Mgeja: Wapinzani ni kama kikombe cha Babu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgeja: Wapinzani ni kama kikombe cha Babu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 23, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Shinyanga, kimesema kelele zinazopigwa na wapinzani katika majukwaa, kwa lengo la kukikashifu na kukichafua chama hicho, ni sawa na dawa ya Kikombe cha Babu wa Loliondo.

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja, aliyasema hayo juzi katika uzinduzi wa kampeni za udiwani wa Kata ya Bungarama, wilayani hapa. Uchaguzi huo unafanyika baada aliyekuwa diwani wa kata hiyo kufariki dunia.

  Alisema kuwa, anavifananisha vyama hivyo na dawa ya Babu wa Loliondo, kutokana na watu wengi kuacha kwenda hospitali kupata matibabu na hivyo kukimbilia kwa babu huyo.

  “Dawa ya Babu iliwavuta wengi bila ya kujali kuwa kulikuwa na sehemu nyingine ya kupata matibabu, ikiwamo hospitalini. Tukio hilo ni sawa na wanaohama Chama Cha Mapinduzi na kukimbilia upinzani, wakidhani huko watapata nafuu.

  “Chama Cha Mapinduzi kwa sasa, ndio chenye dola, kwa hiyo, chuki na kashifa zinazotolewa na vyama vingine juu ya CCM, bado haziwezi kumbadilisha mwananchi kwenda katika upande wa pili.

  “Watanzania bado wana imani na chama chao ambacho ndio kimewatoa mbali, kwa hiyo, wana CCM lazima tushikamane kwa kuacha tofauti zetu,” alisema Mgeja.

  Kwa mujibu wa Mgeja, siyo kila mwanachi anayehamia chama cha upinzani, matatizo yake yatakwisha kwa kuwa vyama hivyo vimekuwa vikihubiri habari za chuki na kauli za kashfa katika majukwaa.

  “Nawaambia siyo kila mtu anayehamia katika chama cha upinzani, matatizo yake yatakwisha, CCM ndiyo chama kilicho madarakani na ndiyo tumaini pekee la Watanzania,” alisema.

  Katika mkutano huo, watu 83 ambao ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) walirudisha kazi akiwamo ya Katibu wa Kijiji cha Buyange ulipofanyika mkutano huo.

  Uchaguzi huo unatarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, kutokana na diwani wa kata hiyo kupitia CCM, Peter Kisiminza, kuuawa na watu wasiojulikana.
   
 2. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  You can fool all the people some of the time, and some of the people all the time, but you cannot fool all the people all the time.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Oct 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Pumba za akina mgeja ndo zinaizika ccm................................hao wanachadema 83 wa kutengenezwa, na kadi za kutengenezwa tulishawazoea.

  Onyo kwa CHADEMA:
  Tabia ya kugawa kadi bila utaratibu kwa kila mtu mwenye hela za kununua kadi zinawarahisishia mafisadi wa CCM kupata mwanya wa kuzinunua, na kuzigawa kwa wanaccm kwa kuwahadaa watanzania kwenye mikutano, kana kwamba ni wanachadema ndo wanarudisha kadi.

  Tuwe makini na ugawaji wa kadi ndugu zangu. kuwe na utaratibu unaoeleweka kuhakikisha kama ni kugawa kadi ijulikane kata fulani imegawiwa kadi ngapi, na kadi ngapi zimebaki and so on.
   
Loading...