Mgodi wa Barrick (Bulyanhulu) wafungwa; kisa NSSF na PPF, wafanyakazi wako tayari kupoteza kazi!

MAGAMBA MATATU

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
646
1,174
Shija Felician, Kahama | Mwananchi | Agosti 03, 2012

WAKATI sakata la kupinga sheria mpya ya mafao ya watumishi wanaoacha kazi katika sekta mbalimbali likizidi kushika kasi, Kampuni ya African Barrick Gold Mines juzi iliufunga mgodi wake wa Bulyanhulu baada ya wafanyakazi wake kugoma wakipinga sheria hiyo.

Habari zilizopatikana katika mgodi huo mkubwa hapa nchini kwa uzalishaji wa madini ya dhahabu na shaba, zilieleza kuwa chanzo cha kufungwa mgodi huo ni mgomo wa watumishi wanaofanya kazi ndani ya mashimo.

Hivi karibuni Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifuko ya Pensheni Nchini (SSRA), ilifanya marekebisho ya mafao ya watumishi wanaoacha kazi ama kufukuzwa kulipwa stahiki zao mpaka watakapofikisha umri wa miaka 55au 60 hatua ambayo ilipingwa na watu wengi.

Ofisa Uhusiano wa Kampuni hiyo Necta Foya, alisema shughuli zote za uzalishaji zimefungwa kwa masaa 48 ingawa zile za utawala zinazofanyika maeneo ya juu ya mgodi zinaendelea kama kawaida na baada ya muda huo watumishi wote waliosimama kazi wataitwa, na kwamba watakaoonekana kukubaliana na masharti wataendelelea na kazi.

Kabla ya hapo uongozi wa mgodi huo uliwataka watumishi hao kuendelea na kazi wakati suala lao likishughulikiwa baada ya kubaini wengi wao waliandika barua za kuacha kazi wakipinga masharti ya malipo ya ya pensheni .

Wafanyakazi wanaofanya kazi shimoni ndio wachimbaji wakuu wa madini katika migodi ya aina hiyo wakisaidiwa na mafundi mitambo, na hivyo kugoma kwao kufanya kazi kunaathiri uzalishaji kwa ujumla.

Hata hivyo baadhi ya watumishi waliokumbwa na hali hiyo jana walikuwa wamezagaaa mjini Kahama wakionyesha wasiwasi wa kurudishwa kazini kutokana na mwajiri wao kuchukizwa na hali ya mgomo huo unaodaiwa kuisababishia hasara kampuni.

Kwa mujibu wa Foya, leo wanatarajia kuongea na watumishi hao waliokuwa wamegoma baada ya masaa 48 kumalizika ambayo yalitolewa juzi wakati wa kufunga uzalishaji katika mgodi huo.
 
tanzania ni zaidi uijuavyo..hiyo sheria mbovu sana,na wasomi wetu ndiyo waliopitisha hiyo sheria..
 
Ni upepo tu unapita!!Liwalo na liwe !!! Kama unaona sheria hii haifai basi katafute kazi sehemu nyingine kwenye sheria unazozitaka!!! Haya ndiyo yatakuwa majibu ya viongozi wetu!!
 
Ni upepo tu unapita!!Liwalo na liwe !!! Kama unaona sheria hii haifai basi katafute kazi sehemu nyingine kwenye sheria unazozitaka!!! Haya ndiyo yatakuwa majibu ya viongozi wetu!!

generally,,,,uende NCHI NYINGINE,TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI UENDAKO
 
Kundi la kwanza kulaumiwa hapa ni BUNGE,,,,,,yaan ndo limezidi kujiharibia kwa kuruhusu hii sheria,,,,,,,
 
Mimi binafsi sielewi kwa nini wabunge wetu waliptisha shera hii. Huenda haiwagusi wao lakini kwa wengi wetu hi sheria ni kandamizi kishenzi hata senti zako usizipate unapoacha kazi wanategemea utaishi kwa kudra ya Mola? chako ni chako upewe uangalie ustaarabu mwingine maana mpaka miaka 60 utakuwa umesahau una salio mahali!
 
Hivi wakati hii sheria inapitishwa wabunge walikuwa wapi na je hawakuiona hasara zake?maana nilisikia kuwa wao wakimaliza muda wao wanapata mafao yao.je wale wabunge wanaokuwa mbele kutetea maslahi ya wanyonge walikuwa wapi?
 
Watarudi kazini jk akikoroma

kumbuka mwajiri atapata hasara sana kwani hata wakirudi production haifanyiki kunakuwa na mgomo baridi..ni mwajiri gani atapenda kuendesha kampuni kwa hasara?
Acha tu huyu Mama SSRA aendelee kuchezea vichwa vyetu
 
kumbuka mwajiri atapata hasara sana kwani hata wakirudi production haifanyiki kunakuwa na mgomo baridi..ni mwajiri gani atapenda kuendesha kampuni kwa hasara?
Acha tu huyu Mama SSRA aendelee kuchezea vichwa vyetu

Wasubiri JK awatume vijana wake wawapeleke Mwabepande
 
Huku ndio sekta binafsi bwana, kwa taarifa yenu, huyo mama Irene ameisha toa tamko tayari na kusema watu wa migodini hii sheria haiwahusu so wataendelea na utaratibu wa zamani kama kawa, for your infor, hawa watu wa migodini wameisha badiri sheria za mafao mara nyingi tu,

Wao wakiacha kazi wala hawalazimiki kusubiri hiyo miezi 6 yenu, yaani yeye akimalizana tu na mwajiri hata kabla hajafika nyumbani kwake anawahi NSSF/PPF na fomu zake, baada ya week 1-4 pesa yake inakuwa imeisha toka, huwezi kuwapeleka mahakamani because sio waajiriwa wa serikali, kwani hamkusikia lile tamka la meneja rasilimali watu wa mgodi wa Geita?

Aliwaambia hawa watu wa SSRA kuwa mtalazimika kulipa fidia ya mgomo uliotokea hapa, hasara yote mwatakiwa kuibeba na jamaa aliishia kuomba msamaha tu, hawa sio madaktari wala walimu!
 
Back
Top Bottom