Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) wasikitishwa na maoni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

kanta

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
343
65
Mgodi wa Dhahabu wa Geita umejibu tuhuma mbalimbali zilizotolewa na CCM

Mnamo Tarehe 23 Novemba 2012, wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM), akiwemo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Bw. Steven Masele walifanya mkutano wa hadhara Geita mjini, katika mkutano huo walilalamikia mgodi wa Geita kwamba unahusika na vifo vya wanajamii wanaofia Mgodini hapa,na pia walizidi kusema kwamba mgodi haulipi kodi ya kutosha na wakazidi kungumza kuwa GGM inasuasua katika kukamilisha mradi wa maji. Kutoakana na kauli hiyo Mkurugenzi wa mgodi huo amelazimika kutolea ufafanuzi madai hayo na kuyaita ya kizushi huku akisisitiza kwamba GGM inafuata misingi ya haki za binadamu ambayo ilikubali kutia sahihi.

Ifuatayo ni taarifa ya mkurugenzi huyo aliyotoa kwa umma na kusambazwa kwa wafanyakazi wote pamoja na wananchi wa Geita.

Kodi na Michango
Mkurugugenzi Mtendaji wa Mgodi Wa Geita (GGM), Bw. Gary Davies alisema kwamba GGM ni kati ya kampuni pekee inayochangia kodi ya mapato kubwa zaidi Tanzania. '‘Tunachangia kulipa kodi ya mapato(Corporate), mirahaba (royalties), utendaji, ada na kodi ya mishahara yetu, michango yetu kwa Serikali ya Tanzania kwa mwaka jana 2011,ilikuwa zaidi ya dola $100M, na huenda mwaka huu 2012 kodi hii ikaongezeka mara mbili na kuwa dola zaidi ya $200M. Mgodi huu unazingatia ulipaji wa kodi kwa mda mwafaka kama inavyotakiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)'', aliongeza.

Malipo ya michango hii ya kodi yanadhibitishwa kwa usahihi kupitia Mpango wa uhamasishaji uwazi katika mapato ya Madini, Gesi na Mafuta (Tanzania Extractive Industry Transparency Initiative (TEITI).

Vifo vinavyohusu wanajamii.
Kampuni ya uchimbaji ya Geita (GGM) inadhibitisha kutokea kwa vifo vya watu 23 wasio wafanyakazi wa mgodi (third party) kwa mwaka huu wa 2012, na kwamba vifo hivi vimesababishwa na wanajamii kujiweka katika hali ya hatari, wanapokuwa wanavamia na hata kuuibia mgodi, wanafanya vitendo hivi bila kuzingatia usalama wa maisha yao na hii hupelekea hata kutokuogopa muingiliano kati ya na Mashine zinazotumika katika uzalishaji (Haul trucks).

'‘Kampuni inahuzunishwa kwa vifo vinavyotokea ndani ya maeneo ya Mgodi, na pindi matukio hayo yanapotokea taratibu zote za kutoa taarifa kwa vyombo husika ikiwemo Polisi na ofisi za Madini hufuatwa'', alisema.

GGM inafanya kazi kwa mujibu wa Kanuni za Umoja wa Mataifa kwa kufuata Usalama na Haki za Binadamu (VPSHR) na inashirikiana kikamilifu na tume ya polisi na serikali katika kufanya uchunguzi panapo hitajika. GGM inadhamini maadili ya uwazi na ukweli kama misingi ya mahusiano ya kuaminiana na kuthaminiana na jamii inayozunguka mgodi.

Urasimishaji wa Wachimbaji wadogo wadogo (ASM).
Bw. Davies alisema kwamba GGM inaunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza tija na kuboresha uchimbaji mdogo wa madini, hali itakayo ipatia serikali fursa ya kujiongezea kipato kwa njia ya mrahaba na pia kuboresha hali ya usalama na mazingira, hali hii pia itapunguza uhalifu na uvamizi unaojitokeza kwa sasa.

