Mgeja awausia wanasiasa, awataka wamuunge mkono Rais Magufuli kwa vitendo!

SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
390
385
WANASIASA nchini wameshauriwa kuitekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya "Hapa kazi tu" iliyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa wao kufanya kazi badala ya kukaa wakiihubiri majukwaani ili watu wengine waitekeleze.

Ushauri huo umetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kijiji cha Nyanende kata ya Kilago wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mgeja ambaye alizungumza na waandishi wa habari akiwa anavuna mpunga katika shamba lake lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 300 ambapo kwa msimu huu amelima ekari 20 alisema imefika wakati wanasiasa wamuunge mkono Rais Dkt. Magufuli kwa kufanya kazi badala ya kuinadi kauli mbiu yake majukwaani.

Alisema yeye binafsi baada ya kupumzika masuala ya siasa hivi sasa amejikita katika shughuli za kilimo ikiwa ni katika kuunga mkono kwa vitendo wito wa Rais Magufuli wa kuwataka watanzania kufanya kazi badala ya kuendeleza masuala ya kisiasa kipindi chote.

Akifafanua alisema kilimo ni uti wa mgongo kwa uchumi wa Tanzania na kwamba ili kuweza kuwa na viwanda vinavyozalisha kwa wingi lazima vipate malighafi za kutosha ambazo nyingi zinatokana na mazao ya kilimo.

“Binafsi naipongeza sana serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kuweka msukumo katika suala zima la kilimo, ufugaji na hata uvuvi, niwaombe watanzania tushirikiane na serikali katika msukumo huu kwa kuhakikisha tunajikita katika shughuli za ujenzi wa nchi yetu ikiwemo kuwekeza katika kilimo,”

“Ukweli watanzania hatuna sababu ya kwenda kuhangaika katika nchi nyingine mfano China, Dubai au kwingineko wakati Tanzania tumejaliwa kuwa na ardhi ya kutosha, hii ardhi yetu ni dhahabu nyeusi, tuna mabonde na mito ya kutosha tuyatumie kwa kuleta mapinduzi ya kilimo, naamini Tanzania tutafika mbali,” alieleza Mgeja.

Aliendelea kueleza kuwa kilimo kina faida kubwa iwapo mtu ataamua kuwekeza kwa dhati na ni uti wa mgongo wa uchumi wa taifa la Tanzania ambapo hata hayati baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika maisha yake muda mwingi baada ya kung'atuka alijielekeza katika shughuli za kilimo.

“Tunapofanya hivi tuelewe pia tunamuenzi baba wa Taifa, hayati baba Julius Kambarage Nyerere, na tufahamu siasa siyo maisha pekee, niombe kufafanua kuwa awali niliposema nimepumzika siasa, nilieleweka isivyo, sikuwa na maana ya kuacha siasa, bali nimepumzika, na nilipopumzika matokeo yake ni haya, nimejikita kwenye kilimo,”

“Kwa sasa nimejielekeza kwenye kilimo, ikifika wakati nitafanya tena siasa, niliyokuwa nikiyasema huko nyuma sasa ninayatafsiri kwa vitendo, ukipumzika siasa unajielekeza kwenye shughuli nyingine ikiwemo pia ufugaji wa samaki, ni vizuri watanzania tusikubali kulazwa usingizi na masuala ya kisiasa,” alieleza.

Kwa upande mwingine Mgeja ametoa wito kwa vijana hapa nchini kujikita katika kufanya kazi badala ya kushinda vijiweni wakipiga soga na kucheza pooltable na kwamba vijana wana nafasi kubwa katika ujenzi wa taifa lao na hawapaswi kuchagua kazi.

"Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, wanapokaa vijiweni wakisubiri kazi za kuajiriwa, ni wazi wanachangia katika kuchelewesha kukua kwa uchumi wetu, niwaombe wabadilike sasa wajikite katika shughuli za kilimo, ufugaji na hata uvuvi, ili mradi kila mmoja afanye kazi, asisubiri ajira za maofisini, hazitoshi,"

“Lazima tuelewe kwamba ili kufikia mafanikio ya nchi yetu kuwa ya viwanda vinavyozalisha, ni budi sisi wenyewe tujikite katika kufanya shughuli zitakazosaidia viwanda hivyo vifanye kazi, na mojawapo ya shughuli hizo ni kilimo, tuzalishe mazao kwa wingi, tufuge kisasa na hata kuendesha shughuli za uvuvi,” alieleza Mgeja.

Alisema iwapo watanzania watadhamiria kwa dhati kufanya mapinduzi ya kilimo, ni wazi nchi itapiga hatua haraka katika nyanja ya uchumi kama ilivyotokea katika baadhi ya mataifa mfano wa Thailand na Malaysia na kwamba ili kuifikia Tanzania ya viwanda na yenye uchumi wa kati lazima watanzania wafanye kazi.

IMG-20190624-WA0042.jpeg
IMG-20190624-WA0039.jpeg
IMG-20190624-WA0037.jpeg
 
Hiyo ardhi ameipataje ?
Ana miliki hekari 300 na amelima ekari 20 bila shaka hizo zilizo baki iwe mali wa umma maana ameshindwa kuziendeleza. Wana Kahama basi chukue hatua mgawane hizo hekari 280 zilizo baki
 
Usimlaumu Spika hata yeye ni mwanamichezo ana haki ya kusema kile anachoamini,Mbona wewe pia umesema unachoamini na amekupinga?Tatizo watanzania mnaongea sana Timu ya Taifa imechelewa kuanza mazoezi mkawa mnasema kwenda ulaya kuweka kambi sio Muhimu leo yamewakuta mkiambiwa eti Spika kakosea.Haya huyu makonda anaenda kufanya maajabu gani?
 
WANASIASA nchini wameshauriwa kuitekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya "Hapa kazi tu" iliyotolewa na Rais Dkt. John Magufuli kwa wao kufanya kazi badala ya kukaa wakiihubiri majukwaani ili watu wengine waitekeleze.

Ushauri huo umetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Shinyanga, Khamis Mgeja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika kijiji cha Nyanende kata ya Kilago wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mgeja ambaye alizungumza na waandishi wa habari akiwa anavuna mpunga katika shamba lake lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 300 ambapo kwa msimu huu amelima ekari 20 alisema imefika wakati wanasiasa wamuunge mkono Rais Dkt. Magufuli kwa kufanya kazi badala ya kuinadi kauli mbiu yake majukwaani.

Alisema yeye binafsi baada ya kupumzika masuala ya siasa hivi sasa amejikita katika shughuli za kilimo ikiwa ni katika kuunga mkono kwa vitendo wito wa Rais Magufuli wa kuwataka watanzania kufanya kazi badala ya kuendeleza masuala ya kisiasa kipindi chote.

Akifafanua alisema kilimo ni uti wa mgongo kwa uchumi wa Tanzania na kwamba ili kuweza kuwa na viwanda vinavyozalisha kwa wingi lazima vipate malighafi za kutosha ambazo nyingi zinatokana na mazao ya kilimo.

“Binafsi naipongeza sana serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa kuweka msukumo katika suala zima la kilimo, ufugaji na hata uvuvi, niwaombe watanzania tushirikiane na serikali katika msukumo huu kwa kuhakikisha tunajikita katika shughuli za ujenzi wa nchi yetu ikiwemo kuwekeza katika kilimo,”

“Ukweli watanzania hatuna sababu ya kwenda kuhangaika katika nchi nyingine mfano China, Dubai au kwingineko wakati Tanzania tumejaliwa kuwa na ardhi ya kutosha, hii ardhi yetu ni dhahabu nyeusi, tuna mabonde na mito ya kutosha tuyatumie kwa kuleta mapinduzi ya kilimo, naamini Tanzania tutafika mbali,” alieleza Mgeja.

Aliendelea kueleza kuwa kilimo kina faida kubwa iwapo mtu ataamua kuwekeza kwa dhati na ni uti wa mgongo wa uchumi wa taifa la Tanzania ambapo hata hayati baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika maisha yake muda mwingi baada ya kung'atuka alijielekeza katika shughuli za kilimo.

“Tunapofanya hivi tuelewe pia tunamuenzi baba wa Taifa, hayati baba Julius Kambarage Nyerere, na tufahamu siasa siyo maisha pekee, niombe kufafanua kuwa awali niliposema nimepumzika siasa, nilieleweka isivyo, sikuwa na maana ya kuacha siasa, bali nimepumzika, na nilipopumzika matokeo yake ni haya, nimejikita kwenye kilimo,”

“Kwa sasa nimejielekeza kwenye kilimo, ikifika wakati nitafanya tena siasa, niliyokuwa nikiyasema huko nyuma sasa ninayatafsiri kwa vitendo, ukipumzika siasa unajielekeza kwenye shughuli nyingine ikiwemo pia ufugaji wa samaki, ni vizuri watanzania tusikubali kulazwa usingizi na masuala ya kisiasa,” alieleza.

Kwa upande mwingine Mgeja ametoa wito kwa vijana hapa nchini kujikita katika kufanya kazi badala ya kushinda vijiweni wakipiga soga na kucheza pooltable na kwamba vijana wana nafasi kubwa katika ujenzi wa taifa lao na hawapaswi kuchagua kazi.

"Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, wanapokaa vijiweni wakisubiri kazi za kuajiriwa, ni wazi wanachangia katika kuchelewesha kukua kwa uchumi wetu, niwaombe wabadilike sasa wajikite katika shughuli za kilimo, ufugaji na hata uvuvi, ili mradi kila mmoja afanye kazi, asisubiri ajira za maofisini, hazitoshi,"

“Lazima tuelewe kwamba ili kufikia mafanikio ya nchi yetu kuwa ya viwanda vinavyozalisha, ni budi sisi wenyewe tujikite katika kufanya shughuli zitakazosaidia viwanda hivyo vifanye kazi, na mojawapo ya shughuli hizo ni kilimo, tuzalishe mazao kwa wingi, tufuge kisasa na hata kuendesha shughuli za uvuvi,” alieleza Mgeja.

Alisema iwapo watanzania watadhamiria kwa dhati kufanya mapinduzi ya kilimo, ni wazi nchi itapiga hatua haraka katika nyanja ya uchumi kama ilivyotokea katika baadhi ya mataifa mfano wa Thailand na Malaysia na kwamba ili kuifikia Tanzania ya viwanda na yenye uchumi wa kati lazima watanzania wafanye kazi.

View attachment 1138369View attachment 1138370View attachment 1138373

Angeanza siku nyingi mbona angekuwa tajiri mkubwa kuliko yale mambo yake kuwa kama kijana wa White hair.
Alime kisasa na aongeze bidii ili kilimo kiwe na tija zaidi kwake, jumuiya na Taifa kwa ujumla.
 
Mkuu usipoteze muda kumpa promo mamluki wa Lowasa.
 
Back
Top Bottom