Mgeja , Makamba wamaliza 'bifu' lao

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Wakati Rais John Magufuli akitangaza msamaha kwa baadhi ya viongozi waliomkosea, mwanasiasa Khamis Mgeja ambaye kwa miaka minne alikuwa hasalimiani na katibu mkuu mstaafu wa CCM, mzee Yusuf Makamba, amemuangukia na kumaliza uhasama.



Juzi, Mgeja alikwenda nyumbani kwa mzee Makamba Kisanga Tegeta jijini hapa na mahasimu hao kukutana uso kwa uso baada ya takriban miaka minne kupita.
Viongozi hao inadaiwa uhasama wao ulitokana na mbio za urais mwaka 2019, wakati mzee Makamba akimuunga mkono mtoto wake, Januari huku Mgeja alimuunga mkono Edward Lowassa.



Baada ya kukutana juzi, walikumbatiana na kuondoa tofauti zao baada ya mzee Makamba kumualika Mgeja nyumbani kwake ili waondoe tofauti. Walitumia muda huo kusoma dua maalumu.



Akizungumza baada ya dua, Mgeja alisema kilicho wasukuma kuondoa tofauti zao ni maadili na misingi ya dini, kwani zinasisitiza kusameheana na siasa iliwafikisha sehemu mbaya.




Naye mzee Makamba alimpongeza mwenzake akiwa katibu mkuu wa CCM na Mgeja akiwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, walikuwa marafiki sana lakini shetani aliingilia kati.



Aliitaka jamii izidishe upendo na kujenga utamaduni wa kusameheana kama walivyofanya. “Waondoe tofauti na huko mbinguni siasa wataaziacha duniani kila mmoja na amalize uhasama tujitahidi kufanya mema na kuzidisha upendo baina yetu,” alisema mzee Makamba.



Baada ya hapo, mzee Makamba alimtembeza Mgeja shambani kuangalia ufugaji wa ng’ombe wa maziwa, kuku, bata na sungura.



Mgeja alimpongeza mzee Makamba kwa ufugaji wa kisasa wa kitaalamu na wenye tija na kwamba, amejifunza anakwenda kuanzisha ufugaji.
 
Nawapongeza Wazee wetu kwa kusameheana. Ni Jambo la heri Sana hili.

Ila wangefanya kimya kimya

Mzee Meko akisikia hili lazima atahamishiwa India.
 
Wote wamekatwa mikia.....Afu Jiwe anawalia taiming......Bora wasameheane tu
 
Back
Top Bottom