Aliongeza kwamba ni vyema kujikita katika kuangalia mazingira endelevu kwa kuboresha hali ya wachimbaji wadogo wadogo (ASM),na alisisitiza kwamba kwa wanasiasa kupendekeza kuwa Kampuni iwapatie wachimbaji wadogo wadogo makapi ya mawe( magwangala) halitakuwa suluhisho la mda mrefu kwani kuna changamoto za Usalama na afya na pia nikinyume kwa mujibu wa sheria za nchi.

Mgodi wa Geita una nia na mpango wa kushirikiana na kufanya utafiti na Migodi mingine, Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia ili kuwawezesha wachimbaji wadogo wadogo nchini.

Kusaidia uramishaji wa wachimbaji wadogo wadogo unao endana na sera ya serikali kuhusu mkukuta ambao unasisitiza kusaidia sekta binafsi kwaajili ya maendeleo na faida kwa watanzania wanaotaka kushiriki katika uchimbaji halali wa madini.

Uwekezaji katika Jamii
BW. Davies vilevile amesema Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) inaendelea kwa haraka iwezekanavyo kumaliza sehemu yake ya ujenzi wa mradi wa maji wa Geita. Kazi hiyo inayohusisha ujenzi wa sehemu ya kuhifadhia na kusafishia maji ilianza mwezi wa sita 2012.

Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) itakamilisha sehemu yake ya mradi ifikapo mwezi wa pili 2013.Mradi huu unatarajiwa kuwapa maji safi na salama yakunywa zaidi ya wakazi 100,000 wa Geita mjini, na unajengwa kwa ufadhili wa Mgodi na ushiriakiano na serikali ya Tanzania.Mchango wa GGM katika mradi huu inakadiriwa kufikia Dola za kimarekani 4.5M' alisema.

Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) inaoanisha uwekezaji wake katika jamii na sera ya umoja wa mataifa (United Nation's Millennium development Goals), unaohusisha matumizi makubwa ya ubia na serikali na jumuia za kijamii za mwaka 2011, kampuni (GGM) imewekeza zaidi ya Dola za Marekani 4M katika miradi ya maendeleo ya jamii. Miradi hiyo inajumuisha shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankunbu; Chuo cha ufundi cha madini Moshi (the Integrted mining Technical Training course at Veta Moshi); Hospitali ya wilaya ya Geita; upasuaji wa midomo ya sungura(cleft palate), Kituo cha Watoto yatima cha Moyo wa Huruma, na matembezi ya kila Mwaka ya Kupanda Mlima kilimanjaro ikiwa ni kampeni ya kupambana na vita dhidi ya Ukimwi (HIV/AIDS).

Mtazamo wangu:

CCM iache kutapatapa kutokana na ukweli kwamba mikataba yote mibovu ya madini imesimamiwa na Serikali yake, haya yanayotokea sasa ni sehemu tu ya utumbo wa mikataba hiyo mibovu, tangu hapo mwanzo walikuwa wapi mpaka sasa ndio wanajifanya wanashtuka, wasubiri tu kiama chao hapo 2015.
 
Tatizo lao wanakopi kila kinachozungumzwa na chadema matokeo yake wanajisiliba kinyesi usoni wenyewe
 
Hizi ni dalili za machafuko 2015. Kama CCM wako radhi kujipaka mavi sasa, hakuna atakayewazua kuua 2015.
 
..., huu mgodi si ndo yule millionea namba tano kwa tanzania ana hisa?
 
Tatizo lao wanakopi kila kinachozungumzwa na chadema matokeo yake wanajisiliba kinyesi usoni wenyewe

Nani sasa anae copy? anae ongoza dola au anae ongozwa na dola ? siku zote dola huwa hai copy, soma siasa za dunia uone
.
 
GGM ndiyo mgodi mkubwa kabisa kuliko migodi yote ya dhahabu Tanzania.

Lakini katika orodha ya walipa kodi wakubwa aliyoisoma Pinda Bungeni GGM haimo. Badala yako kuna ka-Mgodi ka Resolute Pride wa Nzega ambao ni wa pili kwa udogo Tanzania, mdogo kabisa ukiwa Tulawaka.

