Mgodi Kiwila: Mbunge Kimaro kufyata?

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,943
699
Katika siku za hivi karibuni mbunge wa Vunjo Mh. Aloyce Kimaro amekuwa mstari wa mbele kuhoji walakini wa umulikishaji wa mgodi wa Kiwila. Kama tunavyoelewa hapa jamvini, inaaminika kuwa huo mgodi ulimilikishwa fisadily kwa Senior Fisadi Mkapa, Daniel Yona na grupu lao. Mh. Kimaro amekuwa akitafuta ukweli juu ya hilo lakini sasa inaonekana kwamba ameanza kufyata baada ya wenzake kudai na yeye watamuumbua kuhusu kiwanja kikubwa anachomiliki kwa ajili ya ujenzi wa hoteli ya kitalii. Kutokana na tishio hilo, sasa Mh. Kimaro anadai kwa mujibu wa gazeti la Alasiri kuwa hajali huo mgodi unamilikiwa na nani au umiliki wake ukoje, cha msingi anahitaji Capacity charge iondolewe.
Sasa huu ujasiri umeishia wapi jamani? Kwa mwendo huu sijui kama FISADIZ tutawaweza. Kwa habari zaidi soma hapo chini hiyo Alasiri, kisha toa maoni yako kama hutajali.


Mgodi Kiwira moto!

2008-07-05 15:01:22
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Lile sakata la madai ya kumilikishwa kiutata kwa Mgodi wa Makaa ya Mawe ya Kiwira utakaotumika kuzalishia umeme kwa wamiliki wanaodaiwa kuwa ni pamoja na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa limeendelea kuwa moto ambapo sasa baadhi ya wabunge wamepania kulikomalia tena hadi watosheke na maelezo kamili ya Serikali.

Suala hilo, kwa mujibu wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, litatolewa ufafanuzi wa kina na Waziri wa Nishati na Madini, Mheshimiwa William Ngeleja.

Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu leo asubuhi, Mbunge wa Vunjo, Mheshimiwa Aloyce Kimaro ( CCM), amesema hadi sasa, yeye ni miongoni mwa wabunge ambao bado hawajatosheka na maelezo ambayo hadi sasa yameshatolewa kuhusiana na suala hilo Kiwira.

Mheshimiwa Kimaro ambaye ndiye aliyewahi kuonyesha ujasiri wa kutaka ufafanuzi wa kina wa suala hilo bungeni na kueleza hofu yake kuwa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini Bw. Daniel Yona walikiuka maadili ya uongozi kwa kujimilikisha mgodi huo kwa bei poa, amesema kama walivyo wabunge wengine, naye anasubiri kwa hamu kusikia maelezo ya Serikali.

Akasema ufafanuzi kuhusiana na sakata hilo ni muhimu kwani baada ya hapo, wananchi wataweza kuelewa ukweli wa yale yote yanayotiliwa shaka kuhusiana na raslimali yao hiyo.

Amsema Mheshimiwa Kimaro kuwa kwa vile suala hilo lilipoulizwa kwa Waziri Mkuu katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo bungeni lilipatiwa majibu kuwa Waziri Ngeleja ndiye atakayefafanua, na yeye na wengine wamekuwa wakisubiri kwa hamu maelezo hayo.

``Kila kitu kikishazungumzwa lazima kitolewe majibu ambayo yatawaridhisha wabunge na wananchi kwa ujumla. Ni wiki ijayo tu, bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini itawasilishwa bungeni... nadhani tuendelee kusubiri ili tusikie majibu kuhusiana na suala hili la Mgodi wa Kiwira na mengineyo,`` akasema Mheshimiwa Kimaro.

Akifafanua zaidi, Mheshimiwa Kimaro amesema miongoni mwa yale anayosubiri ni kuondolewa kwa malipo gharama ya `capacity charge` ambayo amedai kuwa yanachangia wananchi hivi sasa kuendelea kupandishiwa bili za umeme.

``Hebu fikiria... hii gharama (za capacity charge) imepangwa walipwe kwa kipindi cha miaka 20. Hii sio haki kwa Watanzania. Binafsi nitapenda iondolewe kabisa,`` akasema Mheshimiwa Kimaro.

