Mgodi wa Barrick wapigwa faini Tsh Bilioni 1 kwa uchafuzi wa mazingira

At Calvary

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
4,513
3,554
Mgodi wa Barrick North Mara uliopo mkoani Mara umepigwa faini ya shilingi Bilioni moja na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kosa la uchafuzi wa mazingira baada ya bomba linalopitisha maji taka kutoka kwenye mgodi huo kupasuka na kutiririsha maji katika Mto Tigite unaomwaga maji yake Mto Mara.

Source: ITV

---
Waziri wa Madini, Doto Biteko ameutoza faini ya Sh1 bilioni mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara baada ya kupasuka kwa bomba katika kijiji cha Nyangoto wilayani Tarime.

Pia, amemuondoa katika nafasi yake ofisa mgodi mkazi, Hamad Kallaye kwa madai ya kushindwa kutimiza wajibu wake.

Akizungumza baada ya kufika katika eneo hilo leo Jumapili Aprili 24, 2022, Biteko amesema kuwa faini hiyo inatakiwa ilipwe ndani ya siku 14 kuanzia leo.

" Maji yamevuja kwa zaidi ya saa nne bila kuchukua hatua zozote wakati hapa mtu akiingia na kuiba atapatikana ndani ya nusu saa tu hivi kama haya maji yangekuwa na sumu leo tungekuwa tunaongea lugha gani" amesema Biteko

Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limesema bomba hilo lililopasuka linatoa maji katika bwawa linalokusanya maji kutoka kwenye miamba ya mashimo ya dhahabu kwenye mgodi wa dhahabu wa Barrick North Mara na si kwenye bwawa la sumu kama ilivyodhaniwa awali.

Meneja wa NEMC Kanda ya Ziwa, Jerome Kayombo amesema lipo bwawa maalum linalokusanya maji yanayotiririka kutoka kwenye miamba kwa ajili ya kuhifadhiwa kabla ya kusafirishwa kwa ajili ya kutibiwa na kutumika kwa matumizi ya kawaida.

ADVERTISEMENT

" Lipo bwawa maalum linalokusanya maji kutoka kwenye miamba ambayo kwa asili yana tindikali kwahiyo yakishajaa kwenye bwawa yanasafirishwa kwenye mfumo kwa ajili ya kutibiwa ili kuingia kwenye mfumo wa matumizi ya kawaida," amesema

Amesema kuwa mara baada ya tukio hilo kutokea, juzi wataalam kutoka NEMC walifika katika eneo hilo na tayari wamechukua sampuli za maji kutoka katika maeneo tofauti ikiwemo kwenye mto Tigite ili kupima ubora wa maji hayo.

Naye Meneja wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Ziwa, Musa Kazimila amesema vipimo vya awali vinaonyesha maji katika eneo hilo ni salama, ingawa uchunguzi wa kina unaendelea na majibu yanatarajiwa kutoka Jumatano Aprili 27, 2022.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally lly Hapi amesema Serikali ya mkoa itaweka utaratibu maalum wa kulinda maeneo ambayo ni hatarishi ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea.

Kwa upande wake Meneja wa mgodi huo, Apolinary Lyambiko amesema baada ya kupata taarifa za kupasuka kwa bomba hilo walifika eneo la tukio kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi ili kuzuia hali hiyo.

Mwananchi
 
Mgodi wa Barrick North Mara uliopo mkoani Mara umepigwa faini ya shilingi Bilioni moja na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kosa la uchafuzi wa mazingira baada ya bomba linalopitisha maji taka kutoka kwenye mgodi huo kupasuka na kutiririsha maji katika Mto Tigite unaomwaga maji yake mto Mara.

Source: ITV
 
Mgodi wa Barrick North Mara uliopo mkoani Mara umepigwa faini ya shilingi Bilioni moja na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kosa la uchafuzi wa mazingira baada ya bomba linalopitisha maji taka kutoka kwenye mgodi huo kupasuka na kutiririsha maji katika Mto Tigite unaomwaga maji yake Mto Mara.

Source: ITV
Sasa yale majani yanayotoa mafuta vip
 
Mgodi wa Barrick North Mara uliopo mkoani Mara umepigwa faini ya shilingi Bilioni moja na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kosa la uchafuzi wa mazingira baada ya bomba linalopitisha maji taka kutoka kwenye mgodi huo kupasuka na kutiririsha maji katika Mto Tigite unaomwaga maji yake Mto Mara.

Source: ITV
 
Attachments

  • VID-20220424-WA0023.mp4
    14.4 MB
Masuala ya mgodi wa north mara ni mengi sana watu wanao ishi eneo la mgodi huu wanajua kero nyingi tu hilo suala la maji mbona ni kitu cha kawaida wala halijaanza leo na wala hii haitakuwa mara ya mwisho kwao, huku ndani kila kitu ni siasa tu na maslahi ya wakubwa, ila shida ni nyingi saana
 
Hiyo tume ya uchunguzi inapaswa iundiwe tume ya uchunguzi.😁.

NEMC wenyewe wako kwenye payroll ya hiyo migodi,hapo wamejitutumua tu baada ya report kugonga mwamba.
 
yani una unda kikuundi cha watu kikafanye kazi ya taasisi ambayo ni wabobevu katika eneo hilo na ipo chini ya mamlaka yako (ofisi yako) NEMC
 
Yule profesa uchwara na timu yake wapigwe risas hadharan
Wahuni hao
Prof. Manyele. Sijawahi kuona mfipa incompetent Kama yule'. Alikua mkemia mkuu wa serikali nako huko Bora tu amemaliza muda wake.
Najiuliza hii PhD ya Manyele na ya msukuma zinatofauti?
 
Mgodi wa Barrick North Mara uliopo mkoani Mara umepigwa faini ya shilingi Bilioni moja na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kosa la uchafuzi wa mazingira baada ya bomba linalopitisha maji taka kutoka kwenye mgodi huo kupasuka na kutiririsha maji katika Mto Tigite unaomwaga maji yake Mto Mara.

Source: ITV
Leka du Tigite...
 
Back
Top Bottom