Mgeni Rasmi Kuwa Rastom Azizi

Mhache

JF-Expert Member
Jun 20, 2008
345
24
"Ni fedheha kwa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kumruhusu mtu anayetuhumiwa kwa ufisadi kutumia miibara takatifu kujisafisha", hiyo ni kauli ya viongozi wa kanisa waliyoitoa jana katika mkutano wao wa kujadili suala hilo.

Maswali la kujiuliza ni nani alimwalika Rastom kuwa mgeni rasmi katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Kinondoni? Na je makao makuu ya kanisa KKKT hawakuwa na taarifa kuwepo kwa shughuli hiyo?

Ndugu Rastom Azizi alialikwa na Usharika wa kanisa la Kinondoni kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa Albam ya Kwaya ya Amkeni. Katika uzinduzi huo Mheshimiwa huyo aliahidi kutoa shilingi millioni tano taslim na milioni mbili kwa ununuzi wa vifaa vya kwaya hiyo.

Ninawiwa kusema kwamba KKKT inabidi kulitolea kauli suala hilo na kuwa na utaratibu wa kuwaalika watu walio safi katika uzinduzi wa shughuli nyeti kama hizo. Kanisa ni mahali patakatifu panapohitaji uchaji wa hali si kualika mtu hata anahisiwa kuwa na kosa fulani. Tumwombe Mungu atuongoze katika kutenda na kutoa maamuzi. Maji yakimwagika ni nini chakufanya.
 
Nafikiri ndugu Rostam kama walivyo watu wengine waliokwisha kutuhumiwa katika sakata la ufisadi na mengineyo anayo nafasi yake bado katika masuala ya kijamii.Ni haki kwake kuingia na kualikwa popote pale.

Nafikiri suala la msingi hapa siyo nani kamwalika kanisani na kwanini amealikwa.Kanisa halipaswi kumnyooshea mtu kidole kama halina ushahidi wa kutosha wa kile anachotuhumiwa kwacho.KKKT kwa mtizamo wangu wamejikuta katika kundi moja kubwa ambamo watanzania wengi tumo.Ni kundi lililotengwa na ukweli kumhusu Rostam.Kama serikali na vyombo husika ikiwemo tume ya rais ya kufuatilia suala la EPA vingekuwa wazi tungeshajua kwa hakika kama Rostam anasingiziwa au la.Nadhani katika mazingira ya sasa KKKT(huhusani Usharika wa Kinondoni) wamo gizani kama tulivyo wengi wetu kuhusu Rostam.

Hata hivyo bado naona kuna haja ya taasisi hasa za kiroho kuwa na msimamo thabiti kwenye masuala yanayogusa ustawi wa nchi kama hili la ufisadi.Kama kuna mtu anatuhumiwa Kanisa linapaswa kuibana serikali na vyombo vyake kutokukaa kimya.Huko ndiko kulisaidia taifa na watu binafsi.Kama kanisa lingekuwa limechukua hatua kama hiyo ni wazi mtu kama Rostam angejiuliza mara mbilimbili kabla ya kukubali mwaliko wa kanisa.
 
Back
Top Bottom