Mgodi wa buzwagi na hewa chafu!! Watu watapika na kuzirai

Nyakageni

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
15,048
5,092
Siku ya jumanne tarehe 8/11/2011 kuanzia muda wa saa 9 ya jioni, kulitoka hewa yenye harufu nzito sana iliyosambaa hadi nje ya mgodi wa Buzwagi.

Hewa hiyo ilisababisha wanakijiji pamoja na wanafunzi wa shule jirani kutapika na wengine kuzirai. OCD alitembelea sehemu husika lakini hajatoa tamko. Kuna uwezekano wa wanakijiji kuonesha hisia zao.

Pia visima vilivyokuwa vikitumiwa na wananchi kwa sasa, maji yana madhara makubwa! Kuna kaujanja kanafanywa na mkuu wa wilaya ili kufunika kombe.

MY TAKE: Madhara ya mgodi kwa wananzengo ni makubwa na yanafichwa kisiasa, kwani hali ya kisiasa hapa Kahama ni tete kwa Magamba! Nawasilisha wakuu!!
 
Hivi hapo Buzwagi karibu na hilo bwawa la maji machafu yanayotoka mgodini naona kuna shule ya sekondari ya wasichana inayomilikiwa na masister wa kanisa katoliki, ipo kama mita mia hivi kutoka katika hilo bwawa. Sijui hali ilikuwaje kwa wanetu hao na maji wanayotumia sijui imekaaje hapo.

Nakumbuka Mkapa alifungua hii shule wakiwa na waziri Maige mbunge wa msalala mwaka 2009 sasa kuna umuhimu wa wana Kahama kuonyesha hisia zao kwanza vumbi la mgodini limeuharibu kabisa mji wa Kahama unaonekana kuchakaa kadri siku zinavyokwenda sasa madini yamekuwa adha na adhabu kwa wanaKahama.

Maisha yamekuwa magumu kuliko maelezo bidhaa zimepanda bei kuliko inavyodhaniwa Kahama sasa ni moto vijana wamechoka kabisa hizo ajira zilizosemwa na CCM kipindi cha uchaguzi zimegeuka ndoto ni wageni tu ndio wenye ajira zenye ujira mzuri mgodini.

Ukame umeiandama Kahama kwa miaka mitatu mfululizo sasa,viongozi wa Chadema kuna umuhimu wa kuweka kambi kahama ili tuikomboe vijana wanahamu sana na mabadiliko ilikuwang'oa nduli hawa wanaoitafuna Kahama.
 
@ Micro E-coli, kwa habari ya kutoka shule ya Mwendakulima sekondari watoto walizirai sana, hiyo shule ya masista hawatumii maji ya kile kibwawa bali ni ya bomba toka Mwanza! Ila nao walikuwa affected na OCD alitembelea shule zote hizo
 
Tuyaonapo haya tuimbe ule wimbo mzuri kuliko nyimbo zote "chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi,chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi....

Lowassa ahhh, ajenga nchi...Karamagi aahhhh, ajenga nchi...

Kikwete aghhh ajenga nchi...."
 
Tuyaonapo haya tuimbe ule wimbo mzuri kuliko nyimbo zote "chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi,chama chetu cha mapinduzi chajenga nchi....

Lowassa ahhh, ajenga nchi...Karamagi aahhhh, ajenga nchi...

Kikwete aghhh ajenga nchi...."
Bull shit !!! better I log off.
 
Kuna sheria na taasisi kama sita hivi zinazoweza kuwafungulia mashtaka hao jamaa katika majarada tofauti!! kwanini wasichukue hatua. kwa huo ushahidi tu wa mvuke/moshi/vumbi penalty yake yaweza kufika 50 billion au kufunga mgodi na pengine kufungwa kwa mkurugenzi/Meneja wa mgodi. Swali ni kwamba:- hizo taasisi zinamuogopa nani?!!!!!!!!!!!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom