Mgessa Malongo: Toka DC Bagamoyo hadi RC Arusha kutekeleza azimio la Bagamoyo,Rais asitoke Kaskazini

Statement yako inaonyesha kwamba Rais hawez kutoka nje ya CCM!!!!!

Na ukifuatilia posts zake humu JF anaonekana anatoka upinzani sasa hebu piga picha uone ni kwa jinsi gani wapinzani wenyewe wasivyojiamini kuwa wanaweza and then wanalaumu CCM inaharibu nchi.

Thread moja yangu kati ya chache nilizoanzisha niliandika sijui nimekosa uvumilivu; nimeogopa ama nimekosa imani? Kati ya hivi vitatu wiwili vimenitokea, kinachonishikilia ni kimoja nacho ni Imani yangu kwa yule aliye na agano na mimi kuwa naya weza yote kwake yeye anitiaye nguvu. Nalolote nitakalo omba sawa sawa na mapenzi yake yeye atanipa. Sijui ni wangapi watabaki kama mimi tuikomboe nchi yetu....

Jehova Nisi you are my Ebenezer!
 
Huyo Shirima ni afadhali ameachwa tena ikiwezekana asipewe uongozi tena hafai na hawezi kuongoza.
Malongo ni mchapakazi ameweza kumaliza vita vya wasonjo na wamasai ngorongoro wakati shirima alishindwa, malongo anakemea vitendo vya kifisadi kwa vitendo na sio kwa mdomo tu kama babu lililochoka shirima.

Wewe inabidi ubaki kwenye BAN, ivi jamani kulikuwa na vita kati ya wasonjo na wamasai? nini maana ya vita na amewezaje kuwamaliza vita akiwa mkuu wa wilaya tena ya Bagamoyo?? NISAIDIENI...
 
wakurugenzi lazma wawe na mikataba na performance zao zipimwe na ikilala azolewe sii hii ya kuwa mkurugenzi kufisadi miradi


Unajua bongo dawa ni katiba mpya itayoweka mambo yote wazi kuanzia appointment za viongozi serikalini watavyochaguliwa na responsibilities zao! Manake kwa mfano huku SA position nyingi serikalini na hata kuwa board member wa shirika you apply for it na kunakuwa interview kali, kama ilivyokuwa recently kwa jaji mkuu, it was live kwenye SABC na karibu three days , alikuwa interviewed na judicial commission na kujibu maswali kuprove how competent he is! Sio huko bongo ubabaishaji tu karibu kila kitu!!
 
Na muelewe kuwa kama....Mnataka kuchagulia watu viingozi ..basi kiongozi atatoka mbeya ,arusha au wote tutamuunga mkono Dr Magufuli...ambaye naye tunajuwa wazi kuwa JK hamtaki...tutampigia kampeni hadi atashinda.....muda wa kuongozwa na wasanii umeisha ...tunataka wachapa kazi....na kwenye hili hatuangalii anatoka wapi...Magufuli for 2015!!! YES!! UGALI MOTO MBOGA MOTO!!!!...............EMBE Project zeeeeee ziiii zii zaidi!!!

Bado una imani na CCM?
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Na muelewe kuwa kama....Mnataka kuchagulia watu viingozi ..basi kiongozi atatoka mbeya ,arusha au wote tutamuunga mkono Dr Magufuli...ambaye naye tunajuwa wazi kuwa JK hamtaki...tutampigia kampeni hadi atashinda.....muda wa kuongozwa na wasanii umeisha ...tunataka wachapa kazi....na kwenye hili hatuangalii anatoka wapi...Magufuli for 2015!!! YES!! UGALI MOTO MBOGA MOTO!!!!...............EMBE Project zeeeeee ziiii zii zaidi!!!

Bado una imani na CCM?

Naomba Mungu hii isiwe imetoka katika vinywa vya viongozi wetu CDM...mmmh how if Its Slaa my God what will I do? Oooh thanks my Lord for u said...amelaaniwa mwanadamu amfanyaye binadamu mwenzake kuwa tumaini lake na huku moyoni amemwacha Mungu...