Hata hivyo, akasema hivi sasa, yeye hana tatizo na umiliki wa mgodi huo, bali anachohitaji ni Watanzania kutendewa haki kwa kupata huduma ya nishati hiyo kwa bei poa.

``Suala sio nani kapata Kiwira... bila kujali nani anamiliki mgodi huo, mimi ninachotaka ni kuona hii capacity charge inaondolewa na bei ya umeme inashuka ili wananchi wapate unafuu tofauti na sasa,`` akasema Mheshimiwa Kimaro
 
Unapopambana na billionea asiyelipa kodi na asiye na maadili wala kanuni, inabidi uwe na akili ya kichaa, la sivyo unaweza kuchanganyikiwa.
 
Hawa wabunge wa CCM sasa nao wanatuchanganya! Ukifuatilia kwa makini namna wabunge wa CCM wanavyotoa hoja zao dhidi ya ufisaidi unaona ndani yake kuna dilution fulani!!! Sijui ndio uoga au huwa wanaanzisha hizo hoja kwa maslahi binafsi! Inawezekana huanzisha hoja hizi ili wapate hongo (kizibamdomo) kutoka kwa watuhumiwa (the the blackmailed). Na wengine wanatarajia vyeo! They normally don't come out very clear/completely na hoja, wanabakiza kajitu fulani (proviso) kwa ajili ya kurekebisa hoja yao kukidhi matakwa wakati ukifika!! Si Mwakyembe wala Mama Malechela! Hawa ni wavuguvugu (si baridi wala moto), tuwasahau tuendelee na mapambano ya kuikomboa nchi yetu!!!!
 
Kudeal na mafisadi ni issue na inaitaji moyo ya kujitoa mhanga!
Si unajua wala hela chafu na kuitumia iyo ela ndivyo sivyo ikiwezekana ata kukuangamiza ni suala la kawaida.
 
Hawa wabunge wa CCM sasa nao wanatuchanganya! Ukifuatilia kwa makini namna wabunge wa CCM wanavyotoa hoja zao dhidi ya ufisaidi unaona ndani yake kuna dilution fulani!!! Sijui ndio uoga au huwa wanaanzisha hizo hoja kwa maslahi binafsi! Inawezekana huanzisha hoja hizi ili wapate hongo (kizibamdomo) kutoka kwa watuhumiwa (the the blackmailed). Na wengine wanatarajia vyeo! They normally don't come out very clear/completely na hoja, wanabakiza kajitu fulani (proviso) kwa ajili ya kurekebisa hoja yao kukidhi matakwa wakati ukifika!! Si Mwakyembe wala Mama Malechela! Hawa ni wavuguvugu (si baridi wala moto), tuwasahau tuendelee na mapambano ya kuikomboa nchi yetu!!!!

Mapambano yenu mnayafanyia wapi na kwa njia gani mkuu??????Tafadhali tueleweshane
 
Mapambano yenu mnayafanyia wapi na kwa njia gani mkuu??????Tafadhali tueleweshane

Pambana hapohapo ulipo kama na wewe ni askari mwenzetu! Kama kila mtanzania atakuwa sincere na kutimiza wajibu wake, it can be done!

Au unataka nikuelewesheje. Nikupe personal details zangu?? Ili ufanyeje au unipe nini? Maana kama unachakuniambia unaweza kuniaambia tu hadharani!
 
Mi nakwambia wabunge wa ccm usiwaamini hata siku moja shida nao wengi ni mafisadi watoto, wanaangali jinsi gani watafisadi kwa hiyo wanawasha moto huku wanapuliza kuuzima. Kwani uoni wakina Mzindakaya? ushangai hoja za Rais wetu kuwa fame kwa hiyo akifisadi eti tusiseme?
 
mh kimaro nina wasiwasi mwingi naye! let me keep my finger crossed! kuna siku nitaeleza hapa jf, time will tell

hata hivyo, he has given us a shout! kama hata wanafiki wenzake wa ccm wakitupa-shout itatusaidia kufika mahali fulani
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom