Mgeja, Sitta wadaiwa kuivuruga CCM . wasaliti

sir.JAPHET

JF-Expert Member
May 18, 2012
699
133
Alhamisi, Septemba 06, 2012 06:21 Na Mwandishi Wetu, Mwanza
TUHUMA za usaliti ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willbrod Slaa dhidi ya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, kisha kuungwa mkono na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, zinadaiwa kuanza kukivuruga chama tawala.

Mvurugano huo umekuja siku chache baada ya Mgeja kujitokeza hadharani kumpongeza, Dk. Slaa, kwa madai ameisaidia CCM kutokana na kuweka wazi tuhuma za usaliti wa Sitta anayedaiwa kutaka kujiunga na CHADEMA kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 na kisha kuasisi Chama Cha Jamii (CCJ).

Imeelezwa baadhi ya makada wa CCM wanaonekana kuchukizwa na kauli ya Mgeja ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), juu ya kumpongeza Dk. Slaa kumwanika Sitta.

Imeelezwa kitendo cha Mgeja kujitoa mhanga kuunga mkono kauli ya Dk. Slaa dhidi ya Sitta ambaye pia ni mjumbe wa NEC, kimetajwa kuwa ni cha ujasiri, uwazi, kutoogopa mtu wala si cha kinafiki ndani ya chama.

Mmoja wa makada wa CCM mkoani Mwanza na aliyewahi kuwa Meneja Kampeni wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, James Mbatina, alisema jana kuwa, CCM ya sasa haihitaji kuwa na wanachama wanafiki, waongo na wanaoshabikia usaliti ndani ya chama hicho.

Alisema siku chache baada ya Mgeja kumuunga mkono na kumpongeza Dk. Slaa kwa kufichua ‘madhambi’ ya Sitta, limeibuka kundi la watu wachache, alilodai linatumiwa kuanza kumtuhumu kutokana na kauli yake aliyoitoa katika vyombo vya habari akipendekeza kiongozi huyo atoswe ndani ya chama, kutokana na tuhuma za kukisaliti chama tawala.

“Nikiwa kada wa CCM sioni sababu ya kupiga makofi hata pasipostahili kupigiwa makofi ndani ya chama. Huwezi kumpigia makofi msaliti au mnafiki yeyote mwenye malengo ya kutaka kukigharimu chama changu.

“Mtu yeyote nitampongeza pale anapojitenga na unafiki. Mimi namuunga mkono na kumpongeza Mgeja kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa ndani na nje ya chama changu cha CCM. Lakini wapo wanaochukizwa na msimamo na uwazi kama huu wa Mgeja na Dk. Slaa,” alisema Mbatina.

Aidha, MTANZANIA limeelezwa wapo baadhi ya wana CCM wanaodaiwa kutumiwa na kigogo mmoja anayetajwa kutaka kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Watu hao wanadaiwa kuanzisha harakati za kutaka kuupotosha umma wa Watanzania, kuhusiana na tuhuma nzito zinazoelekezwa kwa wafuasi waliopo katika mlengo wa kigogo huyo.

Kwa upande wake, Francis Paskari, ambaye ni kada maarufu ndani ya CCM Kanda ya Ziwa, alisema haoni haja ya kupingana na kile alichokiita ukweli wa mambo, uliotolewa na Dk. Slaa dhidi ya Sitta na wakati umefika sasa kwa wanachama na viongozi wakubali kukosolewa na kupongeza pale wakosoaji wanapowanyooshea mkono.

“CCM tuondokane na dhana ya ubishi wa kila jambo na hata pale tunapokosolewa na wapinzani. Naamini mtu anayekukosoa anakujenga, hivyo kauli ya Mgeja kumpongeza Dk. Slaa, binafsi naiunga mkono. Inafaa maana si kauli ya woga wala unafiki hiyo ni kauli ya uwazi na ukweli wa mambo.

“Kukijenga chama chenye mtazamo mpya na mzuri kwa jamii ya Kitanzania, viongozi wa CCM wanapaswa wawashughulikie kikamilifu watu wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi, usaliti ndani ya chama pamoja na kuhujumu mikakati ya Serikali. Maana Serikali ni yetu moja sote, tena ya chama chetu tawala".

Hivi karibuni, Sitta alimjibu Dk. Slaa kuhusiana na tuhuma alizozitoa dhidi yake ambapo alisema, yeye hakuomba kujiunga CHADEMA bali chama hicho kilimuomba yeye ajiunge nacho lakini akawakatalia.


[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]
 
Kuhusu Mgeja inawezekana wanamsingizia kwa kuweka ukweli wake hadharani. Lakini Mh. Sitta ni mmoja kati ya maadui wakubwa wa Tanzania, na si CCM pekeyake. Kwakujihabarisha zaidi, fuata link hii: Slaa: Sitta ni Mnafiki - YouTube
 
Back
Top Bottom