Na pata picha kwanini wengine katika upinzani wamekuwa na kusita sita moyoni kama holly spirit alivyoni dokeza nami nikaambiwa niwaambie/tahadharishe Mungu akisha toa majibu ni jukumu la mwenye macho ya rohoni kupokea......Wale wawili wa kaskazini nilio wapigia chapuo sometimes in one of my post hapa JF in the last week; milango i wazi lakini hii haina maana kama ninyi hamtanyanyua miguu yenu kuingia nchi ya ahadi/Jumba takatifu basi hiyo milango itawalazimisheni kufanya hivyo....

Wapo akina commoners na wengine wazee wa busara/wapelelezi mliowatanguliza wanawaambieni..ndiyo mji tumeuona una maziwa kweli na asali ipo ngano usiseme lakini bwana kuna mijitu mikubwa kweli na sisi tunaonekana kama panzi tu mbele yao...Ole wenu msipochukua mioyo ya Kaleb na Joshua ambao kwa imani kati ya wote waliokuwa watu wazima wakati huo katika taifa la Israel, wao tu ndo waliiona nchi hiyo ya ahadi....

Mhubirini wenu nimefanya h/w yangu vizuri nimewatafunia lakini kumbuka kumeza kila mtu amepewa nguvu zake hata kama nawapenda vipi sina huo uwezo!
 
Mbona inafahamika kuwa alitumwa kwenda kudhibiti akina James Millya & co , hebu Fikiria , project ndogo kama hiyo inamfanya mtu anakuwa Mkuu wa Mkoa ! Lazima ataboronga tu .
 
Mbona inafahamika kuwa alitumwa kwenda kudhibiti akina James Millya & co , hebu Fikiria , project ndogo kama hiyo inamfanya mtu anakuwa Mkuu wa Mkoa ! Lazima ataboronga tu .
Kazi zote za kijinga alizotumwa toka Bagamoyo atashindwa.
 
Uyu mjamaa wa magogoni muoneni tu amekaa pale anachekacheka ila anasumu mbaya sana moyoni,ni mtu hatari sana...
 
Philemon Mikael ni mtambo wa ukabila, ukanda na udini hilo ni maarufu haoa JF. Uzi huu hauna kichwa wala miguu anajichanganya mno, hoja eti Mulongo kapelekwa Arusha kutekeleza mkakati wa rais hatoki kaskazini. Nimeisoma post yake na kurudia mara kadhaa sijaona hoja yenye mashiko.

Wadau wanauliza mkuu wa mkoa anawezaje kuzuia Rais asitoke kaskazini? kivipi hakuna jibu badala yake Philemon anatoa msururu wa ma RC wastaafu kutoka kaskazini ku back up hoja yake mfu.
 
Aisee kumbe! Nilipata shida sana kuelewa hasira ile yote huyu Bw Mkubwa ilitokana na nini pale nilipomwona anazungumza na wale watoto wa IAA baada ya kuitwa na Lema. Nimekuwa najiuliza ni kitu gani kilimfanya awe na shari kiasi kile, kwamba umeitwa mahali kuna shida, mtu ameuawa, wanafunzi wanataka kuhakikishiwa uhai wao, yeye anafika na kuweka masharti ya kuzungumza. Tena anafika amevaa kibabe, sijui kinini kifuani halafu kakifunika kwa koti.

Huyu alishapewa maagizo - ni nini cha kumalizia, nafasi ilishajitokeza! Kwa kuitwa na Lema ilikamilisha mipango mizima. Isingekuwa Lema amemuita angefanya kama inavyotarajiwa Mkuu wa Mkoa. Kumbe hili ni pandikizi la siku nyingi. Mungu atatulinda waja wake, hatutakufa bali tutabaki wazima tusimulie matendo haya!
 
Mkuu nakuunga mkono, watu wa kaskazini mulongo yupo huko kwa lengo maalumu kuhakikisha hamtoi rais wa awamu ya tano wa Tanzania, msimpe ushirikiano wowote hapo Arusha!!
 