GGM ni wezi tu, na wizi wao umewezeshwa na Serikali ya CCM.
 
GGM ndiyo mgodi mkubwa kabisa kuliko migodi yote ya dhahabu Tanzania.

Lakini katika orodha ya walipa kodi wakubwa aliyoisoma Pinda Bungeni GGM haimo. Badala yako kuna ka-Mgodi ka Resolute Pride wa Nzega ambao ni wa pili kwa udogo Tanzania, mdogo kabisa ukiwa Tulawaka.

GGM ni wezi tu, na wizi wao umewezeshwa na Serikali ya CCM.

hivi wamebakiza mda gani? maana sidhani kama mjukuu wangu atashuhudia kumalizika kwa mkataba
 
:fencing: hii show kali eh!
hata tukiongea masaa mia hakuna atakae umia hapo,
naona Kinana anataka pesa, kaamua kuwabeep ili wapige!
 
CCM na GGM wasituchezee akiri. Kiini cha yote hato ni serikali zaifu ya CCM pamoja na mikataba feki ya madini. Hata huko Mara wananchi wamelalamika juu ya uchafuzi wa maji kutokana na machimbo ya dhahabu lakini serikali ya CCM haiachukua hatua. Sasa wamebakia kukopi siasa za CDM.
 
Kama watawala (CCM) nao wanalalamika, wananchi wa kawaida tufanye nini sasa? Wana vyombo vyote vya dola vinavyosubiri amri kutoka kwao lakini badala ya kuvitumia wanaenda kulalamika jukwaani geita! Hayo ni Tanzania tu.
 
Ukifika Geita huwezi amini kama ndio sehemu inatoa dhahabu kwa wingi nchini Tanzania

CCM hoyeeeeeeeeeeeee!
 
Kwani Mwl Nyerere aliposema tuache madini yetu ardhini yasubiri uwezo wa watanzania wenyewe kujenga uwezo wa kielimu, kiteknolojia na kimtaji ili tuchimbe madini walifikiri ni mpumbavu sana ila wao ndo wenye akili sana. Basi ngoja tushuhudie historia ikichukua mkondo wake ndani ya chama hicho hicho tawala wakisigana kimtazamo na kiutekelezaji sera zisizo na mashiko kwa mtanzania.
 
Bw. Davies alisema kwamba GGM inaunga mkono juhudi za Serikali za kuongeza tija na kuboresha uchimbaji mdogo wa madini, hali itakayo ipatia serikali fursa ya kujiongezea kipato kwa njia ya mrahaba na pia kuboresha hali ya usalama na mazingira, hali hii pia itapunguza uhalifu na uvamizi unaojitokeza kwa sasa.

UCHAMBUZI:Miongoni mwa Migodi nchini inayodaiwa kuwaonea na kuwanyanyasa wananchi wake ni pamoja na Mgodi huu wa geita(GGM),kuna wananchi wengi sana ambao wameathirika kutokana na manyanyaso ya mgodi huu wakiwemo wale wa Eneo la katoma ambao wamshindwa kuwalipa hadi sasa pamoja na kuchukua eneo lao.

Pili kuna wananchi ambao hadi sasa wanaishi kwenye maturubai tena waliyopatiwa na madhehebu mbalimbali kwenye ofisi za Tarafa baada ya uongozi wa mgodi kuwatumia polisi kuwahamisha usiku na kisha kwenda kuwamwaga kwenye eneo hilo na wanasota kwa miaka takribani saba sasa na wengine walikwishafariki bila kupata haki zao,sasa sijui ni nni ambaye atanufaika na hilo jasho lao,hawa wote walikuwa ni wachimbaji wadogo.

Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGM) inaoanisha uwekezaji wake katika jamii na sera ya umoja wa mataifa (United Nation’s Millennium development Goals), unaohusisha matumizi makubwa ya ubia na serikali na jumuia za kijamii za mwaka 2011, kampuni (GGM) imewekeza zaidi ya Dola za Marekani 4M katika miradi ya maendeleo ya jamii. Miradi hiyo inajumuisha shule ya Sekondari ya Wasichana ya Nyankunbu; Chuo cha ufundi cha madini Moshi (the Integrted mining Technical Training course at Veta Moshi); Hospitali ya wilaya ya Geita; upasuaji wa midomo ya sungura(cleft palate), Kituo cha Watoto yatima cha Moyo wa Huruma, na matembezi ya kila Mwaka ya Kupanda Mlima kilimanjaro ikiwa ni kampeni ya kupambana na vita dhidi ya Ukimwi (HIV/AIDS).

UCHAMBUZI:Miradi ambayo GGM inasema imetekeleza tangu kuanzishwa kwake mwa 2000 haipo isipokuwa ni mradi mmoja tu wa ujenzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Nyankumbu ambayo hata hivyo mgodi huo haujakamilisha ujenzi wake tangu mwaka 2004 ilipouanzisha!

Kwa mujibu wa mkataba baina ya Mgodi na halmashauri ya wilaya hiyo ya Geita shule hiyo ambayo ni ya Bweni ilipaswa kuwa imekamilika na kuanza kupokea wanafunzi tangu mwaka 2005 ikiwa ni kuanzia kidato cha kwanza hadi cha tano huku ikiwa na mahitaji yake yote,mabweni,maabara,nyumba za walimu na kila kitu kinachohitajika kwenye shule na hasa ambayo ni Boding' lakini hadi sasa shule hiyo bado haijakamilika ingawa waliongeza kasi zaidi tangu mwaka huu uane bad ya serikali kuijia juu na kuitishia!

Miradi mingine ile ambayo imetoa michango ya mabati kuchangia ujenzi na hasa kwenye shule za sekondari mwaka 2005 wakati huo wilay ya Geita ikiwa na shule 14 tu za sekondari wakati leo hii kuna jumla ya shule 47 ambazo zimejengwa kwa nguvu za wananchi!

Kwenye hospitali ya wilaya walichochangia ni ukarabati wa chumba cha upasuaji pamoja na ununuzi wa baadhi ya vifa katika chumba hicho,lakini hakuna jengo jipya ambalo wao wamelijenga kwa kutumia fedha zao,na inavyoonekana walikuwa wakitumia mwanya wa kulinda na hao hao viongozi wa ccm ili waendelee kuwaibia watanzania!

Swali langu la msingi hapa hebu huyo mkurugenzi wa mgodi au mtoa mada hii ajitokeze aeleze au aonyosehe mradi ambao umeamzishwa moja kwa moja na GGM na kuukamilisha ka ajili ya kuwsaidia wananchi,geita hakuna hospitali ya mana,hkuna shule ya Bweni ya maana,hakuna barabara za mana ukifika Geita huwezi amini kama uko kwenye eno ambalo linaongoza nchini kwa uzalishaji wa dhahabu,mji ambao unabeba mgodi wa tatu kwa ukubwa Barani Afrika na watano kwa ukubwa Duniani!!!!

Kwenye mita ya mji wa Geita ni mashimo tupu hakuna barabara iliyo nzuri,pita maeneo ya Benki kwenda ikulu ndogo,pita barabara ya CRDB kwenda halmashauri na hospitali ya wilaya,utadhani unapita kenye maporomoko,nenda hospitali ya wilaya kenye wodi ya wakina mama wajawazito,wanalala wawili wawili kitandani,hebu fikiria mwanamke na tumbo lake wanalala kwenye kitanda kimoja wawili huku wnaumwa uchungu,halafu bado mtu anajitokeza na kueleza kwamba wanaisaidia jamii!inaumiza sana wakuu!!

