Mgessa Malongo: Toka DC Bagamoyo hadi RC Arusha kutekeleza azimio la Bagamoyo,Rais asitoke Kaskazini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgessa Malongo: Toka DC Bagamoyo hadi RC Arusha kutekeleza azimio la Bagamoyo,Rais asitoke Kaskazini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Phillemon Mikael, Oct 18, 2011.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  Lile azimio maarufu la Bagamoyo la kuhakikisha Rais hatakaa atoke kasikazini[ref.riz],Azimio hilo lilifikiwa Bagomoyo kwenye mkutano wa CCM ,Mkoa wa Pwani...katika hali inayoonekana wazi ni utekelezaji wa Azimio hilo..Rais alimpandisha ...cheo mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,ndugu Malongo...,na kumfanya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

  Katika kuonesha wazi kuwa bwana Malongo ameenda Arusha kufanya siasa...jana alisimamia maelekezo ya simu aliyopewa na Rizwan kuhakikisha kuwa ofisi ya umoja wa vijana mkoa wa Arusha inatiwa kufuli...na ilibidi anyanyuke ofisini kwenda kusimamia utekelezaji wa agizo la mwana wa mfalme.....,hasa ukizingatiwa kuwa alikuwa amemuudhi kwa kushindwa kuzuia umoja wa vijana kufungua matawi mkoani mwake..safari hii akaona bora aende mwenyewe kuhakiki.

  Sasa wana wa Arusha ..wajiulize ..wana mkuu wa mkoa au kibaraka wa mwana mfalme..na mfalme mwenyewe??? mkoa mkubwa na wenye shughuli nyingi za kiuchumi kama Arusha unapewa mkuu wa mkoa wa kutekeleza mikakati ya kisiasa ya watu au kundi??thats amazing..
  Wakati umefika sasa kwa wakazi wa mkoa huu kutafakari upya kama wanahitaji mkuu wa mkoa kama Mgessa Malongo..

  Tunaomba wenye CV zake waaze kuzimwaga hapa.......ndio maana kila siku tunasema kuwa vyeo vya DC na RC vifutwe..tunataka mameya wawe na role ya mkuu wa mkoa.....meya atakayechaguliwa na madiwani wa mkoa mzima basi awe MEYA wa mkoa au gavana na dc awe ni meya au mwenyekiti wa halmashauri husika ..watendaji wa kuteuliwa toka kwa rais wabakie hao Wakurugenzi wa maendeleo wa mikoa au wilaya..inatosha ...

  Hata uteuzi wa juzi wa wakuu wa mikoa umekuwa na agenda ya siri...kuna wakuu wa mikoa kama Daniel ole Njolay,Shirima na Col Enoc Muphuru wameondolewa tena hata bila ya kuambiwa sababu ...aliyeongelewa ni Hajjat Mrisho wa Pwani ambaye iliongelewa anapewa kazi nyingine......hawa wengine hatujaambiwa...chochote...
  Tumeshoshwa na siasa......

  SEMENI HAPANA.WAKUU WA MIKOA NA WAKUU WA WILAYA NI MZIGO KWA TAIFA!!!!!!
   
 2. Ungana

  Ungana JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 358
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Okaaaaaaaaaaaaaaaaay,naelekea kuelewa jambo hapa!
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako Phillemon Mikael.

  Sioni faida ya hiki cheo cha mkuu wa mkoa katiba mpya inatakiwa iondoe hivi vyeo vya kigavana tungependa kuona katiba inayotoa nafasi za uongozi through sanduku la kura si kuteuana kama ilivyosasa.
   
 4. m

  mharakati JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hizi ni siasa za kawaida hamna la ajabu hapa typical politiking ya Africa, Riz hamtaki EL na habari ndiyo hiyo
   
 5. K

  Kamura JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hakuna DC wala RC mwenye jina hilo. Huyo unayemwita Mgesa Malongo anazuiaje Rais asitoke Kaskazini?
   
 6. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Huyo Shirima ni afadhali ameachwa tena ikiwezekana asipewe uongozi tena hafai na hawezi kuongoza.
  Malongo ni mchapakazi ameweza kumaliza vita vya wasonjo na wamasai ngorongoro wakati shirima alishindwa, malongo anakemea vitendo vya kifisadi kwa vitendo na sio kwa mdomo tu kama babu lililochoka shirima.
   
 7. F

  FJM JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Miaka 50 imetupa experience ya kutosha kuhusu hivi vyeo vya mezani. Katiba mpya ifute kabisa cheo cha mkuu wa Mkoa na wilaya. Wawepo Mayor na madiwani. Na watu wote hawa wapatikane kwa sanduku la kura. Kama tunataka kujenga mfumo wa uwajibikaji ni lazima viongozi wote watokane na ridhaa ya wananchi, full-stop.

  Wakurugenzi wata-apply na kufanyiwa interviews na wawe na mikataba ya kazi. You do not perform unakwenda na maji. Rais atateua baraza la mawaziri tu, hata hivyo idadi ya wizara itajwe kwenye katiba na sio haya mambo ya kuwa na wizara ya zisizokuwa na kichwa wala miguu. Tunataka wizara no more than 15.
   
 8. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Huyu Malongo alipata kuwa Meneja wa Bendi ya Vijana Jazz wan Pamabamoto na baa ya Mango Garden.....
   
 9. M

  Marytina JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wakurugenzi lazma wawe na mikataba na performance zao zipimwe na ikilala azolewe sii hii ya kuwa mkurugenzi kufisadi miradi
   
 10. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #10
  Oct 18, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,002
  Likes Received: 736
  Trophy Points: 280
  Siasa za kiafrika za kutupiana vyeo.
   
 11. K

  Kamura JF-Expert Member

  #11
  Oct 18, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 488
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  So What?
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Oct 18, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  by the way, Kaskazini (Arusha) who is that clean to be a president?
   
 13. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Anaitwa magesa mulongo,elimu yake ni advance diploma ya uhasibu kabla ya kuwa mkuu wa wilaya alikuwa anafanya kazi TTCL-Bukoba mjini kama muhasibu.Ni marafiki sana na mkuu wa kaya na kipindi Jk anagombea uraisi alikuwa amekwisha jitabilia kwamba atakuwa mkuu wa wilaya na kweli hayawi ayawi yakatimi akateuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Bukombe na aliamishiwa Bagamoyo baada ya mkuu wa wilaya ya Bukoba mjini kuwachapa waalim viboko.Kiukweli jamaa ajasota sana yaani kaudumia cheo cha Udc kwa miaka 5 tu na sasa ni mkuu wa mkoa.
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  Magessa Mulongo S.

  Wewe Tu ndio hujaelewa ,kwa vigezo vyako...wenzako wote wameshaelewa..\\\\\\\\\\\\\\\//?

  kanyaga twende...tu..,wewe kalagha bagho!!...

  swali ulilojiuliza ..jibu unalo...yeye alitumwa kwenda kufunga ofisi za umoja wa vijana au kufanya kazi za serikali.....mambo ya ccm awaachie mzee Onesmo oLE nangole ..na mary chitanda au hawaamini???

  Ndio maana in short tunasema vyeo vya kupeana hatutaki tena kwenye karne hii ya 21..Nyerere aliviweka hivi vyeo miaka hiyo kwa kuwa alikuwa na wasomi wachache ..ambao ilibidi awasambaze kote ...,na pia kwa sababu za kitaifa..ambazo kwa sasa sio tishio tena.....viongozi wapatikane kwa kura....na naunga mkono kuwa nafasi za wakurugenzi zitangazwe ..baada ya hapo ziwe vetted .....wanaobakia wawe interviwed kwenye public hearing[kenya wameanza utaratibu wa kufanya interview za wazi ..tena live kwenye televisheni].....anaepatikana apewe mkataba...kalasi!!
   
 15. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #15
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,458
  Likes Received: 5,845
  Trophy Points: 280
  Somebody wanted his CV.....THAT'S WHAT IT IS!
   
 16. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #16
  Oct 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280
  ....Yeah hajasota kama mtu kama Ebrahim Msengi amekuwa mkuu wa wilaya miaka zaidi ya 10 sasa...wakati mtu kama Fatma Mwasa ..[kapu la mama]...ametoka WAMA mwaka juzi tu kazuga pale Kilombero or something like that kwa muda ...then huyooo Tabora........yaani hivi vyeo ni bure kabisa.......sasa utajiuliza alifanya nini cha kutukuka hadi ndani ya miaka 3 ikamtosha Rais kumpa mkuu wa mkoa Tabora......
   
 17. naninibaraka

  naninibaraka JF-Expert Member

  #17
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 656
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  huyu bwana katolewa bagamoyo na kupewa cheo cha ukuu wa mkoa kwa kazi maalumu hapa Arusha,kaja kwa mbwembwe nyingi sana mpaka akatoa number za simu zake za mkononi,tunachoweza mwambia sisi wakazi wa arusha ni kuwa afanye kazi iliyomleta hapa arusha hakutumwa kuja kufanya siasa na kufunga ofis za uv-CCm hapa na kama anatekeleza maagizo ya Riz1 na baba yake JK ajue wazi Arusha itamshinda huku si bagamoyo,Wanachi wa mkoa wa arusha hatutaki kuburuzwa kama vp JK akurudishe ukaongoze mkoa wa pwani si Arusha,hatuitaji unafiki wa umangimeza au ndiyo mzee hapa Arusha vinginevyo chapa mwendo,tumeona Jk jinsi anavyotumia watu kama Nape na wengine kuchafua watu na wewe tunaona unaingia kwenye huo mkenge...
   
 18. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #18
  Oct 18, 2011
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  1. huyo Malongo ana nguvu gani ya kuzuia Rais? si dhani kama hoja yako ina nguvu hivyo unless unamfaham mtu fulani (Lowa.asa) na umeelekeza hoja yako huko. kaskazin ni kubwa ungetoa profile yote kuanzia Kilimanjaro nk.

  2. Meya anaongoza Jiji sio mkoa na pia anachaguliwa na madiwani wa pale tu sio wa mkoa mzima (hivyo tofautisha). pia ujue Meya ni diwani wa kata fulani. labda upendekeza kuwa Mkuu wa mkoa achaguliwe.

  3. hao akina Shirima, Tarimo na wengine wamestaafu (rejea maelezo ya awali), wale ambao hawajastaafu wameambiwa watapewa kazi nyiingine
  nawasilisha
   
 19. o

  oldonyo JF-Expert Member

  #19
  Oct 18, 2011
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 554
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mkuu!raisi mwenyewe aliwahi toa kauli bungeni kwamba nanukuu"kama unataka kula sharti uliwe kwanza ndo uje ule"sasa kauli kama hii inakupeleka wapi?kwaiyo usishangae ivyo ni vitu vya kawaida tu kwa vasco.
   
 20. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #20
  Oct 18, 2011
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  hapa mie mgeni natafuta wenyeji.
   
Loading...