Mgodi wa Kiwira kufufuliwa, Serikali kumiliki hisa zote

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Picha

RAIS John Magufuli amemwagiza Waziri wa Madini, Doto Biteko kukamilisha malipo ya madeni pamoja na kuhamisha hisa za asilimia 70 za Kampuni ya TanPower Resources kuja serikalini ili Mgodi wa Makaa ya Mawe Kiwira uanze kazi mara moja.

Ametoa maagizo hayo jana alipokuwa Kiwira mkoani Mbeya wakati akiwahutubia wananchi wa eneo hilo waliojitokeza kwa wingi barabarani.

Rais Magufuli yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi.
Maagizo hayo ya Rais yalikuja baada ya Waziri Biteko kumweleza kuwa mgodi wa Kiwira ulisimama kufanya kazi tangu mwaka 2005 kutokana na Kampuni ya TanPower Resources iliyokabidhiwa mgodi huo kushindwa kuuendesha na kuamua kuurudisha serikalini.

Kabla hajatoa ufafanuzi zaidi kuhusu mgodi huo, Waziri Biteko alisema kuwa kuna idadi kubwa ya wawekezaji wa nje na ndani ya nchi waliojitokeza kutaka kuwekeza kwenye mgodi huo.

Biteko alisema changamoto iliyokuwepo ni kwamba wakati mwekezaji huyo ambaye ni TanPower Resources anaondoka, aliondoka na deni la Sh bilioni 2.9 ambalo alipaswa kuilipa serikali kama faida itokanayo na mauzo ya rasilimali (capital gain). Alisema ili kuhamisha ubia ule kutoka kwa TanPower Resources, lazima deni hilo lilipwe kwanza.

Ikumbukwe kwamba, Mgodi wa Kiwira ulikuwa unamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali na TanPower Resources. Serikali ilikuwa na umiliki wa asilimia 30 na TanPower Resources asilimia 70.
Biteko alisema TanPower Resources walinunua asilimia 70 ya hisa kwa takribani Sh bilioni 8.

Rais Magufuli aliiagiza Wizara yake kuhamisha hisa zote asilimia 70 za TanPower Resources na kuzirejesha serikalini ili mgodi huo uanze kufanya kazi haraka.

“Wizara ya Madini tumeshakutana na wenzetu wa Wizara ya Fedha na Mipango ili kuona deni hili linaweza kulipwa kwa namna gani, lakini wananchi wanafahamu kwamba yalikuwepo madeni makubwa yaliyoachwa na TanPower Resources na jumla ya Sh bilioni 40.6 zilikuwa zinadaiwa,”alieleza Biteko.

Kutokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la ufisadi nchini, Biteko alisema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani iliamua kufanya uhakiki wa madeni hayo na kubaini kuwa malipo halisi yalikuwa Sh bilioni 1.24 na si Sh bilioni 40.6, na watu waliokuwa wakidai walikuwa 862 tu na siyo 1,862 kama ilivyoelezwa awali.

Alisema Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ilipomtafuta mhusika wa Kampuni ya TanPower Resources hawakuweza kumpata kwa kuwa alitoroka, lakini utaratibu wa kuhamisha hisa za asilimia 70 za kampuni hiyo unaendelea ili mgodi uweze kuanza kazi. Katika ziara hiyo, Rais Magufuli pia alikifungua Kiwanda cha Maparachichi cha Rungwe.

Aliishukuru Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni hiyo kwa kufungua kiwanda hicho ambacho kimetoa fursa kwa wakulima 20,000 kuuza maparachichi yao kiwandani hapo.

Katika kujali maslahi ya wakulima na wafanyakazi, Rais Magufuli aliutaka uongozi wa kiwanda hicho kununua maparachichi ya wakulima kwa bei nzuri pamoja na kuwalipa wafanyakazi wa kiwanda hicho mishahara mizuri ili waone faida ya kazi yao.

HabariLeo
 
Sasa ndio ndio ameongea ukweli, 'kufufua miradi' sio kwenda kuzindua Vilivyopo.

Tunatakiwa tumuone Mkuu akienda kufufua Barabara, Kufufua Viwanda, nk.
 
Mh.Mkapa anasemaje?
Ulitaka asemeje wakati ushaambiwa kuwa mgodi wa Kiwira ulisimama kufanya kazi tangu mwaka 2005 kutokana na Kampuni ya TanPower Resources iliyokabidhiwa mgodi huo kushindwa kuuendesha na kuamua kuurudisha serikalini. Kampuni ya TanPower Resources
 
Mh.Mkapa anasemaje?
ulitaka asemeje wakati ushaambiwa kuwa mgodi wa Kiwira ulisimama kufanya kazi tangu mwaka 2005 kutokana na Kampuni ya TanPower Resources iliyokabidhiwa mgodi huo kushindwa kuuendesha na kuamua kuurudisha serikalini. Kampuni ya TanPower Resources.
 
Kama aliondoka na deni kweli kwanini msimvizie kati ya Same na Segera mumkamate alilipe deni kama mnavyotufanyia sisi?
 
wazo zuri bt unaweza kuta Huyo Tanpower ni mbongo mwenzetu tena yupo Ndan ya serikali

Vema sana ,umeenda mbele zaidi.Tunaweza chezewa Mchezo na tukawa wa kwanza kupiga vigelegele bila ya kujijua.
 
Back
Top Bottom