeyote.Kama upo naomba Wanajf mnitajie. Yaani naomba mlinganishe kinachochimbwa na tunachopata muone kama sio madudu tu.Huyo mbunge na mshukuru sana amesubutu kusema, lakini matatizo ni serikali yake haisikii kamwe masikio yake yamepigiliwa nondo .Hii sio nchi ni uchafu wa nchi yaani mavi matupu sioni kama kuna watu Tanzania asilimia kubwa kama 95 hivi ni wadudu tu.NCHI NYINGINE MADUDU HAYA YANAYOENDELEZWA NA SERIKALI VIBOKO KWA WAKUU VINGEKUWA VIMEPITA SANA NA MIGOMO NA WENGINE WALIO LETA TABU KUBWA KAMA UFISADI TUNGEKUWA TUMEWAUA.Kwani kutokana na ufisadi wao wengi wamekufa pasipo hatia ila ni kwasababu yao.
 
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2008
Messages
1,322
Likes
21
Points
135
Selous

Selous

JF-Expert Member
Joined Jan 13, 2008
1,322 21 135
Tuendako: Naliona anguko la Mh. Kigwangala.

CHADEMA kweli wanawapeleka puta hawa jamaaa, nampa tano walioandaa ilani ya uchaguzi ya CDM.
 
baha

baha

Member
Joined
Oct 18, 2009
Messages
44
Likes
2
Points
15
baha

baha

Member
Joined Oct 18, 2009
44 2 15
Bahati mbaya mimi sijui utaratibu wa mbunge katika kazi zake jimboni, lakini naweza kubashiri kuwa haikuwa sahihi kwa huyu bwana mbunge kuingia nyumbani kwa mtu bila taarifa. Nasema haya kwa sababu naamini kuwa ugeni wake ulihitaji mwenyeji wa kumpokea achilia mbali wakuzungumza naye hayo yaliyompleka pale. Ofisini kila mtu anayo ratiba ya kazi yake ya kila siku, je kwa kushitukiza hivi nani angelaumiwa kama wenyeji wangekataa kuzungumza naye achilia mbali kumtambua! Nikirudi kwenye mazungumzo yake na wenyeji, nakubaliana na majibu ya mwenye mgodi kuhusu kazi za mwekezaji ambazo kwa elimu ya biashara ndogo niliyonayo halazimishwi na mtu wala taasisi yoyote kuhusu kusaidia au kuwa na mahusiano mazuri na jamii (hakuna mwafaka wa jumla kuhusu mahusiano mazuri ni nini) kama siyo kipau mbele cha kampuni husika. Ieleweke hapa kwamba mahusiano na jamii ni mkakati wa kibiashara wa makampuni kama ilivyo mikakati mingine yoyote ambayo hasa ndo namna ya kushindana baadhi ya makampuni huamua kutekeleza.

Serikali ndo yenye jukumu la kuweka sera, sheria, taratibu na hata miundombinu ya namna makampuni ynanavyotakiwa kufanya kazi zao yawapo nchini na kinyume chake ni kubaki omba omba tu tukingoja huruma yao, kama wakichagua kuwa nayo. Mchango wangu huu wa mawazo umejikita zaidi kwenye falsafa ya "The business of business is business". Wenye taaluma ya biashara ya kimataifa pengine watakubaliana nami kuwa kutoa msaada wa maji na vitu vingine vinavyodaiwa na mbunge kwa wapiga kura wake ni "corporate social responsibility (CSR)" ambayo kimsingi bado hakujapatikana mwafaka wa ama ni hiari au lazima kwa makampuni yafanyapo biashara zao duniani.

Ni mtazamo wangu kuwa ama mbunge hajui eneo hili la biashara kwa maana si mtaalam wake au kaamua kuwapima wawekezaji hawa kama hawajui majukumu yao wapate kumtetemekea kwa asili ya kitanzania. Nasema kitanzania kwa sababu nchi za wengine mbunge si Mungu mpaka aingie mahala bila kujulikana muda wala saa anapokusudia kuwasili. Ni kutaka kuwaridhisha wapiga kura walionyimwa elimu ya kujua haya na chama chake. Kama kweli anafanya haya "in utmost good faith" basi aisaidie halmashauri yake kupata mawazo mapya ya kutafuta ongezeko la malipo kwa taratibu za kawaida za mazungumzo kwa sababu ni haki yao kama halmashauri na wananchi kwa jumla kupata a "fair pay" kutoka kwa mwekezaji wao na hata yeye anajua vizuri lakini hawezi kuamusha usingizini wadai wake ili kupunguza "bottom line" ya kampuni.

Vinginevyo tunataka tumsikie bungeni akigeuza madai ya mtangulizi wake Selelii kutoka barabara na kuwa malipo ya mgodi kwa wana wa Nzega. Kinyume chake anapiga kelele bure au anafurahisha wapiga kura wasio na uelewa huu.

Nawasilisha.
 
Forum statistics

Threads 1,237,396
Members 475,533
Posts 29,286,992