Mgodi wa Barrick wafikishwa mahakamani

Pwaaaa

JF-Expert Member
Feb 16, 2013
248
67
Huwezi kuamini, lakini ndivyo ilivyo. Nimedokezwa Jana mkazi wa Nyamongo Tarime mkoani Mara, CHACHA KIGUHA BABERE aliupandisha mahakamani kwa mara ya kwanza uongozi wa mgodi wa Afrikan Barrick Gold Mine.

Kesi ipo mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, na. 9/2013. Kesi imefunguliwa na familia ya Chacha, wanadai walipwe fidia ya sh. bilioni 1 na milioni 200, kwa madai wameathirika mno kiafya kutokana na shughuli za mgodi huo!. Hapo upo mwana JF?.

Picha ya kwanza. Kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu likiwa linaonekana kuunguza sehemu lilipoangukia eneo la mgodi wa Nyamongo.

Picha ya pili. Chacha na familia yake wakiwa home wakitafakari jinsi maisha yalivyomagumu.

Picha ya tatu. Ofisa mmoja wa serikali akisoma barua baada ya kufika nyumbani kwa Chacha. ANGALIZO, kama kuna maelezo mengine ya picha hizi hayana UHAKIKA SANA!.
 

Attachments

  • Bomu la Polisi la moto lililoanguka kwa makazi ya Chacha Kiguha..jpg
    Bomu la Polisi la moto lililoanguka kwa makazi ya Chacha Kiguha..jpg
    510.4 KB · Views: 182
  • Familia ya Chacha Kiguha ikiwa nyumbani kwake..jpg
    Familia ya Chacha Kiguha ikiwa nyumbani kwake..jpg
    363 KB · Views: 156
  • MTENDAJI WA KIJIJI CHA NYAMWAGA JAMES WAMBURA AKIWA NA CHACHA KIGUHA BABERE KATIKA TUKIO LA KUBO.jpg
    MTENDAJI WA KIJIJI CHA NYAMWAGA JAMES WAMBURA AKIWA NA CHACHA KIGUHA BABERE KATIKA TUKIO LA KUBO.jpg
    53.1 KB · Views: 153
Picha ya 2: mbona wote ni wazima tu, jamaa afanye kazi asitafute hela ya mteremko.
 
hatokaa ashinde kesi,ccm wana maslahi ya moja kwa moja kwenye mikataba ya migodi,kwa ufupi vigogo wa ccm ni shareholders kwenye hizo kampuni especialli barick!!!
 
Kabla ya kuanza kuiandama Barrick ni vema mawakili wake wakajua uharamia wa Barrick uliofanyika kule Latin America na kwingineko...Barrick ni zaidi tuijuavyo, hawa jamaa wanajiita game changer madai yao wanaweza kumuweka madarakani rais ama waziri wamtakae...Bajeti ya akina mwigulu pale lumumba karibu yote inatolewa na hawa Jamaa... ANGALIZO tu siyo kuwa nawafagilia ila hawa ni zaidi ya MAFIA tunaowasikia na kuwaona kwenye movie na story books...
 
Tuambie wewe wasemaje badala ya kuathirika kiafya?.

Aeleze kinagaubaga uhusiano wa afya yake kudhoofu na uwepo wa Barrick maeneo hayo anayoishi...
Maana kama kaamua kulipeleka suala hili mbele ya vyombo vya sheria basi inabidi awe amejipanga kwa ushahidi toshelezi...
Naamini kama ana vielelezo makini huenda akapata support toka kwa wanakijiji wenzake ambao nao pengine wamekutwa na athari hizo lakini hawana ufahamu uhusiano wa athari hizo kiafya na uwepo wa Barrick...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom