Mgeja, tumechoka siasa zako za maji taka, lini utaachana na Sitta? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgeja, tumechoka siasa zako za maji taka, lini utaachana na Sitta?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHOST RYDER, Jul 25, 2011.

 1. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mgeja Tumechoka Siasa zako za Maji Taka, Lini Utaachana na Sitta?

  Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga unaonyesha kwa jinsi gani upo kwa masilahi ya kundi fulani kutokana na kuendelea kushabikia siasa zako za maji taka.

  Katika muda huu ambao taifa linahangaika kusaka ufumbuzi wa masuala nyeti na muhimu kama umeme tungefurahi sana kama ungefunga domo kwa sasa na kuacha focus ya watanzania na wapiganaji kuendelea kushinikiza katika mipango ya maendeleo.

  Kila wakati anapoibuka SamwelSitta kuikosoa serikali wewe ndo unajifanya kuwa ngao namba moja ya kutaka kuinusuru serikali na kwa kupitia magazeti yanayowaunga mkono umekuwa ukipewa coverage kubwa kuliko hata hoja muhimu za Kitaifa.

  Nakumbuka wakati Sitta anashutumiwa kwa kuwapa wapinzani nafasi ya kutoa hoja binafsi na kuruhusu mijadala Bungeni inayoikosoa serikali na kuhoji mikataba mibovu ulisimama mstari wa mbele kuomba Mkutano mkuu wa CCM umuengue Sitta katika nafasi hiyo na kumvua kabisa uanachama wa CCM.

  Kwa kuwa hoja zako hazikuwa na Mashiko uliangukia pua, haikuishia hapo wakati wa mbio za kuwania kiti cha uspika ukaibuka tena na kutowaona wagombea wengine wote wa nafasi hiyo na badala yake ukaelekeza karata zako kwa Sitta na kwa bahati nzuri ama mbaya mkafanikiwa kumuondoka katika kiti hicho licha ya kuwa mkamrudishia wadhifa mwingine kupitia mlango wa uani.

  Sasa umeibuka tena na hili la kumuita mnafiki, baada tu ya kuipinga serikali kuhusu mpango usiotekelezeka wa kumaliza tatizo la Mgao wa Umeme Nchini.

  Siiandiki haya kumtetea Samwel Sitta hata Kidogo kwani sina nasaba nae wala hanijui na sihitaji anijue, ila tunakereka na siasa hizi za maji taka ambazo zina lengo la kupoteza Hoja ya msingi kwa kutuelekeza katika kumjadili Sitta na kusahau burning issues kwa sasa kama ulivyo uzozo katika wizara ya Nishati na Madini na Watendaji wake.

  Sijui ni kiasi gani unalipwa kutekeleza propaganda hizi ila Nadhani hebu acha ushabiki huu wa ujira mdogo unaopewa na kutaka kuchanganya mawazo ya watanzania kwa kuleta hoja ambazo zinatupeleka katika matatizo zaidi kuliko kupata ufumbuzi.

  Sijawahi kukusikia ukizungumzia suala lolote muhimu la kitaifa hata katika Mkoa wako kama Mwenyekiti zaidi ya kutumiwa kummaliza Sitta Kisiasa, Una Agenda gani kwa Umma wa Watanzania?

  Dhambi hii itakufuata maisha yako yote usipojirekebisha

  ADIOS
   
 2. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #2
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Nimefurahishwa na utaratibu huu wa MODS kwanza kuikagua thread kbla ya kuipost, sasa sijui ni kwa G.R pekee au wanaJF wote. kama ndivyo basi itajenga discpline na kucontroll utitiri wa thread hasa kwa wajanja ambao hawapendi kutafuta Hoja za msingi zaidi ya kupindua thread za wachangiaji wengine na kuandika mpya.

  Mfano mzuri ni hoja kutoka Bungeni na Siku alipovua Gamba ndugu R.A.

  bravo MODS
   
 3. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Wenyewe kwa wenyewe.
   
 4. n

  ndaru Member

  #4
  Jul 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hoja ya msingi ambayo tunapaswa kuizungumzia ni kwa baadhi ya viongozi ambao ni sehemu ya serikali kuisema serikali hadharani kwa kuwa maamuzi yao huyafanya pamoja na kama kusemana kuna utaratibu wao wa vikao kama viongozi wa kufanya hivyo sasa hii tabia ya akina sita kuisema serikali iliyoko madarakani wakani yeye ni kiongozi katika serikali hiyo haingii akilini.

  Nchi hii kama kila mtu ataamka na na kufanya anachotaka na hasa akiwa kiongozi hatuwezi kufika hivyo hawa wote wanaomkosoa sita na wenzake wana hoja ya msingi,
   
 5. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #5
  Jul 25, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Umejuaje na wewe?
   
 6. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Wenyewe kwa wenyewe + Wenyewe kwa wenywe x Washabiki watanzania wote = kupoteza Hoja za Msingi
   
 7. zululima

  zululima Member

  #7
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 22, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vita vya CCM na CCJ. Wao wanajuana.
   
 8. L

  Luiz JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 342
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huon wanavojibzana?
   
 9. F

  FUSO JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  ndugu wakigombana wewe chukua jembe ukalime.
   
 10. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #10
  Jul 25, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  unapoona m2 unamwambia ukweli ndani lakn akaungana na wajnga wenzie kukukaripia ww ni afadhali ukautoa huo ujinga wanaoushikilia mbele za wa2 ili 2jue nani mjinga.siyo kwamba cta huwa hasemi kwene vikao vyao bali coz of vichwa ngumu na maslahi binafsi ya wakuu we2 ndo maana anaamua kuwalipua hadharani.kiongozi mwenye matakwa ya wengi utamjua 2! Cjackia cta akiongea nje ya vikao ki2 ambacho hakina masilahi ya umma.anakereka na wahuni wanaoshindwa kutekeleza matakwa ya wengi na uwezo upo- God bless u cta.
   
 11. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #11
  Jul 25, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Tatizo ni kukurupuka kwa Viongozi wetu, Sitta alijitia doa kubwa sana na kauli yake ya kujikosha kwa kuwaita wapinzani ni wanafiki na wana hoja za hivyo hivyo tu. Hii ilimpotezea thamani kwa kiasi kikubwa na kuzua maswali mengi juu ya uadilifu wa mzee huyu aliyeaminiwa na wengi katika umma wa watanzania.
   
 12. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #12
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Huyu Mgeja namfahamu vizuri,ni mla rushwa mzuri a.k.a mpenda vya bure.Amekuwa akiishi kupitia ujira wa mwiha kutoka baadhi ya taasisi za Serikali pale Shy bila hata aibu.Anaweza kuvuta sehemu mbili hadi tatu kwa mara moja akidai kuchangia chama mafuta.

  Anapenda kufikia sana Shinyanga Motel anapokuwa akitokea kwake Kahama.Sishangai akiwa mstari wa mbele kutetea mafisadi kwani hata shule ndogo ya kufikiri hana hivyo mbele kwake giza totoro anaona siku zimeganda.
   
 13. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #13
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Kaka hiyo ndio furaha yetu Mkuu wewe unalalamika nini tena, hao ni CCM-Mtandao na CCM-CCJ wananyukana unajuwa Mwenyekiti hana nguvu sasa hivi kwahiyo hayo makundi mawili sasa hivi ni mwaga ugali mi na mwaga mboga sisi ambao tupo pembeni yetu macho
   
 14. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #14
  Jul 25, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Vita vya panzi' teh teh teh teh.
   
 15. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Jamaa ni mwanasiasa Muflisi sana, anafahamu majungu na kushabikia ujinga kwa lengo la kufunika Hoja ya Msingi. Leo tunazungumza haya ni muda mfupi wasimamizi wa TANESCO wanathibitisha si si nyingi kutoka sasa watazima mitambo kutokana na Maji kuelekea chini ya Kiwango.

  Mgeja yeye anaona Sitta katenda dhambi huu ni unafiki wa kisiasa uliopitiliza
   
 16. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Huyu mgeja ametokea wapi wakuu?? Dataz plz!
   
 17. N

  Nyampedawa Member

  #17
  Jul 26, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nakubaliana na wewe mkuu
   
 18. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Wewe punguani nini,S6 anaweza kuikosoa Serikali ambayo yeye ni mmoja wao? Kama ni Bajeti mbovu ya Wizara ya Nishati na Madini alitakiwa kuikosoa katika vikao vya Baraza la Mawaziri na sio maqjukwani. Huyo ni mbabaishaji anataka kutu babaisha kama alivyotubabaisha wakati wa CCJ
   
Loading...