Tatizo liko pale pale,si kwamba hatufahamu,bali hatuchukui hatua.Ni kulalamika then inapita.Ndo maana hata rais wa nchi anasema "ni upepo tu utapita"
 
Jamani kwa ili la wanafunzi wa arusha mkuu wa mkoa hakutumia busara, kwanza swala la mauaji ya mwanachuo ilimpasa atumie busara kuongea na wanafunzi, kimsingi mkuu wa mkoa arusha imemshinda kuongoza, leo tuna rais dhaifu alafu matokeo yake anachagua wasaidizi dhaifu mfano wa mkuu wa mkoa
 
Lile azimio maarufu la Bagamoyo la kuhakikisha Rais hatakaa atoke kasikazini[ref.riz],Azimio hilo lilifikiwa Bagomoyo kwenye mkutano wa CCM ,Mkoa wa Pwani...katika hali inayoonekana wazi ni utekelezaji wa Azimio hilo..Rais alimpandisha ...cheo mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,ndugu Malongo...,na kumfanya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Katika kuonesha wazi kuwa bwana Malongo ameenda Arusha kufanya siasa...jana alisimamia maelekezo ya simu aliyopewa na Rizwan kuhakikisha kuwa ofisi ya umoja wa vijana mkoa wa Arusha inatiwa kufuli...na ilibidi anyanyuke ofisini kwenda kusimamia utekelezaji wa agizo la mwana wa mfalme.....,hasa ukizingatiwa kuwa alikuwa amemuudhi kwa kushindwa kuzuia umoja wa vijana kufungua matawi mkoani mwake..safari hii akaona bora aende mwenyewe kuhakiki.

Sasa wana wa Arusha ..wajiulize ..wana mkuu wa mkoa au kibaraka wa mwana mfalme..na mfalme mwenyewe??? mkoa mkubwa na wenye shughuli nyingi za kiuchumi kama Arusha unapewa mkuu wa mkoa wa kutekeleza mikakati ya kisiasa ya watu au kundi??thats amazing..
Wakati umefika sasa kwa wakazi wa mkoa huu kutafakari upya kama wanahitaji mkuu wa mkoa kama Mgessa Malongo..

Tunaomba wenye CV zake waaze kuzimwaga hapa.......ndio maana kila siku tunasema kuwa vyeo vya DC na RC vifutwe..tunataka mameya wawe na role ya mkuu wa mkoa.....meya atakayechaguliwa na madiwani wa mkoa mzima basi awe MEYA wa mkoa au gavana na dc awe ni meya au mwenyekiti wa halmashauri husika ..watendaji wa kuteuliwa toka kwa rais wabakie hao Wakurugenzi wa maendeleo wa mikoa au wilaya..inatosha ...

Hata uteuzi wa juzi wa wakuu wa mikoa umekuwa na agenda ya siri...kuna wakuu wa mikoa kama Daniel ole Njolay,Shirima na Col Enoc Muphuru wameondolewa tena hata bila ya kuambiwa sababu ...aliyeongelewa ni Hajjat Mrisho wa Pwani ambaye iliongelewa anapewa kazi nyingine......hawa wengine hatujaambiwa...chochote...
Tumeshoshwa na siasa......

SEMENI HAPANA.WAKUU WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA NI MZIGO KWA TAIFA!!!!!!

Ukiangalia jinsi sakata lilivyo kwenda kitaalam, hakuna ubaya LEMA kulisaidia jeshi kwasababu alifika eneo la tukio ns kuzungumza na wanafunzi. Video zilizotolewa zinafaa kwa ushahidi lakini ikumbukwe kuwa haziwezi thibitisha kuwa anachokiongea humo hakuna cha ziada ama imeeditiwa . Kama wakipata ushahidi wa kutosha juu ya uchochezi kwa wanafunzi .... LEMA NINANI ASISHITAKIWE
 
Hoja zidi ya lema kuwa ni mchochezi ni hizi hapa
"Dhambi mbaya na kubwa kuliko zote duniani ni woga" na "Nimepata taarifa kuwa ndani ya dakika 15 Mkuu wa Mkoa atafika, asipofika ndani ya muda huo nitawaongoza kwenda kudai haki yenu ya msingi ya kupatiwa ulinzi."

Hoja nyingine ni "Hawa ndio viongozi wetu, tunaowategemea wanakuja kwenye matatizo wakijivuta utafikiri wanakwenda kwenye send-off."






 
Back
Top Bottom