Hebu angali hao watanzania 23 waliokufa tangu kuanza kwa mwaka huu ndani ya Mgodi kama taarifa ya mkurugenzi huyo ilivyoeleza,hawa ni wale choka mbaya ambao walikuwa wakiingia ndani ya mgodi kwa ajili ya kujikotoea mawe ya dhahabu ili nao wapate kula na kuendesh familia zao,wameuawa wanafunzi ndani ya mgodi huo kwa kupigwa risasi akiwa amekwenda kutafuta mawe ili apate sare za shule,huyu mwanafunzi alikuwa na silaha gani,waliompiga risasi ni walinzi wa mgodi,hawa wote wamepiga wengine kuvunjwa vikombe na walinzi wa mgodi,halafu mtu bado anajitokeza na kujitetea eti waliingia kwa ajili ya kuiba.

Hivi sheria za nchi zinasemaje kuhusu mwizi?,hili sio suala la kutetea hata kidogo,sasa leo wenzao CCM wameona mambo yanakwenda vibay amewageuka na kuanza kufichua siri zao bad ya kubaini kuwa wamekuwa wakisababisha wao wachukiwe na jamii kwa serikali yake kuubeba mgodi huo na kuutetea leo wanasimama na kujitetea eti waniponda CCM,jamani hivi tunakwenda wapi?!!!!

Kuna mengi ya kueleza juu ya Mgodi huu lakini kwa sasa naom,ba niishie hapa lakini tuwe wawazi kwamba huu mgodi hauna faida yoyote ile ka watanzania,kwa sababu kama kila wiki inasafirisha dhahabu yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 45,ni kwa nini misaada kwa jamii inashindikana?,hivi kwani wakiamua potelea mbali kutenga hata shilingi milionin 200 tu kila wiki kusaidia shughuli za kijamii kwenye wilaya hiyo kwa hiyo dhahabu wanyozalisha mpaka sasa si wangekuwa wamekamilisha hata chuo kikuu?



 
Ukifika Geita huwezi amini kama ndio sehemu inatoa dhahabu kwa wingi nchini Tanzania

CCM hoyeeeeeeeeeeeee!

Mkuu ni aibu kubwa sana Geita haifanani kam eneo kuu linalozalisha dhhabu nyingi hapa nchini,inaumiza sana hata barabara tu ukiziangalia utaona kinyaa,ndio maana wale jmaa wa tarime kule wanaamua kujichukulia sheria mkononi kwa kuishughulikia Mgodi,ndiyo maana sasa hivi wale jamaa wa Nyamongo wanatekeleza miradi kwa jamii kama vile hawana akili,cheki wameweka Lami wananchi kwa sasa wanenjoy,lakini naamini hata huko Geita litawaka tu siku moja.
 
GGM na CCM wote ni wezi! Upumbavu wao huu

Yawezekana Mkuu lakini ukifanya ziara siku moja Geita utamini kwamba GGM ni wezi zaidi ya CCM,ndiyo maana unaona CCM wamestuka na kuwageuka bada ya kugundua kwamba wenzao wanaiba zaidi!!!!!
 
CCM wants to benefit from their own wrong doing. Upuuzi mtupu. Ukiiangalia hii mikataba ya hawa wawekezaji unaweza kupasuka kwa hasira. No wonder serikali inadai hii mikataba ni siri. Wanajua madudu yaliyojaa humo.
 
CCM wants to benefit from their own wrong doing. Upuuzi mtupu. Ukiiangalia hii mikataba ya hawa wawekezaji unaweza kupasuka kwa hasira. No wonder serikali inadai hii mikataba ni siri. Wanajua madudu yaliyojaa humo.

Mkuu mikataba ipo na inasomeka vizuri sana yaani ni utumbo mtupu mkuu,hakuna kitu kwenye mikataba hiyo ndiyo mana unasema utapasuka,lakini mi nadhani hatuna haja ya kupasuka bali kudil nao tu hawa jamaa kwa sababu ni jnga la Taifa,yani hebu jaribu siku moja kuitembelea wilaya ya Geita utaihurumia kama si kupasuka kwa kila kitu.yani watu wnaoishi huko ukiwaangalia utawakimbia huwezi amini kwamba ni watu ambao wanatoka sehemu ambayo inazalisha dhahabu kwa wingi.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom